Msemaji wa Simba SC Haji Manara Siku zingine uache Kiherehere cha Kumsifia Mchezaji Mnafiki wa Azam FC Aboubakary Salum 'Sure Boy' mwenye Uyanga mno!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,034
Nilikushangaa sana Wiki hii nzima nilipokuwa kila nikipitia Kurasa zako za Mitandaoni na ukawa unamsifia kwa Mikogo yote huku ukimpamba mno Mchezaji wa Kiungo wa Azam FC Aboubakary Salum 'Sure Boy' tena ukimtia Ndimu kabisa ( ukimchochea ) kuwa katika Mechi ya Leo dhidi ya Yanga SC apambane na aichezeshe Timu yake kwa uwezo wake wote ili Azam FC ishinde.

Binafsi ( GENTAMYCINE ) kama kuna Mchezaji ambaye Simpendi na hata huwa sitaki Kuonana nae njiani ni haka Kapuuzi na Kanafiki Aboubakary Salum 'Sure Boy' kwani ni Mchezaji ambaye Kwanza hafichi kabisa Mahaba yake niue ( makubwa ) kwa Klabu ya Yanga ambayo Kwao wote ukianzia na Baba yake Mzazi Mzee 'Sure Boy' Senior nae ni Shabiki Bandika Bandua wa Yanga SC.

Miaka mitano nyuma nakumbuka niliwahi Kugombana nae wakati tukishuka ngazi za VIP baada ya Kumsema wazi wazi kuwa amezidisha Mahaba yake kwa Yanga SC na kama anaipenda sana basi ahamie huko tujue moja ambako nakumbuka nae alinijibu hovyo na tukataka Kuzichapa Kimtindo ila nashukuru akina Mzee Makoye na Marehemu Mzee Juma Mnonji walituamulia.

Msemaji wangu wa Simba SC Haji Manara labda usichokijua tu ni kwamba rejea kutizama Mechi zote ambazo Azam FC inacheza na Yanga SC halafu haka Kapuuzi Aboubakary Salum 'Sure Boy' kapo ni lazima tu Yanga SC itashinda. Anachokifanya huyu Mchezaji na hata Leo amekirudia kile kile ni Kuua kwa Makusudi 'move' za Mashambulizi ya Azam FC ili wasiifunge Yanga SC.

Nakumbuka kuna Siku tukiwa tumekaa pale uwanja wa Uhuru jirani kabisa na Baa ya kwa Chichi nikiwa na Bandeko Nangai (Muha wa Kigoma), Rafiki na Mtani wangu Kocha Suleiman Matola alitokea aliyekuwa Kocha wao Idi Cheche na nikamwambia Madhaifu ya huyu Mchezaji hasa ikicheza na Yanga SC na kuahidi Kulishughulikia ila cha Kushangaza bado wala hakajabadilika.

Leo kila mara akipata tu Mipira alichokuwa akifanya ni Kuzunguka tu katika Kiungo, Kutoa Pasi nyingi za Lawama, Kuharibu Pasi lakini kubwa zaidi alikuwa akizitafuta sana Kadi na hasa hasa Nyekundu ili mradi tu akipewa Timu yake ya Azam FC iwe pungufu, idhoofike na Timu yake pendwa aliyorithishwa na Baba yake Mzazi 'Sure Boy' Senior ya Yanga SC iibuke na Ushindi.

Haji Manara (Msemaji wangu wa Simba SC) baada ya Kumpamba sana haka Kapuuzi Aboubakary Salum 'Sure Boy' ili akichafue leo walipokuwa wakicheza na Yanga SC na hakufanya lolote hebu nakuomba mtizame katika Mechi yetu (Simba SC) na Wao Azam FC kwani huwa anacheza kwa Kuhaha Uwanja mzima, anatoa Pasi za uhakika, hapotezi muda na anakimbia kila eneo utadhani kawekewa Mota matakoni (makalioni) mwake.

Hata hivyo nitasema yote hapa ila nisiwe Mnafiki na Mchoyo wa Kuipongeza kuikweli Yanga SC wako vyema, wanapambana na walistahili Ushindi.
 
Hii Nnji ina vituko kweliiiiiio!!!! Yaani muziki apigiwe Azam tena Chumbani, halafu mauno anakata Simba tena akiwa mtaa mwingine ugenini. Jamani mtakufa na vijiba vya moyo nyie kinguni wa Mwamedi.
 
Back
Top Bottom