Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Nimeota ndoto, iko hivi.
Mbele kuna mtu yuko mbele ya kichaka kinene na giza, akawa anajiuliza, je kuna nini ndani ya hiki kichaka? Kisha akaamua kuokota jiwe na kulirusha kwenye kile kichaka. Hakujuwa, na wala hakutaka kujuwa nini kitatokea. Lakini ukweli ni kuwa moja katika mambo matatu yafuatayo linaweza kujitokeza:

1.ama hakutakuwa na kitu kitakachotokea kwa sababu ya utupu uliomo ndani ya kichaka hicho chenye giza nene.
2.ama atajitokeza sungura mnyama, nawe waweza kumwacha aende zake, au kumfukuza na ukimkamata utakuwa umepata kitoweo siku hiyo, na
3. ama litaibuka joka kubwa likakuzinga mwilini na kukubana mbavu hadi zikavunjika vunjika na kukumeza.

Yule mtu aliendelea kurusha mawe bila tukio lolote, inawezekana ni kwasababu yule mnyama atakauwa amelala kwa uchovu, au ni kwasababu anavumilia tu akijua huyu ni mpitaji tu ataondoka na kuendelea na safari yake.

Uwezekano wa kuzongwa na hilo joka, unazidi kuwa dhahiri kadiri yule mtu anavyoendelea kurusha mawe, je ni nani shujaa atakayetoa maisha yake ili kumwokoa huyo mtu mchokozi pindi atakapokuwa kinywani mwa lile joka lenye hasira, macho mekundu na njaa? Kuna uwezekano mkubwa kwa marafiki wote wanaoendelea kumchochea na kumsifu kuwa hatadhurika kwa kuwa ana mbio nyingi na anaweza kupiga mbio kali na kujiepusha na hatari yeyote, watakimbia na kumwacha peke yake, au wataliwa pamoja naye! Mbio kali, uchokozi, sifa za maswahiba, kurudia uchokozi, ni dalili ya mtu atakayeishia mdomoni mwa joka na maswahiba watakimbia na kupotea....ama kuliwa pamoja naye. Je nini maana ya ndoto yangu hii niliyoota?
 
Invisible si vyema kupotosha umma, hakuna aliyekamatwa na polisi. Au Msemakweli kwa habari alizotowa hafai kuisaidia polisi katika uchunguzi?
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
wee mwanamke! kwani yeye alikuwa na shida na polisi! au kama ana shida nao havioni vituo vya police? amekwenda kwa Manumba kwa issue zake. police yanawahusu nini! umebaki kuisaidia police, kuisaidia police! unatumia nini kufikiri? masaburii
 
Hivi hawa wanaotetea upumbavu unaoitwa ufisadi ndo walewale wanaofikiria kwa kutumia mas ab uri nini....zao
 
There are currently 491 users browsing this thread. (140 members and 351 guests)

JF Kiboko! Sijui watu wa print media wataandika nini, kufikia kesho hii sio mya tena!
 
Taarifa zilizotufikia wakati huu ni kuwa yule jamaa 'aliyewalipua' Rostam, Manji na wenzao jana; kakamatwa na Polisi toka ofisi ya DCI (Manumba) na anaendelea kuhojiwa.

Taarifa zinadai kuwa Msemakweli alielekea kwa DPP kama alivyoahidi hiyo jana kuwa angeenda kwake na kuambiwa kuwa appointment yake imesogezwa mpaka Jumatatu lakini akiwa njiani kurudi akakamatwa na maofisa wa polisi ambao mpaka sasa wanaendelea kumhoji.

Hatujapata taarifa za nini amehojiwa na nani kamhoji. Tutaendelea kufahamishana kadiri muda utakavyoruhusu.

Huu ni mwanzo tu, kuna mengine yatajiri muda si mrefu!

KUMBUKA KAULI YAKE:


UPDATES:

Maelezo mapya:

Msemakweli alikamatiwa ofisini kwa DPP. DCI Manumba alienda kwa DPP asubuhi akiwa na timu yake kisha Msemakweli alipofika na kuambiwa arudi Jumatatu akawakuta nje ya ofisi wakiwa wanamsubiria, akachukuliwa na kwenda naye Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani kwa DCI kabla ya kumchukua kwenda naye Mikocheni zilipokuwa ofisi za tume ya EPA.

Update 1:

Update 2:

Msemakweli yupo huru kuongea na simu lakini si kama kaachiwa, mida hii (02:00PM) anaelekea kuandika maelezo.

Update 3:

Hii ni dhahiri kabisa Fisadi papa anaweweseka na vikuwadi vyake alivyovituma hapa JF. Msemakweli anawakilisha mamillioni ya umma wa Watanzania walipa kodi wa nchi hii ki mawazo, kama wanafikiri Msemakweli atanywea au Watanzania watanywea imekula kwao.
 
kweli hawa wahindi wameiweka serikali ya JK mikononi mwao..ingekuwa enzi za mwl yani hawa wahindi wangerudishwa kwao India..
 
Wahenga walinena "MSEMAKWELI NI MPENZI WA MUNGU", kwa ushahidi ule ulioshuhudiwa na taifa na mataifa, wanaoleta mizengwe (DPP na DCI) wamechelewa. Wasipofunuliwa, tiketi zao kwenda The Hague zinatayarishwa.
 
Polisi wako sahihi kabisa katika hili: Wamedhihirisha wazi kabisa kwamba hawako kwa ajili ya raia bali wao kazi ya ya msingi ni KUWALINDA WAKUBWA mambo yao yasiwaendee vibaya.

Mpaka hapa ni wazi kwamba ROSTAM AZIZ bado ndiye bosi mkuu nchini pamoja na kule 'kujibadilishia kiti' kwa jina la kuvua Gamba kama ilivyodaiwa.

duh! inadhihirika sasa kuwa serikali hii yote ni corrupt! yaani mtu anatoa taarifa za watu wanaohujumu uchumi wetu badala ya polisi kumlinda wao wanamtafuta wakamhoji? aisee!
 
Invisible si vyema kupotosha umma, hakuna aliyekamatwa na polisi. Au Msemakweli kwa habari alizotowa hafai kuisaidia polisi katika uchunguzi?
Kizazi cha aina yako kikipotea tutakuwa tumejikomboa.............
 
kweli hawa wahindi wameiweka serikali ya JK mikononi mwao..ingekuwa enzi za mwl yani hawa wahindi wangerudishwa kwao India..
Way forward sasa baada ya Msemakweli kufunguka. Tuseme waziwazi kuwa tumewachoka kuwekwa mifukoni mwa mafisadi. Hapa ndipo penye subira tuliyoingoja kwa wakati mrefu. Siyo Igunga, bali kwa huyu aliyejitoa sadaka kwa ajili ya taifa hili.

Tunatoa angalizo kwa vyombo vya usalama kuwa sasa ni wakati wa utaifa na si maslahi binafsi
 
polisi si wapo kwa maslahi ya mafsadi jamani
nashindwa kuwatofautisha na mbwa koko
ye ni kiumbe wa kuendeshwa tu
polisi wetu nao!!!!!
 
Itakua mahojiano tu ya kawaida,watamuachia na kuwasilisha ushahidi wake DPP! Nasikia Chadema wamemkasilikia sana Msemakweli kuwa amepola hoja yao ya Kagoda!
Umesikia wapi kiongozi??tunaomba source ili tusije tukarukia band wagon ambayo hatujui wimbo uimbwao unamaana gani!!!
 
Nasema ya kagoda mbona dogo sana, lipo kubwa linaloigusa ikulu moja kwa moja na linakuja niliahidi kuleta hapa nikishajiridhisha!!

Usilete hapa.
peleka kwenye tv station halafu siku ya pili yake peleka kwa DPP.
 
kweli hawa wahindi wameiweka serikali ya JK mikononi mwao..ingekuwa enzi za mwl yani hawa wahindi wangerudishwa kwao India..

Suala la serikali ya JK kuwa mfukoni mwa wahindi liko wazi sana, na bahati mbaya sana JK mwenyewe anawaogopa wahindi kama mungu wake hawezi kuthubutu hata kuwagusa. Na wao kwa jeuri ile ile wanazidi kutudhihirishia kila siku kwamba serikali hii ya JK ni yao, sisi hatuna chetu.

Sasa utashangaa mzalendo aliyejitolea kuisaidia serikali kuwajua wezi wetu, wanaanza kumsumbua na kumgasi.
 
Nadhani sasa Watanzania hasa tulio hapa Dar, tupange namna ya kumsaidia Msemakweli kama hawa watu watataka alale mahabusu kwa sababu zozote watakazo zitoa, mimi naufuatilia kwa karibu sana huu mchakato. So far naamini wanachukua maelezo kutoka kwa msema kweli ili wayafanyie kazi na si kum-embarrass
 
Kama sikosei si huyu aliyetajaga Mafisadi wa Elimu na wakatishia kwenda mahakamani hadi leo hakuna aliyekwenda na CCM inazidi kuwatunuku vyeo zaidi kwa degree zao feki?

Pigana kaka Tz iko nyuma yako, fanya kama yule mwanaharakati wa India

Na wewe uko nchi gani.
Au unasubir wenzio wapambane halafu wewe uje usherehekee matunda. Jisikie aibu.
 
Msemakweli ni watanzania wachache wanaweza kuwa jasiri hivo. Umeonyesha uzalendo wa hali ya juu. Tatizo la watanganyika tulio wengi ni "bora liende". Waibe sawa! wapandishe bei poa! Cjui wapi tulipotea njia na cmjui aliyetupotezea huku.

Kuna kitu gani uliwahi kukifanya kwa ajili ya wanyonge walio wengi?
 
Back
Top Bottom