Afande Sele amchana Kikwete kavukavu!

kamanzi

Senior Member
Oct 28, 2007
100
23
Mimi ni mmoja wa watu wanaodharau wanamuziki wa bongofleva hasa pale wanapomkatikia kiuno Mkwere hasa kwenye matukio ya uchaguzi. Naona mambo yanaanza kubadilika. Alianza Sugu na Mkoloni. Safari hii Selemani Msindi, narudia tena SULEMAN amenukuliwa akisema yafuatayo dhidi ya Kikwete:

"Ah, huyu JK kwa tamko lake hili kuhusu studio aliyowapa THT na Ruge anaonyesha jinsi gani asivyo kiongozi makini na kwa mtazamo halisi anaonyesha ni jinsi gani hakustahili kuwa mkuu wa nchi.

Anajenga makundi ya chuki na uhasama katika kila sekta kuanzia kwenye chama chake, serikali yake na sasa kwenye sanaa na haswa mziki wetu ambao ndio amekuwa akijinadi kuusaidia kumbe katika hii awamu yake ndio mziki umepotea mwelekeo.

Sasa kama anasema studio aliwapa waliomuomba mbona mimi na watu wengine wenye misimamo tulikuwepo siku ile alipoahidi studio hatujui lolote na hatujaonyeshwa hiyo studio?"

Chanzo: k-massive-music
 
Mwenye macho haambiwi tazama, afande SELE umenena hata sisi tunalalamika kila leo kuwa huyu mkuu wa nchi ni mtu wa makundi na chuki, leo tena kamtuma sheikh mkuu kuwachonganisha watanzania kwa kutumia kichaka cha udini.TUMEKWISHA
 
sidhani ,hawa wasanii siwaamini sana wana njaa sana,kumbe siku ya ahadi ya studio na yeye SELE alikuwepo??kwa hiyo ametoswa na wenzie sio?/kama angeshirikishwa na kupewa shavu kwenye studio hiyo haya angeyaona lini????

UNAFKI
 
Kwa nini watu wengi tunasilika ya kuto-akcnowledge failures zetu - na mara nying tunasukumia wengine. Dhambi ya Adamu na Eve inatuumiza sana. Ni nyoka ndiye kanidanganya (Eve) ; ni huyu mwanamke ndiye kanipa tunda(Adam).

Sasa JK kashindwa uongozi- anasema eti sababu yeye ni mslimu ( wakati tunda la ufisadi amekula yeye kwa roho yake nyeupe). Tubu ni njia salama sana na kuacha kutenda maovu tena
 
Jamani hivi hatuwezi kuchangia bila ya kuingiza udini?
 
Shida inafundisha, wasanii walikuwa wanafurahia posho za kumfanyia JK kampeni, wakati wanaambiwa nchi inateketea na ufisadi unatumaliza, wenyewe wanatuimbia kuwa "JK ni kiongozi bora na mwenye busara mfano wa mfalme selemani" . Sasa shida imewafungua macho na wameuona ukweli na wameanza kupata ujasiri wa kuuzungumza ukweli huo hadharani

JK na CCM inabidi wastuke wale waliodhani ni wjinga sasa wanafunguka, 2015 ni wakati wa ukombozi kwa WATANZANIA
 
"Mzalendo kama Jakaya hadi anaondoka Ikulu hajasomesha mtoto Ulaya",nakumbuka kibao chake msanii huyu cha kumpamba JK na leo hii anakuja kulalamika baada ya kutoswa!
 
Hivi wengine mkoje humu ndani? Hii ni reflection ya kushindwa kwetu kufanya analysis ya mambo, tunashindwa kuangalia swala analozungumzi sele sasa hivi tunamhesabu kwa jana na juzi kwa hiyo kama katoswa asiseme? Huku nako kunachosha kwa sasa
 
kazi kweli kweli nadhani ni wakati wa kuwaacha watanzania wajue nini madhara ya uamuzi mbovu wanaoufanya kipindi cha chaguzi kwa upande wangu nadhani ni vema vitu vikapanda bei na maisha yakawa magumu kwa kipindi hiki ili liwe fundisho la kufanya chaguzi sahii mpaka 2015 kilo ya unga iwe buku kumi shs 10000
 
"Mzalendo kama Jakaya hadi anaondoka Ikulu hajasomesha mtoto Ulaya",nakumbuka kibao chake msanii huyu cha kumpamba JK na leo hii anakuja kulalamika baada ya kutoswa!

Hicho kipande cha kumfagilia JK kiko ktk wimbo wa 'Karata Dume' wa Sele. Naona mambo yamemgeuka, sasa analalamika. Ningemshauri Sele (kama ana muda wa kupita JF) asikilize albamu ya Sugu iitwayo Antivirus, asikie ujumbe wa Sugu kuhusu hiyo studio waliyopewa THT na maudhui yake, huenda akaelewa somo kuhusu kazi ya studio hiyo. Albamu hiyo ipo hapa JF, sehemu ya 'downloadz'
 
"Mzalendo kama Jakaya hadi anaondoka Ikulu hajasomesha mtoto Ulaya",nakumbuka kibao chake msanii huyu cha kumpamba JK na leo hii anakuja kulalamika baada ya kutoswa!

uzuri wa mungu hapendi wanafki, malipo ni hapa hapa. kwanza mimi hawa nataka waishi kwa kutegemea maconcert tu lakini sio kuuza cd zao, kwa jinsi walivyo wapuuzi mimi nadowload manyimbo yao ya kipuuzi na nazigawa bure kabisa, mbwa hawa.
 
...Nyerere alisema huyu jamaa bado sana CCM wakampa nchi. sijawahi ipigia kura CCM hata siku moja so sijawahi changia uozo wa huyu jamaa kweli majuto ni mjukuu
 
"Mzalendo kama Jakaya hadi anaondoka Ikulu hajasomesha mtoto Ulaya",nakumbuka kibao chake msanii huyu cha kumpamba JK na leo hii anakuja kulalamika baada ya kutoswa!

ha ha ha ha................. umenikumbusha hili mkuu na sitaki kuamini kuwa huu ndo wakati muafaka wa Afande kuamka na kuona kwamba yule aliyemsifia hakustahili kuwa rais wa nchi!!! N way hujachelewa mkuu karibu vitani
 
Kwa nini watu wengi tunasilika ya kuto-akcnowledge failures zetu - na mara nying tunasukumia wengine. Dhambi ya Adamu na Eve inatuumiza sana. Ni nyoka ndiye kanidanganya (Eve) ; ni huyu mwanamke ndiye kanipa tunda(Adam).

Sasa JK kashindwa uongozi- anasema eti sababu yeye ni mslimu ( wakati tunda la ufisadi amekula yeye kwa roho yake nyeupe). Tubu ni njia salama sana na kuacha kutenda maovu tena

Naona mada imesha haribiwa ngoja nitafute nyingine ya kuchangia...............
 
sidhani ,hawa wasanii siwaamini sana wana njaa sana,kumbe siku ya ahadi ya studio na yeye SELE alikuwepo??kwa hiyo ametoswa na wenzie sio?/kama angeshirikishwa na kupewa shavu kwenye studio hiyo haya angeyaona lini????

UNAFKI

nimeipenda hii, kwa maana nyingine hata watanzania waliompigia kura jk kwa ahadi ya maisha bora wakati wanazidi kufikwa na ugumu wa maisha nao wao ni Wanafiki!
 
Afande umefilisika sana. siku zote ulikuwa wapi au ndo unakumbuuka jamvi wakati kumekuchwa?
 
Very stupid JK kasema wazi wapeleke MAombi yatashughulikiwa wasanii wote Tanzania sio lazima watumie mastering studio moja. Na Kama wanayo hao wakina Ruge si yaweza kutumika ki utaratibu Basata should be able to organize this. Huyu Afande Sele aache kumsakama JK kwa hili Hana hoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom