dada white
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 1,228
- 515
Ni habari njema kwa wapenda mabadiliko. Lakini kimtazamo wa kisiasa na kimuziki huwezi kumlinganisha Sugu na Prof. Sugu alianza harakati tangu enzi ya chama Kimoja na ni pure hardliner na ni risk taker(single yake ya kwanza alitoa 1985 ikiitwa "Ni mimi" enzi hizo akiitwa 2-Proud).Baada ya hapo aliendelea kutoka na nyimbo za kiharakati kama "niko mikononi mwa polisi".Harakati zake hakikuishia majukwaani tu. Mara kwa mara alikua anagombana na Ruge na kusaga (Mawingu studio then clauds) kwa kudai haki yake wala hakuogopa kwamba nyimbo zake zitaminywa na Radio/TV station kwa kudai haki yake.
Prof. Jay amekuja earlier 1990s chini ya Hard Blasters na amenogesha sana Bongo flava-ninamkubali.Japokua nae ana nyimbo kadhaa za kiharakati kama "Kikao cha dharura..aka ndio mzee". Lakini bado kimtazamo huyu ni soft ukilinganisha na Sugu. Sugu ameonesha njia. Prof. Jay karibu kwenye harakati za ukweli muwaokoe watanzania na CCM iliyopoteza dira ya kuongoza na sasa kinatawala.
Hapa hatuangalii ukongwe na uzee hapa tunaangalia u smart wa mtu.Katika mtu aliimba siasa vizuri na kufichua mambo ya ajabu ya serikali hapa nchini lazima umtaje ROMA na Prof Jay mi binafsi simkubali sugu kuanzia nidhamu na hata maamuzi yake anayofanya katika mambo yake ya kiharakati,Huenzi kuniambia harakati zake mheshimiwa mkubwa kama yule anatengeneza kundi la kuimba matusi makubwa(tafuta kundi linaitwa Anti virus wamejaa wajinga wanaoimba kwa hisia za bangi likiongozwa na yeye) alafu leo uje kunifananishia jay na sugu.Muangalie hata akiwa bungeni utaelewa nazungumzia nini.Sugu kaingia bungeni kwa umaarufu tu lakini sio kama yupo nondo ki siasa.Kama unabisha angalia interview ya sugu uje uangalie na interview ya prof jay utaelewa nini nazungumzia.Pale CHADEMA tunapazia sio mlango.