Mshahara wa Mrisho Ngasa KUFURU!

M6 bado sio hela ya kumpa kiburi tutokana na hali ya maisha ya sasa ila ni hela nzuri kama atajipanga vizuri na tutoongeza mke au kukimbizana na masister du ambao ni mastaa.Ajifunze kwa Hashim Thabeet yaliyotaka kumkuta.
 
Pesa ya ugali na boga tu hiyo ndugu zanguni! ikikatwa kodi na mazagamazaga mengine kwisha habari...
 
mkuu Rejao hata mi nashangaa wanavyomshangaa kwa kupokea mil. 6..... mbona pesa kidogo ukilinganisha na mishahara ya vijana wengi humu nchini???... labda afafanue huo ukufuru kwa maana ipi???

charminglady, naona huyu atakwa hajafanya utafiti wa mishahara ya watu hapa nchini. Naona kama vile ni mwandishi wa habari kwenye moja magazeti ya shigongo!!!
 
Last edited by a moderator:
milioni sita ni kufuru??????
Kodi yao ipoje?
Cost of living sudan ipoje?
On my view naona kama ni hela ndogo sana!!!

watanzania utawaweza? Ukitumia mshahara wako, ukaninunua squater, ukachukua mkopo benk, ukafanikiwa kujenga ka nyumba ka kisasa, wanakuita fisadi au free mason. Kuna jamaa alibadilishwa idara kwa kujenga nyumba tu wakati ameitumikia nchi for more than 25yrs
 
Acheni kuandika kama sio ma-great thinkers basi. Neno "KUFURU" inaweza ikawa ni "RELATIVE TERM')".

Career ya Mrisho Ngassa ni mcheza mpira,na nchi atokayo ni Tanzania, hili halina ubishi. Hivi tukiorodhesha wachezaji wote wa Tanzania na Mishahara hao, huyu hayupo top-10??

Mnamlinganisha Ngassa asie na hata Diploma moja labda na Engineer aliesota miaka kibao akikesha kwenye mbu ndio mnasema sio kufuru??

Kwa alichowekeza Ngassa mpaka kuja kupata hizo 6Mil ni hela nzuri tu tofauti na wengine wailliowekeza kwenye elimu, tena kwa kusotea kutoboa usiku, boom linachelewa mwezi mzima, unatumia akili nyingi kufikiri leo unakuja kujitapa eti unamzidi Ngassa mshahara!!!!

Tuna kina Felix Sunzu na Emanuel Okwi ambao ndio professional wetu hapa, wanalamba hizohizo, tena kwenye timu kama Simba ambayo naamini ni ndogo kuliko El Mereikh, why tusione kwamba kiwango hicho ni kikubwa kwa Mtanzania kupokea??

Fikirieni kwa umakini tena
 
charminglady, naona huyu atakwa hajafanya utafiti wa mishahara ya watu hapa nchini. Naona kama vile ni mwandishi wa habari kwenye moja magazeti ya shigongo!!!

Huyo huyo Shigongo si ndiye anayekulisha wewe na familia yako?,hivi ni kwa nini umtaje mtu ambaye unaamini katika moyo wako kwamba hausiki na jambo unalolizungumzia?,huu ni ukosefu wa hoja na upungufu wa uelewa!!!!!!,kubwa hapa ni kujadili hoja na sio kuanza kumuingiza mtu asiyemo tena kibaya zaidi ni kwamba hata hajachangia hoja husika.
 
Acheni kuandika kama sio ma-great thinkers basi. Neno "KUFURU" inaweza ikawa ni "RELATIVE TERM')".

Career ya Mrisho Ngassa ni mcheza mpira,na nchi atokayo ni Tanzania, hili halina ubishi. Hivi tukiorodhesha wachezaji wote wa Tanzania na Mishahara hao, huyu hayupo top-10??

Mnamlinganisha Ngassa asie na hata Diploma moja labda na Engineer aliesota miaka kibao akikesha kwenye mbu ndio mnasema sio kufuru??

Kwa alichowekeza Ngassa mpaka kuja kupata hizo 6Mil ni hela nzuri tu tofauti na wengine wailliowekeza kwenye elimu, tena kwa kusotea kutoboa usiku, boom linachelewa mwezi mzima, unatumia akili nyingi kufikiri leo unakuja kujitapa eti unamzidi Ngassa mshahara!!!!

Tuna kina Felix Sunzu na Emanuel Okwi ambao ndio professional wetu hapa, wanalamba hizohizo, tena kwenye timu kama Simba ambayo naamini ni ndogo kuliko El Mereikh, why tusione kwamba kiwango hicho ni kikubwa kwa Mtanzania kupokea??

Fikirieni kwa umakini tena

Mkuu tatizo la watu wengine kama unavyowaona waningia humu wakiwa tayari wamekunywa Bangi,lakini kikubwa na wivu wa maendeleo hawataki kuona mtu anainuka,akiinuka lazima waponde ili akte tamaa,afadhali yako wewe ambaye una akili timamu umeliona hili,ushauri wako ni wa mana sana lakini yatakuja majamaaa humu na Ba..g.i zao za kunya aubuhi asubuhi na kuanza kutoka mapovu tena meusi midomoni.Hongera mkuu kwa kuliona hili!
 
Ndumbaro alisema kuwa wakati akiwa Gefle, Boban alikuwa akilipwa mshahara wa kila mwezi wa Dola za Kimarekani 5,000 (sawa na Sh. Milioni 7.4), na kushangazwa na kauli kuwa kiungo huyo alikuwa hataki fedha hiyo ikatwe kodi.

Ndumbaro alisema vile vile kuwa, Boban alikuwa akihitaji kulipwa fedha zinazotokana na mapato ya milangoni, pengine kama utaratibu wa nchini ulivyo , jambo ambalo katika nchi zilizoendelea halipo.

Alisema kuwa kabla ya kueleza hoja hizo, Boban alianza kukacha mazoezi ya timu kwa kudanganya kuwa ni mgonjwa, jambo ambalo lilimfanya akose motisha ya Dola za Kimarekani 200 kwa kila mechi (sawa na Sh. 295,000), ambazo zilikuwa zikitolewa na uongozi wa klabu hiyo.
........
 
Kibongobongo tunaona ni pesa nyingi ingawa kuna wachezaji wanaolipwa zaidi ya Ngassa.
 
Madem watamkoma..........

Nasikia ana muvi moja kali sana ya ngono baadh ya wa2 wanayo, waliyoiona wanasema jamaa c mkali kwenye soka pekee, bali hata kwenye kuibanjua amr ya sita jamaa anatisha!
 
Mbona kidogo? akikodi nyuma, usafiri, chakula na nyingine za kutumia familia atabaki na nini?
 
Mbona kidogo? akikodi nyuma, usafiri, chakula na nyingine za kutumia familia atabaki na nini?

Angebaki bongo angepata hizo??
Maisha Khartoum sio ghali kihivyo, hizo gharama pengine hata angekua bongo angezibeba tu.

Tanzania ina watu wazima wanaojitegemea wangapi? Labda tuseme 20Mil. Sasa wagawe sehemu kuu labda mbili zilizo sawa accordingly to their income, huyu Ngassa ataangukia kundi lipi??

Wagawe tena hao 20Mil katika sehemu tatu zilizo sawa, unafikiri ataangukia kundi lipi napo?

Fanya tena hivyo kwa kugawa mafungu manne ya watu 5Mil according to their level of income, unafikiri napo Ngassa ataangukia wapi??
 
Huyo huyo Shigongo si ndiye anayekulisha wewe na familia yako?,hivi ni kwa nini umtaje mtu ambaye unaamini katika moyo wako kwamba hausiki na jambo unalolizungumzia?,huu ni ukosefu wa hoja na upungufu wa uelewa!!!!!!,kubwa hapa ni kujadili hoja na sio kuanza kumuingiza mtu asiyemo tena kibaya zaidi ni kwamba hata hajachangia hoja husika.
:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid::iamwithstupid:

Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!:coffee: --------Invisible
 
Nikusahihishe neno tishio,

Milioni 6 sio tishio, Samatta analipwa 15m mshahara tu, 15m akifunga goli klabu bingwa afrika, 5m akifunga goli ligi ya kongo,

Sasa samata ameibuka mfungaji bora wa TP Mazembe akipiga bao 24 kati ya hizo 6 ni za klabu bingwa tu.

Jumlisha kavuna kiasi gani mwaka huu wa 2012?

Hiyo habari huenda
ilitolewa kabla ya simba kuingilia kati,

Nijuavyo ni kuwa wasudani wameachana na mpango wa kumsajili ngasa, hivyo ataendelea kukipiga VPL Tz tu!

mpira wa bongo fitina nyingi,na hasa unapochezea kilabu za Simba na Yanga.
 
Nikusahihishe neno tishio,

Milioni 6 sio tishio, Samatta analipwa 15m mshahara tu, 15m akifunga goli klabu bingwa afrika, 5m akifunga goli ligi ya kongo,

Sasa samata ameibuka mfungaji bora wa TP Mazembe akipiga bao 24 kati ya hizo 6 ni za klabu bingwa tu.

Jumlisha kavuna kiasi gani mwaka huu wa 2012?

Hiyo habari huenda
ilitolewa kabla ya simba kuingilia kati,

Nijuavyo ni kuwa wasudani wameachana na mpango wa kumsajili ngasa, hivyo ataendelea kukipiga VPL Tz tu!
Mkuu hizi data huwa unazitoa wapi??

Ochan auzwa kwa mbovu za Mil.80 | darhotwire

Naye wakala wa Samatta, Damas Ndumbaro, alisema kuwa kulikuwa na mvutano wa hapa na pale baina ya viongozi wa Mazembe na mchezaji huyo ambapo mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika walikuwa wanataka wamsainishe mkataba wa miaka mitano jambo ambalo wamelikataa.

Ndumbaro alisema kuwa wao walipendekeza Samatta asaini mkataba wa miaka mitatu na vile vile wahakikishe kwamba anapatiwa nyumba na motisha zake za kila mechi zielezwe kwenye mkataba huo.
Kwani Samatta atakapoanza kuichezea Mazembe atakuwa analipwa mshahara wa Dola za Marekani 5,000 (sawa na Sh. Milioni 7.5) huku pia akiwa amelipiwa bima.

MICHUZI: mcheza soka mbwana samatta na mchuma wa nguvu Lubumbashi
 
Milioni sita ni kufuru??????
Kodi yao ipoje?
Cost of Living sudan ipoje?
On my view naona kama ni hela ndogo sana!!!

Mkuu, umeandika maswali ya msingi, dola 4000 siyo kufuru hata hapa Bongo, PAYE ni kama 25% sawa na $1000, accomodation $300, petrol $200, monthly stipend $2100, savings $400.
 
Ngasa+1.JPG

* Sasa anunuliwa kwa milioni 240 na kuweka rekodi

* Simba, Azam zalamba Milioni 80 kila moja, Ngassa naye alamba mil 80 na mshahara mnono.

Klabu ya El Mereikh ya Sudan imetoa dola 100,000 (shs 160 million) kuzilipa klabu za Azam FC na Simba SC ili kuondoa mgogoro wa usajili wa mchezaji Mrisho Ngassa.

Awali El Mereikh ililipa Dola za Kimarekani 75,000 (shs million 120) kwa klabu ya Azam FC pekee kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyo na kuzua mtafauku mkubwa dhidi ya klabu ya Simba na kuamua kuweka pingamizi katika Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), CAF na Fifa.

Simba ilidai kuwa Ngassa ni mchezaji wao halali kutokana na ukweli kuwa ilimnunua kwa shs milioni 25 zilizotakiwa na Azam FC na kumlipa stahiki zake zote kwa mujibu wa mkataba huo.

Pamoja na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa timu ya Azam FC kutokana na ukweli kuwa Ngassa alikuwa akiichezea Simba kwa mkopo, Simba iling’ang’ania na msimamo wake na kupeleka suala hilo mbele ya vyombo vya sheria vya TFF ili kupata haki yake.

TFF ilishauri klabu hizo kukaa meza meza moja ili kuona kuwa wanaondoa utata huo, jambo ambalo lilifanyika Jumatatu na Jumanne na kufikia muafaka huo na El Mereikh kulipa fedha zaidi na kumfanya mchezaji huyo kusajiliwa kwa Dola za Kimarekani 150,000 (Milioni 240 ukijumuishs Dola za Kimarekani 50,000 atakazolipwa Ngassa na El Mereikh) na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa kitita hicho hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa wamefarijika sana na makubaliano hayo na wao kutoa kipingamizi cha Ngassa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya mjini Khartoum kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Mtawala alisema kuwa hayo ni matunda ya kujadili mambo katika meza moja na wala si kwa kutimia vyombo vya habari kwani wao walijua haki yao ipo wapi.
afisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd alithibitisha makubaliano hayo na kusema uongozi wa klabu hiyo chini ya makamu mwenyekiti, Shan Christoms na Twalib Suleiman aliyemwakilisha katibu mkuu, Nassoro Idrissa ndiyo waliofikia makubaliano hayo.

Simba SC iliwakilishwa na Mtawala na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange Kaburu aarufu kwa jina la Perez.“Ni faraja kwetu kufikia maamuzi haya, lengo ni kumfanya Ngassa atomize ndoto yake katika soka na wala si vinginevyo,” alisema Idd.

source : Michuzi
 
Back
Top Bottom