Mabingwa wa CAF Al Ahly ya Misri yapigwa faini nzito ya milioni 276

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,151
7,918
Kamati ya Nidhamu ya CAF imeipiga faini ya USD 120,000 (takribani shilingi milioni 276) timu ya Al Ahly ya Misri kutokana na matukio yaliyojitokeza katika mechi yake dhidi ya Al Hilal ya Sudan iliyofanyika 01 April 2023. Tukumbuke hii ilikuwa mechi muhimu kwa Al Ahly ambayo walikuwa wanaponea chupuchupu kutolewa katika hatua ya makundi katika Kombe la Klabu Bingwa. Al Ahly baada ya kuvuka hatua hiyo walienda kutwaa ubingwa.

Faini hiyo imegawanyika mara mbili:
1. USD 20,000 kwa kosa la urushaji wa vitu kama chupa za maji kwa wachezaji wa Al Hilal
2. USD 100,000 kwa kosa la kutoweka ulinzi na usalama wa kutosha uwanjani

Mawazo yangu: Al Ahly na timu nyingi za Afrika Kaskazini hawawakilishi mpira wa kistaarabu wa Africa. Hapa bado nasubiria faini kutokana na makosa haya haya waliyoyafanya kwenye mechi ya kwanza ya fainali dhidi ya Wydad.
 
270M sio kitu kwa hizi timu za kasikazini kama kweli CAF wanataka kukomesha haya mambo iwe kufungiwa kucheza nyumbani full tournament, kama mechi ya Yanga Vs USM Alger, Wydad Vs Simba, Wydad Vs Al Ahly ni mfano wa mechi za hovyo
 
Hawa waarabu wanaendekezwa sana na upumbavu wao. Pengine kuna namna bahasha zinatembezwa kuwafunga mdomo viongozi wa CAF.
 
Back
Top Bottom