Msemakweli kasema ukweli kuhusu mafisadi wa elimu?

dr.mussa assad wa udsm aliwahi kuandika makala kwenye gazeti la sundays news kuelezea vihiyo hawa wa elimu.pia unaweza kujiridhia na kwa kumtafuta dr.mussa assad akakupa vielelezo kwani naye kafanya tafiti nyingi juu ya elimu za hao viongozi wetu.


Au tizama mjadala uko hapa jf wenye kichwa cha habari baadhi ya malecturer wa mzumbe wa phd feki including vc wao.

Kwa haya unataka tuelewe kuwa Msemakweli amerepublish kazi ya Dr Assad, je amemuaknowledge au kurecite article ya Assad kijaridani.
 
Mimi nimekisoma lakini kurasa chache za mwanzo.I expected more analysis na badala yake ni tuhuma zilezile tu tulizokuwa tumeshazisoma katika magazeti na hata hapa JF......Ninachoweza kusema ni kuwa:
1. Mwandishi kama amewakashifu walioorodheshwa kama mafisadi wa elimu basi asubiri demand note kama ishara ya kushtakiwa.
2. Waliorodheshwa humo wamepewa changamoto ya kuweka mambo bayana.
3. Taasisi husika ziwasaidie watanzania pale inapoonekana wanataka kuingia mkenge.Tanzania kuna tatizo moja na siyo kwenye hili la vyeti tu.Kila inapotokea kuwa mtu au watu wanafanya kitu kinyume, taasisi husika hukaa kimya na kuangalia bila kuchukua hatua yoyote hadi mtu anapopoteza nguvu nyingi sana na kukamilisha kitu ndipo utasikia kuwa HAPANA HUKUPASWA KUFANYA JAMBO FULANI..NI KINYUME NA TARATIBU AU SHERIA.( Angalieni hata watu wanavyojenga nyumba inakaribia kuisha ndipo utaona mamlaka husika zikija na kuandika kwa rangi nyekundu BOMOA! STOP ORDER NO XYZ /2010! sijui siku zote wanakuwa wapi!)
 
MAFISADI WA ELIMU

Jana nilikinunua kijarida kilichoandikwa na Ndugu Msemakweli ambacho kina orodha ya majina baadhi ya Waheshimiwa Mawaziri, Wakuu wa Mkoa na Wabunge ambao inadaiwa wana vyeti ambavyo Msemakweli anaviita feki. Kijarida hicho kinauzwa shs 3,000.

Baada ya kukisoma kile kijarida ninayo maoni yafuatayo:

1. Nampongeza Ndugu Msemakweli kwa kuwa mjanja wa kubuni njia ya kupata fedha kiurahisi. Yeye mwenyewe anakiita kitabu. Namshangaa kwa sababu kwa mtu aliyesoma kama yeye tena sheria iweje anashindwa kupambanua kati ya kijarida na kitabu. Katika ulimwengu wa kisomi kitabu ili kiwe kitabu kinapaswa kuwa na majina ya publishers na references nyingine muhimu kama vile year of publication; bibliography na kadhalika. Hicho kitabu hakina ndiyo maana mimi nakiita kijarida.

Alichofanya Ndugu Msemakweli ni kukaa kwenye laptop yake au keyboard yake na kuandika hayo aliyoyaandika na kuprint na kukiingiza sokoni. Katengeneza nakala 89000 ukizidisha mara shs 3000 atazipata takribani shs 267 milioni!! Hizo fedha anazipata kwa njia ya kuwakashifu waheshimiwa hao. Huu ni ujanja kweli kweli. Naye kwa vile alitangaza ni mwanachama wa CHADEMA hiyo hela itamsaidia wakati wa uchaguzi. He is very smart in a country of fools as it were. Na kwa sababu sisi watanzania tunapenda sana habari za umbea kwa upumbavu tulionao tutanunua tu hicho kijarida na yeye atapata hizo pesa bila ya jasho.

2. Maelezo aliyoyatoa ya kila mheshimiwa utaona yana mapungufu katika authentication. Alichopaswa kufanya kwa kila mmoja wao ni kutoa ushahidi wa maadishi kutoka vyuo husika vikikiri kuwa hivyo vyeti havikutoka kwenye vyuo vyao na kwamba hao waheshimiwa hivyo vyuo hawakuwahi kuwa wanafunzi wao. Hilo hakufanya. Na kwa njia hii Msemakweli kama msomi kajitia doa na mimi usomi wake pia nautilia mashaka. Yeye alichofanya ni kumponda Rais Kikwete kuwa naye ameshiriki kuwabeba hao waheshimiwa. Jambo ambalo ni upuuzi. Katiba ya Tanzania haisemi kuwa Rais atateua mawaziri kufuatana na degree au diploma zao. Katiba inasema Rais atamteua mtu ambaye ni mbunge kuwa Waziri. Sasa hizo lawama dhidi ya Rais hazina mantiki hata kidogo.

3. Picha inayojitokeza ni Msemakweli kiu yake kubwa ilikuwa ni kumcharaza Rais Kikwete. Usomapo hizo tuhuma zake kama vile safari za Rais nje ya nchi mimi naona hazina hoja hata kidogo. Hivi huyu Kikwete ambaye analaumiwa kwa kila kitu afanyacho ambacho kinatokana na wadhifa wake kama Rais hivi kweli tunamtendea haki? Mwacheni Kikwete afanye kazi zake za Kirais.

4. Kijarida cha Msemakweli ni majungu ambayo yamejaa fitina na chuki tu. Naomba mnielewe. Mimi sijasema kuwa hao Waheshimiwa wana vyeti halali au vya kughushi. Mimi niachosema ni kuwa maelezo ya Msemakweli hayawezi kukubalika kirahisi bila ya kuwa authenticated scientifically. Na huo ndiyo usomi. Msemakweli anadai kuwa waheshimiwa hao ni mafisadi wa elimu na yeye je? Kundi lake ni lipi. Anajiita mwanasheria. Hivi mwanasheria utafanya madai bila ya kuyathibitisha na vielelezo?

No. Come on ndugu Msemakweli fanya mambo kisomi . Mimi ningekuwa naisahihisha hiyo thesis yako ningekupa D kwa sababu ya muda ulioupoteza kuandika hayo uliyoandika.

Kwa taarifa yako diallo alimfungukia kesi,na huyo mswmakweli alienda kuomba kesi imalizwe out of court na alimuomba radhi diallo,maana diallo aliwasilisha uthibitisho kutoka hivyo vyuo alivyosoma

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom