Msanii gani kufunika fiesta 2018?

Ni kweli kuwa social network ina nguvyu kuliko radio na tv ila tazama pia ni nani ana sauti kwa wasanii kati ya WCB NA CMG. Hivi kuna msanii yupo tayari kuzinguana na CMG kwa kutegemea msaada wa WCB? Okay labda ikatokea siku kukawa na viwanja viwili huku WCB wanapiga show halafu kule CMG wanapiga show, wasanii watamiminika upande gani?
lets assume wasanii watajaa CMG ila kumbuka kuna wasanii wakubwa pia wataenda WCB na kwa hali ilivo sasa watu watajaa kwa WCB n CMG watazid kudharaulika
 
Fiesta saivi wanapata backup ya Tigo tuu,lakini matamasha hayajazi kama zamani.Nakumbuka kuna mwaka pale leaders walijifanya kuweka mitambo mipya (Wasanii waliperform wengine mitambo ikagomaaa,kilichofuatia ETI SHOW IKARUDIWA KESHO YAKE IKAWA FREE).Kuanzia hapo ndiyo wakaanza kutengeneza Wasanii kipindi cha Mpito Darassa,mara Aslay,mara Alikiba (kumdanganya Dogo Aslay eti apambane na WCB).Saivi hata Mikoani hatusubiri Fiesta pekee.Kuna Matamasha kibao yanafanyika sasa hivi (currently_Mzikimnene_EFM).Mimi nilikuwa MPENZI/MDAU MKUBWA WA FIESTA MARA YA MWISHO KUIFURAHIA NI ILE AMBAYO JUMA NATURE ALIPIGA SHOW YA KUFUNGA NA LILY KIM.
 
Wewe ni mmoja wa wahusika wa Fiesta?

hapana aiseee
Nimeandika hivyo kwasababu Wengi humu ni kama mnawahakikishia wasanii kulipwa vizuri baada ya wasafi festival Hata kabla haijaanza!

Wengi wanasema clouds wanawapa promo baadhi ya wasanii ili wawatumie!
Jamani hivi nani hapendi faida kama unahisi nikimpa promo mtu flani ambae kwa kipindi hicho anafanya vizuri show itabamba?

Ni mtazamo tu lakini usichukulie personal sana mkuu
 
Kwakweli uoga wa wasanii umepungua, Diamond alisema mwanzoni wasanii walikuwa wanaogopa hata kufanya jingle ya WASAFI TV, ila kwa sasa wanajipeleka wenyewe kuomba interview na kutambulisha wimbo. CMG haiwezi kufa leo wala kesho but ukweli ni kwamba ule utabe wao na uMungu mtu umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kusimama WCB na uwepo wa social medias. Mgogoro wa hizi pande mbili unaathari kubwa zaidi kwa CMG kuliko WCB, tumeona wasanii wote wa WCB (excluding Mavoko na Queen Darleen) wameweza kufanya vizuri sana mwakahuu kiasi kwamba wameweza kudominate kwenye social medias hadi mtaani. Mimi ni muhudhuriaji mzuri sana wa harusi na Club, huko kote nyimbo za WCB zinachukua nafasi kubwa sana. Yaani unaweza fikiri Tanzania ina wasanii kutoka WCB tu. Huwa najaribu kupitia trendings za nchi kama Kenya, utakuta zimejaa nyimbo/habari za WCB, ni nadra kukuta za msanii mwingine kutoka bongo. Jamaa wametengeneza brand kubwa, wataendelea kuwapa tabu sana CMG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom