Msanii gani kufunika fiesta 2018?

Fiesta ndio tayari imeshatangazwa, na mwaka huu haitakuwa tena na msanii wa nje.

Ukiangalia trend ya mwaka mzima.
Unatabiri msanii gani atakuwa kivutio kwenye fiesta ya mwaka huu?

Mimi binafsi naona Maua Sama atafanya vizuri sababu ya wimbo wake mpya iokote.
Sasa uo ni wimbo? sample ya KWANGWARU na ambavyo atuwapendi wasanii wakike hapo ndo atajua kusoma na kuandika.
 
Fiesta hii itakuwa doro sababu ya beef zao za kipumbavu na WCB. WCB hawakwepiki wameitawala social networking na digital platforms kwa 80%, angalia instagram, fb, YouTube, boomplay nk zote zao na siku hizi radio na TV hazina nguvu upande wa promo na hata ukiangalia 70% hits zote tz ni za WCB na hata ukienda angalia ktk hizi website zinaoupload nyimbo eg kideboy, chart yote wametawala wao, YouTube views, kuanzia no 1 mpaka kumi zao so FIESTA 2018 itakuwa si ktk ubora ule uliozoeleka Diamond na WCB, wamewashika kubaya CMG hata kama hawata admit, wamemsababishia millard ayo views ktk acc yake ya YouTube zipungue kwani mda si mrefu GPL na Dizzim watampita.
Fact kabisa
 
Hawapo ila Tanzania hii kuna wasanii wengi kushinda hao WCB naamini itafanya vzr...japo Mimi sitahudhuria kulingana na umri wangu kwa sasa!!!ila wapo!!!
Kama mwaka Jana ilidolora na beef ilikuwa ndo inaanza,mwaka huu ndo beef liko on fleak ko fiesta imepotea basi.
 
Eti namimi ndio Nashangaa me bado naamini Fiesta ze best burudani. Kama dogo Janja mbona anahit song, uje Nandi uje fidq, uje linah, uje mauwa Sama, billnass, uje richmavoko, uje rubby, uje kuna kundi hivi lavijana watatu Jina Lao nimelisahau kidogo mbona wasanii tunao kibao jamani ukiachana na WCB
Wapo but wanaoingia hawatakuepo wengi kulinganisha na zamani ko lazima ipoe tuu,time will tell itakuwa Zaidi hata ya mwaka Jana.
 
Clouds siku hizi ni wa kawaida sana maana hata wasanii wanawachukulia kawaida sana tofauti na zamani
Zamani kulikuwa na iman et usipoenda kutambulisha wimbo wako clouds (xxl) basi hiyo nyimbo haitakuwa hiti lakin sahiv wasanii hawaendi kutambulisha na ngoma zinakuwa hit mfano kwangwaru haijatambulishwa clouds lakin ndio ngoma kubwa mwaka huu mfano mwingine dogojanja wimbo wake wa #banana hakwenda kutambulisha clouds lakin ni wimbo unaofanya vizuri ikumbukwe tu banana wimbo wa dogojanja ulitambulishwa kwa mala ya kwanza wasafi TV
Fact wacha waisome namba weee,si wameitaka wenyewe
 
Kusoma hujui hata picha huoni hits songs za mwaka huu WCB wametawala kwa 70%(fb, instagram, YouTube, iTunes Kenya, Boomplay, kideboy nk huko kote wanatrend wao) ,kwa hiyo WCB wao wenyewe wanauwezo wa kujaza kiwanja bila msanii yoyote yule (refer wasafi festival Iringa mwaka juzi). Mwanzo wa beef la WCB na CMG, wasanii walikuwa wanaisusa WCB kwa kuwaogopa CMG , lkn sasa hivi Ben pol, Dully Sykes wamepiga collabo na Harmonize, juzi Jux na Ben pol walikuwa ktk final za Jibebe Challenge na kama haitoshi birthday ya Romy Young Dee na Giggy walikuwa ktk party ya WCB na kama hiyo haitoshi week iliyopita Romyjones ametoa nyimbo ndani ameshirikishwa Country Boy, kwa kifupi CMG inapoteza ule ubabe wake, sio kama zamani na bado wengi sana wata hang out na WCB, wasanii wamechoka kupiga show zisizokuwa na hela, kwani CMG inatengeneza mastaa masikini wenye majina makubwa kwa kigezo cha promo.
Kwakweli uoga wa wasanii umepungua, Diamond alisema mwanzoni wasanii walikuwa wanaogopa hata kufanya jingle ya WASAFI TV, ila kwa sasa wanajipeleka wenyewe kuomba interview na kutambulisha wimbo. CMG haiwezi kufa leo wala kesho but ukweli ni kwamba ule utabe wao na uMungu mtu umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kusimama WCB na uwepo wa social medias. Mgogoro wa hizi pande mbili unaathari kubwa zaidi kwa CMG kuliko WCB, tumeona wasanii wote wa WCB (excluding Mavoko na Queen Darleen) wameweza kufanya vizuri sana mwakahuu kiasi kwamba wameweza kudominate kwenye social medias hadi mtaani. Mimi ni muhudhuriaji mzuri sana wa harusi na Club, huko kote nyimbo za WCB zinachukua nafasi kubwa sana. Yaani unaweza fikiri Tanzania ina wasanii kutoka WCB tu. Huwa najaribu kupitia trendings za nchi kama Kenya, utakuta zimejaa nyimbo/habari za WCB, ni nadra kukuta za msanii mwingine kutoka bongo. Jamaa wametengeneza brand kubwa, wataendelea kuwapa tabu sana CMG
 
Kusoma hujui hata picha huoni hits songs za mwaka huu WCB wametawala kwa 70%(fb, instagram, YouTube, iTunes Kenya, Boomplay, kideboy nk huko kote wanatrend wao) ,kwa hiyo WCB wao wenyewe wanauwezo wa kujaza kiwanja bila msanii yoyote yule (refer wasafi festival Iringa mwaka juzi). Mwanzo wa beef la WCB na CMG, wasanii walikuwa wanaisusa WCB kwa kuwaogopa CMG , lkn sasa hivi Ben pol, Dully Sykes wamepiga collabo na Harmonize, juzi Jux na Ben pol walikuwa ktk final za Jibebe Challenge na kama haitoshi birthday ya Romy Young Dee na Giggy walikuwa ktk party ya WCB na kama hiyo haitoshi week iliyopita Romyjones ametoa nyimbo ndani ameshirikishwa Country Boy, kwa kifupi CMG inapoteza ule ubabe wake, sio kama zamani na bado wengi sana wata hang out na WCB, wasanii wamechoka kupiga show zisizokuwa na hela, kwani CMG inatengeneza mastaa masikini wenye majina makubwa kwa kigezo cha promo.
Mkuu weka akiba ya maneno!
Mpaka pale utakapoona hiyo wasafi festival itawalipa hao wasanii pesa ndefu!!
 
Fiesta ipo katika kipindi chake cha mwisho mwisho inabidi kiingilio kiwe buku buku tu watu wajae,lakini ndo kujifunza taasisi si vyema kujiingiza ktk mabifu yasiyo na tija maana nyakati zimebadilika sasa ule muda wa utemi umeshapitwa na wakati,sasa ni ulimwengu wa technology watu wengi wanatumia njia mbadala kujitangaza na kuifikia jamii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom