Mshauri wa CCM na Msekwa: JamiiForums tishio kwa CCM; wadai ni ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Enheee...mwingine huyu hapa! Nae tushamchukua CDM tayari asalaaalee!
Lisemwalo lipo. Nafikiri nimeshaweka angalizo mara mbili kwa kukupa facts na kukuhimiza kufata ethics za uandishi wa habari .

ACHA USHABIKI.
 
Hii inadhihirisha jinsi gani watanzania walivyochoka na usanii wa ccm miaka 50 sasa bila maendeleo yoyote,watanzania tumeamka tunatambua haki zetu,thats why tunaichukia ccm.
 
Hii ni hadithi ya mfa maji ambaye huwa haachi kutapatapa............ccm mfa maji
 
Katika ripoti hiyo, kwa mfano mtandao wa Jamii Forum unatajwa kuwa unamilikiwa na Chadema na kwamba umetumiwa sana kuichafua CCM ndani na nje ya nchi.
.........................!!!
Kamati imedhamiria kuwa CCM nayo ifanye bidii kutumia fursa hizo za mawasiliano kama vile kuanzisha vyombo vyake ambavyo vitapambana na hasimu wao kama Jamii Forum.
Naona hawa "Consultants" ni wasomaji haswa wa michango ya humu JF, lakini kinachonikera ni kufikiri hii ni forum ya Chadema!!!!!
Mimi sijifichi ni mwana CCM lakini nakerwa sana na ufisadi na mafisadi.

CCM imelilea hili tatizo kwa makusudi, sasa viongozi wetu walitegemea nini haswa?-kupongezwa kwa kula na kunywa na mafisadi? Na je wao kweli hawkuliona hili tatizo hadi waambiwe na the so-called "Consultants".

Hapa ndipo panaponisikitisha maana nakitakia mema chama changu, na je vikao vingi vinavyo endesha chama vimeshindwa kuona makosa yanayotendeka?

I fear for CCM.

Uzuri wa JF ni kutoa maoni huru ili kujenga na kusahihisha makosa, kwa ripoti ya "Consultants" inaelekea ujumbe umefika panapostahili na hatua zimechukuliwa-this is a positive move.

Kwa mantiki ya kufikiri kuwa JF ni ya Chadema CCM itafanya kosa la kuanzisha forum yake ambayo itakosa mvuto kama itakuwa kazi yake ni kusifia viongozi na kuwapamba-kama afanyavyo Issa Michuzi na blogspot yake. Fuatilia kwa makini Issa Michuzi Blogspot na utaona idadi ya watu wanaotembelea pale imekuwa ikipungua kadri sifa za viongozi (hata wale mafisadi) zinavyozidi kupambwa.
 
Kwa mantiki ya kufikiri kuwa JF ni ya Chadema CCM itafanya kosa la kuanzisha forum yake ambayo itakosa mvuto kama itakuwa kazi yake ni kusifia viongozi na kuwapamba-kama afanyavyo Issa Michuzi na blogspot yake.

Mkuu Lole, jana nilianzisha Mada nikiwapongeza CCM kufuata nyayo za CHADEMA, Nikatoa Mfano walivyoamua kufata approach ya CHADEMA ya kuwekeza kwa Wasomi wa Vyuo kwa Kuvialika Vototo vya Chekechea kwenye Public Hearing ya Katiba pale karimjee.

Sasa nawashauri vile vile Waanzishe Forum lakini nawasihi wasije wakaikimbia baada ya Wiki Moja na Kusingizia inamilikwa na CHADEMA, nakumbuka Daily news walianzisha Forum yao nadhani ilikaa kwa muda wa Mwezi Mmoja tu Ikafa

So CCM anzisheni Forum tutawafuata huko huko na nawahakikishieni Mtatuachia hiyo Forum
 
Kwa mantiki ya kufikiri kuwa JF ni ya Chadema CCM itafanya kosa la kuanzisha forum yake ambayo itakosa mvuto kama itakuwa kazi yake ni kusifia viongozi na kuwapamba-kama afanyavyo Issa Michuzi na blogspot yake.Fuatilia kwa makini Issa Michuzi Blogspot na utaona idadi ya watu wanaotembelea pale imekuwa ikipungua kadri sifa za viongozi(hata wale mafisadi) zinavyozidi kupambwa.
hapo kwenye red umenena, ukikaa kwenye aina fulani ya maisha kwa muda mrefu inatokea kujisahau na ndicho kinatokea kwa CCM. Hizi blogs 'zinacheza' na akili za kile watu wanataka hivyo kama JF ni 1+1=2 wanataka kutuaminisha kuwa ukipiga vizuri propaganda na domo utamuaminisha mtu kuwa 1+1=11. Ni watu wachache sana wanaoweza kuaminishwa kihivyo kwa wakati wa leo maana hata asiyeelewa anataka aelewe! Ndiyo maana wanadhani Nape/Januari anaweza kushindanishwa na Mnyika au Lema
 
Utata tuu! Sasa mbona mtu anapoelimisha anaambiwa anafanya "ushabiki"....why?! Kusema "kwa hili CCM mmedangaya" amekua mshabiki? Wew kama founder wa kitu kwa nia njema ya kuitumikia jamii unaambiwa chombo ulichokianzisha kinamilikiwa na kutumiwa na mtu mwingine kwa uhasama,ukae kimya tuu si utaitwa *****. Mie huwa sioni post za founders wa JF hovyo hovyo isipokua kuna habari au taarifa muhimu tu. Infact siwaoni hata wakichangia mijadala mbalimbali inayoendelea humu ndani. Ethics gani zinakikwa hapa hebu dadavua kwa mifano na viambata (maana hiyo ndiyo moja ya sifa kubwa ya JF,). Sasa kama kuna mtu au kikundi cha watu wanafanya mambo ambayo yana-qualify kuwa NEWS kwanini wasiandikwe? Haya, hii ni forum, kuna michango ya watu mbalimbali. Ikitokea kwamba watu wengi wamechangia in favor of kundi hili au lile, suala la ethics za uandishi wa founder linatokea wapi tena? Au kuna mtu maoni yake yalibanduliwa hapa kwa kuwa ni ya mwana- CCM? Au yapo ambayo yaliandikwa kwa font kubwa zaidi kwa vile ni ya mwana-CDM? Aaaahh jamani...why?

Halafu na hawa CHADEMA hawa whoever they are,mbona wana maguvu sana hivi aah!

  1. Wao wanaweza kuwanunua wasomi wa vyuo vikuu na kuwapeleka kutibua mijadala ya katiba mpya
  2. Wao wanaweza kuitisha maandamano yanayotishia amani ya nchi
  3. Wao wanaweza kuwakokota maaskofu wakubwa na kuwafanya wawaunge mkono
  4. Wao wanaweza kunikokota hata mie ambaye hawajawahi kuniona na kunishawishi nijiunge na JF pamoja na wana JF wengine woooote (majority)
  5. Wao wanamiliki Tanzania daima na Mwanahalisi wakati wenzao wana uhuru na mzalendo tuu
  6. Wao wanaiba nyaraka za siri za serikali

Haaa hawa vipi hawaa!!!
Ukiwa kama nahodha wa chombo unatakiwa ujue ukubwa wa chombo chako na kujua mwelekeo wa kule unakotaka kukifikisha chombo hicho. lakini vile vile unatakiwa ujue vizuri sana mwelekeona hali halisi ya njia unayopita na tabia zake za hali ya hewa.

Sasa kama kiongozi wa forum hususan hii ya waTanzania unatakiwa ujue nafasi yako katika jamii hiyo. Kiandishi tunasema kuwa kazi yako kubwa ni kuelimisha jamii, kuipasha habari jamii na kuiburudisha jamii. Kama kiongozi wa jamii huruhusiwi kabisa kushabikia au kuitolea maamuzi binafsi habari na kuipeleka kwa jamii. Kwani tunaamini kuwa kalamu ya mwandishi ni hatari kuliko bomu la nyuklia.

Nikipembua haraka haraka sana katika forum zako na maandishi mengi sana. ume base sana upande wa Chadema na kuwa forum yako kama tawi la Chadema na yeyote alie kinyume na matakwa ya Chadema basi ni adui yako pia.

Ni vizuri kusimamia haki za kuruhusu kila pande kutoa hoja zake na kuiachia jamii isome na kuamua. Wewe kazi yako kuu ni kuondoa lugha chafu na hatarishi kwa jamii.

Vile vile unatakiwa ujue wazi kuwa jamii ya tanzania hususan tanganyika sasa ina matatizo makubwa sana ambayo sio siri tena ni ushabiki wa udini. Dini moja kujiona superior than others na hilo lipo wazi kuanzia kwenye Serikali zenu mpaka vyama vya siasa. Sasa kama mwandishi na msimamizi wa forum unatakiwa kuliweka bayana hilo na kulikemea kwani so long as limejitokeza kwa wingi basi huwezi kulifumbia macho.

lakini la mwisho nazidi kukusisitizia kufata sheria na ethics za kiuandishi kwani hizo siku zote zitaifanya forum yako iwe makini na kuondoa malalamiko kwa jamii ikiwa pamoja na kupata wachangiaji makini kama walivyokuwa katika Youngafrican.
 
Kwenye biashara mtu anayefanikiwa ni yule anayeweza kugundua "FURSA" zilizopo na kuzitumia vizuri. Mfano huu naulinganisha pia kwenye siasa na kuiona JF kama 'FURSA' iliyokuwa wazi kwa yoyote yule anayetaka kuitumia na si Chadema na CCM tu bali CUF, NRA, TLP, UDP na kile chama cha DOVUTWA UPDP nk.

Kushindwa kuitumia "Fursa" iliyopo na kuanza kuituhumu ni udhaifu wa kiuongozi na ni upungufu wa MUONO/VISION.

Kwa mfano mpaka wiki iliyopita hakukuwa na mawasiliano ya simu (FURSA) kule Samunge, Loliondo kwa Babu na tumeona majuzi wafanyakazi wa Airtel wakimpa Babu simu kumaanisha mtandao wa simu unafika Loliondo. Miezi michache ijayo ataibuka mtu na kusema babu ameingia 'DILI' na AIRTEL ndiyo maana hataki kutoka kijijini kwake kunapopatikanika mtandao wa Airtel pekee. Kumbuka tangia issue ya Babu inaanza mawasiliano ya simu yalikuwa ni "FURSA" inayosubiri mtu makini kuitumia.

Nashauri badala ya kuilahumu JF, waitumie vizuri kujijenga. Hata kama wataanzisha mtandao wao na kuruhusu mawazo huru kwa kila mtu, watashangaa maoni watakayopata na kuishia kusema mtandao wetu umenunuliwa na Chadema na sijui hapo watamlahumu nani!!
 
JK jana alitumia muda mwingi tu kueleza yale waliokubaliana na wenzake wa NEC ya CCM waende kuyafanya. Moja kati ya waliokubaliana ni kujibu hoja za wapinzani haraka na kwa ukweli. Nadhani Nape atajikita humu JF kutujibu kama anavyofanya Dr Slaa, Mh Mnyika, Mh Regia na wengine wengi wa CHADEMA.

Max, wakati fulani mlikwenda Dodoma nadhani. Kumbe mlikubaliana kutokubaliana katika mambo ya msingi kwa Taifa letu. Endeleeni na msimamo huu. Nje ya JF, uhuru wa kujieleza kungineko ni taabu tupu.
 

Katika ripoti hiyo, kwa mfano mtandao wa Jamii Forum unatajwa kuwa unamilikiwa na Chadema na kwamba umetumiwa sana kuichafua CCM ndani na nje ya nchi.

[/FONT]

Mkuu Max, maoni kama haya si ya kubeza kwani ndio tafsiri halisi ya watazamaji wanaoingalia JF kwa nje.

Kwa mfano; katika kipindi cha miezi 6 hivi kuanzia kampeni hadi kuelekea uchaguzi wa 2010, 'cyber army' wa CDM walifurika sana hapa hadi ikaonekana kama vile CDM wanapewa 'air-time' kubwa sana hapa JF; sina uhakika kama ni by accident or design.
Nakumbuka vilevile kipindi cha 2006 - 08, wakati JK akiwa kwenye kilele chake, watu wengi walifikia kusema eti JF inamilikiwa na uliokuwa 'MTANDAO' wa ccm.

Tumieni maoni kama haya ama Changamoto na ma-MODs wajaribu kutoonyesha ushabiki katika mijadala. Pengine si vibaya; kutegemea na agenda husika, JF wakatangaza msimamo wao kuunga mkono upande mmojawapa kama tunavyoona katika Media House nyingine.
 
Hivi huyu "Consultant" alijipa muda kidogo kufikiria anasema nini?...yaani JF against all media powers za CCM akaona JF ni mwiba? just think of it ..Magazeti: Uhuru, Mzalendo, Daily News, Rai, Mtanzania etc Radio: Uhuru FM, Clouds FM, TBC Radio...TVs: TBC 1 and 2, Star TV etc na bado wana complain kuhusu JF ambayo coverage yake haizidi watu 500,000 ni upuuzi..!
 
Mapendekezo na resolutions hizo ni nzuri sana, but kinachotakiwa ni utekelezaji ambao kwa maoni yangu utekelezaji huo unahitaji, watu ambao ni intelligent, diligent, highly committed, not selfsh, high degree of integrity na viongozi wenye kujali watu na wenye uchungu wa kutatua kwa dhati matatizo ya nchi hii.Talking is always easy but walking the talk is a gigantic and painful task.Let us wait and see.
 
Mkuu,

Nilicheka tu baada ya kuiona hii habari lakini nikaja kuwaza sana; hivi CCM wanadanganywa kiasi hiki? Hawa 'consultants' wanatumia vigezo gani kuwasilisha maoni yao kwa viongozi wetu wa kitaifa?

CHADEMA wanapewa credit nyingi ambazo hata mtu huwezi kuamini kama wanapewa; ni wazi CCM wanaiogopa CHADEMA sasa kwa kuamini ina hela nyingi sana mpaka inaweza kufadhili vitu vingi tu.

Twitter, FaceBook etc nazo naona zinawatisha CCM kwa ushauri huu wa 'consultant'; huu ni upotoshaji wa wazi. Nilikuwa napuuzia lakini nahisi kuna tatizo ambalo linatakiwa kuwa addressed kwa viongozi wa kiserikali na hata vyama, hivi wao ni vilaza kuambiwa uwongo wa mchana na kuuamini?

Nina wasiwasi 'consultants' hawa wanafanya kazi kwa hisia tu

Mkuu toa tamko kali via media kwa kutuhumiwa kuichafua ccm. Ikiwezekana tufungue kesi. Hawa jamaa wamezidi kulopoka yaani hakuna mwenye uafadhali, i can say ccm is over.
 
Nimesoma habari hii chini nikabaki kujiuliza; "Kama huyu ndiye Consultant wa Chama Tawala; hivi washauri wa serikali wanatoa ushauri wa namna hii pia?"

Napata wasiwasi kuwa Consultant huyu kafanya kazi kwa hisia na si kiutaalam kama mlivyotarajia; kama ndiyo njia iliyotumika pia kwa kina Lowassa na wenzake basi kuna uwezekano wengi wameonewa kwa kisingizio cha 'consultant' (Kinana!)

Nitarejea nikiwa na maelezo marefu na ya kina juu ya ni nini JamiiForums na nani yupo nyuma ya JamiiForums. Kwa kuanzia wananchi watawasaidia viongozi wa CCM ambao mnapita hapa kujua mengi juu ya JF.

Habari yenyewe ni hii:

Siri ya Kamati Kuu kufyeka mafisadi hii

Na Mwandishi wetu (Nipashe)
12th April 2011

Maumivu makali yanatarajiwa kuwakabili baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye tuhuma za rushwa kama mapendekezo ya Kamati Kuu yaliyopitishwa na sasa yanasubiri baraka za Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) yatakubalika.

Vyanzo vya ndani ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM iliyokaa Jumamosi iliyopita na kuona sekretarieti ikivunjwa, vinasema kwamba ripoti ya Kikosi Kazi kilichoteuliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kutoa hotuba juu ya haja ya chama hicho kujivua gamba ambayo aliitioa mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya CCM Februari mwaka huu, inabainisha wazi kuwa tuhuma dhidi ya chama hicho kukumbatia wala rushwa zimewagharimu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kikosi Kazi hicho ambacho ni watu wanaoelezwa kuifahamu vizuri CCM na wakiwa wametakiwa kutafiti sababu ambazo zinakifanya chama hicho kikongwe kuwa katika hali mbaya kama kilivyo sasa, wanataja bila kutafuna maneno kwamba maamuzi juu ya kuwang’oa wenye tuhuma za ukiukaji wa maadili ndani ya chama ni lazima yafanyike sasa.

“Utafiti umebaini kwamba suala la rushwa limekwisha kuwa ni mzigo mkubwa kwa chama chetu. Pamoja na juhudi kubwa ambazo serikali ya CCM imezifanya katika kupambana na rushwa nchini ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mpya dhidi ya rushwa; kuunda upya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa; na kutunga sheria ya udhibiti matumizi ya fedha katika uchagzui; bado wananchi wengi wanainyooshea vidole CCM kwa kuishutumu kwamba inakumbatia wala rushwa,” imesema sehemu ya ripoti hiyo na CC kukomelea msumari kwa kusema kwamba:

“Tunataka kufanya mageuzi yatakayotuondoa katika muonekano huo, ili tuonekane kuwa ni chama kinachopambana na rushwa kwa vitendo.”

Jopo la watafiti pia limeweka wazi kuhusu taswira ya CCM kuwa imeathiriwa sana na migogoro ya viongozi, hususan makundi yanayozozana ndani ya chama hicho.

Wataalam hao pia wamesema CCM imeathiriwa na tuhuma za ufisadi, kwa kuwa ni chama kinachokumbatia mafisadi; udhaifu wa vikao vya maamuzi kutofanyika; kujipenyeza kwa kasi kwa wafanyabiashara wasio waaminifu na adilifu katika vikao vya chama; baadhi ya viongozi kujilimbilizia vyeo; CCM kushindwa kusimamia serikali kiasi cha kuiacha kuingia katika mikataba mibovu isiyokuwa na maslahi kwa taifa; kufifia kwa utamaduni wa kuwajibishana; kupotea kwa sifa ya chama kuwa cha wanyonge.

Ili kutibu maradhi hayo, Kamati Kuu imeadhamiria kuwa: “Kwa hiyo, tunawajibika kufanya mageuzi ambayo yataonyesha kwa vitendo kuwa CCM bado ni chama kinachojali maslahi ya wanyonge; na kwamba CCM si chama kinachokumbatia mafisadi wala walarushwa.”

Suala la ukoloni mamboleo ambao uimetajwa kama utandawazi pia umeelezwa kuwa umeathiri sana CCM kwa kuwa kwa nguvu ya mawasiliano ya kompyuta kama simu za mkononi, intaneti, blogs, twitters, facebook na you tube, vimechafua sana CCM ndani na nje ya nchi.

Katika ripoti hiyo, kwa mfano mtandao wa Jamii Forum unatajwa kuwa unamilikiwa na Chadema na kwamba umetumiwa sana kuichafua CCM ndani na nje ya nchi.

Kadhalika, CC imeelezwa kwamba fedha nyingi kutoka nje ya nchi zimekuwa zikiingizwa nchini kusaidia harakati ya kuiondoa madarakani CCM kama ilivyo kwa vyama vingine vikongwe barani Afrika, na kwamba fedha hizo zinatolewa kwa vyama vya siasa na hata kwa vyombo vya habari. Hata hivyo, hakuna chama wala chombo cha habari mahususi vimetajwa.

Kamati imedhamiria kuwa CCM nayo ifanye bidii kutumia fursa hizo za mawasiliano kama vile kuanzisha vyombo vyake ambavyo vitapambana na hasimu wao kama Jamii Forum.

Wataalam pia wamezungumzia hatari ya CCM kuchukiwa na kundi la vijana, ikisema kwamba ndani ya vyuo vya elimu ya juu vijana wengi wamejiunga na vyama vya upinzani na kuwapa wakati mgumu wale wanaoshabikia CCM; kwa hiyo juhudi sasa zinatakiwa kuelekezwa kuwavuta vijana zaidi katika chama hicho.

Hali ngumu ya maisha imetajwa kama moja ya sababu za kuchukiwa kwa CCM, na chama kimetaka juhudi zaidi zielekezwe kutatua ugumu wa maisha ili kauli mbiu ya ‘maisha bora kwa kila Mtanzania’ inafanikiwe.

Matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 yametajwa kama kuwika kwa jogoo anayeamsha watu, kwa sababu ushindi wa CCM kwa maana ya idadi ya kura za urais na hata viti vya ubunge vimepungua sana ikilinganishwa na mwaka 2005, huku vyama vya upinzani vikizidi kujiimarisha na kujongezea ushindi.

Ili kukabiliana na mwelekeo huo, CCM sasa imedhamiria kubuni mikakati ya kuwa karibu na makundi mbalimbali ya kijamii, kama wafanyakazi, washirika, wanafunzi, ambao kwa sasa wako nje ya jumuiya tatu za Chama, yaani UVCCM, UWT na Wazazi.

CCM imedhamiria kuwa hata muundo wake ni tatizo na kwa maana hiyo mageuzi ya muundo wa chama ni muhimu kwa sasa; miongoni mwake ni kuachana na ngazi ya chama kata na mkoa; kuanzisha kuchagua Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Wilaya na kuachana na nafasi ya mkoa, kupunguza wajumbe wa kwenye kapu ambao ni 85; kuachana na utaratibu wa viongozi wastaafu kuwa wajumbe wa vikao vya kudumu vya chama kwa kuwa ni kuwasumbua na badala yake kuanzishwa kamati ya viongozi wastaafu watakaotoa ushauri wa mambo nyeti ya kitaifa yatakapohitajika.

Mengine ni kuchaguliwa kwa makatibu wa mikoa na wilaya katika ngazi ya NEC ya maeneo yao; kuajiria kwa ujuzi na weledi, kuanzisha kamati ya ajira kuepusha upendeleo; kuanza utaratibu wa kupata maoni ya wanachama kwa kila ngazi walau kwa siku moja kwa mwezi.

Chama hicho pia kimejielekeza katika kujikomboa kiuchumi kwa kupendekeza harakati za kutafuta fedha na si kusubiri wakati wa uchaguzi, harambee za kuchangia chama ziwe endelevu na zikipatikana fedha ziwekezwe.

Kimepania kuzungumza na wapangaji wake kwa nia ya kuongeza pango; kuwekeza katika viwanja vyake; kutafuta wabia, kutafuta hati pale ambako hakuna na kuuza baadhi ya viwanja vya michezo ili kupata fedha za kiwekeza kwenye faida zaidi.

Kadhalika, chama kinataka kuimarisha mfumo wa uwekaji wa kumbukumbu za mapato na matumizi, kustaafisha waliofikia umri wa kustaafu.

Wataalam pia wamegusia mambo ya uchaguzi na sasa Kamati Kuu inapendekeza kwa NEC chaguzi zote za chama sasa zifanyike mwaka mmoja kuliko kuwa na mlolongo wa chaguzi kwa miaka minne, kwani kila uchaguzi huzaa majeruhi wanaohasimiana.

Kuhusu jumuiya za chama, UVCCM imepewa changamoto ya kuvutia vijana zaidi, UWT kuendelea kuwaunganisha wanawake, lakini imeonekana kuwa Wazazi inazidi kukosa mshiko na kwa maana hiyo inapendekezwa ifutwe.

Sababu kubwa ni kwamba wanachama wake pia wako UVCCM, UWT na CCM kwenyewe, lakini pia kazi yake ya kuendeleza shule nayo imepitwa na wakati kwa sababu ifikapo mwaka 2015 elimu ya lazima kwa kila Mtanzania itakuwa ni ya sekondari na baada ya mfumuko wa shule za kata shule zake hazitakuwa na nguvu tena.

MBIO ZA URAIS

MBIO za urais wa mwaka 2015 zimetajwa kuwa mwiba mkali dhidi ya mshikamano wa CCM na sasa Kamati Kuu ya CCM inakusudia kuwasilisha kwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) pendekezo la kutafutwa kwa utaratibu wa kumpata mgombea urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Uamuzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa matokeo ya utafiti wa Kikosi Kazi kilichopewa majukumu ya kuchunguza sababu za CCM kupoteza umaarufu katika siku za hivi karibuni na hatua zinazostahili kuchukuliwa kudhibiti hali hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka ndani ya CCM, utaratibu huo unapekezwa katika ripoti ya Kamati Kuu kwenye ajenda ya Hoja na Haja ya Kufanya Mageuzi Ndani ya Chama Cha Mapinduzi, kipengele kilichopea jina la “kanuni za uchaguzi za chama na mbio za urais katika uchagzuzi wa 2015.”

Kamati Kuu imethibitisha kwamba mbio za urais wa mwaka 2015 ni miongoni mwa mambo ambayo yanakiumiza sana chama ndani kwa ndani, hali inayohitaji ufumbuzi wa haraka.

Kamati Kuu imebaini kwamba makundi ya vinara wanaowania urais yamewagawa wanachama na kuathiri mshikamano ndani ya chama kwa kiwango kikubwa.

“Imeonekana kuwa kiini cha tatizo hili ni utaratibu wa kupata wagombea wa CCM ambao unatumika hivi sasa, kulingana na Kanuni za Uchaguzi wa kuingia katika vyombo vya Dola zilizopo,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ambao NIPASHE imeiona.

Kamati Kuu imesema kwamba katika kipindi cha uongozi kilichopita, NEC iliunda kamati ya kutafuta utaratibu bora wa kupata viongozi wa dola wanaoingia kwa tiketi ya CCM.

Ililezwa kwamba kamati hiyo iliongozwa na Dk. Mohamed Gharib Bilal, sasa Makamu wa Rais, na kwa maana hiyo NEC inashauriwa iunde kamati nyingine kama hiyo.

Kamati hiyo kwa mujibu wa Kamati Kuu itafanya utafiti na kuwasilisha mapendekezo yake juu ya utaratibu bora zaidi wa kumpata mgombea urais kupitia CCM.

Utaratibu unakusudiwa utumike mwaka 2015 na ulenge kuzuia matumizi makubwa ya fedha kwa nia ya kununua kura za wajumbe wa vikao vya uchujaji na vya uteuzi wa mwisho katika mchakato ndani ya CCM.

Sharing is Caring......... for sure mon ami
 
Mkuu toa tamko kali via media kwa kutuhumiwa kuichafua ccm. Ikiwezekana tufungue kesi. Hawa jamaa wamezidi kulopoka yaani hakuna mwenye uafadhali, i can say ccm is over.

wale jamaa watatoa tamko kuhusu jf muda si mrefu
 
Mkuu Max, maoni kama haya si ya kubeza kwani ndio tafsiri halisi ya watazamaji wanaoingalia JF kwa nje.

Kwa mfano; katika kipindi cha miezi 6 hivi kuanzia kampeni hadi kuelekea uchaguzi wa 2010, 'cyber army' wa CDM walifurika sana hapa hadi ikaonekana kama vile CDM wanapewa 'air-time' kubwa sana hapa JF; sina uhakika kama ni by accident or design.
Nakumbuka vilevile kipindi cha 2006 - 08, wakati JK akiwa kwenye kilele chake, watu wengi walifikia kusema eti JF inamilikiwa na uliokuwa 'MTANDAO' wa ccm.

Tumieni maoni kama haya ama Changamoto na ma-MODs wajaribu kutoonyesha ushabiki katika mijadala. Pengine si vibaya; kutegemea na agenda husika, JF wakatangaza msimamo wao kuunga mkono upande mmojawapa kama tunavyoona katika Media House nyingine.

Kipindi hicho kuelekea uchaguzi hata cyber army ya CCM iliingia kwa nguvu wengine wakiwa na identities zaidi ya 5....remember Malaria Sugu???...CCM ilikuwa na ofisi maalum ya IT pale upanga na nadahni bado ipo.
 
Huu ni UJINGA wa hali ya juu. Yaani mie kuwa JF tayari nimekuwa MALI ya Chadema?

Mtu mwenyewe hata Kadi ya chama chochote sina na leo unaambiwa "umemilikiwa na Chadema."

JF ni watu na wala siyo Maxence Melo au sijui nani. Wale ni wadhamini wetu tu.

Ukitaka kuamini hilo, jiulize kitu kimoja: Kuna forum nyingi sana za Watanzania na Blog kibao ila kwa nini JF ndiyo inatesa namna hiyo? Ni kwa makala za wadhamini wa JF au MEMBERS wa JF?

Michuzi Blog ingeliweza kuwa kwenye nafasi ya JF leo hii ila kutokana na Michuzi kubania thread za watu na comments za watu, Michuzi blog imebakia kuwa kama kitawi cha CCM na Bwawa la Maini. Blog nyingine ya wauza nywele nayo iko juu na sababu ni kuwa wanafanya vizuri sana katika Issue ambazo wameamua wazifanye. Hata Ze-Utamu na yeye alifanikiwa saaana kwa sababu HAKUBANIA habari za watu.

JF imekuwa wazi kwa watu na kuachia habari ziandikwe na kuachwa hata kama ni SIRI NZITO ya Serikali. Zimeondoloewa tu zile ambazo au zinatukana au zina majungu. Kuachia habari huku zisomwe na watu wote wanaoingia JF ndiyo kumeifanya JF iwe hapo ilipo na kuwapa SIFA za UJASIRI wadhamini wa JF.

Ila leo mtu akija na kusema JF ni mali ya Chadema ni sawa na kusifia Jiko fulani linapika vizuri na LIMEDHAMINIWA na fulani na unasahau kuwa WAPISHI wake wakihama, jiko litabako historia. Wanataka kusema mtu kama FMes ni Chadema? Kibunango ni Chadema? Malaria Sugu, Mwiba, Junius, Kishonga, Ndalu, Tumaini, Ngongo, X-Pasters na wengine wengi wanaoshinda hapa wakimtukana Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla na wao wamekuwa ni Chadema?

Hebu mwangalia Waberoya na makala zake, unataka kusema huyo ni Chadema?

Kweli MFA MAJI, HAACHI KUTAPATAPA.......... Atashika hata kitoto cha Ndege/bata ili asizame.

Umesahau Zemarcopolo, Mr Mak, Hafif na Bado nipo nipo wanaoponda chochote kuhusu cdm
 
CCM ina matatizo ya kufikiri sana.Ni kweli leo hii UVCCM haina kazi tena kwani vijana wengi hawaipendi tena na hii ni kwa sababu ya kuwa na upendeleo wa kindugu kama kuwajaza kina Ridhiwani na makamba January. Watoto wa wakulima siku hizi hawana nafas tena ndani ya Uvccm.

Huku vyuoni hivi sasa kila mtu hataki tena kusikia habari ya ccm. Hata wale wanachama wao sasa hivi ni waoga hata kujitambulsha kuwa wao ni wana uvccm. Katu chadema haitarudi nyuma. Sisi wana JF tunaendelea kuwatoa mawazo yetu hapa DAIMA NA CCM HAITAPATA KITU TENA. UWEZO WA KUFIKIRI CCM UMEKWISHA
 
Hao nao wameishiwa sera. Hiyo JF nani anaifahamu huko mitaani kwetu, na bado wanaichukia CCM!!!!!!!!!!

babangu miaka 45 hali mbaya. ccm imemtupa. ccm haijawahi hata kumpa kofia wala fulana.
hana hata simu ya mkononi. JF ataijulia wapi?

lakini hataki tena nyoka anayeitwa ccm
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom