Msanii BARAKA THE PRINCE Ajiondoa ROCKSTAR4000

HB.com

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
607
638
“Nimeondoka Rockstar sio sababu Alikiba ni Boss” – Baraka the Prince

Kama utakumbuka mwaka 2016 mwimbaji Baraka Da Prince alisaini mkataba wa kufanya kazi na label ya Rockstar 4000 lakini baadae zikaanza kusambaa taarifa ambazo zilidai kuwa staa huyo ameachana na label hiyo.

Leo July 21, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM Baraka the Prince amethibitisha kuwa hayupo tena chini ya Rockstar4000 na kuwa anafanya kazi zake binafsi akidai kuna mambo hayapo sawa kati yake na Management huku akisisitiza siyo kwa sababu Alikiba amekuwa Wakurugenzi wa label hiyo.

>>”Kuna vitu lazima uvihoji na ukiona watu unaofanya nao kazi kama kampuni wanakuwa hawajali kitu unachotaka kufahamu kuhusu makubaliano yenu ya kazi inakuwa na mashaka kidogo”

“Naweza kusema sipo chini ya Rockstar kwa sababu mimi ndio boss wa muziki wangu halafu mimi ndio nafanya kazi, kukiwa na vitu haviko sawa kwa upande wangu mimi ndio naweza kutoa kauli ya mwisho, sipo chini ya Rockstaar”

“Kuna vitu haviko sawa hilo neno boss zito sana, unaponiambia mtu ni boss wangu, how? Boss kivipi kwangu? Alikiba kuwa director wa Rockstar mimi ndio nijitoe, hapana…. kuna vitu haviko sawa na uongozi wa Rockstar”

“Nilipokwenda Rockstar4000 sikusaini chini ya AliKiba, mimi nina matatizo binafsi na uongozi na kama mambo hayapo sawa ukiona kitu jua kipo chini ya Baraka” – Baraka the Prince.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh huyu Jamaa atapotea sio muda!
Aliondoka kwa kidbway Mara akakataa kama ngoma zake haijawahi andikiwa Na lollypop......
Juzi nimesikia wimbo mpya wa ommydimpoz nikakumbuka mikato ya Baraka da prince wa Siwezi .....
Nikajisemea haya mashari ya lollipop Na hii beat angesimama Baraka tena ingekuwa balaaaa tena kama ngoma zake za mwanzo!
Anyway ngoja tuone ila binafsi siuoni muelekeo mzuri
 
Mmmh huyu Jamaa atapotea sio muda!
Aliondoka kwa kidbway Mara akakataa kama ngoma zake haijawahi andikiwa Na lollypop......
Juzi nimesikia wimbo mpya wa ommydimpoz nikakumbuka mikato ya Baraka da prince wa Siwezi .....
Nikajisemea haya mashari ya lollipop Na hii beat angesimama Baraka tena ingekuwa balaaaa tena kama ngoma zake za mwanzo!
Anyway ngoja tuone ila binafsi siuoni muelekeo mzuri
Nasikia anaelekea WCBOO kwa sauti ya harmorapa

brain is the beautiful part of the body.
 
Rockstar ndio nini? Angalia opportunities acha kupoteza muda chukua form WCB ngoma moja unanunua gari, Muziki upo WCB rockstar ni Michael jackson peke yake.

Sent from my Blackberry DTEK70 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom