Hivi boss wangu ananichukuliaje..?

Hivi boss wangu ananichukuliaje..?

Koloko

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2026
Posts
249
Reaction score
458
Mimi hapa kuna kitu nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu boss wangu.

Kuna muda anaweza kukaa kimya kabisa, hata kazi ikiwa ipo, hanitafuti. Lakini akiona status yangu nimeenda sehemu fulani, nimealikwa kwenye hafla, nimevaa vizuri au kwa ujumla anaona kama maisha yangu yanaendelea vizuri, ghafla ananikumbuka na kunipa kazi zake.

Mara nyingi ni kazi za kumtumia barua, kumpelekea vitu, kukimbiza documents au mambo mengine yanayohitaji mtu wa kumsaidia.

Cha kushangaza ni kwamba siku za kawaida huwa hanitafuti sana. Lakini akiona nimeonekana sehemu fulani au nimepiga hatua fulani, ndipo anaanza kunitafuta. Wakati mwingine hata ananipigia simu au kunitumia ujumbe bila issue kubwa ya kazi, anaulizia hali na kuanzisha mazungumzo.

Sasa nimekuwa nikijiuliza, huyu mtu ananiona vipi?

Je, ni kwamba ananihitaji lakini huwa ananikumbuka tu anapoona ninaendelea na maisha yangu? 😅

Au anaona labda nikifanikiwa zaidi, nikawa busy na mambo yangu, nitamzidi au sitakuwa available tena kufanya kazi zake?

Au labda ni coincidence tu, na mimi ndiye ninayefikiria sana hii situation?

Watu wenye uzoefu naomba mnisaidie kuielewa hii hali. Boss anayekutafuta zaidi anapoona una-progress kwenye maisha yako, huwa kuna maana gani nyuma yake?
 
Hizi simu smart zinaleta washamba wengi sana.
Kuna mabinti na watu wazima huko insta wanaonyesha mbunye zao Live sasahivi kivificho uchi wa mnyama.
Sasa mdau ni km hao wauza mbususu huko.
Unaanika sana mambo yako ubaoni,boss wako nae mtu wa mitandao anakuchora tu.
Ndio hapo anakurudia ukae mstarini.
Think Big
 
Back
Top Bottom