Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mzee Msekwa akiwa kwenye mjadala uliendeshwa na TBC1 kuhusu swala la Mwafaka wa Zanziba.
Mzee Msekwa alijikuta ukweli juu ya yaliotokea Butiama ukitoka wenyewe na kama kawaida ya ukweli huwa unatabia ya kutoka wenyewe ukizuiwa kwa mda mrefu.
''Baada ya kubanwa sana na wajuzi wakuuliza maswali alikiri inabidi awe wazi na aseme ukweli na kusema wajumbe wa kutoka Zanziba walio wengi hawakukubali ile rasimu ya mwafaka na kupelekea kuirudisha hoja hiyo kwa wananchi wa zanziba ili waweze kufanya maamuzi juu ya Mwafaka.
''Katika mjadala huo pia msekwa alibainisha mambo mengi sana ya ndani ambayo yalifichwa sana na pengine kwa mtizamo wangu ufafanuzi ulitakiwa kutolewa kwa uwazi kuhusu kilichotokea ili wananchi wajue tatizo hasa ni nini kuliko kuendelea kuficha na alivyoeleza msekwa baada ya kubanwa sana ndio akaamua kusema ukweli.
''Pia kuna mafunzo ambayo niliyapata kutokana na mjadala huo kuwa viongozi wetu wanapaswa kujua pia wananchi wanauelewa mkubwa sana juu ya mambo yanayotokea kwahiyo viongozi wajiepushe kuficha mambo na mfano mzuri ni maswali mazuri aliyoulizwa msekwa na kumpelekea kusema ukweli.
''Funzo la pili ni kuwa viongozi wanapaswa kujua kuwa hakuna siri ya watu wengi kama waliokutana butiama ni wazi pia kilichotokea ni lazima kingesemwa na baadhi ya wajumbe kwahiyo viongozi wanapaswa kutoa maelezo kwa kina kuepusha kutokueleweka vizuri na umma.
''Mwisho nauliza swali kutokana na hayo yaliyotokea je CUF wangetoa kauli ipi? ama wafanyeje kutokana na haya yaliyotokea?