Msanii Kalapina kutembeza kichapo bungeni

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,272
27,631
Kama nafanikiwa kuingia Bungeni kwa mambo kama haya ninavyoyaona WABUNGE nitawapiga sana ngumi: PINA


Katika sakata linaloendelea hivi sasa bungeni juu ya pesa za Tegeta Escrow kuwa na sintofahamu ya ni za wananchi au la, maoni ya mwanahiphop aliewahi kujitangaza kugombea ubunge mwaka ujao Kala Pina" amesema haya

"Maoni yangu zile ni pesa sa umma ama si bana na repoti ya watu wasoni na yenyee imechunguza imetoa ripoti yake kwamba hawa watu inabidi wafilisiwe mali zao na wapandishwe kwenye mahakama ili kuweza kujibu tuhuma zinazowakabili, wanaotakiwa kutoa maelezo ya kina ambao ni mawaziri wamekuwa wakijiumauma sana ujue,

hawanyooshi maelezo. kwa namna moja au nyingine tunajikuta tunalipia umeme kila siku unapenda bei unit moja 500 sijui kutokana na michongo kama hiyo siyo, madeni yakwao wao baadhi ya mafisadi wachache lakini wanaleta ujanja ujanja mwisho wa siku madeni hayo yanakuja kumwangukia mwananchi wa kawaida.." amesema Kala Pina


"na mi najipanga kugombea jimbo la Kinondoni " aliendelea kusema Piana "sema nachosema mimi kama nafanikiwa kuingia Bungeni kwa mambo kama haya ninayoyaona wabunge ntawapiga sana watu ngumi b ungeni kwasababu masihara mwengi, ntatumia nguvu zangu za ziada kukabiliana na mafisadi"

Chanzo:djfettytz
 

Amezoea kuwapiga mateja kina Chid anajiona Mayweather siyo?


 
kalapina jiangalie ndg yangu,kuna baadhi ya watu kule mjengoni wanapiga ngumi nzito pasi na mfano.

kama huyu mzee wa msituni aka mzee wa vitoto vidogo vidogo,nasikia ana black belt toka japan karate academy.
1. John Komba akizungumza nyumbani kwake. Kushoto ni Mkewe  Salome Andrew Komba.jpg
john-komba.jpg
 
kura yangu ameshaikosa

tunahitaji mtu mwenye kuchukizwa na ufisadi kitu ambacho baadhi ya wanasiasa hawana kwa kauli yake hii ninampa kura yangu akaongeze nguvu bungeni.nadhani anatufaa kinondoni akipitia ukawa
 
huyu jamaa huwaga anatembeza vichapo sijawahi kusikia amekamatwa ina maana police wanamuogopa? ila kiboko yake ni wahuni wa Arusha!

kubwa jinga huyo, ana mambo ya kizamani sana, yaani katika vitu vyote vya kufanya ye anaona ngumi ndo ujanja. Kundi lake la Kikosi cha MIJINGA waliwahi kuwafanyia fujo na kuwapora TMK WANAUME FAMILY. T.M.K wakatoa ngoma na Ngwea wanamchana.... Juma Nature akamwambia " We unafikiri usela ni kuwapora watu, kulazimisha watu eti walale saa tatu ". KR akamchana anamwambia " Anko Dili zimekushinda sasa umeanza kuwanga ". Kabla ya hapo Ngwea aliwahi kumchana anamwambia " Unakaza sauti halafu unatoka nje ya biti "

Wimbo :https://www.youtube.com/watch?v=RY9oyxN3Wss
 
Sioni tatizo, kwa ujinga wanaoonesha wasomi bungeni naamini kabisa tunahitaji watu wenye hulka na akili tofauti... Kura yangu kapata
 
kubwa jinga huyo, ana mambo ya kizamani, yaani katika vitu vyote vya kufanya ye anaona ngumi ndo ujanja. Kikosi cha MIJINGA waliwahi kuwafanyia fujo na kuwapora TMK WANAUME FAMILY. T.M.K wakatoa ngoma na Ngwea wanamchana Juma Nature akamwambia " We unafikiri usela ni kuwapora watu, kulazimisha watu eti walale saa tatu ". KR akamchana anamwambia " Dili zimekushinda sasa umeanza kuwanga ". Kabla ya hapo Ngwea aliwahi kumchana anamwambia " Unakaza sauti halafu unatoka nje ya biti "

Wimbo :https://www.youtube.com/watch?v=RY9oyxN3Wss

Acha hao kuna ally van damme alimkimbia sweet corner magomeni kwenye ulingo
siku nyingine alikuja na bastola huyu ni chizi
 
Back
Top Bottom