Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

dah! amekufa bila kulipa hela zetu????

Taifisha mali zake huyo marehemu aende huko akahojiwe na mwenye heri baba wa Taifa kwanini wanawasababishia umasikini watanzania...... na bado tutasikia mengi tu Mungu yupo nasi wanyonge wa nchi hii
 
atakuwa kavushwa mipaka huyo akina sobhai walisindikizwa mpaka mpakani kukimbia kesi

Mkuu ya wezekana kweli eti eeeh!! wanaweza chonga kinyago chenye sura yake ili kuwadanganya watz... alafu bahati mbaya sasa tukisema tuipeleke maiti kwa mkemia mkuu wa serikali kwa uchunguzi ndo yale yale magamba yanayolinda mfumo ....kazi tunayo ila yanamwisho...
 
mwili upimwe dna, kwani balali kafa au yuko hai!? Sijashawishika..........

balali hajafa kwani haujui serikali yetu,bongo moviesi na wezi wa fedha zetu?kwani hujui why bongo wasani4 wanavyopendwa?ni kwasababu wanaplay wapa mbinu za kuwaigizia watanzani kwani wanajua wabongo wanapenda fixes ili mambo yaende.'kwasasa wamechemsha kwani watu wanata live.they will soon watch and see-they will hear and understand that we are knowledgeable.
 
Most likely!
Tujue wana bodi maana ya limited liability!
Fedha hiyo si ajabu ilikwisha tangulizwa India , UK au Canada ambako mkono wa Kova au TRA haufiki kirahisi.

hapa Taifa limekula hasara Jaji inabidi ataifishe mali hizo kwa faida ya Taifa
 
Kafa wapi?
Kuna,alieiona maiti yake?
Hawa jamaa hua wanachomaga watu, so wanaenda wanachoma mabua then tunazugwa ndie wakati mtu anakula kuku Canada
 
Siku hizi ukifa anakulilia mamako mzazi na mke analia kimachale. Mafisadi wamechokwa ila hawajikubali tu. Poleni beneficiaries.
 
Mafia wa Kihindi ndo mchezo wao huo, I bet hajajiua bali kauawa...hatahivyo inaonekana kesi hiyo imeandaliwa kushindwa, iweje waibe zaidi ya 5M, mahakama ithibitishe kuwa wameiba 2.2B then atakiwe kulipa faini ya 400M? ...?
Vinasaba vya marehemu vichukuliwe na uchunguzi ufanyike wa kutosha kama kweli marehemu ndo mwenyewe... usije kuta kuna mhindi mwingine kafa natural death wao wakampiga risasi kisha haraka haraka wataenda kumchoma moto!!!
 
Mafia wa Kihindi ndo mchezo wao huo, I bet hajajiua bali kauawa...hatahivyo inaonekana kesi hiyo imeandaliwa kushindwa, iweje waibe zaidi ya 5M, mahakama ithibitishe kuwa wameiba 2.2B then atakiwe kulipa faini ya 400M? ...?
Vinasaba vya marehemu vichukuliwe na uchunguzi ufanyike wa kutosha kama kweli marehemu ndo mwenyewe... usije kuta kuna mhindi mwingine kafa natural death wao wakampiga risasi kisha haraka haraka wataenda kumchoma
Wananchi hawaiamini serikali yao.
 
Amejua bado miaka miwili jamaa amalize muda wake sasa akili zikagomea hapo.
 
Nani kashuhudia maiti yake?
Au ndio kama yale yale ya yule mtzusa?
 
serikali ya jk ni ya kihuni sana, tunahitaji udhibitisho wa picha na video..hawakawi kutufanyia kama walvyofanya kwa balali, pili sisi hatumtak mtu tnataka chetu, mama zetu wengi bado wanajfungulia sakafuni huku wadogozetu wakiendelea kukatia 'gogo' vichakani.....
Jamani hii nchi inahitaji shujaa haraka sana kusafisha huu ukoko wa uozo wa a.k.a dhaifu!

oyaa jamaa hajafa yupo kajificha anakula hela ya watanzania
 
Kwa kesi ya madai itaendelea na family yake itarudisha pesa zetu ingekua kesi ya jinai ingefutwa.

Haya mambo ya vidagaa kujiua na mapapa yakitimua vumbi si ya kuyashabikia. Badala ya kumjadili huyu dagaa tuchukulie hali hii kama hoja ya kushinikiza mapapa yawajibike. Kwanza hatujaelezwa wazi mazingira yaliyopelekea yeye kujiua. Nani ana uhakika kwamba alijiua mwenyewe wakati uchunguzi wa polisi bado unaendelea?

Mimi namsikitikia sana kwa kifo chake cha ghafla na ingekuwa vizuri kuvishinikiza vyombo vya maamuzi ya kisheria kupeleleza mazingira ya kifo chake pamoja na kutueleza kwa nini washitakiwa mapapa bado hawajawa katika hali ya kuchukua risasi kujipiga wenyewe?
 
[h=1][/h]

jai-chotalal-somani-mtuhumiwa-epa-ajiua-kwa-risasi.jpg



Marehemu Jai Somani (kushoto, mwenye shati la kijani) alipokua akiingia mahakamani na watuhumiwa wenzake, enzi za uhai wake
MSHITAKIWA katika kesi ya wizi wa zaidi ya Shilingi bilioni 5 za Benki Kuu ya Tanzania kutoka katika Akaunti
ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), Jai Chotalal Somani amejiua kwa kujipiga risasi.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kujiua jana
asubuhi nyumbani kwake, mtaa wa Mindu, Upanga katika Manispaa ya Ilala. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Parang Somani ambayeni kaka yake hajui kwa nini mdogo wake amejiua.


Source - habarileo
 
Kidumu chama cha mapinduzi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Haya mambo ya hivi yanaleta giza sana. Hivi kweli mtu anayekabiliwa na kesi kubwa ya wizi wa ufisadi eti anajiua halafu tunaambiwa kirahisi rahisi hivi bila kuwa na uthibitisho usio na shaka. Hivi hakuna wenye hekima kushauri namna ya kudeal na mambo tata kama haya sawa na lile kifo cha Balali kweli?

Sikiliza. Ombudsman mimi nasema hapa tunautaka msululu wa watu wenye dhamana wathibitishe kifo hiki pasi na shaka kuwa aliyekufa ndiye na pia hatua gani zinachukuliwa kutoka katika mali zake maana bado anahitajika kufilisiwa kulipa fedha zetu.

Hakuna mchezo hapa katika mambo kama haya ambayo kila mwananchi ana hitaji kujua kwa uwazi, unatakiwa kuwashirikisha washiriki wengi wenye dhamana na waseme wazi mbele ya press conference na picha na video kututhibitishia ukweli huu uonekane: Hawa ni kama vile:
Mkemia Mkuu wa Serikali akishiriana na Chief Pathologist, Mkurugezi wa mashitaka ya makosa ya jinai, Jaji Mkuu, Mbunge wa eneo analokaa marehemu, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wake, Diwani wake, kiongozi wa chama cha waandishi wa habari, Usalama wa Taifa, na mashuhuda wananchi wa kawaida wakiwemo viongozi wa dini ili siku moja ikionekana kuwa kuna uzushi au kuwa tulidanganywa basi wote hao wanahusika wanawajibishwa!

Kwa nini tunapenda kurahisisha mambo sana na usiri katika kesi nyeti za namna hii?
 
Back
Top Bottom