Msemaji wa JWTZ usifanye jukumu hilo kama mwanasiasa

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,348
4,807
Miaka ya nyuma hili jeshi ilikuwa ni nadra sana kusikia wanatoa matamko kwenye vyombo vya habari, na ikitokea kutoa taarifa basi itakuwa ni taarifa ambayo ni nzito sana na kila mwanachi anakuwa na shauku ya kuisikia.

Pia walikuwa wakitoa taarifa au tamko basi ni mara moja na hutaona wakirudia tena au kukuta wanaonekana kwenye majadiliana katika vipindi vya TV kama ilivyofanyika juzi juzi kwenye tamko la kusaka nguo za jeshi ambapo kwa muda mfupi tunaona jinsi Afisa habari wa jeshi ametoa matamko ya hoja hiyo kila mara, pia haikuishia hapo bali amekuwa akionekana kwenye vipindi vya TV na radio kama vile clouds nk.

Wakubwa wa jeshini ni vema kukiangalia kitengo hiki ili kiendane na hadhi ya jeshi letu. Angalia hata juzi akatoa taarifa iliyoibua maswali mengi aliposema wananchi waingie Google wataona kuwa jeshi letu ni miongoni mwa majeshi SITA bora duniani kiutaalam, weledi na zana.

Halafu ni vema taasisi kubwa kama hiyo ikawa na mtu mzima kiumri na aliyepevuka vizuri zaidi.

Nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa ni jeshi la polisi lilikuwa linatoa matamko ya kuwasaka wanaovaa nguo za kijeshi kinyume na sheria za nchi, sasa leo kweli ndio tunaona jeshi linatoa matamko kwa hizi nguo raia wanazochukuwa mitumbani.

On my opinion I see it as a very very and very MINOR issue, it should have been done by Police na kama kuna haja sana kutolewa na jeshi basi angalau iwe tamko moja tu.

Na hata ile ya kuwapeleka wanajeshe kariakoo kwenye mitumba kutafuta hizo nguo, jamani jamani jamani mbona kama mnalishushia hadhi jeshi letu kiasi hiki, tunachoelewa ni kwamba jeshi ndani ya nchi huingia kazini pale vyombo vyingine vinaposhindwa, sasa kweli hii ya kutafuta nguo za mitumba!!!!!!!!!!!

Na huenda haya yanayofanyika huwa yanafanyika kwa maelekezo ya viongozi wa kati maana siamini kama Mkuu wa majeshi anayafahamu kabla

Tusiwasononeshe makamanda wetu wastaafu ambao hawakuyaacha haya.
 
Jamaa ana mikwara hatari sana yule.

Eti tunachukua sare tunakupa na chai
 
Nakumbuka miaka ya nyuma ilikuwa ni jeshi la polisi lilikuwa linatoa matamko ya kuwasaka wanaovaa nguo za kijeshi kinyume na sheria za nchi, sasa leo kweli ndio tunaona jeshi linatoa matamko kwa hizi nguo wanazochukuwa mitumbani.
Ulidhani issue ni nguo za Jeshi? Jaribu kuwaza Kwa mapana na marefu! Ni Zaidi ya hayo, lile vuguvugu la west linawatisha! Kwahio hawa ambao ni Pro inabidi kiwatisha...kuonyesha presence yao
 
Kuna Raia wanasema hawa wameongezewa shekeliiiiii baada ya sakata la bandari,lakini hata polisi ,Sasa dalili ya awali kabisa ambayo tunaiona Kwa jeshi hili limevamiwa na mdudu CCM ,maana wenzao kule magharibi wameapa kulinda rasilimali zao Sasa hawa naona hawafuati sheria zao na hawaelewi hizo sheria zinatumikaje ndio Kwa kujihami wanakuja na maneno ya kwenye kanga ohooo,uhhhu,ohhhh kifupi kama humu mnasoma mumeingia kwenye kikundi cha watu 23
 
Mambo ambayo yanajadiliwa na uhalisia ni vitu vingine kabisa ndani ya Muundo na utawala. Ops ni nyingine kabisa
 
Pls jeshi langu Linda mipaka ya nchi yangu, ndio kiapo chako, sasa zimekuwa ni porous borders, kukimbizana mitaani na raia ni kulidhalilisha jeshi
 
Hana tofauti na wakina manara kitenge mandonga huyo
Kik kik nyingi .....mara kawaita wasani

Ova
 
Back
Top Bottom