Msekwa Atoboa siri ya Butiama

Alikuwa mwenyekiti ya bodi ya vodacam, mnafiki tu hana lolote...bei inajulikana na anachukua mshiko yuko kwenye pay roll, baba wa taifa ni mtaji wa kisiasa, nimeona hata mnyika anatafuta umaarufu kwa kutumia the same old fashion..hakuna wa kutudanganya
 
Msekwa akiri ufisadi umeiumbua CCM kwa sababu ya kulindana

  • Kuanzisha Chuo Kikuu cha Maadili Iringa

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, amesema kashfa za ufisadi zinazowakabili baadhi ya viongozi wake, zimekiumbua chama hicho pamoja na serikali yake.

Akiwahutubia wanafunzi wa matawi ya CCM ya vyuo vikuu vilivyopo jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere jana, alisema ufisadi ambao umewakumba wengi umesababishwa na tabia ya viongozi kulindana na kutosimamia kikamilifu maadili ya uongozi yaliyoainishwa ndani ya katiba ya CCM.

Alisisitiza kuwa tabia hiyo ni kinyume na misingi ambayo Baba wa Taifa, aliwaachia Watanzania.

"Mara kwa mara Baba wa Taifa alikuwa anatumia methali inayosema; 'Mficha maradhi, kilio humfichua'. Katika utaratibu huu wa kumkumbuka na kumuenzi, hatuna budi kukiri upungufu huo tulio nao wa kutoweka usimamizi makini wa maadili ya viongozi wetu na ndiyo kiini cha kuwepo ufisadi na uzembe," alisema Msekwa na kuongeza:-

"Kwa kuwa tulificha maradhi hayo, sasa kilio dhidi ya vitendo viovu vya baadhi ya viongozi wetu, ambavyo vimepewa jina la ufisadi, vimetuumbua".

Msekwa alisema kwa sasa serikali inapaswa kuchukua hatua za kujisahihisha; kwa kuhakikisha kuwa viongozi wote watakaobainika kujiingiza katika ufisadi wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

"Lengo la kuwachukulia hatua mara moja viongozi wanaokiuka maadili mema, linatukumbusha mafundisho mengine ya Baba wa Taifa, aliyokuwa akiyatoa kwa kutumia methali isemayo: "Mtoto akichezea wembe, utamkata pale pale, hausubiri mpaka baadaye" alisema Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM.

Alifafanua, "Matumizi ya methali hiyo yalikuwa maelezo rasmi kwa vikao vyenye mamlaka ya kuwachukulia hatua, vifanye hivyo mara moja bila kuchelewa".

Msekwa ambaye mara kwa mara alikuwa akinukuu methali alizokuwa akitumia Mwalimu Nyerere kwenye hotuba zake; alisema katika kujaribu kurudisha maadili ya viongozi, CCM iko katika mchakato wa kujenga Chuo Kikuu kitakachokuwa kinatoa mafunzo ya Itikadi na Maadili ya Viongozi.

Alisema chuo hicho kinatarajiwa kujengwa mkoani Iringa na tayari Mzee Kikunge Ngombale Mwiru ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa maandalizi ya mchakato huo.

Alisema mkakati huo ni miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM ilipofanya kikao chake Butiama, mkoani Mara eneo ambalo alizaliwa na kuzikwa Mwalimu Nyerere.

Alisema pia kuwa CCM, iliazimia kuweka utaratibu bora zaidi wa kuwachuja wagombea wa nafasi za uongozi katika chama na vyombo vya dola, ili kuweza kubaini mapema wasio waadilifu.

Katika hutoba yake hiyo ambayo aliisoma kwa takriban saa moja, Msekwa alisema kupiga kelele za mafisadi majukwaani pekee hakutoshi; bali inatakiwa wapambane kwa sheria kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.

"Leo mkisimama jukwaani na kusema sisi ndio wapambanaji wa ufisadi haitosaidia. Inatakiwa tutekeleze kwa sheria kama Mwalimu alivyofanya," alisisitiza Msekwa huku akitolea mfano wa waziri mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa rushwa enzi za Mwalimu Nyerere.

Msekwa alisema waziri huyo (ambaye hakumtaja jina), alihukumiwa adhabu ya kwenda jela na alichapwa viboko 12 wakati wa kuingia na baada ya kumaliza kifungo kwa kosa hilo.

Msekwa aliwataka viongozi wasitumie kigezo cha kutokuwepo kwa Mwalimu kufanya mambo kinyume na misingi ya uadilifu aliouacha.

Alisema viongozi walio wengi wamesahau vitendo kama vya umoja, maendeleo sawa kwa wote, mambo ambayo Mwalimu Nyerere aliyapigania.

"Mwalimu alifuta serikali za mitaa baada ya kuona baadhi ya maeneo yanapata maendeleo kuliko mengine. Aliona hali hiyo inavuruga amani na umoja wetu. Kwa mfano, Moshi (Kilimanjaro) ilikuwa na maendeleo sana," alisema Msekwa akifafanua:

"Hata barabara zake nyingi zilikuwa na lami wakati maeneo mengine kama Lindi yakiwa nyuma sana kimaendeleo. Maendeleo ya Moshi yalipatikana chini ya Chifu Thomas Marealle.

"Maendeleo haya yaliyotishia uhai wa umoja wetu na amani yaliletwa na serikali za mitaa. Mwalimu baada ya kuzivunja alirudisha jukumu la kuleta maendeleo kwa taifa katika Serikali Kuu."

Pia aliwataka viongozi kujitahidi kupunguza pengo la wenyenacho na wasionacho.

Katika hatua nyingine mkongwe wa siasa nchini, Mzee Kingunge, aliwataka vijana kufuata fikra za Mwalimu na kuwa muasisi huyo wa taifa hili aliamini zaidi kuwa vijana ndio watakaoweza kulisaidia taifa.

Alisema pia kuwa CCM ilifanikiwa kuhamasisha suala la miiko ya viongozi kutoka kuwa la viongozi na kuwa la wanachama wote; hivyo sasa kila mwanachama ana wajibu wa kusimamia maadili.

“Kwa mfano, Azimio la Zanzibar lilipitisha miiko hiyo na NEC huko Dodoma chini ya Mwalimu, ambaye bado alikuwa mwenyekiti wa chama na baadaye iliwekwa kwenye katiba," alisema Kingunge.

Aliongeza, "Hatua ya mwisho ilifanyika Zanzibar, lakini yeye Mwalimu hakuwepo".

Azimio la Zanzibar ndilo lililofuta Azimio la Arusha ambalo msingi wake ni Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea iliyokuwa na sera na maadili yake ikiwemo miiko ya uongozi.
 
Sasa tatizo mnalijua(ufisadi) na source mnajua(kulindana) mnashindwaje kulitatua? Na wanaofanya ufisadi hawaja vunja tu katiba ya CCM bali na katiba ya nchi kwa hiyo wawajibishwe na chama na wapelekwe na mahakamani. Blah blah zimekua too much.
 
Hivi mtu mzima ukichukua nyama katika chungu na kuila wakati mwanao anakuangalia, je huyo mwanao naye akichukua tonge la nyama kwenye chungu akala wewe kama mzazi unaweza kumkaripia? CCM kama mzazi ndio ya kwanza kuchukua "nyama" kwenye Chungu (BoT) na watoto (makada/wakereketwa) nao wakachukua. CCM haiwezi kupata kifua cha kuwakemea mafisadi maana wote tunajua kilichotokea 2004/2005. Kama kuna mtu anabisha atwambie kwa nini Malegesy ni "untouchable" mpaka sasa katika sakata la EPA.
 
Alikuwa mwenyekiti ya bodi ya vodacam, mnafiki tu hana lolote...bei inajulikana na anachukua mshiko yuko kwenye pay roll, baba wa taifa ni mtaji wa kisiasa, nimeona hata mnyika anatafuta umaarufu kwa kutumia the same old fashion..hakuna wa kutudanganya

Ni katika harakati za kuwazuga Watanzania kuelekea 2010 ili wapate tena ushindi wa kishindo wenyewe wanaita TSUNAMI baada ya kutumia "mbinu" zao za kutoa rushwa za aina mbali mbali, kutumia vyombo vya dola kuwatisha na kuwanyanyasa Viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani na pia kuiba kura.
 
Na ndiko hapa ambako ndio mambo yote yanaanzia hapa kwa kila kitu maana hakuna kitu kibaya kama hiki
 
Hizi zote ni tambo za kuelekea uchaguzi mkuu wazee wangu


Waingereza nasema "jumping on the bandwagon". Kwa hapa ni kama mdundiko. Ngoma ya mdundiko wengi wetu hatujui inaanzia wapi lakini ikipita tunajiunga na kucheza na wakati mwingine watoto upotea! Mdundiko huu ulianzia pale Mwembe Yanga Sept 2007 na sasa upo Moroco kuelekea Msasani na Pius Msekwa amejiunga nao na Kibwagizo kipya cha " CCM imeumbuka, CCM inatubu, CCM....". Mimi nina hakika mdundiko huu ukikaribia pale Mayfair kuelekea kwa Mwalimu (Kituo cha mwisho 2010) Mzee Msekwa atajiengua kwa kibwagizo " CCM mtajiju!". Nani anabisha?
 
Alikuwa mwenyekiti ya bodi ya vodacam, mnafiki tu hana lolote...bei inajulikana na anachukua mshiko yuko kwenye pay roll, baba wa taifa ni mtaji wa kisiasa, nimeona hata mnyika anatafuta umaarufu kwa kutumia the same old fashion..hakuna wa kutudanganya

Kweli Msekwa alikuwa M/kiti wa vodacom lakini kwa kutumiwa na Rostam bila yeye mwenyewe kujua awali ya yote kuwa pale alikuwa anatumiwa kwa vile alikuwa Spika wa bunge!! Na hao hao ndio walimtoa Uspika wa bunge na kumpa Mr SIX!! Kwa misingi hiyo bwana Msekwa has an axe to grind na hawa mafisadi wakina RA na EL; na kwavile hawa ndio mafisadi papa, huyu bwana akiwapatia nafasi atawalipizia kisasi walichomfanyia kuutema uspika!! Hapa hakuna itikadi ni VENDETTA tu.
 
Uzee dawa.At least huyu bwana ameangalia kunakotakiwa kuangalia. Nawashangaa jamaa wanaokataa hakuna tatizo wakati lipo bayana na linahitaji solution
 
- Yale yale ya politics as usual, ni siku ya kumkumbuka Mwalimu kwa hiyo politically ni lazima yasemwe maneno yanayoweza kwenda samba samba na the day kuonyesha kwamba bado wanamjali Mwalimu, na hasa this times za kuelekea uchaguzi mkuu, na baada ya kubanwa sana na mabalozi wa nje nchini kuhusu NEC yao na Sitta,

- Hivi Msekwa hakuwemo kwenye kile kikao cha aibu ya the century cha NEC na Sitta? Kwanini hakusimama na kusema haya maana pale ndio hasa palikuwa mahali pake haya maneno yake mazuri sana kwa taifa, no! kule alinyamaza kimyaa, lakini kwa kuwa wa-Tanzania ni wasahaulifu sana au huwa hawajali yaliyopita anyways, basi siku ya Mwalimu ndio inafaa kuyasema haya as if wabongo wote tumelala usingizi,

- Halafu kwa nini anazunguka mbuyu na maneno mengi ya ubabaishaji, Tanzania tunataka utawala unaoheshimu sheria sio maadili ya uongozi wa CCM, kwa sababu CCM imeshatuthibitishia kwamba haina uwezo wa maadili wala heshima kwa mali za wananchi, sasa wanaanzishaje chuo cha maadili ya CCM badala ya kujenga jela maalum kwa ajili ya mafisadi kutoka ndani ya chama chake Msekwa ambao mwenyewe anakiri kwamba wamejaa huko na wanalindwa na chama chake, kwani hicho chama kinachowalinda hao mafisadi ni nani hao kama sio pamoja na yeye mwenyewe?

- Alipokuwa anamfanyia kazi Rostam kule Vodacom huku akiwa Spika wa bunge la jamhuri akichukua mshahara wa jamhuri na shillingi Millioni tatu kwa mwezi za Voda, yalikuwa ni maadili yapi hayo ya CCM ya Mwalimu au ya Azimio la Zanzibar? Hawa viongozi bwana, either kuleni kimya kimya au nyamazeni tu mpaka tutakapopata viongozi wa kweli, wasioogopa kuwasema mafisadi kwa majina na wizi wao, wasioogopa kusema ukweli mahali panapostahili kwenye NEC na kusubiri eti kwenye mkutano wa vijana wa CCM somewhere, mkutano ambao hata kwenye katiba ya jamhuri haufahamiki hayo Msekwa ni matusi kwetu wananchi, tulioamka!

Ahsante.

William.
 
I am an unashamedly a CCM coconut, why did it take so long for these stalwarts to figure it out?
Je pesa za mafisadi iliwapofusha?
Makamba,Chiligati,Msekwa na wengine wengi waliokuwa 100% pro mafisadi, huu ulokole wa kupinga ufisadi wameupata wapi?
 
Jamani mambo ya kibongo mmeyasahau???? usanii kibaaaao, hiyo ni danganya toto tu watanzania ili ku-create nafasi za kujipatia vijisenti vya kujikimu pamoja na kujitafutia umaarufu hasa kipindi hiki chao cha uzeeni. Mnataka wakale wapi??? Polisi????
 
Msekwa defends CCM-NEC treatment of Speaker Sitta

THIS DAY


It was "perfectly normal" for the Chama Cha Mapinduzi (CCM) national executive
committee (NEC) to reprimand the Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, for the manner in which he has been running parliamentary proceedings, CCM top politburo member Pius Msekwa reiterated yesterday.

"Normal procedure was followed in questioning Sitta's conduct. When I was Speaker of the National Assembly, I was also summoned to a CCM-NEC meeting and subjected to a grilling. But I wasn't fired from my job. The goal (of these NEC meetings) is to put things right," Msekwa, the ruling party's vice-chairman for Tanzania mainland and Sitta's immediate predecessor as the head of parliamentary business, told a news conference in Dar es Salaam.

Msekwa is now part of a three-man committee entrusted with the task of overseeing efforts to restore CCM internal unity and fix the ruling party's current image problems. The committee, dubbed 'The Three Wise Men', is led by ex-president Ali Hassan Mwinyi and also includes former Speaker of the East African Legislative Assembly, Abdulrahman Kinana.

Flanked by Mwinyi himself, Msekwa told reporters at the ex-president's residence in the city that there has historically been rifts amongst senior CCM stalwarts since the party's birth in 1977, and even within its predecessor TANU since independence in 1961.

He said it was "normal procedure" for CCM to summon members associated with such rifts that occur within the party from time to time, as part of the healing process.

The CCM secretariat, under secretary-general Yusuf Makamba, has come under heavy public criticism for allowing Speaker Sitta to be literally �crucified� in the last CCM-NEC meeting held in Dodoma a couple of months ago.

It is understood that the vitriolic attacks against Sitta by various NEC members at the meeting were part of a plot hatched by a network of corrupt CCM leaders to get him removed from the Speaker's seat because of his firm stance against major corruption scandals such as the Richmond power generation deal.

On the task facing the Mwinyi-Msekwa-Kinana committee, the CCM vice-chair said they would begin by meeting with members of the Zanzibar House of Representatives representing the ruling party next week.

Since the House of Reps began its latest session in Zanzibar on Thursday of last week, several CCM reps have already made fiery remarks about aspects of the Union between mainland Tanzania and Zanzibar and the future of sharing of potential oil reserves in the Isles.

From Zanzibar, the 'three wise men' will move to Dodoma for a similar meeting with members of the CCM parliamentary caucus, Msekwa said.

He explained that the ultimate goal is to restore harmony between various ruling party backbenchers in the august House and government ministers, in the wake of reports of animosity between elements of both camps.

According to Msekwa, the committee has been tasked by CCM-NEC to address those differences and restore unity within the party ahead of the 2010 general elections.

He said the committee will address all CCM legislators in the parliamentary caucus and conduct frank and open discussions with them about the way forward.

Msekwa echoed the recent observation by President Jakaya Kikwete the CCM chairman that deep mistrust does currently exist among certain CCM members of parliament, to the extent (as observed by the president) that some MPs fear they could even end up being poisoned by their colleagues.
 
stupid!! normal is not the same as "legal" or "constitutional"! there are a lot of things CCM is doing that we have accepted as normal but in fact they are very illegal! Msekwa should know the difference!
 
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, amewataka wabunge wanaolalamika kuwapo kwa fedha chafu zinazomwagwa majimboni mwao waache hadithi na badala yake wapeleke ushahidi.

Msekwa amesema ofisini kwake kuwa, madai hayo pamoja na ya CCM kutumia fedha za mafisadi, yamekuwa sawa na hadithi inayochosha.

“Haya madai sasa yamekuwa kama hadithi … hao mafisadi ni akina nani, tumechoka kusikia, ila ningeshauri kuwa wanaosema hivi wangewataja hao wanaozimwaga hizo fedha chafu na wanapozitoa,” alisema Msekwa.

Alisema madai hayo ni moja ya dalili za kuwapo kwa vuguvugu la uchaguzi na wasiwasi, kwa vile sasa Tanzania inaelekea katika mwaka wake wa uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

“Kama nilivyosema hapo mwanzo haya yote ni vuguvugu na joto la uchaguzi watu wana wasiwasi na nafasi zao, wanasema tu lakini hakuna mwenye ushahidi,” alisema.

Juzi gazeti moja la kila siku, liliwakariri baadhi ya wabunge wakilalamikia ‘kumwagwa’ kwa ‘fedha chafu’ katika majimbo yao, ili kuhakikisha kuwa nafasi zao zinachukuliwa na hawafurukuti katika uchaguzi ujao.

Gazeti hilo liliwataja wabunge hao kuwa ni Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko (CCM) na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Wajumbe hao nao walidai kuwa watazipokea fedha zinazodaiwa kutolewa kwa ajili ya uwashawishi wa kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu mwakani lakini hawatadanganyika.
 
Choka siku nyingi sana mzee wa watu; alikuwa intellectual sana miaka ile ya sabini, lakini leo hii ni puh!!
 
mmmmmmh sasa sijui hata mama na ile zawadi yake ya zuma anashindwa kumsaidia jamani embu amsitiri kidogo mumewe;walipendana bungeni wapendane na mtaani jamani
 
MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango- Malecela (CCM) amesema, siasa chafu zimeanza hivyo wananchi wawe makini na kauli za wanasiasa na wapambe wao wakati huu kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Kilango amesema, siasa hizo hazimtishi au kumyima usingizi hivyo wanaotaka wakamwage fedha kwa wananchi jimboni kwake.

“Hata siku moja sikosi usingizi. Siamini kama wananchi wataacha kunichagua kutokana na kumwagiwa mapesa. Kama wapo wanaotaka kupeleka magunia ya pesa ruksa. Nawaambia wapiga kura wangu zikiletwa pesa watafune. Hizi siasa chafu hazinipi tabu, tena nalala usingizi.”

Amewaeleza hayo waandishi wa habari nyumbani kwake Dar es Salaam, katika hafla fupi ya kukabidhiwa mchango kwa ajili ya waathirika wa maporomoko ya udongo na mawe yaliyosababisha watu 24 kupoteza maisha katika kijiji cha Goha kata ya Mamba Miamba wilayani Same.

Baada ya kupokea mchango wa takribani Sh milioni 2.8 kutoka Chama cha Haki za Binadamu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliokabidhiwa na Mwenyekiti wake, Fredy Kihwelo, Kilango alisema zimekuwapo porojo na siasa za uongo kutoka kwa watu wanaotafuta kura, wakidai kwamba misaada inayotolewa kwa ajili ya waathirika wa maporomoko hayo haiwafikii wahusika.

“Tumeingia mwaka 2010 ambao ni wa uchaguzi. Watanzania wawe makini na maneno ya wanasiasa au wapambe wao,” alisema Kilango bila kutaja wanaofanya hivyo kwa kusisitiza kwamba wananchi wawe makini kwa kuwa si tu ni siasa za kuwachafua wabunge bali pia kuichafua Serikali.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, licha ya kamati anayoisimamia ambayo imekuwa ikikusanya misaada, vile vile ipo Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Same inayosimamiwa na Mkuu wa Wilaya, Ibrahim Marwa, ambayo pia aliitetea kuwa imekuwa ikifanya kazi yake vizuri na misaada kuwafikia walengwa.

Mbunge huyo ambaye pia alielezea kuguswa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutembelea waathirika na kuahidi kuwajengea nyumba, alitoa mchanganuo na mgawanyo wa vyakula, vifaa na fedha taslimu zilizokwishatolewa na wasamaria wema, ambavyo alisema kamati yake inasimamia.

Alisema vinagawanywa kwa kuzingatia kiwango cha athari kwa wahusika. Maporomoko hayo yalitokea Novemba mwaka jana.

Akielezea mtazamo wake kuhusu siasa chafu yakiwamo madai kwamba wapo watu wanaokwenda kwenye majimbo wakitoa fedha kushawishi wapiga kura, Mbunge huyo alisema haamini kama wananchi wanaweza kushawishiwa kwa fedha wakaacha kuchagua mbunge wanayemwamini kuwa atawatumikia.

Kilango amesema, katika uchaguzi mkuu ujao atakayekuwa na wakati mgumu ni mtu binafsi na wala si CCM tofauti na ambavyo imekuwa ikifikiriwa.

Alisema CCM ni chama kikubwa chenye wanachama zaidi ya milioni 1.4 ambacho haiwezekani ufisadi wa mtu binafsi ukachukuliwa kuwa ni wa chama kizima.

Alisema hata vyama vingine vya siasa vimekuwa katika migogoro ya kugombea ruzuku, lakini haiwezekani kuvihukumu kutokana na tabia ya watu binafsi.

Mbunge huyo alisema anawashangaa wanaomsema kwamba anapiga kelele na hapambani dhidi ya ufisadi. Alibeza pia wanaomtaka atoke nje ya chama ndipo akosoe na kusisitiza kwamba anachofanya, ni kutekeleza Ilani ya CCM inayoelekeza mapambano dhidi ya ufisadi.
 
Hata Kingunge mwaka 2007 ilipotolewa orodha ya mafisadi alisema sio kweli na wenye ushahidi wapeleke, sasa huyu anasema mafisadi ni nani asome orodha ya aibu ya Dr.Slaa ya mwaka 2007 mwezi September tarehe 15 na inapatikana kwenye website hii www.chadema.or.tz
 
Back
Top Bottom