mshahara /kipato kwenye ndoa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mshahara /kipato kwenye ndoa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ndechumia, Feb 2, 2012.

 1. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wajamen kuna kisa kimemtokea rafiki yangu nikabaki naduwaa!!!
  Kuna mdada tunafahamiana nae anafanya kazi katika Taasisi fulan hapa nchini, ameolewa na ndoa yao ina kama miaka 7 hivi.

  Mimi kwa mtazamo wangu watu wanapokuwa kwenye ndoa wanakuwa wanawekana wazi vipato vyao ili kuweza kupanga shughuli za maendeleo kutokana na hicho kipato chao.

  Cha ajabu mwishon mwa 2011 huyo rafiki angu(Mdada) mishahara yao ilikosewa na wahasibu wa bank, wakalipwa malipo ambayo hawakustahili (walilipwa kiasi kikubwa zaidi)

  Mi cha kunishangaza huyu rafiki yangu hakumweleza mumewe tukio hilo ingawa yy aligundua kuwa kalipwa zaidi ya staili yake.

  Sasa limetokea tatizo, bank wamegundua kosa walilolifanya, na wamehamua kukata kwenye acc yake kiasi ambacho walimwongezea wakati huo.

  kwa kuwa aliongezewa kiasi kikubwa sana mshahara wake hauwezi ku compasate hilo deni so wamekata mshahara wote na bado inaonekana deni halijaisha, labda mshahara wa mwezi unaofuata.

  Dada rafiki yangu hana hata sent moja kumwambia mumewe kilichotokea akiogopa manake hilo ongezeko hakumshirikisha na amelitumia kwa matumizi ambayo anayajua YY tu.

  Sasa anatakiwa kulipa ada shuleni na matumizi mengine, kuomba kwa mumewe anaogopa coz anajua alichofanya.

  Sasa ananiomba ushauri aanzeje kumweleza mumewe ili aweze kumsaidia maisha yaende.

  Naomben ushauri nimpe huyu mdada.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Yeye ndo analipia watoto ada?
   
 3. m

  mitishamba JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpe wewe halaf mmalizane
   
 4. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Mwambie atafute buzi.
   
 5. ENDLESS

  ENDLESS Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwambie akope mahali halafu arudishe mwisho wa mwezi ama akae na mumewe amueleze ukweli kuhusu matumizi ya hiyo fedha
   
 6. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  hata mimi nimeshtuka kidogo hapo....labda hatujamuelewa.
   
 7. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,631
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Mwanamke analipa ada makubwa hayo
   
 8. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mume ndo huwa analipa, ila kwa kipindi hiki alikopa pesa akanunua mabati, so akamwambia mkewe alipe kipindi hiki coz mshahara wake alishautumia
   
 9. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  anasaidiana na mumewe kulipa, na matumizi mengineyo.
  Mdada anabahati kaajiriwa sehemu ambako anapata mshahara mkubwa kuliko mumewe so mumewe ndo akawa anataka ampige tafu kipindi hiki ili yy amalizie ujenzi wa nyumba yao
   
 10. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ndo alikuwa anajaribu kukopa ikiwa kila mahali anagonga ukuta, si wajua tena sikukuu, na mwaka mpya watu wengi wameharibu stock
   
 11. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Huyo mwanamke ni mjinga...ingekua mke wangu ningemsaidia kulipa but angekoma after that! We unaongezewa tu pesa hata huendi kukagua bank statement ujue kama ndo stahili yako? She is so stupid hata kama watu wana shida ya pesa but sio kihivyo...anyway the best way ni hiyo kumwambia baba watoto ujinga aliofanya.wanaume tumejaliwa roho za kubeba matatizo na kuhandle solutions za ghafla
   
 12. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Matatizo makubwa ni rafiki yako huyo wakike si mme wake....Rafiki yako ni mwizi na si mwaminifu mara nyingi mwizi anapewa punishment na mungu haendi mabli, angekuwa sio mwizi angerudisha toka mwanzo hizo pesa sababu si halali yake...za mwizi arubaini zimefika wacha ukipate cha mtema kuni mara ya pili akiona pesa sio halali yake asichukue :biggrin:
   
 13. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #13
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,393
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  hivi kila siku nyie wanawake mnalalamika haki sawa, yani unashangaa yeye mwanamke kulipa ada ya mwanawe et mpaka mwanaume ndo alipe. kwa mtindo huo kujikomboa nyie bado sana na mtabaki kuwa nyuma hata mpige kelele vipi. bwe...ge nyie.

  inakuwaje katika hii dunia ya leo familia zinapigania mabadiliko bado watu wengine mnawaza upupu.

  :focus:
  mwambie aongee na jamaa kikubwa tuu hope atamwelewa. asimdanganye kitu.
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asiogope ajiamini, aseme kilichotokea.
  Mke hawajibiki kihivyo kujieleza kuhusu mshahara wake kama vile yeye ni kijakazi wa mume.Kwanini anaogopa hivyo aukuna kitu anaficha?Ingemtokea mume, ina maana mume angekuwa anatetemea hivyo hivyo?Pia alifanya makosa makubwa kutumia pesa huku akijua siyo stahili yake.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mke "Hunny, unajua zile fedha ambazo tulizipata mwishoni mwa mwaka nikadhania ni bonus na tukatumia kwa x, y na z?"
  Mume: "ooh yeah nakumbuka"
  Mke "Well, kumbe kampuni ilifanya makosa tu na sasa wameamua kunikata kwenye mshahara"
  Mume "Really, ndio maana nilishangaa sana; ok angalau hawakufukuzi kazi"
  Mke "Yeah, sasa tutapungukiwa kwenye mambo ya ada za shule n.k"
  Mume "Oh don't worry hun I'll cover that, ila angalau zilitusave wakati wa Krismass"
  hahahahaha
  Hahahahah


  But here is the problem: Mwamanme hata hajui kuliko na ongezeko na lilitumika vipi na kwanini yeye anaitwa kuokoa jahazi wakati jahazi lilipoondoka bandarini hawakuaga!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Khaaa sasa kwanini aliitumia akijua fika sio stahili yake tena bila kumshirikisha mwenzake?

  Kilichobaki sasa ni kumweleza tu. Hopefully alifanyia hata kitu cha maana/chenye faida kwa familia maana hapo anaweza akaeleweka kirahisi zaidi. Akisema akope kwingine atakua anaendelea kukuza hilo jambo na likija kumlipukia ndio atashangaa mume anaanza kurudi nyumbani asubuhi huku amelewa.
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Hapo ndipo "kwa shida na raha" comes in handy..Nina hakika kama ni mume amefanya blunder, mke angeokoa jahazi hata kama atabaki na maswali au manung'uniko.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hawa dada zetu hawa? Kama hajakuambia "nenda huko huko ulikopeleka hizo fedha mwanaharamu mkubwa we!; unafikiri na miye nashindwa kupata fedha pembeni? ati umezitumia na hujuli ulivyotumia! kha!" Hata kulala ndani hakutalalika.
   
 19. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nadhani kusema ukweli siku zote kunasaidia sana. Anayesikia ukweli huo kwa mara ya kwanza lazima utauma na anaweza akachukia kabisa - lakini kama familia kusema ni jambo jema. Ameanza vyema kwa kukwambia wewe, sasa ampigie timing mumewe halafu amwambie! Kama amenunua kitu aseme tu, kama amehonga aseme tu! mumewe atachukia lakini yatapita.
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tatizo hapo huyo mwanamke alitumia hizo pesa kwenye matumizi yasiyo ya muhimu au haramu kabisa ndio maana anakuwa mwoga kumwambia.Au alimuhonga bf wake wa pembeni anunue gari?
   
Loading...