Msemakweli kasema ukweli kuhusu mafisadi wa elimu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msemakweli kasema ukweli kuhusu mafisadi wa elimu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Marigwe, Feb 17, 2010.

 1. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  MAFISADI WA ELIMU

  Jana nilikinunua kijarida kilichoandikwa na Ndugu Msemakweli ambacho kina orodha ya majina baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri, Wakuu wa Mkoa na Wabunge ambao inadaiwa wana vyeti ambavyo Msemakweli anaviita feki. Kijarida hicho kinauzwa shs 3,000.

  Baada ya kukisoma kile kijarida ninayo maoni yafuatayo:

  1. Nampongeza Ndugu Msemakweli kwa kuwa mjanja wa kubuni njia ya kupata fedha kiurahisi. Yeye mwenyewe anakiita kitabu. Namshangaa kwa sababu kwa mtu aliyesoma kama yeye tena sheria iweje anashindwa kupambanua kati ya kijarida na kitabu. Katika ulimwengu wa kisomi kitabu ili kiwe kitabu kinapaswa kuwa na majina ya publishers na references nyingine muhimu kama vile year of publication; bibliography na kadhalika. Hicho kitabu hakina ndiyo maana mimi nakiita kijarida.

  Alichofanya Ndugu Msemakweli ni kukaa kwenye laptop yake au keyboard yake na kuandika hayo aliyoyaandika na kuprint na kukiingiza sokoni. Katengeneza nakala 89000 ukizidisha mara shs 3000 atazipata takribani shs 267 milioni!! Hizo fedha anazipata kwa njia ya kuwakashifu waheshimiwa hao. Huu ni ujanja kweli kweli. Naye kwa vile alitangaza ni mwanachama wa CHADEMA hiyo hela itamsaidia wakati wa uchaguzi. He is very smart in a country of fools as it were. Na kwa sababu sisi watanzania tunapenda sana habari za umbea kwa upumbavu tulionao tutanunua tu hicho kijarida na yeye atapata hizo pesa bila ya jasho.

  2. Maelezo aliyoyatoa ya kila mheshimiwa utaona yana mapungufu katika authentication. Alichopaswa kufanya kwa kila mmoja wao ni kutoa ushahidi wa maadishi kutoka vyuo husika vikikiri kuwa hivyo vyeti havikutoka kwenye vyuo vyao na kwamba hao waheshimiwa hivyo vyuo hawakuwahi kuwa wanafunzi wao. Hilo hakufanya. Na kwa njia hii Msemakweli kama msomi kajitia doa na mimi usomi wake pia nautilia mashaka. Yeye alichofanya ni kumponda Rais Kikwete kuwa naye ameshiriki kuwabeba hao waheshimiwa. Jambo ambalo ni upuuzi. Katiba ya Tanzania haisemi kuwa Rais atateua mawaziri kufuatana na degree au diploma zao. Katiba inasema Rais atamteua mtu ambaye ni mbunge kuwa Waziri. Sasa hizo lawama dhidi ya Rais hazina mantiki hata kidogo.

  3. Picha inayojitokeza ni Msemakweli kiu yake kubwa ilikuwa ni kumcharaza Rais Kikwete. Usomapo hizo tuhuma zake kama vile safari za Rais nje ya nchi mimi naona hazina hoja hata kidogo. Hivi huyu Kikwete ambaye analaumiwa kwa kila kitu afanyacho ambacho kinatokana na wadhifa wake kama Rais hivi kweli tunamtendea haki? Mwacheni Kikwete afanye kazi zake za Kirais.

  4. Kijarida cha Msemakweli ni majungu ambayo yamejaa fitina na chuki tu. Naomba mnielewe. Mimi sijasema kuwa hao Waheshimiwa wana vyeti halali au vya kughushi. Mimi niachosema ni kuwa maelezo ya Msemakweli hayawezi kukubalika kirahisi bila ya kuwa “authenticated scientifically”. Na huo ndiyo usomi. Msemakweli anadai kuwa waheshimiwa hao ni mafisadi wa elimu na yeye je? Kundi lake ni lipi. Anajiita mwanasheria. Hivi mwanasheria utafanya madai bila ya kuyathibitisha na vielelezo?

  No. Come on ndugu Msemakweli fanya mambo kisomi . Mimi ningekuwa naisahihisha hiyo thesis yako ningekupa D kwa sababu ya muda ulioupoteza kuandika hayo uliyoandika.

   
 2. C

  Chechenya Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kojoa kalale
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,187
  Likes Received: 2,714
  Trophy Points: 280
  Ahhhggggggg inatia hasira hizi mada nyingine unaweza ukajiua!!

  Mtu anakuja ana andika upuuzi mtupu au kwa sababu kuandika hapa ni bure?
   
 4. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  You spot....ameeleza bila kuweka reference. Hata kama allagetion zake ni za kweli, siwezi kuamini kwa sababu hajatoa sababu za kuniaminisha. Tufikirie inside and outside, left and right, top and down, parallel and perpendicularly.

  Msemakweli anaweza kuwa kasema kweli, but what is the authentication anayoyasema. Kila mtu akipublish speculation zake itakuwaje nchi hii?
   
 5. m

  mwakipesile Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona bwana Msemakweli ameamua kijtafutia umaarutu kwa gharama ya kuandika zile pumbas bila kufanya tafiti za kisomi na kutoa reference, kuna spelling mistake nyingi sana sijui alikuwa ana haraka gani bila ya kufanya proof reading. lakini ameonesha njia wengine tuige kwa kuto ogopa. Next time utulie uandike vizuri. Bravo!!!! Kijana
   
 6. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuwe wakweli...Msemakweli amesema kweli kwa takwimu ambazo yeye anazo..Hivyo hao unawaita waheshimiwa kama Wamekashifiwa wende Mahakamani..kwani huko ndo haki hupatikana na Msema wongoi na Msemakweli atajulikana...sasa wewe ndugu yangu..unataka akupe reference ili iwe nini..alichokisema anakiamini kutokana na ushahidi aliokuwa nao...nway.. may be uko pamoja na hao mafisadi wa Elimu...But na wewe kosoa kwa hoja na sio as yo did..I hope ur Tsh 3000 is nothing kwa msemakweli...Kipi bora ur 3000 au to be Jailed..We vipi....Think critically pumbavuuu....!!!
   
 7. M

  Mtoto wa jiji Member

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilisema watu wananiponda....... asante sana Marigwe. Mimi niliwambia wana JF kuwa KM ni fisadi wa elimu kwa kuandika upuuzi ambao hauendani na shahada ya sheria.
  Ila nchi wa watu wajinga, mjinga anaandika ujinga na watu wananunua na kusoma ujinga hivyo ku-promote mjinga!!!!!!!!!
  Kainerugaba Msemauongo ni fisadi no. 1 wa elimu mwanasheria anaeandika kama mjinga wa schoo drop-out!!!!!!
   
 8. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 747
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kwa nini mnawasemea walio kashifiwa/walioandikwa?. kwa hawa waliondikwa hawaoni kama wameonewa?.Na mimi si mtetei Msemakweli. Ila si vema mtu akakuchafua kama inavyodiawa na wewe ukakaa kimya. Kwa nn hawa walitajwa kwenye kitabu wasiende mahakamani?. Msije hapa kuwasemea, waacheni waende mahakamani ili mambo mengi yawe hadharani.Kwa elimu yangu niliyonayo, mtu akija leo akisema ni feki,si vema kunyamaza, itabidi nimsaidie ktk uelewa wake mdogo.
  Wasaidieni waende mahakamani maana Jamaa kawachafua sana.
   
 9. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ndugu CHECHENYA unataka nikojoe nikalale. Ili iwe nini? Kwa vile nimemkosoa Msemakweli? Ndiyo nikojoe nikalale? Nikikojoa halafu nikalale wakati huo wewe ukiwa wapi? Come on man. Answer constrcuctively and stop acting like a fool man!!
   
 10. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ndugu Kibanga umekasirika kwa sababu nimetoa arguments za kisomi au? Narudia kusema I decided to challenge Msemakweli on his own ground. Yeye kaja na maelezo hayo akijifanya kuwa ni msomi ilihali katuletea umbea. Nimesema mimi nisichokubaliana naye siyo kuwa hao waheshimiwa ni wasomi fake au kinyume chake. Hapana. Mimi ninasema hoja zake hazina msingi wa kisomi. Ndugu Kibanga try to control your emotions by being objective. Kuandika hapa hata kama nigetakiwa kulipa ningelipa tu. Sema sasa la sivyo just shut up man!!
   
 11. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Ndugu Jambo1 ninaposema authenticity nina maana ya kuwa kila mheshimiwa ambaye amemtaja kuwa ana vyeti fake, yeye Msemakweli angechukua hatua ya ziada kuonyesha mawasiliano ya kimaandishi kutoka vyuo husika ambayo yanathibitisha madai ya Msemakweli. That is all. Ninajua baadhi yenu na huenda na wewe ni mmoja wa hao huwa mnasikia raha wakubwa wanapodhalilishwa kwa vile it gives you an ego massage. Si jambo zuri kwa sababu linaonyesha kuwa ndani ya jamii huna mbele wala nyuma but just a failure. Mtu yoyote ambaye ni mstaarabu hawezi kufurahishwa kuona mtu mwingine anavuliwa utu wake kihunihuni tu. Hapana jamani. Ni vizuri wanajamii wa JF mkaonesha kuwa nyinyi ni tofauti na watu amabo hawajaenda shule. Vipi wewe Jambo1? Use your brains man!!
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 0
  Acheni ku-demarket kazi za watu. Ninachokiona hapa ni roho ya kwa nini apate Tshs 267M. Mmmesahau kuwa msemakweli kasema watu. Kama hawa watu wanaona alichoandika ni uongo kwa kukosa reference basi waende mahakamani wakamdai fidia kwa kuchafuliwa jina. Wakiendelea kukaa kimya maana yake aliyoyasema msemakweli ni ya kweli kabisa pasi na shaka yoyote kwani kitabu chake kina nia ya kuondoa uozo uliopo.

  Nina hakika kuwa msemakweli kama mwanasheria ameisha jiandaa kutoa vielelezo vyote mahakamani kwa madai yake. Mnataka reference ya nini? ili mtafute strategy ya kumshinda?, Pelekeni kesi makamani halafu ndiyo mtajua kuwa aliyoyasema yana reference au hayana.

  HII THREAD IMEKAA KIKOROSHO SANA, IT DOESN'T INVITE GREAT THINKERS IDEAS AT ALL.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Marigwe huna lolote washauri waliokashfiwa waende mahakamani
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  huna lolote kama umelipwa vijisenti basi kanywee gongo
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Kama waliokashfiwa wanaona Msemakweli kawaonea si waende mahakamani? Kelele zako na wengine ni za nini au ndo ninyi mmebadili majina? Mnalo mwaka huu kuwa na PhD ya kweli si mchezo.
   
 16. mundele

  mundele Member

  #16
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  upuuzi mtupu,ukiona mtu amejitoa muhanga kiasi hicho basi ujue ushahidi anao,hakukuwa na sababu ya kuweka ushahidi kwenye kitabu hicho.kama ameweza kuwataja majina basi waliotajwa kama wataona wamedhalilishwa waende mahakamani full stop. eti "tunasikia raha wakubwa wanapodhalilishwa..."tuondolee ujinga na ufikirie hao wakubwa wamekudhalilisha kimaisha kwa miaka mingapi sasa...

  Big up msemakweli,ila i hope unalipa income tax kwakuwa nina uhakikia serikari inatafuta pa kukubania....
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,893
  Likes Received: 9,497
  Trophy Points: 280
  Mimi sijasoma kijitabu.

  Lakini jambo moja ni la msingi, na kama atakuwa ame li address atapata support yangu, na kama haja li address hapati support yangu, ingawa kuwa expose makajanja ni muhimu, lakini hatutaki kajanja mwingine akatumia kuwa expose makajanja kama deal ya kutokea.

  Swala gani hili ninalolisema kwamba ni muhimu sana?

  Naongelea bodi ya kutambua au kutotambua vyuo na shahada/stashahada zazo na vyeti vingine.Na jinsi gani tambuzi hizi zitakuwa enforced.

  Kama hakuongelea hili anapiga geresha tu, no matter how grave the situation is. Kwa sababu atakosa hata reference point ya kusema chuo gani ni valid na kipi si valid.
   
 18. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Katika democracy hulazimishwi kusoma kitabu chochote.
  Wale walioandikwa kama wanaona kuna kitu sio sahihi ,kuna mahakama !
  Hapa kuna watu wanakula na watu wenye Phd fake,naona hawakubali the fact
   
 19. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,658
  Likes Received: 727
  Trophy Points: 280
  Mmakonde nakupa senksi
  kinachoonekana hapa ni kundi la mafisadi wengine ambao labda nao wako katika mkondo huo huo wa kupata hizo fake Phds, sasa wanawashwa na Msemakweli.

  Kama hutaki usisome, na TUC imewashauri wapeleke vyeti vyao kujisafisha sasa tatizo liko wapi?, siwapeleke.

  Na mwisho kama hilo halitoshi ili wajisafishe zaidi waende mahakamani kumshitaki Msemakweli si kawachafua.

  Acheni udwanzi wa kuteteana hapa ni mafisadi na Msemakweli Big Up, huu ni mwanzo mzuri, with spelling mistakes or not... ujumbe umefika loud and clear!!!

  Wasalaam
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,893
  Likes Received: 9,497
  Trophy Points: 280
  Kama hajaongelea mzizi wa fitna nilioutaja hapo juu hana tofauti na post za JF tulizozitoa mara kibao hapa. Zaidi tofauti itakuwa yeye kachapisha kijarida tu.

  Mtu anapojitia usomi na kuandika kitabu tunategemea level fulani ya research, authentication na originality. Kama hajaleta kipya na yeye atakuwa kihiyo kama hao vihiyo anaowakandya.

  Na kum hold to a higher standard hakuna maana kwamba tunaunga mkono vihiyo wala tunafaidika na uzushi wao, wengine tuko nchi za watu mbali huku na tushakata links na uzushi uzushi wa kibongo, lakini tunajua kitu kinaitwa standards.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...