Msanii Afande Sele amponda JK

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,514
11,277
Wakuu hii nimeikuta kwenye Blog moja ya Kitanzania Afade Sele akionesha hisia zake juu ya ujanja ujanja wa Mheshimiwa Rais wetu JK. Kwa maelezo yake anaona kuwa JK anakusudia kuleta tofauti miongoni mwa watu wa kada mbali mbali:

Msanii huyu anasema hivi:

"Ah, huyu JK kwa tamko lake hili kuhusu studio aliyowapa THT na Ruge anaonyesha jinsi gani asivyo kiongozi makini na kwa mtazamo halisi anaonyesha ni jinsi gani hakustahili kuwa mkuu wa nchi.
Anajenga makundi ya chuki na uhasama katika kila sekta kuanzia kwenye chama chake, serikali yake na sasa kwenye sanaa na haswa mziki wetu ambao ndio amekuwa akijinadi kuusaidia kumbe katika hii awamu yake ndio mziki umepotea mwelekeo.
Sasa kama anasema studio aliwapa waliomuomba mbona mimi na watu wengine wenye misimamo tulikuwepo siku ile alipoahidi studio hatujui lolote na hatujaonyeshwa hiyo studio?"
 
Kwanza huyu mkuru anajuwa anachokifanya??zaidi anafata mkumbo tu etii mziki hicho ndio anachojuwa sio kuangalia watu wenye maisha duni na kumwaga hizo hela kwao.....
 
wakuu hii nimeikuta kwenye blog moja ya kitanzania afade sele akionesha hisia zake juu ya ujanja ujanja wa mheshimiwa rais wetu jk. Kwa maelezo yake anaona kuwa jk anakusudia kuleta tofauti miongoni mwa watu wa kada mbali mbali:

Msanii huyu anasema hivi:



BLOG IPI??

link please!!!!

 
kaka naona kama umefumba macho mwache jk kama alivyo kabanwa pande zote zote jk aliyeingia madarakani 2005 ni tofauti na huyu tunayemwona ni kama mwili tu umebaki anaendesha tanzania ilimradi siku ziende hatari sana kabidilika sana suala dogo tu kama la studio katoa mpya badala ya kuwapa wasanii wote ajabu yeye kadai anawapa wale waliomwomba ajabu kweli kwani waliopewa ndio walioomba kwani mimi nilivyoona wengi waliokuwepo siku hiyo sijaona hata mmoja aliyefikiriwa matokeo yake kasababisha migogoro baina ya wasanii sasa migogoro imehama kutoka ndani ya ccm hadi kwa wasanii kugombea studio ya jk huyo ndio jk na kauli yake kwanini tugombanie fito wakati tunajenganyumba mmoja.
 
Yaani afande sele anashtuka leo kuwa JK msanii? mbona Lipumba alishasema toka 2005 KUWA JAMAA LABDA APEWE WIZARA YA MICHEZO!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom