Msanii Joseph Haule (Prof. Jay) ajiunga CHADEMA

Msanii Joseph Haule (Prof. Jay) ajiunga CHADEMA

Piga makofi tafahali!!! Weka mbali tembo zetu na kinana tafadhali!!!!
 
Safi sana wasanii wengi walikuwa na uoga wa kizamani kama walivyokuwa wanafunzi wengi vyuoni kwa kuamini kuwa ukijiunga na upinzani basi hutafanikiwa katika mambo yako. hata hao waliotumika na chama hawajafanikiwa chochote. ujumbe uwafikie na wengine wote waache uoga.
 
nataka kudhamini pambano la nani zaidi kati ya makundi haya.
prof j.sugu,jide na roma.
dhidi ya vick kamata,komba,nakaaya na dokii.
 
lakini twende turudi hivi j uwezo wake wa akili kujenga hoja upoje make kama utakuwa kama wa sungu itakuwa ni kituko hasa kwenye vikao itakuwa ni vituko tu nadhani atakuwa naibu waziri kivuli wa michezo wa chadema.
 
nataka kudhamini pambano la nani zaidi kati ya makundi haya.
prof j.sugu,jide na roma.
dhidi ya vick kamata,komba,nakaaya na dokii.

Umenifanya nicheke sana tena kwa sauti. U made my day thank u

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nafurahi kuona kile nilichomshauri Profesa_Jay mwaka jana leo amekitimiza, namtahadharisha Emanuel Nchimbi ajiandae kung'oka
 
Last edited by a moderator:
...mwendo mdundo proffffff mpaka kisomeke na kieleweke....
 
Kama unajua jinsi ya kutafuta hela bila kuitegemea CCM karibu sana CHADEMA,ila kama wewe ni kilaza na huwezi kujituma kaa huko huko CCM!

imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu ila kwa kila nenolitokalo kwa bwana,
 
Huyu ni jembe kushinda hata Joseph Mbirinyi. Alitakiwa achukue nafasi ya Sugu.

Ni habari njema kwa wapenda mabadiliko. Lakini kimtazamo wa kisiasa na kimuziki huwezi kumlinganisha Sugu na Prof. Sugu alianza harakati tangu enzi ya chama Kimoja na ni pure hardliner na ni risk taker(single yake ya kwanza alitoa 1985 ikiitwa "Ni mimi" enzi hizo akiitwa 2-Proud).Baada ya hapo aliendelea kutoka na nyimbo za kiharakati kama "niko mikononi mwa polisi".Harakati zake hakikuishia majukwaani tu. Mara kwa mara alikua anagombana na Ruge na kusaga (Mawingu studio then clauds) kwa kudai haki yake wala hakuogopa kwamba nyimbo zake zitaminywa na Radio/TV station kwa kudai haki yake.

Prof. Jay amekuja earlier 1990s chini ya Hard Blasters na amenogesha sana Bongo flava-ninamkubali.Japokua nae ana nyimbo kadhaa za kiharakati kama "Kikao cha dharura..aka ndio mzee". Lakini bado kimtazamo huyu ni soft ukilinganisha na Sugu. Sugu ameonesha njia. Prof. Jay karibu kwenye harakati za ukweli muwaokoe watanzania na CCM iliyopoteza dira ya kuongoza na sasa kinatawala.
 
lakini twende turudi hivi j uwezo wake wa akili kujenga hoja upoje make kama utakuwa kama wa sungu itakuwa ni kituko hasa kwenye vikao itakuwa ni vituko tu nadhani atakuwa naibu waziri kivuli wa michezo wa chadema.



Hoja zake zitakuwa bora kuliko za Mwigulu, Lusinde, Mzee wa F..k You pamoja na Mkamia.
 
Mara walisema CDM inazidi kupoteza mvuto,mara ooh chama cha kaskazini n.k.
Kwa mwendo huu Waziri Nchimbi 2015 bye bye,
 

Msanii wa bongo fleva mwenye mvuto na kupendwa na watu wote ni Diamond, wengine hakuna kitu kwa sasa. Na yeye ndiye anaye ongoza kwa kipato ndani ya bongo fleva. Prof. Jay hakuna kitu tena, ni oil chafu hiyo mkuu
weee usinichekeshe..eti diamond mvua nguo anapendwa na watu wote...Prof..ndo all time best musiciaN ukimcompare na Diamond mchonga skendo
 
bado nachalenge uwezo wa j katika kujenga hoja ila katika kukimbia kimbia wamepata mtu ila kwa maana ya weledi bule kabisa.
 
CHADEMA mnazidi kuongeza majanga; Joseph Haule hana tofauti na Joseph Mbilinyi kwa mipasho isiyokuwa na hekima
wangelikuomba ushauri kwa hiyo ungeliwambia wamchukue daimondo kuwafundisha vijana uzinifu kama wanavyomtumia magamba?
Binadamu anachoongea kiko more likely kuwa ndicho anachofikiri na mwishowe kuweza kutenda. Maneno ya Joseph Haule hakuna kijana asiyeyajua na hata wazee waliipenda na kuikubali bongofleva kwa sababu ya mchango wake.
I can not imagine how clouds will cover the event especially 'fremu ya kilima'
 
Hilo haliwezi tokea na kama ikitokea yatakuwa makosa makubwa mno, wasiwasi wangu ni kuona chama cha upinzani kikiwa na idadi kubwa ya wasomi wa level ya form ambao kiuhakika hawawezi kuiwakilisha vizuri nchi yetu hasa katika mambo ya msingi hasa kusaini mikataba mbalimbali otherwise watakuwa wapigadomo tu ila katika utendaji wataboronga.

Kwanza naomba ujue Joseph Haule siyo form four level kama unavyodhani. Fanya utafiti kabla hupost chochote. Halafu ndo kusema akina Chenge waliosain mikataba ya Radar ni form four leavers. Sometimes try to utilize well your brain brother.
 
Kunishinda mimi ni kufanya jua kuwa baridi .
By Professor J.

J tunakuzimia@yahoo.com
Pande zote utakwenda lakini bongo Ndo home.

Big Up Professor J.

Malaika wako wakulinde na wenye wivu na chuki.
 
Dah! Kesho utasikia amefunguliwa kesi kwa kosa la kuvaa suruali ya kijeshi.
"Chezea magamba weye"
Ni kweli saudari. Kwa jinsi magamba walivyo, watasema hana leseni ya kufanya muziki hapa nchini!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom