Ukimya wa Vyombo vya Usalama juu ya Sakata la Bandari

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Leo ni kumbukumbu ya ni 911, fumbo la ghorofa pacha la world trade center ambalo halipo tena.

Mgawanyo wa madaraka na majukumu

TISS kufuatilia usalama wa nchi/taifa, viashiria, mipango, wahusika, wafadhili, na hata utekelezaji wa jambo lolote baya linalohusika na taifa katika ujumla wake bila kuwasahau viongozi.

JWTZ, Jeshi la wananchi wenye nchi - Jukumu kubwa ni kulinda mipaka ya nchi/Taifa isiingiliwe na maadui, pia kwenda vitani inapohitajika nk.

Jeshi la Polisi Tanzania - Kulinda usalama wa raia na mali zake pamoja na majukumu mengine yote yanayohusika na usalama wa wananchi na mali zao.

Majeshi mengine yote ni wasaidizi tu toka hayo hapo juu.

Tumekuwa na kipindi kama cha mpito tangu sakata la bandari lilipoanza zaidi ya miezi mitatu sasa. Mambo yamekuwa mengi mno kulihusu mema na mabaya.

Ni ngumu kuwalaumu TISS kwakuwa hawa huwa hawaendi front, na kwa mtazamo wa kawaida unaweza kudhani hawajafanya kitu, lakini pengine kwenye hili sakata wanapaswa kushukuriwa pakubwa sana!

Linapokuja suala la mipaka ya nchi, kwa maana ya anga, nchi kavu na majini, mhusika mkuu ni JWTZ kwa msaada wa TISS. Suala la bandari ni mojawapo ya maingilio ya nchi kutoka mipaka ya majini.

Utendaji wa JWTZ ni tofauti sana na Jeshi la polisi. JWTZ sio watu wa matamko wala press conferences kwakuwa hawadili na wananchi moja kwa moja na ndio maana unaposikia Jeshi linataka kutoa tamko ama linataka kuongea na waandishi wa habari, tashwishwi huwa kubwa.

Matamko ya kutaka wananchi wasivae nguo zinazofanana na za kwao, matamko ya kutaka kuingia mitaani kusaka nguo/sare zinazofanana na za kwao, matukio yanayosambazwa mitandaoni wanajeshi wakiwaadhibu wananchi wanaokutwa na nguo zinazofanana fanana na zao, naomba niseme sio level za Jeshi letu ni kukiuka katiba na kuingilia majukumu ya wengine!

Kama tunaweza kuipongeza TISS kwenye sakata hili la bandari, basi sasa macho na masikio ya wananchi yana tashwishwi ya kusikia neno toka kwa mhusika mkuu wa mipaka na malango ya taifa. Matamko ya sare sio case sensitive kama ishu ya mipaka.

Kama KITI kimeamua kukaa kimya. Inaweza kuwa ni hasara kubwa yenye faida kwa wengine kama nalo likisema. Funika kombe mwanaharamu apite.

d93307cfa96595166a2f05d5ab5c64cb.jpg
 
Kwani wamesha maliza kukusanya mitumba 🤔🤔 nilishangaa Sana walivyo toa tamko la kutafuta mitumba inayo fanania na nguo zao, hatujakaa sawa mwingine akakurupuka huko eti "jeshi letu ni namba 6 kwa ubora duniani" hapo ndio nikabaki mdomo wazi kabisa.

Hivi vitu vya hovyo wameanza kufanya vina wavunjia heshima waliyo kua nayo kwa wananchi, tumeanza kuwachukulia poa kabisa.
 
Kumbukizi Leo ni 911.. Fumbo la ghorofa pacha la world trade center.. Ambalo halipo tena..!!!

Mgawanyo wa madaraka na majukumu
TISS kufuatilia usalama wa nchi/taifa.. Viashiria, mipango, wahusika, wafadhili, na hata utekelezaji wa jambo lolote baya linalohusika na taifa katika ujumla wake bila kuwasahau viongozi.
hapo JWTZ apo ndio umenikosha.
Japo wanawajibika 24/7 kwa raia namba moja, na actualy huyo ndie anapaswa kutujuza kama Taifa kua tuko salama kiasi gani au la baada ya kupokea tarifa kutoka kwao, na kwakweli amefanya hivyo mara chachechache nikimskia.

apo kwenye kuingia mtaani na eti kupekua sare za jeshi kwenye manyumba ya raia, pana tia kinyaa na kichefuchefu.
mbaya zaidi kwenye kuwatesa na kuwadhalilisha raia waliobainika kua na hizo sare, panaamsha hasira kali mno ya jamii dhidi yao.

na ndio maana saa zingine baadhi ya raia hususani waliopitia madhila yao wanafurahiaga hawa jamaa wanapota ajali au kufariki, japo si ungwana pia.

saa zingine huwa najiuliza huko missions DRC si wawe wanaenda na ujasiri na ukatili kama huu wanaowafanyia hawa raia wanaowakuta na sare zao? au ndo ile jogoo wa shamba.

pamoja na udhaifu huo.
Bado nalipongeza sana kwa weledi ktk utendaji wake ktk maeneo mengine. zaidi sana kuwa watulivu na kuwajibika ipasavyo kwa raia namoja amabae ni kiongozi wetu tunae mpenda na ni wa maana sana.

hayo mapungufu machache wanayoyafanyaga dhidi ya raia, yanaharibu sifa na weledi wao uliyotukuka na kuipaint taasisi hiyo nyeti vibaya kwa jamii.

Mungu Ibariki Tanzania.....
 
MSHANA naamini una uwezo mkubwa sana wakuchambua mambo,, hii thread ungeipotezea tu ipo kisiasa zaidi.
anauwezo mkubwa kuchambua mambo, halafu unamshauri au kumshawishi aachene na hili jambo:rolleyes: ?
nafsi itamsuta. siyo mchoyo mtu huyu.

mwenye uwezo mkubwa maana yake ni mtaaluma huyo, haachi kushirikisha jamii anachodhani ni vema watu kukijua, whether unakipenda au unakichukia, whether ni siasa, uchumi, technolojia au vinginevyo.

kumdibiti ni vigumu japo inawezekana akiwa na njaa :p
 
kumdibiti ni vigumu japo inawezekana akiwa na njaa
20230911_071306.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama KITI kimeamua kukaa kimya.. Inaweza kuwa ni hasara kubwa yenye faida kwa wengine kama nalo likisema.... Funika kombe mwanaharamu apite...
Mshana una uandishi wa kifasihi wenye maana nyingi tofauti kutegemeana na upande aliosimama msomaji. Uandishi wa namna hii hudumu!

Kuhusu JWTZ, hili jeshi lilikuwa na heshima sana kipindi cha nyuma na lilipendwa na kuheshimiwa sana na wananchi wakati na baada ya vita ya Uganda.
Heshima hii ilianza kuporomoka baada tu ya wajeshi kuanza kuingizwa kwenye vyeo vya kisiasa.

Ukiangalia utendaji wa hili jeshi kwa sasa ni kama viongozi wanatoa matamko ili kuweka kumbukumbu kwa wanasiasa wakitarajia kuteuliwa kwenye nafasi za kisiasa.

Heshima ya Jeshi letu irudi.
.
 
hakuna jeshi hapo, jeshi lolote Duniani nidhamu ni kitu cha kwanza kabisa sasa jeshi lisilo na nidhamu haliwezi kushinda vita yoyote na ndiyo maana wanageukia defense less people kuwaonyesha umwamba feki kama wanataka kuonyesha umwamba waende wakapambane na Wanajeshi wenzao rwanda au Kongo huko au Somalia.
tanzania tuko incompetent kwenye kila kitu isitoshe jeshi lolote Duniani linahitaji moral support ktk kwa wananchi sasa ni wananchi gani watawasapoti siku mkitumwa vitani kama mnawatesa kama wanyama?

ukiona nchi jeshi linatesa wananchi wake wenyewe ujue hapo hakuna nchi bali ni uharamia tu …
 
Kumbukizi Leo ni 911.. Fumbo la ghorofa pacha la world trade center.. Ambalo halipo tena..!!!

Mgawanyo wa madaraka na majukumu
TISS kufuatilia usalama wa nchi/taifa.. Viashiria, mipango, wahusika, wafadhili, na hata utekelezaji wa jambo lolote baya linalohusika na taifa katika ujumla wake bila kuwasahau viongozi.

JWTZ Jeshi la wananchi wenye nchi.. Jukumu kubwa kulinda mipaka ya nchi/Taifa isiingiliwe na maadui nknk.. Lakini pia kwenda vitani inapohitajika nknk

JESHI LA POLISI TANZANIA kulinda usalama wa raia na mali zake pamoja na majukumu mengine yote yanayohusika na usalama wa wananchi na mali zao

Majeshi mengine yote ni wasaidizi tu toka hayo hapo juu..!
Tumekuwa na kipindi kama cha mpito tangu sakata la bandari lilipoanza zaidi ya miezi mitatu sasa. Mambo yamekuwa mengi mno kulihusu mema na mabaya

Ni ngumu kuwalaumu TISS kwakuwa hawa huwa hawaendi front.. Na kwa mtazamo wa kawaida unaweza kudhani hawajafanya kitu.. Lakini pengine kwenye hili sakata wanapaswa kushukuriwa pakubwa sana!

Linapokuja suala la mipaka ya nchi, Kwa maana ya anga, nchi kavu na majini.. Mhusika mkuu ni JWTZ kwa msaada wa TISS..Suala la bandari ni mojawapo ya maingilio ya nchi kutoka mipaka ya majini

Utendaji wa JWTZ ni tofauti sana na Jeshi la polisi.. JWTZ sio watu wa matamko wala press conferences kwakuwa hawadili na wananchi moja kwa moja.. Na ndio maana unaposikia Jeshi linataka kutoa tamko ama linataka kuongea na waandishi wa habari, tashwishwi huwa kubwa..

Matamko ya kutaka wananchi wasivae nguo zinazofanana na za kwao, matamko ya kutaka kuingia mitaani kusaka nguo/sare zinazofanana na za kwao.. Matukio yanayosambazwa mitandaoni wanajeshi wakiwaadhibu wananchi wanaokutwa na nguo zinazofanana fanana na zao.. Naomba niseme SIO LEVEL ZA JESHI LETU na ni kukiuka katiba na kuingilia majukumu ya wengine!

Kama tunaweza kuipongeza TISS kwenye sakata hili la bandari, basi sasa macho na masikio ya wananchi yana tashwishwi ya kusikia neno toka kwa mhusika mkuu wa mipaka na malango ya taifa
Matamko ya sare sio case sensitive kama ishu ya mipaka!
Kama KITI kimeamua kukaa kimya.. Inaweza kuwa ni hasara kubwa yenye faida kwa wengine kama nalo likisema.... Funika kombe mwanaharamu apite...

View attachment 2745533

Sent using Jamii Forums mobile app

Kaka Mkubwa, nakupongeza kwa kuwa positive na matumaini na hii nchi, Mimi nilishapoteza, hakuna nachokitegemea.
 
Mshana una uandishi wa kifasihi wenye maana nyingi tofauti kutegemeana na upande aliosimama msomaji. Uandishi wa namna hii hudumu!

Kuhusu JWTZ, hili jeshi lilikuwa na heshima sana kipindi cha nyuma na lilipendwa na kuheshimiwa sana na wananchi wakati na baada ya vita ya Uganda.
Heshima hii ilianza kuporomoka baada tu ya wajeshi kuanza kuingizwa kwenye vyeo vya kisiasa.

Ukiangalia utendaji wa hili jeshi kwa sasa ni kama viongozi wanatoa matamko ili kuweka kumbukumbu kwa wanasiasa wakitarajia kuteuliwa kwenye nafasi za kisiasa.

Heshima ya Jeshi letu irudi.
.
Ukiangalia utendaji wa hili jeshi kwa sasa ni kama viongozi wanatoa matamko ili kuweka kumbukumbu kwa wanasiasa wakitarajia kuteuliwa kwenye nafasi za kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MSHANA naamini una uwezo mkubwa sana wakuchambua mambo,, hii thread ungeipotezea tu ipo kisiasa zaidi.

Itakuwaje Kama hapa ndipo uwezo wake umeishia?

Mshana Jr wa JamiiForums analitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo CIC ni Rais Samia, litoe waraka kuhusu sakata la Bandari za Tanganyika vs Mwekezaji DP World kutoka Dubai
alieletwa na Serikali ya Rais Samia.
 
Kumbukizi Leo ni 911.. Fumbo la ghorofa pacha la world trade center.. Ambalo halipo tena..!!!

Mgawanyo wa madaraka na majukumu
TISS kufuatilia usalama wa nchi/taifa.. Viashiria, mipango, wahusika, wafadhili, na hata utekelezaji wa jambo lolote baya linalohusika na taifa katika ujumla wake bila kuwasahau viongozi.

JWTZ Jeshi la wananchi wenye nchi.. Jukumu kubwa kulinda mipaka ya nchi/Taifa isiingiliwe na maadui nknk.. Lakini pia kwenda vitani inapohitajika nknk

JESHI LA POLISI TANZANIA kulinda usalama wa raia na mali zake pamoja na majukumu mengine yote yanayohusika na usalama wa wananchi na mali zao

Majeshi mengine yote ni wasaidizi tu toka hayo hapo juu..!
Tumekuwa na kipindi kama cha mpito tangu sakata la bandari lilipoanza zaidi ya miezi mitatu sasa. Mambo yamekuwa mengi mno kulihusu mema na mabaya

Ni ngumu kuwalaumu TISS kwakuwa hawa huwa hawaendi front.. Na kwa mtazamo wa kawaida unaweza kudhani hawajafanya kitu.. Lakini pengine kwenye hili sakata wanapaswa kushukuriwa pakubwa sana!

Linapokuja suala la mipaka ya nchi, Kwa maana ya anga, nchi kavu na majini.. Mhusika mkuu ni JWTZ kwa msaada wa TISS..Suala la bandari ni mojawapo ya maingilio ya nchi kutoka mipaka ya majini

Utendaji wa JWTZ ni tofauti sana na Jeshi la polisi.. JWTZ sio watu wa matamko wala press conferences kwakuwa hawadili na wananchi moja kwa moja.. Na ndio maana unaposikia Jeshi linataka kutoa tamko ama linataka kuongea na waandishi wa habari, tashwishwi huwa kubwa..

Matamko ya kutaka wananchi wasivae nguo zinazofanana na za kwao, matamko ya kutaka kuingia mitaani kusaka nguo/sare zinazofanana na za kwao.. Matukio yanayosambazwa mitandaoni wanajeshi wakiwaadhibu wananchi wanaokutwa na nguo zinazofanana fanana na zao.. Naomba niseme SIO LEVEL ZA JESHI LETU na ni kukiuka katiba na kuingilia majukumu ya wengine!

Kama tunaweza kuipongeza TISS kwenye sakata hili la bandari, basi sasa macho na masikio ya wananchi yana tashwishwi ya kusikia neno toka kwa mhusika mkuu wa mipaka na malango ya taifa
Matamko ya sare sio case sensitive kama ishu ya mipaka!
Kama KITI kimeamua kukaa kimya.. Inaweza kuwa ni hasara kubwa yenye faida kwa wengine kama nalo likisema.... Funika kombe mwanaharamu apite...

View attachment 2745533

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnawatafuta ubaya mandava wa watu.
Wao wanasubiri muda waingie kitaa kusanga sare zao
 
Back
Top Bottom