FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 716
Nitarejea nikiwa na maelezo marefu na ya kina juu ya ni nini JamiiForums na nani yupo nyuma ya JamiiForums. Kwa kuanzia wananchi watawasaidia viongozi wa CCM ambao mnapita hapa kujua mengi juu ya JF.
Nimesoma habari hii chini nikabaki kujiuliza; "Kama huyu ndiye Consultant wa Chama Tawala; hivi washauri wa serikali wanatoa ushauri wa namna hii pia?"
Napata wasiwasi kuwa Consultant huyu kafanya kazi kwa hisia na si kiutaalam kama mlivyotarajia; kama ndiyo njia iliyotumika pia kwa kina Lowassa na wenzake basi kuna uwezekano wengi wameonewa kwa kisingizio cha 'consultant' (Kinana!)
Nitarejea nikiwa na maelezo marefu na ya kina juu ya ni nini JamiiForums na nani yupo nyuma ya JamiiForums. Kwa kuanzia wananchi watawasaidia viongozi wa CCM ambao mnapita hapa kujua mengi juu ya JF.
mbona ccm wana radio uhuru, radio tz,tbc fm, magazeti ya uhuru, mzalendo television tbc1 pia ni ya kwao. Mimi nadhani hao ma-consultants wanatoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Tatizo sio media, tatizo ni kwamba ccm imeshindwa kutatua matatizo na umasikini wa waTZ kwa miaka 50 tangu uhuru. CCM wasitafute mchawi, unatoa makamba mkubwa unaweka makamba mdogo.
Hali ngumu ya maisha imetajwa kama moja ya sababu za kuchukiwa kwa CCM, na chama kimetaka juhudi zaidi zielekezwe kutatua ugumu wa maisha ili kauli mbiu ya ‘maisha bora kwa kila Mtanzania' inafanikiwe.
Ili kukabiliana na mwelekeo huo, CCM sasa imedhamiria kubuni mikakati ya kuwa karibu na makundi mbalimbali ya kijamii, kama wafanyakazi, washirika, wanafunzi, ambao kwa sasa wako nje ya jumuiya tatu za Chama, yaani UVCCM, UWT na Wazazi.
Mkuu Max, maoni kama haya si ya kubeza kwani ndio tafsiri halisi ya watazamaji wanaoingalia JF kwa nje.
Kwa mfano; katika kipindi cha miezi 6 hivi kuanzia kampeni hadi kuelekea uchaguzi wa 2010, 'cyber army' wa CDM walifurika sana hapa hadi ikaonekana kama vile CDM wanapewa 'air-time' kubwa sana hapa JF; sina uhakika kama ni by accident or design.
Nakumbuka vilevile kipindi cha 2006 - 08, wakati JK akiwa kwenye kilele chake, watu wengi walifikia kusema eti JF inamilikiwa na uliokuwa 'MTANDAO' wa ccm.
Tumieni maoni kama haya ama Changamoto na ma-MODs wajaribu kutoonyesha ushabiki katika mijadala. Pengine si vibaya; kutegemea na agenda husika, JF wakatangaza msimamo wao kuunga mkono upande mmojawapa kama tunavyoona katika Media House nyingine.
Hapo kweli huyo consultant kawadanganya, kuna sehemu hata mitandao ya simu ni shida kupatikana lakini watu wanaichukia ccm. Humu mbona wapo members wengi tu wa ccm?