Msanii Nikki Mbishi amuomba msamaha Kikwete

i think kabla hauja comment sikiliza na soma huo wimbo...then changanua muziki ni sanaa...JK alifanya mema yake akatuleta mpaka hapa tulipo.aliheshimu demokrasia,alitukanwa matusi yote aka heshimu katiba
JPM ana mwaka sema madudu yaliyopo katika serikali yakeni mengi kuliko mazuri aliyoyafanya.maana karudisha nidhamu makazini ila sheria kali anazotumia zinajenga na kubomoa zaidi
kama kuna mtu ana amini katika sekta ya elimu tunaenda sawa basi inabidi aende akafanye check up mirembe, sekta ya afya( madawa na chanjo) upungufu huu haukuwepo before,sakata la sukari nadhani unalikumbuka,maneno aliyozungumza baada ya kukusanya mabillion ya KAGERA, Tanzania ya viwanda inavyoenda , watu hatukufurahishwa na JK ila tulisahau kuwa muda unapita atakuja mwingine.
muziki mzuri...sorry JK maana niki alimponda enzi akiwa Raisi
Umenena ndugu
 
Huyu atakuwa alizoea kujiita msanii na kutofanya kazi zake kwa bidii, bali kutegemea kupokea bahasha za mamboz ya mkato. Ndio wale wale njia zao za kitumwa kujipatia mkato zimekufa, hapa kazi tu.

Mvivu mkubwa bila aibu, na aisome namba na bado. Anatia aibu wasanii wengine.
 
We miss baba lidhiwani bora ww tuligawana kasungura kadogo sasa tunasubiri kasungura kawe kambuzi ndyo tupewe wasalimie msoga ila tunakumiss
 


=====

Song: "I'M SORRY JK"

Hook:
It will one day make sense/Nikisema hakuna president kama JK/
Tanzania inakumiss yaani daily/
Kwa niaba ya wabongo I'M SORRY JK/

Lyrics:1
I'm sorry JK nimeona tu niseme/
Mzuka huu niliupata nikiwa Juu Kijenge/
Mikopo hakuna tena huendi chuo kikuu kizembe/
Bungeni wanalewa wanabonga tu king'eng'e/
Wakitwanga wanatamba wakisanda wanatubu/
Simuoni tena Jay tangu akutane Sugu/
Scorpion amegeuka ghostface mwema/
Aliyeota Rais atakufa anaitwa Godbless Lema/
RC na Wasafi uswazi madefender/
Hapa Kazi tu mtaani njaa kali sio sinema/
Kama kuisoma tushaisoma namba/Ungegombea awamu ya tatu ingekuwa bora labda/

Lyrics:2
Enzi za bibi cheka wengi walikuita babu cheka/
Hawakujua kuwa nyakati zinakuja nakusepa/
Ulivunga wakibeza kuwa unapenda sana bata/
Na kiki ka" Makonda za Wasafi kuwafuata/
Wabongo watakumbuka kwenye sekta ya michezo/
Mpaka Taifa Stars nayo ikaonesha mauwezo/
Ukaongeza vigezo nyenzo matengenezo/
Leo Samatta ndo kinara na hachezi soka la dezo/
Tuzungumze magazeti Bunge wanaedit/
Hakuna mikakati bwana kumbe wanaekti/
Demokrasia demoghasia za Field Force/
Wengi wanafear ukweli kuwaambia Unju siogopi/
Mabenki yanafilisika madeni yanamimika/
Hali imekuwa ngumu hadi wageni wanasikitika/
Hatusheshi na shisha yaani sio fresh inatisha/
Bar mwisho saa sita siku hizi hatukeshi kabisa/

Lyrics:3
Kila taarifa ya habari leo JPM/
Pesa imepotea kimazingara David Blaine/
Waathirika hawaelewi juu ya mipango ya Bukoba/
Tetemeko wasije kula michango ya Msoga/
Tumekosa usitupe laana tucorrect/
Weka kando chama tuwe wana tuconnect/
Hela imefichwa nyuma ya Pazia la viwanda/
Njoo Sogodo uone Tanzania ya vibanda/
Uone chafu moja na askari mia wakisanda/
Chocho za Panya Road mixer pwiya la miganja/
Kuna nyakati nilikudiss JK/
Now I'm calling for the peace, DAMN! We miss JK/

By Nikki Mbishi 2017

Wasanii gani hawa? Walidhani nchi inaweza endelea kwa mistari ya sifa? Ahadi kibao! Nitawanunulia studio. So what? Tusome tukiwa studio wakati madarasa hayana madawati! toeni uchafu huu!
 
Samahani kwenda nje kidogo ya mada, hivi kesi ya uchochezi adhabu yake huwa ni nini kwa mjibu wa sheria zetu
Adhabu yake unakopeshwa milioni 10 kwa ubunifu wa unachokisema na kukiamini amacho ni tofauti na kila we ndugu unachoamini.

Nafikiri nimekujibu, na utaridhika. Vinginevyo fungua ukurasa wa 100 wa kitabu cha Sheria za demokrasia ya kweli by Geoge Utamwiko/ New edition.
 
Sina ujuzi wa kuiweka hapa ila tayari imezagaa mitandao yote.

Ngoma hii imeeleza wazi mazuri ya Jk ambayo hatukuyaona kwa wakati ule na kuuponda utawala wa sasa wazi wazi na kusema si Tanzania ya viwanda bali ni ya vibanda, hivyo kumuomba msamaha Jk kwa kuwa alikuja lakini hatukumtambua.

Ndani ya ngoma hii Nikki amesikitika sana kuwa uchumi umeyumba, ma bank yamefilisika na ni utawala wa mabavu kwa kutumia polisi.

Nikki mbishi ni msanii wa kwanza kabisa kujitoa mhanga ndani ya utawala huu huku wenzake wengi kama kina Roma wakisanda.
 
Sina ujuzi wa kuiweka hapa ila tayari imezagaa mitandao yote.

Ngoma hii imeeleza wazi mazuri ya Jk ambayo hatukuyaona kwa wakati ule na kuuponda utawala wa sasa wazi wazi na kusema si Tanzania ya viwanda bali ni ya vibanda, hivyo kumuomba msamaha Jk kwa kuwa alikuja lakini hatukumtambua.

Ndani ya ngoma hii Nikki amesikitika sana kuwa uchumi umeyumba, ma bank yamefilisika na ni utawala wa mabavu kwa kutumia polisi.

Nikki mbishi ni msanii wa kwanza kabisa kujitoa mhanga ndani ya utawala huu huku wenzake wengi kama kina Roma wakisanda.
Nimeingia Google na kuusikiliza nimebaki kinywa wazi! Amesema yale yanayoogopwa kusemwa na wengi kipindi hiki.
 
Kama umesikiljiza wimbo mpya wa Nikki mbishi tuzungumzie alichokisema katika mitazamo yote hasi na chanya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom