DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,154
Msanii wa muziki Shilole amepata ajali ya gari akiwa njiani kurejea Dodoma kutoka mkoani Kigoma, alikokuwa ameshiriki katika shughuli ya kijamii iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Babalevo, iliyojulikana kama Pilau Day.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Mbunge wa Kigoma Mjini Baba Levo amethibitisha tukio hilo akisema
“Jana usiku dada yangu Shilole alipokuwa anatoka Kigoma kurudi Dodoma alipata ajali ya gari aina ya Alphard baada ya kugonga ng’ombe maeneo ya Maragalasi. Tunafuatilia afya yake kwa ukaribu, kwa sasa anaendelea kupata matibabu Tabora.”
Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali ya afya ya Shilole inaendelea kufuatiliwa kwa karibu huku akiendelea kupatiwa matibabu mkoani Tabora.