Msanii Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA rasmi

Msanii Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA rasmi

Kama alitoka Lowasa halafu CCM ikashinda kwa kishindo, Wema Sepetu mbwia madawa akihamia Chadema mambo yatakuwaje?
 
Chadema hujidharirisha sana,wale wote wenye mawaa wakigundulika CCM basi kimbilio lao ni Chadema,waliotajwa kuuza unga wamepata nyumba mpya,wasingetajwa wangebaki nyumba ya zamani.

Maxhoko tulieni dawa iwaingie kisawasawa.
 
Tukio lililowakutanisha watu Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam jana ni kesi ya kikatiba ambayo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemfungulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mbowe amemshitaki Makonda kuhusu uamuzi wake wa kutuhumu watu kwenye kadamnasi na kuamuru wafike Polisi kwa mahojiano. Mbowe anataka Mahakama itamke kuwa Makonda hana mamlaka hayo.

Vilevile Mbowe anataka Mahakama itamke kuwa Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inayowapa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mamlaka ya kuamuru watu kuwekwa mahabusu kwa saa mpaka 48 imepitwa na wakati na inakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kimsingi kesi ambayo Mbowe ameifungua ni muhimu kwa taifa. Inatakiwa ipewe nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari hatua kwa hatua, maana uamuzi wake kwa namna hukumu itakavyotolewa na Jaji, itaweka historia mpya nchini.

Sheria hiyo ya mtu kwa kutumia mamlaka yake kuamuru watu wawekwe ndani kwa saa 48 ni moja kati ya sheria kandamizi ambazo taifa linapaswa kujitenga nazo.

Hata hivyo, pamoja na unyeti wa kesi yenyewe, kilichopata msukumo mkubwa kwenye vyombo vya habari ni tukio la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, kumsindikiza Mbowe mahakamani.

Taarifa za kuhusu kesi zimekosa mvuto, eti Wema ndiye kapamba! Binafsi wala silaumu. Huyo ndiye Wema ninayemfahamu kwa miaka 11 sasa. Mrembo asiyeshuka thamani mbele ya vyombo vya habari.

Ukiniambia Wema hajiheshimu nitakukubalia. Ukininong’oneza kuwa Wema ana kashfa nyingi mbaya nitakuunga mkono. Ukithubutu kutamka Wema hana nguvu ya ushawishi nitakupinga hapohapo.

Wema ni mrembo mwenye nyota yake. Tangu mwaka 2006 alipotangazwa Miss Tanzania, ikawa ndiyo tiketi. Mrembo umaarufu umegoma kushuka. Vituko na upuuzi wake, watu wanampenda hivyohivyo.

Likitokea jambo ambalo linaweza kuwafanya watu wamwone thamani yake imeshuka na kwamba labda atafifia na kupotea, ndiyo kwanza jambo lenyewe humwongezea umaarufu. Mimi namwangalia tu, maana huyu Wema si wa leo wala kesho.

KAMA UTANI MWANANGU

Wema Chadema! Shangaa kisha lipo swali, je, ulitaka afanye nini? Unadhani Wema hajitambui kiasi cha yeye kufa kikondoo?

Eti Wema amekosea, ili apatie ulitaka afanye nini? Kwa wakati huu Wema kuhamia Chadema kwani amepoteza nini?

Wema angeendelea kubaki CCM na aliyehamia Chadema yupi ambaye thamani yake ni kubwa? Je, angebaki CCM au huyu aliyetangaza kujiunga Chadema?

Nani mwenye hasara katika kuhama kwa Wema? Ni CCM iliyokimbiwa na mwanachama wake au Chadema iliyosajili mwanachama aina ya Wema? Je, ni Wema mwenyewe kajipoteza?

Wema amejiunga Chadema kwa hasira ili kulipiza kisasi cha yeye kutajwa na Makonda kwenye kashfa ya dawa za kulevya. Je, hasira zikiisha na kusahau ya Makonda ataendelea kuwa mwanachama mtiifu wa Chadema?

Wema amemfuata Mbowe mwathirika mwenzake wa tuhuma za Makonda. Maana Mbowe pia ni mtajwa wa biashara ya dawa za kulevya. Je, sakata la dawa za kulevya na majina ya Makonda likishapita Wema atakuwa mguu sawa na Mbowe pamoja na Chadema?

Ni mwaka mmoja na nusu uliopita Wema alizunguka nchi nzima kumwombea kura Rais John Magufuli na makamu wake, Samia Suluhu Hassan.

Naamini Wema hakupambana bure, alilipwa na chama. Pamoja na hivyo, Wema siyo mjinga kiasi cha kutotambua yeye ni muhimu kiasi gani. Angekuwa siyo muhimu CCM wasingemtumia.

Eneo hilo ndilo ambalo linampa kiburi Wema. Anajiona mwenye thamani ya kunyenyekewa na siyo kuchukuliwa poa. Anajiona alihusika kuiweka madarakani Serikali iliyopo, kwa hiyo anaumia kuchukuliwa kama mtu asiye na thamani.

Na sasa Wema anataka kuonesha nguvu zake. Wema anataka kuthibitisha kiburi chake. Wema anataka kuzionesha mamlaka za nchi kuwa wao wana madaraka lakini yeye ana watu ambao wanampenda.

Asije kukwambia mtu, kuwa na watu wengi wanaokupenda ni mtaji namba moja katika maisha ya kila binadamu. Ni mtaji huu ambao Wema anao. Bila fedha wala madaraka lakini Wema ni kipenzi cha watu. Si bahati ambayo anaweza kuipata kila mtu. Hiyo ni karama, ni majaala ya Mwenyezi Mungu.

WEMA ANA AKILI SANA

Niamini mimi, Wema hajafanya uamuzi wa kujiunga Chadema kama taahira, ametumia akili. Naweza kusema kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake tangu nimemfahamu, safari hii Wema ametumia akili kuamua.

Je, Wema amefanya papara kuhamia Chadema? Hapana, ametazama nafasi yake kulingana na wakati uliopo. Wema emekwenda Chadema ili kufanikisha mambo mawili, mosi ni nusura yake, pili ni kupata jukwaa la kuwaonesha maadui zake wapya (CCM) kuwa anaweza kuwasumbua kutokana nguvu alizonazo kijamii.

Wema hakuwa kiongozi CCM, hakuna maslahi yoyote aliyokuwa anayapata ndani ya CCM, kwa hiyo hata baada ya kuondoka hakuna ambacho ni hasara kwake.

Ni kwa sababu hiyo, hata CCM hawawezi kuona athari kwa wakati huu kwa sababu hiki siyo kipindi cha kampeni. Watapata wakati mgumu kama utatokea uchaguzi mdogo au ukifika Uchaguzi Mkuu 2020, Wema akiwa kwenye kiwango kikubwa cha ushawishi.

Naomba nifafanue ni kwa nini nimesema Wema ametumia akili; Wema anakabiliwa na mashitaka ya matumizi ya dawa za kulevya. Alitangazwa katika awamu ya kwanza ya majina ya Makonda.

Wema alipoitikia wito wa Makonda Polisi, aliwekwa mahabusu sawasawa na wenzake wote aliotajwa nao. Hata hivyo, wenzake wote walilala mahabusu kwa siku tatu, wakafikishwa mahakamani kisha kuachiwa huru japo walipewa sharti la kuwa chini uangalizi.

Upande wa Wema, alilala mahabusu siku saba, akapelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali kupimwa matumizi ya dawa za kulevya kisha akafikishwa mahakamani. Kwa sasa yupo nje kwa dhamana.

Utaona kuwa Wema alichukuliwa tofauti na wenzake wote. Ama kwa viashiria vingi vya mashitaka alivyokutwa navyo au vyvyote vile, jawabu ni lilelile kwamba Wema alichukuliwa tofauti na wasanii wenzake waliotajwa naye katika awamu ya kwanza.

Ikumbukwe pia mtaja majina ni Makonda. Zikavujishwa sauti za Wema akimtuhumu Makonda kuwa anapendelea, kwamba alimruka mwanamitindo Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa sababu ana uhusiano naye wa kimapenzi na amempangia nyumba Makongo, Dar es Salaam.

Kuvuja kwa sauti hizo za Wema, kukawa na mfuatano wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, kumtolea taarifa Wema kuwa alikutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake. Wakati Siro akitoa taarifa hiyo, alikuwa na Makonda.

Tafakari; kwa nini Wema atolewe taarifa peke yake ya kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake? Alikuwa akishikiliwa na wenzake, sasa kwa nini yeye peke yake? Je, ni kwa nini taarifa ya msokoto wa Wema ilitolewa baada ya sauti za Wema kumtuhumu Makonda? Endelea kutafakari!

Ni kwa nini Wema hakufikishwa mahakamani siku moja na wenzake, yeye akaachwa kwa siku nne zaidi? Ni kwa nini hilo lilitokea baada ya sauti za Wema akimtuhumu Makonda kuvuja na kusikilizwa na wengi? Tafakari pia na hili!

Sasa jiulize; haiwezekani ripoti ya Siro kuhusu msokoto wa bangi pamoja na tukio la Wema kubakishwa mahabusu kwa siku nne zaidi, sababu ikawa zile sauti za Wema alizomsema Makonda?

AKILI YA WEMA ILIPO

Wema ni msanii tu wa Bongo Movie, hana nguvu yoyote ya kushindana na Makonda ambaye ni gavana wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tafakuri za juu, zinatosha kukuonesha kuwa Wema na Makonda hawapo kwenye wakati mzuri. Na siku zote dhaifu akishindana na mtu mwenye mamlaka lazima aumie tu.

Nani wa kumtetea Wema na kumkinga dhidi ya Makonda? Hali ilishakuwa mbaya upande wa Wema. Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye, alijaribu kutoa sauti kukosoa utaratibu wa Makonda, akakutana na sauti kali kutoka juu.

Sauti kali ilitoka kwa Rais John Magufuli ambaye aliwaonya watu kutomwingilia Makaonda, akasema hata kama angekuwa mke wake atajwe. Kila mtu baada ya hapo akaufyata. Nani wa kumzuia Makonda serikalini ikiwa Rais Magufuli amemwashia taa ya kijani?

Wema ni mwana CCM, ni kweli alifanya kampeni kwa ajili ya CCM Uchaguzi Mkuu 2015. Kampeni ya kuhamasisha vijana kuichagua CCM, wakaiita Mama Ongea na Mwanao.

Mtu wa juu kabisa ndani ya CCM ambaye angeweza kumtetea ni Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais Magufuli. Ikiwa Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye alifanyiwa kampeni na Wema, amempa kibali Makonda, je, Wema angekimbilia kwa nani ndani ya CCM?

Baada ya hali kuwa hivyo, Wema alitakiwa kunyoosha mikono na kuomba radhi ili afanywe maonesho kama ilivyotokea kwa Mnyama Khalid Mohammed ‘TID’.

Ni kwamba TID alitumika vizuri na Makonda kama maonesho, kuhalalisha hatua ambazo alizichukua kutaja majina ya wahusika wa biashara ya dawa za kulevya.

Bila shaka Wema angekiri kutumia dawa za kulevya na kumwomba msamaha Makonda kwa maneno aliyotamka kuhusu mkuu huyo wa mkoa na Masogange kisha kutumika kama onesho la mfano mithili ya TID alivyotumika, amani ingekuwepo.

Ubishi wa Wema ni sababu ya mlolongo wote huo. Na kwa sababu Wema anasimamia hoja kuwa hatumii mihadarati, maana yake ndani yake anahisi kuonewa. Je, aende kwa nani? Mwenyekiti wa CCM yupo na Makonda. Afanye nini?

Mpaka hapo ni wazi Wema alitakiwa kuchagua mambo mawili, ama kumpigia magoti Makonda au kusimama imara na kupambana.

Katika hayo mawili, utaona kuwa Wema alichagua kupambana kutetea kile ambacho anaona ni haki yake. Je, uwezo wa kupambana peke yake anao?

AKILI ILIVYOFANYA KAZI

Kati ya busara zilizoachwa na mwanafalsafa wa Kanisa Katoliki, Mtakatifu Thomas Aquinas ni andiko la Kilatini kuhusu Nadharia ya Vita (Jus Bellum Iustum), kwa tafsiri ya Kiingereza ni Just War Theory.

Nadharia hiyo ina pande mbili, kwanza ni Usahihi wa Kuingia Vitani (Jus Ad Bellum) na Usahihi wa Jinsi ya Kupigana Vita (Jus In Bello).

Kipengele cha kwanza tayari Wema ameshajiona anao usahihi wa kupigana vita, kwamba anajiona anaonewa. Jinsi ya kupigana vita ni kupitia eneo la sheria. Anataka kuuthibitishia umma wa Watanzania kuwa Makonda alimsingizia. Je, ubavu huo anao?

Ni hapo Wema anaamua kuuchukua msemo kutoka kwenye lugha ya falsafa ya Kihindu, Jain, Buddha na Sikhi inayoitwa Sanskrit inayoeleza kuwa Adui wa Adui Yako ni Rafiki Yako (Enemy of Your Enemy is Your Friend).

Kwamba ukiwa na adui, halafu huyo adui yako akawa adui mwingine, maana yake wewe na yule adui wa adui yako, mnakuwa mnachangia adui mmoja. Na kwa vile adui yenu ni mmoja, basi mnatakiwa kuwa marafiki ili mshirikiane kupambana na adui yenu.

Wema anataka kuthibitisha kuwa Makonda alimsingizia. Hapohapo anamshuhudia Mbowe naye akipambana na Makonda. Hivyo, Mbowe ni adui wa adui wa Wema.

Ni hapo sasa Wema anajiunga na Mbowe kwa sababu wanachangia adui ambaye ni Makonda ili kupambana naye kisheria.

Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema, na Chadema ina wanasheria, ni hapo Wema anapata mpaka wanasheria wa kumsimamia kesi yake dhidi ya Makonda. Na kwa vile Chadema ni mwanga wake katika mapambano yake dhidi ya Makonda, ameamua kuvaa gwanda kabisa.

Nilishasema Wema ana akili; siku chache kabla hajajiunga na Chadema, aliweka picha Instagram ya Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, akaandika ujumbe wa kumhurumia Manji kisha akaahidi kuwa naye bega kwa bega.

Manji naye ni mwathirika wa tuhuma za Makonda kuhusu dawa za kulevya na alishaahidi kuwa atamfungulia mashitaka. Kwa hiyo, Manji naye ni adui wa adui wa Wema, kwamba Manji na Wema wanachangia adui.

Hivyo basi, Wema hajaenda Chadema kwa bahati mbaya, ni kwamba yupo kwenye harakati za kuunganisha jeshi dhidi ya Makonda. Tayari ameshafanikiwa kwa Mbowe, sasa tungoje itakuwaje kwa Manji. Nasisitiza; Wema ana akili timamu.

SI RAHISI KUREJEA CCM

CCM ya Magufuli ni tofauti na zilizopita. Magufuli ana falsafa mbili, mosi hataki kufanya maridhiano na wanaokihama chama ili warejee, pili anabana matumizi.

Kuhusu kutotaka maridhiano, falsafa hiyo inajidhihirisha kwenye hotuba yake Julai mwaka jana, alipokabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama. Aliwatambulisha wenye kuhama CCM na kurejea sawa na ng’ombe waliokatwa mkia, kwamba hawawezi kuwa sawa na waliobaki kundini siku zote.

Kwa msingi huo, hakuna dirisha la maridhiano ambalo linaweza kufunguliwa CCM kwa ajili ya Wema, vinginevyo Rais Magufuli abadilike sana.

Na kwa vile Magufuli ni Rais wetu na tunaifahamu hulka yake ya kutopenda kujishusha, ni rahisi kubashiri kuwa dirisha la maridhiano halitafunguliwa.

Falsafa ya kubana matumizi inaondoa kabisa uwezekano wa Wema kurejea CCM. Kwani njia rahisi ya kumfanya Wema arudi CCM ni fedha. Kwa CCM ya Rais Magufuli, fedha hizo za kumhonga mtu mmoja zinatoka wapi?

Rais Magufuli ni mtu wa kufungia vioo hata wapinzani wenye kujiunga CCM. Zamani mpinzani alipojiunga na CCM alipewa heshima maalum na hata nafasi ya uongozi. Wakati huu, watu wanatangaza kujiunga na CCM pamoja na kumwagia sifa kemkemu Rais Magufuli lakini mwenyewe kama haoni wala kusikia.

Njia pekee ambayo inaweza kumfanya Wema arejee CCM kwa siku zijazo ni yeye mwenyewe kukubali kujirudisha bila kupewa thamani yoyote, jambo ambalo litamshushia thamani yake.

Wema amehamia Chadema ili kuonesha kuwa yeye ni Wema. Hivyo ni vigumu tena kurudi kujishusha. Na kwa mkazo wa sasa wa Rais Magufuli kwenye chama chake ni wazi Wema ataendelea kuwa mpinzani.

Je, Chadema wamepata? Ndiyo! Chama kinahitaji watu. Wema anao ushawishi wa kundi kubwa la watu. Na kwa vile kila mtu humaanisha kura moja, hivyo Wema ni mtaji mzuri kwa Chadema ambao kama chama wanajivunia kuupata.

Kuhusu Chadema kuchafuka kwa kashfa za Wema. Chadema itachafuka kivipi? Wema ni mwanachama wa kawaida tu, angekuwa kiongozi na akawa na kashfa hapo ndiyo angekipaka matope chama.

Je, alipokuwa mwanachama wa CCM, kuna wakati chama hicho kilidhalilika kwa sababu ya Wema? Hapana, sanasana kilivuna faida ya nguvu yake ya ushawishi kwa vijana hasa wanawake ambao wanampenda sana. Na ndiyo sababu walimtumia sana kwenye kampeni za mwaka 2015. Chadema pia itakuwa hivyo.

Wema anafuatiliwa na mamilioni ya watu mitandaoni. Zaidi ya watu milioni 2.6 wamejiorodhesha kuwa wafuasi wa Wema Instagram. Lipo kundi kubwa ambalo halijajiorodhesha na wengine hawapo hata mitandaoni. Hivyo, Wema anaweza kushawishi mamilioni ya kura.

Ndimi Luqman MALOTO
Nanijikuta nakosa cha ku criticize kutokana na hizo "ndondo".
 
Mlinzi wa mwenyekiti wa chadema hayupo makini ukiangalia hiyo video mtagundua makosa kibao
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
LUMUMBA MKAE KIMYA HUU MTEKENYO UTAZIDI ULE WA JIDE KWA GARDNER ..ze ndii ndii ndii
Eti wivu mnaongeza gharasa kiukweli..
.....
....Gharasha ungekesha hapa cho
 
Mtoto achekwaye siku zote ndio mtoto. Hawa watu waliponda xn majukwaan cdm Leo the same part kmekuwa kimbilio
 
CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari na kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo msanii Wema Sepetu.

View attachment 473709
Mbowe na Lissu leo wanawasilisha ile hati ya mashitaka iliyorekebishwa na kumuongeza Mwanasheria Mkuu. Wema Sepetu yupo Katikati ya Esther Bulaya na Mbowe hii leo. Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura
View attachment 473719 View attachment 473718
Baada ya hapa Mbowe ataongea na Waandishi.

Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani. Msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kukutwa na bangi. Kesi hiyo ya Wema iliahirishwa hadi Machi 15.

Alikalishwa jembe la watanzania ambalo mimi pia nlimukubali mh. Lowasa itakuwa kwa wema[emoji2] [emoji1] [emoji1] I can now see ni kivipi chadema wamekosa muelekeo kwa kutumia serious issue kuwa siasa na kuanza kutetea watu waovu[emoji49] [emoji49] [emoji49]

Sent from my G630-U10 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom