Mshahara wa Februari

N
Sasa nani atapeleka huko mahakama kuu hata mahakama za kawaida kama hatutaishia kulalamika tu na ubumbuwazi wetu vichwani
 
Walio tajirika hawakusoma hivyo vitabu.
Yani hapo unamfanya aliye andika hicho kitabu awe tajiri kwa sababu umetoa pesa yako mfukoni na kumchangia huku yeye akikuacha na bla blaa kibao kichwani
Kweli mkuu umenena jambo. Huwa nashangaa sana machinga wanaouza vitabu vyenye kichwa JINSI YA KUWA TAJIRI KWA SIKU KUMI NA NNE. Ukiwaangalia wao hali zao ni bora ya jana, huwa najiuliza kwani hawasomi hivyo vitabu? Daaaaaah
 
Lipeni pesa za bodi kipindi mnaandama na kugoma kudai mikopo mlijua ni bure tena lipeni kama vipi acheni kazi kukopa harusi kulipa matanga leo hii povu linawatoka ilitakiwa hata kulipa muandamane na kugoma kama mlivyofanya huko nyuma
 
Lipeni pesa za bodi kipindi mnaandama na kugoma kudai mikopo mlijua ni bure tena lipeni kama vipi acheni kazi kukopa harusi kulipa matanga leo hii povu linawatoka ilitakiwa hata kulipa muandamane na kugoma kama mlivyofanya huko nyuma
Ni zamu ya bodi ya mkopo kuandana ili walipwe.

Kama unashabikia hili unatia shaka, watu hawashindwi kulipa ila mkataba wa kukopeshwa haukusema makato yatakua 15%
Mkataba ulisema makato ni 8%.
Hili ndilo linalolalamikiwa.

Kama huelewi hilo basi hata chuo hukufika mkuu na utakua unawachukia waliosoma chuo
 
Niwachukie waliosoma chuo kwani wanaleta msosi nyumbani kwangu awamu hii kila mtu atabeba msalaba kivyake kilichopo lipeni pesa za bodi mlikuwa na kihere here sana mnaandamana na kugoma kuishinikiza bodi iwape boom lenu sasa hivi mnalalamika mimi nasema wangekata 25% ni zamu ya serikali kudai pesa zake kwa nguvu kama nyie mlivyokuwa mnaandama kupewa mikopo braza usinichukie acha kazi njoo huku tuendeshe malorry tugombane na wenye nayo achana na serikali wanataka chao
 
Kama mkataba umekiukwa si muiburuze serikali mahakamani? sasa mnavyolialia nyuma ya keyboard hapa ndo mtapata haki yenu?
[emoji13]
 
Yaani kwa waliokopa nawaonea huruma sana. Hapo ukiinclude tax na madude mengine unakuta karibia 50% ya mshahara wote siyo yako kabla haijakufikia mkononi.

Najua sababu ya kupandisha makato ni ukosefu wa pesa basi, sidhani kama kuna sababu nyingine. Ukimwambia mkubwa pesa hakuna inaitwa polisi kesho yake kwa kosa la uchochezi. Uzuri the truth always comes out one way or the other.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…