Msanii Besta yupo wapi?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Hapo zamani si sana, katika anga za burudani za Tanzania, kulikuwepo na dada mmoja ambaye jina lake likitajwa, kila mtu alikuwa na simulizi lake. Sio tu kuimba, bali hata alipokanyaga jukwaani kwa kucheza, watu walibaki mdomo wazi. Hakuwa kama hawa watoto wa 2000 ambao hurukaruka tu na bado kusifiwa eti wanajua “kucheza” – huyu dada alikuwa ni somo, mwalimu wa stage, na mvuto wa kipekee.

Kila hatua aliyopiga, kila kiuno alichokipindua, kilikuwa na hadithi ndani yake. Mashabiki walihisi muziki wake ukiwazunguka kama upepo wa jioni wenye harufu ya maua, na kucheza kwake kulikuwa kama filamu ya moja kwa moja. Besta – ndiyo, yule Besta aliyemaliza mioyo ya wengi – baadaye aliolewa na Marlaw, jambo lililowavunja moyo mashabiki wengi wa kiume waliokuwa wakimtamani kwa siri.

Leo hii, hakuna anayejua yupo wapi. Kuna wanaodai aliweka ustaarabu na kujiondoa kwenye macho ya uma, wengine wanasema amejikita kwenye maisha ya kifamilia. Lakini ukweli unabaki kuwa, aliuacha ulimwengu wa burudani ukiwa na pengo lisilojazwa. Wale waliomuona jukwaani wanajua – huyu dada alikuwa ni historia, na historia hiyo itabaki kupigiwa saluti milele.
 
Hivi nini kipo ndani yetu....
Ukiwa namii...

Oooohh oooh... kwani wameachana? Yupo kwa Marlaw

Alikuwa ananikosha saana....Sema hapo kwa viuno mchawi Ray C.
Hii nyimbo ilivyokuwa inaanza aisee vijana tulikuwa tunapigia 💧
Your browser is not able to play this audio.
 
Muziki wa 2000 Kuja 2009 hautawahi Kuja kutokea Tanzania.

Hatukuwa na big 5[Mondi, Alikiba, Konde sijui na kina nani] kama ilivyokuja baadae....karibu wasanii 20 walikuwa wakubwa na kila mmoja na hits za kutosha.
Golden Bongo Fleva Generation Mkuu! Fiesta walikuwa wanaimba na watu
 
Npo nae hapa, kwani unatakaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…