Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa umeshamwambia Boss wako Rais Samia kuwa Bure yake iliyoleta Fujo jana Yanga SC na Tanzania zitapewa Adhabu Kali?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,119
Sifa zenu (yake) ya kutaka Kupendwa na wanamichezo (hasa Mashabiki wa Mpira wa Yanga na Simba) nchini Tanzania kwa kuwapa Pesa na Kununua Tiketi ili waingie bure Uwanjani huku mkiwalazimisha waingie na Mabango yenye Picha yake Rais Samia na Chams Cha Mapinduzi (CCM) inaenda kuwatokeeni puani.

Taarifa ikufikie popote ulipo Mwanamichezo, Rais Samia na Mr. Kiherehere na Unafiki Gerson Msigwa (Msemaji wa Serikali) kuwa Kitendo cha Kihuni na cha Kishamba kisichovumilika na Wapenda Soka Wastaarabu (GENTAMYCINE nikiwemo) kilichofanywa Jana Uwanja wa Mkapa na Mashabiki wa Yanga SC cha Kuvunja Mageti, kufanya Fujo na kusababisha Kifo na Majeruhi kadhaa kimeiweka Hatarini Klabu ya Yanga kukumbwa na Adhabu Kali kutoka CAF lakini pia nchi ya Tanzania Kufungiwa Kushiriki Michuano ya Kimataifa na Uwanja wa Mkapa Kufungiwa kwa muda usiojulikana.

Haya GENTAMYCINE nawaombeni endapo CAF watatoa hizi Adhabu tulizojitakia kwa Sifa zetu za Umaarufu wa Kisiasa na Kuibeba Klabu Moja kwakuwa ina Vinasaba na Chama Tawala cha CCM mkikata Rufaa huko CAS nashauri mkipeleka Viambatanisho msisahau na kubeba Mabango yenye Picha za Rais Samia na ya CCM (Chama Cha Mapinduzi) tunayoyaona Kutwa Uwanja wa Mkapa ili vitusaidie Kushinda Kesi na Yanga SC pamoja na Tanzania kutofungiwa.

Binafsi Adhabu zikitolewa kwa Yanga SC na Tanzania kama nchi nitafurahi sana kwani tulishashauri (na nimeandika mno hapa JamiiForums) kumtaka Rais Samia asiendelee na huu Utaratibu kwani umekaa Kisiasa zaidi na siyo kwa Lengo la Kuendeleza Michezo nchini Tanzania sikueleweka ila naamini kama likitokea la kutokea ndipo mtakubaliana nami kuwa Mimi ni Nabii nisiyeimbwa hapa JamiiForums na Tanzania na kwamba sijawahi Kutahadharisha Jambo halafu lisije Kutokea ama kwa muda huo huo au baadae.

Chanzo cha Taarifa ya Tanzania na Klabu ya Yanga Hatarini Kufungiwa na CAF kwa Makosa ya Jana ( Fujo na Uharibifu mkubwa wa Miundombinu ya Uwanja wa Mkapa ) ni Kipindi cha Michezo cha Spoti Leo Usiku huu wa leo.
 
Sifa zenu ( yake ) ya kutaka Kupendwa na wanamichezo ( hasa Mashabiki wa Mpira wa Yanga na Simba ) nchini Tanzania kwa kuwapa Pesa na Kununua Tiketi ili waingie bure Uwanjani huku mkiwalazimisha waingie na Mabango yenye Picha yake ufungiwa na CAF kwa Makosa ya Jana ( Fujo na Uharibifu mkubwa wa Miundombinu ya Uwanja wa Mkapa ) ni Kipindi cha Michezo cha Spoti Leo Usiku huu wa leo.
Kolo katika ubora wako ,mtafute na mgunda aje akusaidie kuandika


USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom