Tunavuna tulichopanda, nasimama na Rais wangu

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
KILA siku nashuhudia wananchi wenzangu wakikalamika. Natamani kujibu. Naacha. Natamani kuwakumbusha wananchi wenzangu. Naacha. Nasema mbona sisi ni wepesi wa kusahau? Natamani kuwakumbusha wabunge wenzangu. Naacha. Nasema name sasa nipo kwenye serikali. Ni mtunga sera, ni mfanya maamuzi, nikisema watasema huyu ni 'naibu waziri'. Lakini kwa kweli nina hamu na shauku ya kuzungumza na wananchi wenzangu. Nami nitoe yangu ya moyoni. Kama mwananchi mwingine yeyote yule tu. Nina haki hiyo. Haki yangu inalindwa na katiba pamoja na sheria za nchi yetu.

Leo nimeona acha nipumue kidogo. Niseme. Niuvue u-serikali wangu. Niseme kama mwananchi mwingine yeyote yule. Nianze kwa kuweka wazi kabisa hapa, kwamba; haya ni yangu. Si ya serikali.

Serikali ni ya Rais Dk. John Magufuli, tumempa dhamana, ndiyo. Hili halibishaniwi. Tumempa kazi, ndiyo. Hili pia halibishaniwi. Lakini kazi hii anaifanyaje? Tunazijua changamoto anazokumbana nazo? Je, ana nia ya kuzitatua? Ni maswali ambayo yanastahili majibu. Kwenye makala hii nitajaribu kuyafafanua kidogo kwa mtazamo wangu kadri nitakavyojaaliwa.

Pamoja na kumpa dhamana Rais wetu, ni lazima tufahamu kuwa nasi tuna wajibu wa kutimiza kwa taifa letu. Tuna kazi ya kufanya kumsaidia Rais wetu kubeba mzigo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwenye taifa letu. Tusimuachie huu mzigo peke yake. Tuubebe sote.

Nchi ina changamoto nyingi sana, siyo kwamba Rais ama serikali yake haizifahamu ama haina nia ya kuzitatua, ama Rais Magufuli amesinzia, ama anastarehe; kila siku anahangaika kukuna kichwa, usiku na mchana kuzitafutia ufumbuzi. Nadhani hili halina ubishani sana kwa mpenda kweli. Binafsi, sina shaka kabisa juu ya uwepo wa nia thabiti ya kuleta mapinduzi. Sina.

Kwenye biashara ya kujenga nchi changamoto haziishi siku moja. Ukimaliza moja, nyingine inaibuka, na nyingine zinazaliwa kutokana na majawabu ya changamoto uliyoitatua.

Hivi karibuni nilisema kuhusu mfumo wa afya wa nchi kubwa kama ya Marekani kuwa na changamoto ya kuwabagua watu masikini na wale wa tabaka la kati na kwamba unajenga matabaka makubwa sana yanayowanyima fursa sawa baadhi ya watu kwenye jamii. Na kwamba ObamaCare inajaribu kutoa majibu yanayolenga kuleta usawa kwa kuwabana wenye kipato cha juu ili kuwahudumia wenye kipato cha chini. Tayari imeonekana kuwa kuna changamoto za kuwakamua zaidi watu wa daraja la kati, badala ya wale wa tabaka la juu kama 'design' na muundo wa awali ulivyolenga, kwa kuwatwisha mzigo wa watu masikini, na kwamba mpango huu kwa baadaye hautohimilika. Bado wanaendelea kubishana! Juzi tumeshuhudia Rais Donald Trump wa Marekani amekwama kwenye jaribio la kuurekebisha. Kazi ya kutatua changamoto ipo na inaendelea kwenye taifa kubwa la Marekani lenye miaka zaidi ya 200 ya demokrasia.

Mfano, tazama changamoto mpya iliyokuja na sera ya CCM kutoa elimu bure mpaka kidato cha nne. Tamko hili la kisera limeleta changamoto nyingi za kiutekelezaji. Kwanza, limeleta urahisi kwa familia nyingi kuona hakuna sababu ya watoto wao, hata mmoja, kukosa elimu hii ya msingi. Wakati tunapitisha sera hii hatukujua kuwa kuna watoto wengi kiasi hiki tunachoshuhudia sasa walikuwa wakikosa fursa (missed opportunity) ya elimu kwa sababu ya gharama ndogo ndogo.

Tumeondoa gharama hizi tumekutana na ongezeko kubwa la watoto kuandikishwa shule. Mlipuko wa wanafunzi kuingia darasa la kwanza kwenye shule za msingi kwa wingi umezaa changamoto mpya za upungufu wa madawati, vyumba vya madarasa, idadi ya matundu ya vyoo, idadi ya walimu na mengine ya aina hiyo. Tukumbuke vizuri kuwa juzi tu hapa serikali ilikuwa inaajiri walimu kwa kipaumbele cha juu kabisa kwa miaka mitano mfululizo, ambapo walimu wote waliohitimu waliajiriwa!

Uchumi wetu unakua kwa kasi nzuri, kama ni ndege ndiyo inaongeza kasi ili ipate nguvu ya kupaa; bado uchumi hauna uwezo wa kuhimili mahitaji yetu 'yote' ya matumizi ya kila siku kama tunavyotamani, achilia mbali ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kadri tunavyodiriki kuota ndoto zetu. Mfano, kwenye ajira bajeti ya watumishi (wage bill) inaongezeka kila siku. Hili tu ni sehemu ya mahitaji makubwa na nyeti sana kiuchumi.

Zamani nilipokuwa mbunge – bila u-serikali, kilichokuwa kinanikera ni kwamba, pamoja na changamoto tulizonazo watu wengine walikuwa wanaishi kama wako peponi na wengine wanaishi kama wako motoni, hawa wa peponi wengi wao walifika huko kwa wizi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi za umma, siyo kwa uchapakazi wala ubunifu. Tena bila huruma kwa waliokuwa wakiishi kama vile wapo motoni. Huku wakiwa na dhamana ya kuwaondoa motoni wananchi wenzetu waliobaki huko!

Leo Rais Magufuli anakosolewa kwa kubana mianya ya rushwa, wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka na uchumi wa ujanja ujanja, mambo ambayo nakumbuka mimi na wenzangu kwenye Bunge la 10 tuliyapigia kelele kwa nguvu sana, tena kwa uzalendo wa hali ya juu na bila hata kuogopa kuwa tunapowashughulikia hawa ndugu wa peponi tunashusha imani ya wananchi kwa chama chetu pia.

Sisi tuliamini kwamba hawa ni lazima tushughulike nao. Tuwaondoe ili kukisafisha chama. Tulikuwa wachache sana. Tulipigana kuwaondoa watu wa aina hiyo na tuliwatoa. Na kwa kiasi kikubwa tulimkataa mwana-CCM mwenzetu, Edward Lowassa, kwa sababu tuliamini yeye na kundi lake (lilikokuwa kubwa ndani ya CCM) wangegawana na kuimaliza nchi yetu. Ilihitaji uwe ‘mwendawazimu’ kumkataa ndugu huyu. Lakini tulikita mguu waziwazi na kumkataa.

Tulionekana wasaliti wenye kustahili kufukuzwa katika chama. Na wengine tulikifikiriwa kufukuzwa chama na baadhi ya viongozi wapuuzi, wakiamini viongozi wa aina yetu hawakutakiwa, mpaka vikao vya juu vilipopuuzia ndipo tulipona. Tulifika huku kwa sababu kulikuwa na kundi la wachache waliokuwa wanafaidika na mfumo uliokuwepo, hivyo waliona sisi tunachafua maji yao ya kuogelea. Mpaka alipokuja Kanali (mstaafu) Abdulrahaman Kinana na kutupongeza wabunge wa aina yetu akisema, jitengeni na ushenzi wa baadhi ya watu wanaochafua taswira ya serikali ya chama chetu ndipo tulipopumua.

Kuna njia mbili tu zinazoweza kutumika kutatua changamoto zinazotukabili nchini kwa uhakika. Nasema kwa uhakika kwa sababu ni aibu kubwa kuinjika chungu cha ugali nyumbani kwako na kuwapa wanao uhakika wa ugali kumbe unategemea unga wa kuomba ama kuazima kutoka kwa jirani! Vipi akikunyima?

Ukichaguliwa kuwa Rais, moja kwa moja unakuwa na ahadi sambamba na dhamana kubwa mabegani mwako, una hamu na shauku kubwa ya kuanza kuzitekeleza, una ndoto nyingi za kutaka kuleta mapinduzi kwenye nchi yako kwa heshima kubwa uliyopewa, unataka kuacha alama isiyofutika!

Unachungulia hazina unakutana na madeni, mahitaji, utaratibu na masharti; unatazama makusanyo uliyonayo. Unachoka kabisa! Nguvu zinakuishia kabisa. Hamasa yako inavurugwa na uhalisia.

Unakumbuka ushauri wa wabunge kila siku bungeni – 'tubane matumizi…tukate matumizi yasiyo ya lazima…tuweke kodi hii…ile…serikali ni dhaifu kwenye kukusanya kodi….tutanue wigo wa kodi….kwa nini Tanzania na utajiri wote huu bado tunategemea misaada kutoka nje kwenye bajeti yetu – mwishowe tutapewa pesa zenye masharti magumu (mambo ya ushoga nk)…tuanzishe mahakama maalumu ya mafisadi, nk!'

Unaanza kutekeleza yote haya kama yalivyo – unalaumiwa! Tusiwe wepesi wa kusahau. Tusiwe wanafiki. Ni nani hakuwahi kukerwa na watumishi hewa? Ni nani hakukerwa na safari za nje? Ni nani alilalamika kuhusu uwepo wa uwiano wa bajeti ya matumizi ya kawaida kubwa kuliko bajeti ya maendeleo? Rais Magufuli tangu aingie madarakani, haya ndiyo maswali anayojaribu kuyapatia majawabu.

Njia za kupata fedha za kutatua changamoto kwa uhakika ni hizi mbili: mosi – ubane matumizi, ili unachokusanya ukipeleke kwingine kikasaidie kupunguza changamoto zako. Ndicho anachokifanya Rais Magufuli kila siku tangu amechaguliwa. Sisi wenye macho ya kizalendo na kiuhalisia tunaona jitihada zake.

Pili, ukusanye zaidi na ubane mianya ya kuvuja kwa mapato. Ndicho kinachofanyika. Kwa mwaka unaoisha makusanyo ya mapato ya serikali yamepita malengo.

Kuna njia nyingine za kupata fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji yetu. Japokuwa haina washabiki wengi na inapigwa vita sana na watunga sheria na wanaharakati mara nyingi. Hii ni ile ya misaada kutoka kwa wafadhili na mikopo (ya ndani na nje). Hizi njia mbili zote zinapigiwa kelele sana kwa sababu; kwanza, kwamba itasababisha tupewe pesa zenye masharti magumu tusiyoyaweza, na nyingine, kwamba deni letu linakua sana – mwisho halitohimilika! Njia ya mikopo ya ndani wanasema inaumiza uchumi wetu.

Kwa sasa tunachotakiwa kufanya ni kuongeza uzalishaji ili wigo wa serikali kukusanya kipato chake utanuke zaidi. Na hili si la Rais peke yake, ni letu sote. Kila mtu awe mzalishaji. Shime twende shambani, twende viwandani, twende sokoni!

Kwangu mimi, kama hali inakuwa ngumu kwetu sote na iwe tu, ili mradi wasiwepo kati yetu wanaofaidika na serikali ya watu huku wengine hawana chakula, hawana dawa, hawana madawati. Napenda usawa, haki na uwajibikaji. Namuunga mkono Rais wangu kwa sababu analeta usawa kwa watu wetu. Nasimama na Rais wangu.

Kwangu hili la usawa, haki na uwajibikaji kwa wote ni kubwa sana. Linagusa historia ya machozi, jasho na damu ya makuzi yenye maumivu makali na furaha nyakati nyingine kipindi cha makuzi yangu na watoto wengine wa masikini kwenye Tanzania ya miaka ya 1970 na 1980. Maana mimi ni zao la mfumo uliotoa haki na usawa kwa wote. Bila Tanzania hiyo mtoto wa masikini kama mimi, hata ningekuwa na bidii na kipaji cha namna gani, nisingefikia kusoma mpaka kuwa daktari, na hata kufikia kutamani kugombea nafasi ya ubunge. Sitaki kufikiri labda ningekuwa wapi mimi leo!

Tufanye kazi kwa bidii na maarifa, zama zimebadilika. Hakuna mtu atakayethubutu kutuibia kwenye zama hizi. Walau hili ni la uhakika.

Na zile kesi za rushwa, wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa mali ya umma sasa zifike kwenye mahakama yake na kesi zikimbie ili tuone haki ikitendeka.

Huwezi kupanda mchicha ukasubiri ukuwe kwa matarajio ya kuvuna bangi. Tulimpa kura zetu Magufuli, mwenye rekodi ya uchapakazi, uaminifu na uadilifu, basi tutarajie uchapakazi, uaminifu na uadilifu; mwenye rekodi ya kuacha alama ya kazi yake, basi ni lazima tutarajie kuona kazi itakayoacha alama. Si vinginevyo.

Tungempa mla rushwa, tungeshuhudia rushwa. Tumevuna tulichopanda. Tumevuna kazi tu. Tutulie tuone kazi. Tuamke tufanye kazi. Tushiriki kujenga Tanzania tuitakayo.

Mwandishi wa makala hii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Raia Mwema
 
Lazima ulinde kibarua mh Kigwangala!Hoja zako ni nyepesi mno!Ruhusuni watu wawe na platform ya kuzungumza,kuna mengi mnayoyakosa!
 
hivi kuna watu walipitiwa na somo la kusamalizei vitu, gazeti looote ndani upupu
 
Teh teh teh teh
Ndefu mpaka kero. Zile pesa zetu za Acacia lini watatupa au ilikuwa kiki ya msimu?
 
Tupo pamoja kaka fanya kazi tujenge nchi yetu,watu uwa wepesi wa kusahau na awapendi maslahi yao yaguswe tena maslahi ya kifisadi,rushwa,ujanja ujanja kila mtu avune jasho lake ,tumeache raisi afanye kazi tuiunge mkono serikali yetu
 
Atakayesoma na kuelewa aje atupe Summary na naomba ani tag
 
Hivi ni kipi hasa mlichobana matumizi?! Moja ya mambo ambayo nchi hii yamekuwa yakilalamikiwa kama matumizi ya hovyo ya serikali ni magari ya bei mbaya ambayo pia yanatumia mafuta mengi!

SWALI 1: Je, unakubali magari yanayotumika kwa mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa hadi ni ma-DC ni ya gharama sana kwa kuzingatia uchumi wetu au kelele zile hazikuwa za msingi?! Kama magari yanayotumika yanaigharimu sana serikali; serikali hii inayobana matumizi imefanya nini cha maana kwenye hilo?

Kubana huku kwa matumizi ni kule mlikutuonesha kwenye picha wajumbe wa Baraza la Mawaziri wakila chips mayai kwenye kikao wakati wengine wametumia pesa nyingi kutoka Dodoma hadi Dar es salaam ambako anaishia kubana matumizi kwenye kula chips mayai?

SWALI 2: Unasema kwamba hamkufahamu ni namna gani kuodoa ada mashuleni kungeleta wimbi la wanafunzi wapya: Ina maana kwa miaka zaidi ya 50 serikali ya CCM ilikuwa haifahamu idadi ya watu wake, kwenye hii context watoto wanaotakiwa kuandikishwa shule?! Ile sensa inayotumika mabilioni ya pesa kuifanya ina maana gani sasa ikiwa bado inashindwa kutoa takwimu sahii ya makundi mbalimbali ya watu?!

Swali la nyongeza: How come unasema hamkufahamu idadi ya kubwa ya wanafunzi ambao hatimae wangeandikishwa ikiwa lengo la kutoa ada mashuleni ilikuwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi?!

SWALI 3: Unakiri kwamba idadi kubwa ya wanafunzi imeongeza changamoto nyingine ya ukosefu wa waalimu! Kwa kumbukumbu zangu, miaka 2+ imepita na serikali bado haijaajiri walimu!! Nitaamini vipi kwamba serikali ipo concerned na hizo changamoto wakati hata changamoto ya wazi kabisa kama ya ukosefu wa walimu inaonekana?

Swali la ziada: Wengi wanaamini moja ya matatizo ya serikali yenu ni kushindwa kufahamu muanze na kipi kisha kifuate kipi... one word, VIPAUMBELE! Hapo juu unadai
Njia za kupata fedha za kutatua changamoto kwa uhakika ni hizi mbili: mosi – ubane matumizi, ili unachokusanya ukipeleke kwingine kikasaidie kupunguza changamoto zako. Ndicho anachokifanya Rais Magufuli kila siku tangu amechaguliwa.
Nakubaliana na wewe kwa 101%! Lakini je, ni kweli JPM anafanya hayo uliyosema? Kwa maoni yako wewe binafsi: Unadhani changamoto kubwa ya Watanzania ilikuwa ni ukosefu wa usafiri wa anga uliopelekea kununua ndege au upungufu wa hao walimu uliokiri na bila shaka ukosefu wa madaktari na manesi?

Kama changamoto ilikuwa ni usafiri wa anga... unaweza kunitajia jambo moja TU ambalo lilikuwa linashindwa kufanyika kwa sababu tu ATCL hawakuwa na ndege?

Aidha umesema:
Kwa sasa tunachotakiwa kufanya ni kuongeza uzalishaji ili wigo wa serikali kukusanya kipato chake utanuke zaidi. Na hili si la Rais peke yake, ni letu sote. Kila mtu awe mzalishaji.
Mwanzoni kabisa mwa utawala wa JPM mtu hakuhitaji kuwa mtalaamu sana kuona ni namna gani private sector ilikuwa inaelekea hatarini!!!

Siku za mwanzo tulipokuwa tunaongelea hatari inayoielekea microeconomic sector, wale wenzangu na mimi walichofanya ni kutukejeli kwamba tulizoea kuishi kwa madili wakati wengine hatujawahi hata siku moja kula pesa ya serikali directly mbali na ku-enjoy huduma zake! Hata hivyo, yale yale tuliyokuwa tunayasema hivi sasa yapo wazi!!!

Now tell me: Ni kipi kilichofanywa cha ku-stimulate ukuaji wa microeconomic sector zaidi ya kuanza kuikamua hiyo sector kila upande bila ya kuonekana hiyo mipango ya ku-stimulate ukuaji wake?!

Mwisho:
Kwangu mimi, kama hali inakuwa ngumu kwetu sote na iwe tu, ili mradi wasiwepo kati yetu wanaofaidika na serikali ya watu huku wengine hawana chakula, hawana dawa, hawana madawati.
Kwangu mimi hii ni kauli iliyojaa elements za ujima hasa ikitoka kwa mtu aliye serikalini!! Na kwa hakika ni element hii ya kiujima ndiyo inayowafanya watu wawe wanapiga makofi hovyo hovyo kama mazuzu... kwamba, kama ni hali ngumu basi tupigike wote!!!

Kwangu hiyo ni kauli iliyojaa elements za ujima kwa sababu, serikali haitakiwi kushadadia kama wote kuwa na hali ngumu bassi poa tu kuliko wengine kuwa na hali nzuri na wengine kuwa na hali mbaya! Kinachotakiwa na serikali ni kuhakikisha watu wote wanakuwa na hali mzuri! Btw, hivi kwanini mnaamini kila aliyekuwa na maisha mazuri alikuwa na maisha mazuri kutokana na kuiba?

SWALI: Hivi kweli kabisa kutoka ndani ya nafsi yako unaamini wale waliokuwa wanaiibia serikali hivi sasa wanakiona cha mtema kuni?! SERIOUSLY? Hivi kabisa unaamini wale walioiba au kufaidika na Kagoda, Deep Green, EPA, Radar Scandal, Ndege ya serikali, Richmond, Escrow and the like hivi sasa hao watu wanaisoma namba kwa kuwa na maisha magumu?! Au unazungumzia hawa wala rushwa uchwara waliopo kwenye ofisi za serikali?! Hivi kabisa unaamini yule Kamishina wa TRA, Masamaki hivi sasa anaisoma namba?! Hivi kabisa unaamini familia ya Rugemalila hivi sasa inaisoma namba kwa kupigika?! Hivi kabisa unaamini yule aliyesema 10 million ni pesa ya mboga hivi sasa anaisoma namba?! Hivi kabisa unaamini Joka la Makengeza hivi sasa linaisoma namba?!

Swali la mwisho la ziada: Wadau huku mtaani wanaamini ununuzi wa ndege ni moja ya next EPA kwa hoja kwamba hata tenda ilikotangazwa hakufahamiki!!! Wewe ukiwa mtu wa serikalini unaweza kusema with confidence huku ukijua kabisa kwamba Mungu anakuona... Je, ununuzi wa zile ndege umefuata taratibu za manunuzi?!
 
Ndugu Kalulukalunde, wapinzani tulionao ambao kwa kiasi kikubwa ni CHADEMA sera yao iliyobaki ni "kosoa kosoa".

Hawana sera, hawana jipya, wivu umewashika kwamba kaka Magu anafanya kweli. Hawaelewi kwamba unaweza kuwa mpinzani kwa kuunga mkono mazuri yanayofanywa na serikali, provided yanapelekea maendeleo ya kweli ya wananchi walio wengi.

Ndo mana walianza kwa kulipa watu wapige propaganda kwenye mitandao ambazo hazing base yeyote. Sasa wanasubiri Lisu kasema nini kisha wana duplicate kwenye magroup mengine ya whatsap na mitandao mingine.
Kujenga hoja hawawezi zaidi ya matusi tu. Yaani akili zao zimeshikiliwa na kauli za viongozi, bila kuichambua wanaanza kuirudia Kama kasuku.

Wakati mwingine nikisoma comments zao nabaki nacheka kweli CHADEMA iligeuka baada ya gia angani!!
 
Bigup Chige, katika watu wanaolitendea haki jukwaa hili ww ni mmoja wapo. Hiyo post yako hapo juu huwezi choka kuisoma kwa mtu anayeelewa maana. Kwa ukweli kama huu sioni haja ya kuandamani iki kufikisha ujumbe kama huu. Kuna watu wanaandamana kwamba mkuu aongezewe muda na sisi wengine tunasema muda wa hilo bado sana kutokana na maelezo hayo hapo juu. Hali ya mwananchi wa kawaida inazidi kuwa mbaya na majibu halisi ya matatizo hayo ndio kama hayo aliyo nayo Hamis Kigwangwala. Anyway labda tutoe muda lakini naona hali ile ya uchumi kuyumba kama enza za Nyerere.

Cc: msemajikweli
 
KILA siku nashuhudia wananchi wenzangu wakikalamika. Natamani kujibu. Naacha. Natamani kuwakumbusha wananchi wenzangu. Naacha. Nasema mbona sisi ni wepesi wa kusahau? Natamani kuwakumbusha wabunge wenzangu. Naacha. Nasema name sasa nipo kwenye serikali. Ni mtunga sera, ni mfanya maamuzi, nikisema watasema huyu ni 'naibu waziri'. Lakini kwa kweli nina hamu na shauku ya kuzungumza na wananchi wenzangu. Nami nitoe yangu ya moyoni. Kama mwananchi mwingine yeyote yule tu. Nina haki hiyo. Haki yangu inalindwa na katiba pamoja na sheria za nchi yetu.
... Mheshimiwa si mwananchi mwingine yeyote yule, yeye ni Naibu Waziri. Na andiko lake analimiliki kama mtendaji wa Serikali!

Pamoja na kumpa dhamana Rais wetu, ni lazima tufahamu kuwa nasi tuna wajibu wa kutimiza kwa taifa letu. Tuna kazi ya kufanya kumsaidia Rais wetu kubeba mzigo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwenye taifa letu. Tusimuachie huu mzigo peke yake. Tuubebe sote.
... Kwanini abebe yeye mzigo? Hata wewe kwa maana hiyo. Sie ndio tunapaswa kufanya kazi, ninyi mtuongoze! Tena kwa upendo na busara.

Nchi ina changamoto nyingi sana, siyo kwamba Rais ama serikali yake haizifahamu ama haina nia ya kuzitatua, ama Rais Magufuli amesinzia, ama anastarehe; kila siku anahangaika kukuna kichwa, usiku na mchana kuzitafutia ufumbuzi. Nadhani hili halina ubishani sana kwa mpenda kweli. Binafsi, sina shaka kabisa juu ya uwepo wa nia thabiti ya kuleta mapinduzi. Sina.
... Unahubiria kwaya. Tunafahamu Rais anahangaika kila siku. Tunamwona!

Kwenye biashara ya kujenga nchi changamoto haziishi siku moja. Ukimaliza moja, nyingine inaibuka, na nyingine zinazaliwa kutokana na majawabu ya changamoto uliyoitatua.
... Hamna siku zitakwisha, mpaka mwisho wa Dunia! Kitu cha muhimu ni kuzitatua moja baada ya nyingine. Mtafanya kipande chenu mtamaliza, watakuja wengine nao watafanya kipande chao. Kazi itaendelea!

Hivi karibuni nilisema kuhusu mfumo wa afya wa nchi kubwa kama ya Marekani kuwa na changamoto ya kuwabagua watu masikini na wale wa tabaka la kati na kwamba unajenga matabaka makubwa sana yanayowanyima fursa sawa baadhi ya watu kwenye jamii. Na kwamba ObamaCare inajaribu kutoa majibu yanayolenga kuleta usawa kwa kuwabana wenye kipato cha juu ili kuwahudumia wenye kipato cha chini. Tayari imeonekana kuwa kuna changamoto za kuwakamua zaidi watu wa daraja la kati, badala ya wale wa tabaka la juu kama 'design' na muundo wa awali ulivyolenga, kwa kuwatwisha mzigo wa watu masikini, na kwamba mpango huu kwa baadaye hautohimilika. Bado wanaendelea kubishana! Juzi tumeshuhudia Rais Donald Trump wa Marekani amekwama kwenye jaribio la kuurekebisha. Kazi ya kutatua changamoto ipo na inaendelea kwenye taifa kubwa la Marekani lenye miaka zaidi ya 200 ya demokrasia.
... Sidhani kama kuna unafahamu wa kutosha kwa kinachoendelea katika mjadala wa ku-repeal and replace Affordable Care Act. Siasa ni nyingi na Republicans kwa kipindi cha miaka saba -toka walipopinga kupitishwa kwa ACA- hawajawahi kuwa na mpango mbadala wa maana.

... Trump hajawahi kuwa na mpango wa kurekebisha ACA. Mpango wake ni repeal and replace! Hata hivyo hawajajiandaa -in the real sense of the word- na hawana mpango madhubuti wa kutimiza ahadi hiyo.

Mfano, tazama changamoto mpya iliyokuja na sera ya CCM kutoa elimu bure mpaka kidato cha nne. Tamko hili la kisera limeleta changamoto nyingi za kiutekelezaji. Kwanza, limeleta urahisi kwa familia nyingi kuona hakuna sababu ya watoto wao, hata mmoja, kukosa elimu hii ya msingi. Wakati tunapitisha sera hii hatukujua kuwa kuna watoto wengi kiasi hiki tunachoshuhudia sasa walikuwa wakikosa fursa (missed opportunity) ya elimu kwa sababu ya gharama ndogo ndogo.
... It was so obvious kwamba kutakuwa na watoto wengi -kushinda uwezo wa shule- pale elimu itakapofanywa "bure". Usiseme hukujua! Hint; Sensa na tafiti kwenye sekta ya elimu zipo muda mrefu.

Tumeondoa gharama hizi tumekutana na ongezeko kubwa la watoto kuandikishwa shule. Mlipuko wa wanafunzi kuingia darasa la kwanza kwenye shule za msingi kwa wingi umezaa changamoto mpya za upungufu wa madawati, vyumba vya madarasa, idadi ya matundu ya vyoo, idadi ya walimu na mengine ya aina hiyo. Tukumbuke vizuri kuwa juzi tu hapa serikali ilikuwa inaajiri walimu kwa kipaumbele cha juu kabisa kwa miaka mitano mfululizo, ambapo walimu wote waliohitimu waliajiriwa!
... Upungufu wa madawati upo muda mrefu sasa! JICA imeshafadhili ujenzi wa vyoo katika mashule kadhaa miaka ya nyuma. Changamoto hizi zipo toka tumepata uhuru. Zitaendelea kuwapo! Kitu cha muhimu ni kuzipunguza!

Uchumi wetu unakua kwa kasi nzuri, kama ni ndege ndiyo inaongeza kasi ili ipate nguvu ya kupaa; bado uchumi hauna uwezo wa kuhimili mahitaji yetu 'yote' ya matumizi ya kila siku kama tunavyotamani, achilia mbali ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kadri tunavyodiriki kuota ndoto zetu. Mfano, kwenye ajira bajeti ya watumishi (wage bill) inaongezeka kila siku. Hili tu ni sehemu ya mahitaji makubwa na nyeti sana kiuchumi.
... Unasoma ripoti za Benki Kuu?

Zamani nilipokuwa mbunge – bila u-serikali, kilichokuwa kinanikera ni kwamba, pamoja na changamoto tulizonazo watu wengine walikuwa wanaishi kama wako peponi na wengine wanaishi kama wako motoni, hawa wa peponi wengi wao walifika huko kwa wizi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi za umma, siyo kwa uchapakazi wala ubunifu. Tena bila huruma kwa waliokuwa wakiishi kama vile wapo motoni. Huku wakiwa na dhamana ya kuwaondoa motoni wananchi wenzetu waliobaki huko!
... Duniani matabaka huwapo kutokana na nafasi katika jamii, uwezo na juhudi za mtu binafsi, ugawaji wa keki ya taifa, n.k. Matabaka yataendelea kuwapo, kitu cha msingi ni tofauti kati yake. Tofauti haitakiwi kuwa kubwa mno.

... Wewe una maisha mazuri mno kuliko mwalimu wa shule ya msingi kijijini kule unakotokea. Si kosa lako, ni hali ya Dunia!

Kuna njia mbili tu zinazoweza kutumika kutatua changamoto zinazotukabili nchini kwa uhakika. Nasema kwa uhakika kwa sababu ni aibu kubwa kuinjika chungu cha ugali nyumbani kwako na kuwapa wanao uhakika wa ugali kumbe unategemea unga wa kuomba ama kuazima kutoka kwa jirani! Vipi akikunyima?
... Kwanini uhinjike chungu wakati hakuna unga? Kuna haraka gani? Pata unga -haijalishi unaupataje- ndio uhinjike chungu. Watoto lazima wale! haijalishi unga umepatikana vipi, unless unawaacha wafe njaa!

Ukichaguliwa kuwa Rais, moja kwa moja unakuwa na ahadi sambamba na dhamana kubwa mabegani mwako, una hamu na shauku kubwa ya kuanza kuzitekeleza, una ndoto nyingi za kutaka kuleta mapinduzi kwenye nchi yako kwa heshima kubwa uliyopewa, unataka kuacha alama isiyofutika!
... And you must be realistic, as there is only so much you can do. Otherwise you may end up disillusioned!

Unakumbuka ushauri wa wabunge kila siku bungeni – 'tubane matumizi…tukate matumizi yasiyo ya lazima…tuweke kodi hii…ile…serikali ni dhaifu kwenye kukusanya kodi….tutanue wigo wa kodi….kwa nini Tanzania na utajiri wote huu bado tunategemea misaada kutoka nje kwenye bajeti yetu – mwishowe tutapewa pesa zenye masharti magumu (mambo ya ushoga nk)…tuanzishe mahakama maalumu ya mafisadi, nk!'
... Unaweza ukawa unamiliki ardhi kubwa yenye rutuba, lakini huna maarifa ya kulima au mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa kitakachotumia vya kutosha uwezo wa ardhi yako.

... Utajiri ulipo chini na juu ya ardhi bila nguvukazi bora yenye maarifa na ujuzi, hauna faida. Hautaweza kuvunwa na kutoa faida ya maana!

... Soko la kututajirisha liko wapi? Tunalifahamu na kulimudu vya kutosha? Tuna ushawishi wa kutosha?

Njia za kupata fedha za kutatua changamoto kwa uhakika ni hizi mbili: mosi – ubane matumizi, ili unachokusanya ukipeleke kwingine kikasaidie kupunguza changamoto zako. Ndicho anachokifanya Rais Magufuli kila siku tangu amechaguliwa. Sisi wenye macho ya kizalendo na kiuhalisia tunaona jitihada zake.

Pili, ukusanye zaidi na ubane mianya ya kuvuja kwa mapato. Ndicho kinachofanyika. Kwa mwaka unaoisha makusanyo ya mapato ya serikali yamepita malengo.
... Tatu, uhakikishe uzalishaji wa bidhaa na huduma unakua na kuongezeka, ili ukuze mapato ya Taifa!

Kuna njia nyingine za kupata fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji yetu. Japokuwa haina washabiki wengi na inapigwa vita sana na watunga sheria na wanaharakati mara nyingi. Hii ni ile ya misaada kutoka kwa wafadhili na mikopo (ya ndani na nje). Hizi njia mbili zote zinapigiwa kelele sana kwa sababu; kwanza, kwamba itasababisha tupewe pesa zenye masharti magumu tusiyoyaweza, na nyingine, kwamba deni letu linakua sana – mwisho halitohimilika! Njia ya mikopo ya ndani wanasema inaumiza uchumi wetu.
... Hii ni muhimu sana, kama inatumiwa ipasavyo! Unakumbuka The Marshall Plan? Unafahamu kwamba misaada na mikopo imeisaidia sana Rwanda?

... Tukipata msaada au mkopo wa kusambaza maji safi na salama D'salaam nzima, tukafanya kazi hiyo ipasavyo, tutapongezwa na kukumbukwa au tutashtumiwa na kupigiwa kelele?

... Kazi nzuri ikifanyika, hamna atakayefungua mdomo!

Kwangu hili la usawa, haki na uwajibikaji kwa wote ni kubwa sana. Linagusa historia ya machozi, jasho na damu ya makuzi yenye maumivu makali na furaha nyakati nyingine kipindi cha makuzi yangu na watoto wengine wa masikini kwenye Tanzania ya miaka ya 1970 na 1980. Maana mimi ni zao la mfumo uliotoa haki na usawa kwa wote. Bila Tanzania hiyo mtoto wa masikini kama mimi, hata ningekuwa na bidii na kipaji cha namna gani, nisingefikia kusoma mpaka kuwa daktari, na hata kufikia kutamani kugombea nafasi ya ubunge. Sitaki kufikiri labda ningekuwa wapi mimi leo!
... Bado kuna kazi kubwa ya kufanya hapa.

Tufanye kazi kwa bidii na maarifa, zama zimebadilika. Hakuna mtu atakayethubutu kutuibia kwenye zama hizi. Walau hili ni la uhakika.
... Not so fast. Wizi bado upo na utaendelea kuwapo. Vigilance is a must!
 
KILA siku nashuhudia wananchi wenzangu wakikalamika. Natamani kujibu. Naacha. Natamani kuwakumbusha wananchi wenzangu. Naacha. Nasema mbona sisi ni wepesi wa kusahau? Natamani kuwakumbusha wabunge wenzangu. Naacha. Nasema name sasa nipo kwenye serikali. Ni mtunga sera, ni mfanya maamuzi, nikisema watasema huyu ni 'naibu waziri'. Lakini kwa kweli nina hamu na shauku ya kuzungumza na wananchi wenzangu. Nami nitoe yangu ya moyoni. Kama mwananchi mwingine yeyote yule tu. Nina haki hiyo. Haki yangu inalindwa na katiba pamoja na sheria za nchi yetu.

Leo nimeona acha nipumue kidogo. Niseme. Niuvue u-serikali wangu. Niseme kama mwananchi mwingine yeyote yule. Nianze kwa kuweka wazi kabisa hapa, kwamba; haya ni yangu. Si ya serikali.

Serikali ni ya Rais Dk. John Magufuli, tumempa dhamana, ndiyo. Hili halibishaniwi. Tumempa kazi, ndiyo. Hili pia halibishaniwi. Lakini kazi hii anaifanyaje? Tunazijua changamoto anazokumbana nazo? Je, ana nia ya kuzitatua? Ni maswali ambayo yanastahili majibu. Kwenye makala hii nitajaribu kuyafafanua kidogo kwa mtazamo wangu kadri nitakavyojaaliwa.

Pamoja na kumpa dhamana Rais wetu, ni lazima tufahamu kuwa nasi tuna wajibu wa kutimiza kwa taifa letu. Tuna kazi ya kufanya kumsaidia Rais wetu kubeba mzigo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kwenye taifa letu. Tusimuachie huu mzigo peke yake. Tuubebe sote.

Nchi ina changamoto nyingi sana, siyo kwamba Rais ama serikali yake haizifahamu ama haina nia ya kuzitatua, ama Rais Magufuli amesinzia, ama anastarehe; kila siku anahangaika kukuna kichwa, usiku na mchana kuzitafutia ufumbuzi. Nadhani hili halina ubishani sana kwa mpenda kweli. Binafsi, sina shaka kabisa juu ya uwepo wa nia thabiti ya kuleta mapinduzi. Sina.

Kwenye biashara ya kujenga nchi changamoto haziishi siku moja. Ukimaliza moja, nyingine inaibuka, na nyingine zinazaliwa kutokana na majawabu ya changamoto uliyoitatua.

Hivi karibuni nilisema kuhusu mfumo wa afya wa nchi kubwa kama ya Marekani kuwa na changamoto ya kuwabagua watu masikini na wale wa tabaka la kati na kwamba unajenga matabaka makubwa sana yanayowanyima fursa sawa baadhi ya watu kwenye jamii. Na kwamba ObamaCare inajaribu kutoa majibu yanayolenga kuleta usawa kwa kuwabana wenye kipato cha juu ili kuwahudumia wenye kipato cha chini. Tayari imeonekana kuwa kuna changamoto za kuwakamua zaidi watu wa daraja la kati, badala ya wale wa tabaka la juu kama 'design' na muundo wa awali ulivyolenga, kwa kuwatwisha mzigo wa watu masikini, na kwamba mpango huu kwa baadaye hautohimilika. Bado wanaendelea kubishana! Juzi tumeshuhudia Rais Donald Trump wa Marekani amekwama kwenye jaribio la kuurekebisha. Kazi ya kutatua changamoto ipo na inaendelea kwenye taifa kubwa la Marekani lenye miaka zaidi ya 200 ya demokrasia.

Mfano, tazama changamoto mpya iliyokuja na sera ya CCM kutoa elimu bure mpaka kidato cha nne. Tamko hili la kisera limeleta changamoto nyingi za kiutekelezaji. Kwanza, limeleta urahisi kwa familia nyingi kuona hakuna sababu ya watoto wao, hata mmoja, kukosa elimu hii ya msingi. Wakati tunapitisha sera hii hatukujua kuwa kuna watoto wengi kiasi hiki tunachoshuhudia sasa walikuwa wakikosa fursa (missed opportunity) ya elimu kwa sababu ya gharama ndogo ndogo.

Tumeondoa gharama hizi tumekutana na ongezeko kubwa la watoto kuandikishwa shule. Mlipuko wa wanafunzi kuingia darasa la kwanza kwenye shule za msingi kwa wingi umezaa changamoto mpya za upungufu wa madawati, vyumba vya madarasa, idadi ya matundu ya vyoo, idadi ya walimu na mengine ya aina hiyo. Tukumbuke vizuri kuwa juzi tu hapa serikali ilikuwa inaajiri walimu kwa kipaumbele cha juu kabisa kwa miaka mitano mfululizo, ambapo walimu wote waliohitimu waliajiriwa!

Uchumi wetu unakua kwa kasi nzuri, kama ni ndege ndiyo inaongeza kasi ili ipate nguvu ya kupaa; bado uchumi hauna uwezo wa kuhimili mahitaji yetu 'yote' ya matumizi ya kila siku kama tunavyotamani, achilia mbali ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kadri tunavyodiriki kuota ndoto zetu. Mfano, kwenye ajira bajeti ya watumishi (wage bill) inaongezeka kila siku. Hili tu ni sehemu ya mahitaji makubwa na nyeti sana kiuchumi.

Zamani nilipokuwa mbunge – bila u-serikali, kilichokuwa kinanikera ni kwamba, pamoja na changamoto tulizonazo watu wengine walikuwa wanaishi kama wako peponi na wengine wanaishi kama wako motoni, hawa wa peponi wengi wao walifika huko kwa wizi, rushwa, ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi za umma, siyo kwa uchapakazi wala ubunifu. Tena bila huruma kwa waliokuwa wakiishi kama vile wapo motoni. Huku wakiwa na dhamana ya kuwaondoa motoni wananchi wenzetu waliobaki huko!

Leo Rais Magufuli anakosolewa kwa kubana mianya ya rushwa, wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka na uchumi wa ujanja ujanja, mambo ambayo nakumbuka mimi na wenzangu kwenye Bunge la 10 tuliyapigia kelele kwa nguvu sana, tena kwa uzalendo wa hali ya juu na bila hata kuogopa kuwa tunapowashughulikia hawa ndugu wa peponi tunashusha imani ya wananchi kwa chama chetu pia.

Sisi tuliamini kwamba hawa ni lazima tushughulike nao. Tuwaondoe ili kukisafisha chama. Tulikuwa wachache sana. Tulipigana kuwaondoa watu wa aina hiyo na tuliwatoa. Na kwa kiasi kikubwa tulimkataa mwana-CCM mwenzetu, Edward Lowassa, kwa sababu tuliamini yeye na kundi lake (lilikokuwa kubwa ndani ya CCM) wangegawana na kuimaliza nchi yetu. Ilihitaji uwe ‘mwendawazimu’ kumkataa ndugu huyu. Lakini tulikita mguu waziwazi na kumkataa.

Tulionekana wasaliti wenye kustahili kufukuzwa katika chama. Na wengine tulikifikiriwa kufukuzwa chama na baadhi ya viongozi wapuuzi, wakiamini viongozi wa aina yetu hawakutakiwa, mpaka vikao vya juu vilipopuuzia ndipo tulipona. Tulifika huku kwa sababu kulikuwa na kundi la wachache waliokuwa wanafaidika na mfumo uliokuwepo, hivyo waliona sisi tunachafua maji yao ya kuogelea. Mpaka alipokuja Kanali (mstaafu) Abdulrahaman Kinana na kutupongeza wabunge wa aina yetu akisema, jitengeni na ushenzi wa baadhi ya watu wanaochafua taswira ya serikali ya chama chetu ndipo tulipopumua.

Kuna njia mbili tu zinazoweza kutumika kutatua changamoto zinazotukabili nchini kwa uhakika. Nasema kwa uhakika kwa sababu ni aibu kubwa kuinjika chungu cha ugali nyumbani kwako na kuwapa wanao uhakika wa ugali kumbe unategemea unga wa kuomba ama kuazima kutoka kwa jirani! Vipi akikunyima?

Ukichaguliwa kuwa Rais, moja kwa moja unakuwa na ahadi sambamba na dhamana kubwa mabegani mwako, una hamu na shauku kubwa ya kuanza kuzitekeleza, una ndoto nyingi za kutaka kuleta mapinduzi kwenye nchi yako kwa heshima kubwa uliyopewa, unataka kuacha alama isiyofutika!

Unachungulia hazina unakutana na madeni, mahitaji, utaratibu na masharti; unatazama makusanyo uliyonayo. Unachoka kabisa! Nguvu zinakuishia kabisa. Hamasa yako inavurugwa na uhalisia.

Unakumbuka ushauri wa wabunge kila siku bungeni – 'tubane matumizi…tukate matumizi yasiyo ya lazima…tuweke kodi hii…ile…serikali ni dhaifu kwenye kukusanya kodi….tutanue wigo wa kodi….kwa nini Tanzania na utajiri wote huu bado tunategemea misaada kutoka nje kwenye bajeti yetu – mwishowe tutapewa pesa zenye masharti magumu (mambo ya ushoga nk)…tuanzishe mahakama maalumu ya mafisadi, nk!'

Unaanza kutekeleza yote haya kama yalivyo – unalaumiwa! Tusiwe wepesi wa kusahau. Tusiwe wanafiki. Ni nani hakuwahi kukerwa na watumishi hewa? Ni nani hakukerwa na safari za nje? Ni nani alilalamika kuhusu uwepo wa uwiano wa bajeti ya matumizi ya kawaida kubwa kuliko bajeti ya maendeleo? Rais Magufuli tangu aingie madarakani, haya ndiyo maswali anayojaribu kuyapatia majawabu.

Njia za kupata fedha za kutatua changamoto kwa uhakika ni hizi mbili: mosi – ubane matumizi, ili unachokusanya ukipeleke kwingine kikasaidie kupunguza changamoto zako. Ndicho anachokifanya Rais Magufuli kila siku tangu amechaguliwa. Sisi wenye macho ya kizalendo na kiuhalisia tunaona jitihada zake.

Pili, ukusanye zaidi na ubane mianya ya kuvuja kwa mapato. Ndicho kinachofanyika. Kwa mwaka unaoisha makusanyo ya mapato ya serikali yamepita malengo.

Kuna njia nyingine za kupata fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji yetu. Japokuwa haina washabiki wengi na inapigwa vita sana na watunga sheria na wanaharakati mara nyingi. Hii ni ile ya misaada kutoka kwa wafadhili na mikopo (ya ndani na nje). Hizi njia mbili zote zinapigiwa kelele sana kwa sababu; kwanza, kwamba itasababisha tupewe pesa zenye masharti magumu tusiyoyaweza, na nyingine, kwamba deni letu linakua sana – mwisho halitohimilika! Njia ya mikopo ya ndani wanasema inaumiza uchumi wetu.

Kwa sasa tunachotakiwa kufanya ni kuongeza uzalishaji ili wigo wa serikali kukusanya kipato chake utanuke zaidi. Na hili si la Rais peke yake, ni letu sote. Kila mtu awe mzalishaji. Shime twende shambani, twende viwandani, twende sokoni!

Kwangu mimi, kama hali inakuwa ngumu kwetu sote na iwe tu, ili mradi wasiwepo kati yetu wanaofaidika na serikali ya watu huku wengine hawana chakula, hawana dawa, hawana madawati. Napenda usawa, haki na uwajibikaji. Namuunga mkono Rais wangu kwa sababu analeta usawa kwa watu wetu. Nasimama na Rais wangu.

Kwangu hili la usawa, haki na uwajibikaji kwa wote ni kubwa sana. Linagusa historia ya machozi, jasho na damu ya makuzi yenye maumivu makali na furaha nyakati nyingine kipindi cha makuzi yangu na watoto wengine wa masikini kwenye Tanzania ya miaka ya 1970 na 1980. Maana mimi ni zao la mfumo uliotoa haki na usawa kwa wote. Bila Tanzania hiyo mtoto wa masikini kama mimi, hata ningekuwa na bidii na kipaji cha namna gani, nisingefikia kusoma mpaka kuwa daktari, na hata kufikia kutamani kugombea nafasi ya ubunge. Sitaki kufikiri labda ningekuwa wapi mimi leo!

Tufanye kazi kwa bidii na maarifa, zama zimebadilika. Hakuna mtu atakayethubutu kutuibia kwenye zama hizi. Walau hili ni la uhakika.

Na zile kesi za rushwa, wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya ofisi na ubadhirifu wa mali ya umma sasa zifike kwenye mahakama yake na kesi zikimbie ili tuone haki ikitendeka.

Huwezi kupanda mchicha ukasubiri ukuwe kwa matarajio ya kuvuna bangi. Tulimpa kura zetu Magufuli, mwenye rekodi ya uchapakazi, uaminifu na uadilifu, basi tutarajie uchapakazi, uaminifu na uadilifu; mwenye rekodi ya kuacha alama ya kazi yake, basi ni lazima tutarajie kuona kazi itakayoacha alama. Si vinginevyo.

Tungempa mla rushwa, tungeshuhudia rushwa. Tumevuna tulichopanda. Tumevuna kazi tu. Tutulie tuone kazi. Tuamke tufanye kazi. Tushiriki kujenga Tanzania tuitakayo.

Mwandishi wa makala hii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Raia Mwema
Non-sense
Povuu hilooo
 
Hivi pesa za maendeleo zimetolewa asilimia ngapi kwenye mwaka wa fedha 2016-17??? Maana Kigwangala anatuaminiaha kuwa pesa zimetolewa kwenye matumizi ya kawaida
kwenda kwenye maendeleo.

Kweli kuitetea CCM lazima baadhi ya nati ziwe zimelegea
 
Hivi ni kipi hasa mlichobana matumizi?! Moja ya mambo ambayo nchi hii yamekuwa yakilalamikiwa kama matumizi ya hovyo ya serikali ni magari ya bei mbaya ambayo pia yanatumia mafuta mengi!

SWALI 1: Je, unakubali magari yanayotumika kwa mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa hadi ni ma-DC ni ya gharama sana kwa kuzingatia uchumi wetu au kelele zile hazikuwa za msingi?! Kama magari yanayotumika yanaigharimu sana serikali; serikali hii inayobana matumizi imefanya nini cha maana kwenye hilo?

Kubana huku kwa matumizi ni kule mlikutuonesha kwenye picha wajumbe wa Baraza la Mawaziri wakila chips mayai kwenye kikao wakati wengine wametumia pesa nyingi kutoka Dodoma hadi Dar es salaam ambako anaishia kubana matumizi kwenye kula chips mayai?

SWALI 2: Unasema kwamba hamkufahamu ni namna gani kuodoa ada mashuleni kungeleta wimbi la wanafunzi wapya: Ina maana kwa miaka zaidi ya 50 serikali ya CCM ilikuwa haifahamu idadi ya watu wake, kwenye hii context watoto wanaotakiwa kuandikishwa shule?! Ile sensa inayotumika mabilioni ya pesa kuifanya ina maana gani sasa ikiwa bado inashindwa kutoa takwimu sahii ya makundi mbalimbali ya watu?!

Swali la nyongeza: How come unasema hamkufahamu idadi ya kubwa ya wanafunzi ambao hatimae wangeandikishwa ikiwa lengo la kutoa ada mashuleni ilikuwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi?!

SWALI 3: Unakiri kwamba idadi kubwa ya wanafunzi imeongeza changamoto nyingine ya ukosefu wa waalimu! Kwa kumbukumbu zangu, miaka 2+ imepita na serikali bado haijaajiri walimu!! Nitaamini vipi kwamba serikali ipo concerned na hizo changamoto wakati hata changamoto ya wazi kabisa kama ya ukosefu wa walimu inaonekana?

Swali la ziada: Wengi wanaamini moja ya matatizo ya serikali yenu ni kushindwa kufahamu muanze na kipi kisha kifuate kipi... one word, VIPAUMBELE! Hapo juu unadai Nakubaliana na wewe kwa 101%! Lakini je, ni kweli JPM anafanya hayo uliyosema? Kwa maoni yako wewe binafsi: Unadhani changamoto kubwa ya Watanzania ilikuwa ni ukosefu wa usafiri wa anga uliopelekea kununua ndege au upungufu wa hao walimu uliokiri na bila shaka ukosefu wa madaktari na manesi?

Kama changamoto ilikuwa ni usafiri wa anga... unaweza kunitajia jambo moja TU ambalo lilikuwa linashindwa kufanyika kwa sababu tu ATCL hawakuwa na ndege?

Aidha umesema:Mwanzoni kabisa mwa utawala wa JPM mtu hakuhitaji kuwa mtalaamu sana kuona ni namna gani private sector ilikuwa inaelekea hatarini!!!

Siku za mwanzo tulipokuwa tunaongelea hatari inayoielekea microeconomic sector, wale wenzangu na mimi walichofanya ni kutukejeli kwamba tulizoea kuishi kwa madili wakati wengine hatujawahi hata siku moja kula pesa ya serikali directly mbali na ku-enjoy huduma zake! Hata hivyo, yale yale tuliyokuwa tunayasema hivi sasa yapo wazi!!!

Now tell me: Ni kipi kilichofanywa cha ku-stimulate ukuaji wa microeconomic sector zaidi ya kuanza kuikamua hiyo sector kila upande bila ya kuonekana hiyo mipango ya ku-stimulate ukuaji wake?!

Mwisho: Kwangu mimi hii ni kauli iliyojaa elements za ujima hasa ikitoka kwa mtu aliye serikalini!! Na kwa hakika ni element hii ya kiujima ndiyo inayowafanya watu wawe wanapiga makofi hovyo hovyo kama mazuzu... kwamba, kama ni hali ngumu basi tupigike wote!!!

Kwangu hiyo ni kauli iliyojaa elements za ujima kwa sababu, serikali haitakiwi kushadadia kama wote kuwa na hali ngumu bassi poa tu kuliko wengine kuwa na hali nzuri na wengine kuwa na hali mbaya! Kinachotakiwa na serikali ni kuhakikisha watu wote wanakuwa na hali mzuri! Btw, hivi kwanini mnaamini kila aliyekuwa na maisha mazuri alikuwa na maisha mazuri kutokana na kuiba?

SWALI: Hivi kweli kabisa kutoka ndani ya nafsi yako unaamini wale waliokuwa wanaiibia serikali hivi sasa wanakiona cha mtema kuni?! SERIOUSLY? Hivi kabisa unaamini wale walioiba au kufaidika na Kagoda, Deep Green, EPA, Radar Scandal, Ndege ya serikali, Richmond, Escrow and the like hivi sasa hao watu wanaisoma namba kwa kuwa na maisha magumu?! Au unazungumzia hawa wala rushwa uchwara waliopo kwenye ofisi za serikali?! Hivi kabisa unaamini yule Kamishina wa TRA, Masamaki hivi sasa anaisoma namba?! Hivi kabisa unaamini familia ya Rugemalila hivi sasa inaisoma namba kwa kupigika?! Hivi kabisa unaamini yule aliyesema 10 million ni pesa ya mboga hivi sasa anaisoma namba?! Hivi kabisa unaamini Joka la Makengeza hivi sasa linaisoma namba?!

Swali la mwisho la ziada: Wadau huku mtaani wanaamini ununuzi wa ndege ni moja ya next EPA kwa hoja kwamba hata tenda ilikotangazwa hakufahamiki!!! Wewe ukiwa mtu wa serikalini unaweza kusema with confidence huku ukijua kabisa kwamba Mungu anakuona... Je, ununuzi wa zile ndege umefuata taratibu za manunuzi?!
Hapa hawezi kurudi....anatamani hata kuifuta hii makala yake ya kinafiki.
 
Wezi-in-chief ambao hata yeye Magufuli alikuwa moja wa sakari wao ni Mkapa na Kikwete...je ni kweli Mkapa anaisoma namba? Je ni kweli Kikwete anaisoma namba? Je familia zao zinaisoma namba? Mbona moja wao mkewe kapewa ulaji na huyo huyo Magufuli? Okay, yawezekana wanalindwa na Katiba, je amefanya juhudi gani kuirekebisha hiyo Katiba ili wezi wetu wakuu nao waweze kuisoma namba? Utajengaje Tanzania mpya bila msingi imara wa Katiba?
 
Back
Top Bottom