Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 5,308
- 14,207
Mwimbaji wa Bongofleva na mwanachama wa JamiiForums, Haitham Kim amefariki dunia hospitali ya Temeke alipokuwa anapatiwa matibabu. Meneja wake amethibitisha.
Hivi karibuni Wasanii na Wadau wengine walianzisha kampeni ya kusaidia kuchangisha pesa kwa ajili ya matibabu yake.
Bryson ambaye ni Mume wa Marehemu alisema hali ya Haitham ilibadilika ghafla siku saba zilizopita akisumbuliwa na upumuaji ambapo ilianza kama homa ya kawaida lakini baadaye akawa anakosa pumzi hadi kupelekea kuwekewa mashine na kuchomwa sindano za kila siku zilizogharimu shilingi laki 7 kwa siku.