Msala ambao siwezi usahau kamwe

Msala ambao siwezi usahau kamwe

Nilipokuwa mdogo katika michezonya kibaba tulioana Mimi na mtoto wa Mama yangu mdogo

Sitosahau tulipiga denda French kiss chini ya shuka

Ile incident inatembea Hadi Leo japo tukikutana no salamu tu sijui yeye anakumbuka
 
Niliiba dawa ya mtoto (mdogo wangu) hizi syrup tamu za watoto, nikaimimina kwenye glass, nikakatakata vipande vya viazi nikaweka mezani najifanya padre naongoza ibada,
ile syrup nimefanya ndio divai na vile vipande vya viazi ndio mkate, wadogo zangu ndio waumini Kipigo nilichokipata siku hiyo sitakisahau,

Mkuu ungeenda kusomea upadri tu sasa
 
Enzi hizo sasa ukikaribia mwaka mpya mnatengeneza vi baruti mnaweka kwenye vichwa vya spoku za baiskeli mkiona watu wamekaa mnavitest pwaaaa watu wakishituka mnakimbia kwa furaha, lengo ni kwamba ikifika saa 6:01 kuanza mwaka mwingine mnavipiga kama kusherehekea mwaka mpya (watoto wa siku hizi hawayajui hayo)......

Basi bwana mwaka fulani huo nilidhamiria kuvunja rekodi ya kutengeneza baruti itakayounguruma kuzidi baruti nyingine zote pale mtaani na ikibidi mitaa ya jirani, mzee wangu alikuwa fundi makenika, kwenye makorokoro yake nilipata jeki moja ndogo ambayo ilikuwa imetolewa utumbo ikabaki wazi katikati.

Kuna kaka yangu alikuwaga ametoka Moshi (kama sikosei), huko alikuwa anafanya kazi kiwanda cha kutengeneza viberiti, alikuja na kisado kizima kimejaa unga wa baruti (sijui nae alikileta kwa madhumuni gani tu).....mi nikaiba ule unga wa baruti kwa ajili ya kutengeneza mzinga wangu.

Siku ya tar 31 December nikafanya maandalizi yote, lakini nikapata wazo moja kwamba sitoweza kwenda kukamua ile device pale ili kusababisha mlipuko, nilichokifanya nikategesha jiwe zito juu ya usawa wa lile komboro langu, nilikuwa nimelitega nyuma ya banda la mbuzi nyumba ya jirani yetu........

Bwana weeeeeee.......

Nikamshirikisha kijana wa ile nyumba ambae tulikuwa rika moja tu kuhusu mpango wangu, akataka aende akaangalie.....kufika akakuta nilivyolitega akasema eti nimekosea, akaanza kuliseti upya......

Aiseeeeeeee..........

Ilikuwa yapata kama saa 11 hivi za jioni mzigo ukaitika pale.......boonge ya kishindo, vumbi zito likatimka hewani, banda la mbuzi likaporomoka lote, harufu ya baruti ikasambaa eneo lote......cha kwanza nikakimbia hadi nyumbani, sina amani wazazi wanakimbizana kutafuta watoto wao.

Taarifa za baadae zikatoka......yule jamaa alikatika vidole vitatu vya mkono wa kushoto, ndama wawili wa mbuzi walikufa kifo cha kikatili sana......lakini yote kwa yote yule rafiki yangu (R.I.P) hakusema chochote kuhusu uhusika wangu kwenye kadhia ile.

Mama akajua moja kwa moja kuwa mimi ndio injinia wa ule mpango......jamani nilipigwa sio mchezo, hadi kuna muda nilikuwaga najiuliza kama mama hajawahi kupitia kozi zozote za kijeshi, maana nilipigwa staili zote za kwenye mieleka kuanzia hizi Rko za Rand Orton pigwa sana 619 za Rey Mystereo, chomeshwa kichwa chini kama Under taker, mara nibanwe mguu mmoja huku nimevutwa shingo kwa nyuma John Cena anavyofanyaga.......yani kilikuwa ni kipigo mchanganyiko. hadi nilipokuja kuanza kuangalia mieleka nikajiuliza hawa jamaa walimuiga mama au.......

Hilo likapita.....miezi kadhaa baadae nilikuja kuvurumua msala mwingine mzito sana, kwa kweli siwezi kuuelezea maana ulikuwa uondoke na roho yangu.
Nimempenda maza wako
 
Dah nmecheka sn mkuu, aisee umenikumbusha mbal sn izo mambo zakutega vibaruti, ila hii invention yako ilikua next level yakutumia jek ilokufa.
 
hahahahaha asee jamaa umenikumbusha mbali sana misala kama hii ndio utajua nguvu ya ushikaji......nakumbuka miaka flani nasoma advance niko form six nina kadem kangu form five shule moja na maskani kwa mjomba nilipokuwa nakaa kipindi hiko nina kademu kengine form four nikawa nacheza game kote sasa ikaja ikatokea nikawapa wote mimba ndani ya mwezi mmoja madem wote wana vibendi kudadek na kibaya maisha ya boading sina hata shilingi mia ya kusema nitalipia galama za abortion...... ila katika maisha ya shule nguvu ya ushikaji huwa ni kubwa sana ikabidi nikae chini na mwanangu tupange cha kufanya.....jamaa akanishauri tudeal kwanza na ka olevel ndio hakajakomaa akili.. alafu yule wa advance nimwambie akaze azae mimi nimikimaliza pepa niondoke nae maskani yaani nimuoe,,,,maana dakika za mitihani ya kidato cha sita ilikuwa imekaribia,,, hii jamaa alinishauri nifanye hivyo maana dem wa advance atajiongeza ila ka olevel ukikaambia ni kweli katakaza haya bana gemu ikaanza sasa anaoaje jamaa angu akaniambia akichemsha majivu na chumvi nyingi itatoka ikabidi nimsemeshe dem nimpange ili atoe na jamaa angu aliniambia hii njia ni hatari dem anaweza kufa kwa hiyo kabla hajanywa chochote inabidi kwenye simu yake usionekane ushahidi wa mawasiliano yangu basi bana nikampanga dem kila kitu akaandaa alafu nikamwambia afute sms zote na call history ikitokea amezidiwa wasione kitu na asinitaje, ndo dem katoa ila ishanlah alipona japokuwa aliponea chupuchupu na hakunitaja kabisa japokuwa kwao walimkuta katika hali mbaya....kazi ikabaki kwa yule dem wa advance nikamkazia akomae nayo nikimaliza pepa nasepa hom na akigundulika akafukuzwa aunganishe nyumbani tukakubaliana ila dem baadae alijiongeza mwenyewe siku moja kanipigia simu kadai alikuwa anacheza na mwenzie bwenini akaangukia tumbo cha ajabu akashangaa dam zinatoka na mimba ikatoka, nilizuga kama nimemind ila mission ikawa complited..... ujana una mambo mengi sana nilikuwa namwambia nitamuoa na hom sina hata kitanda wala chumba'. watoto wa shule wanawazia ngono tu

Sent from my SM-G988N using JamiiForums mobile app
 
kuna kota fulani za tanesco sehemu zilikuwa wazi nyumba kama nne hivi,nikiwa mkubwa tu wa form 1.nikagundua uwepo wa nyuki katika moja ya paa la nyumba zile.

kusogea karibu nagundua kumbe wapo pale na wamezalisha na asali kabisa,nikatafakari nini nifanye ili kuivuna asali ile,sijui tu ilikuwajenikachukua manyasi nikayafunga kwenye fito ndefu nchani na kuyatia moto yakaanza kufuka moshi.mchana wa saa saba jua kali ng'ai ng'ai,baharia nataka niwatapeli nyuki asali yao,naona wakasemezana,sijakaa vyema nikachezea kama misumari mitatu hivi ya mkononi na usoni,nikaachia fito na kutoka mbio,hapa ndio niriharibu shughuli sasa.nyuki walisambaa wakafunga mtaa mzima,nikaingia ndani na kuanza kupiga kelele watu wafunge madirisha na milango,bahati yao waliwahi.

sasa aina ile ya kota madirisha yalikuwa ya vioo,watu wote ndani tukawa tunashuhudia watu wanavyopewa kibano na jeshi lililochokozwa mchana wa jua kali,kota zile zilikuwa jirani na za jeshi.wanajeshi waliokuwa wanatoka uraiani kwenda kambini kwao,walikutana na wanajeshi wenzao ambao wamevurugwa zaidi.basi movie ikawa ni kubwaga baiskeri na kutimua mbio itakavyowezekana maana jamaa wanaupiga mwingi sio kawaida.
muda ambao nilijutia upuuzi nilioufanya ni wakati ambao dada wa makamo akiwa na mtoto mgongoni na kuni na jembe katoka shamba,akakutana na wataleban wale,walimpa vitu mpaka akabwaga mtoto chini mbiooo,mtoto akawa analia pale chini,nyumba zote tukaanza kupiga mayowe asimwache pale lakini hasikii maskini,ole wako ufungue hata kioo kimoja waingie ndani,utajua hujuililikuwa tukio baya sana.Mungu mkubwa nyuki wakiwa kwenye taharuki namna ile huwa hawa deal na adui aliyelala.kwahiyo mtoto yule alilizwa na majeraha ya kwanza akiwa mgongoni.aliposhushwa hakuguswa tena.

wale jamaa walitawala anga wakafanikiwa kuchukua nchi ile kwa masaa kadhaa,mpaka jioni saa 11 ndio tukaanza kuona kama pilika zinarudi,watu wanapita bila pingamizi.yule mtoto kalia pale chini mpaka sauti imekauka,tukafungua vioo kwa machale,na kuanza kuelekea kule aliko,tunamkuta hajajeruhiwa kiivyo,ana kauvimbe tu kisogoni.mama yake alirudi usiku kumfata.

kesho yake nikawa mpole sana,jamaa mmoja akaniuliza,uliishawahi ona wapi asali inavunwa kienyeji mchana!!!nimetoa macho tu.
 
kusogea karibu nagundua kumbe wapo pale na wamezalisha na asali kabisa,nikatafakari nini nifanye ili kuivuna asali ile,sijui tu ilikuwajenikachukua manyasi nikayafunga kwenye fito nchani na kuyatia moto yakaanza kufuka moshi.mchana wa saa saba jua kali ng'ai ng'ai,baharia nataka niwatapeli nyuki asali yao,naona wakasemezana,sijakaa vyema nikachezea kama misumari mitatu hivi ya mkononi na usoni,nikaachia fito na kutoka mbio,hapa ndio niriharibu shughuli sasa.nyuki walisambaa mtaa mzima,nikaingia ndani na kuanza kupiga kelele watu wafunge madirisha na milango,bahati yao waliwahi.

sasa aina ile ya kota madirisha yalikuwa ya vioo,watu wote ndani tukawa tunashuhudia watu wanavyopewa kibano na jeshi lililochokozwa mchana wa jua kali,kota zile zilikuwa jirani na za jeshi.wanajeshi waliokuwa wanatoka uraiani kwenda kambini kwao,walikutana na wanajeshi wenzao ambao wamevirugwa zaidi.basi movie ikawa ni kubwaga baiskeri na kitimua mbio itakavyowesekana maana jamaa wanaupiga mwingi sio kawaida.
muda ambao nilijutia upuuzi nilioufanya ni wakati ambao dada wa makamo akiwa na mtoto mgongoni na kuni na jembe katoka shamba,akakutana na wataleban wale,walimpa vitu mpaka akabwaga mtoto chini mbiooo,mtoto akawa analia pale chini,nyumba zote tukaanza kupiga mayowe lakini hasikii maskini,ole wako ufungue hata kioo kimoja waingie ndani,utajua hujuililikuwa tukio baya sana.Mungu mkubwa nyuki wakiwa kwenye taharuki namna ile huwa hawa deal na adui aliyelala.kwahiyo mtoto yule alilizwa na majeraha ya kwanza akiwa mgongoni.aliposhushwa hakuguswa tena.

wale jamaa walitawala anga wakafanikiwa kuchukua nchi ile kwa masaa kadhaa,mpaka jioni saa 11 ndio tukaanza kuona kama pilika zinarudi,yule mtoto kalia pale chini mpaka sauti imekauka,tukafungua vioo kwa machale,na kuanza kuelekea kule aliko,tunamkuta hajajeruhiwa kiivyo,ana kauvimbe tu kisogoni.mama yake alirudi usiku kumfata.

kesho yake nikawa mpole sana,jamaa mmoja akaniuliza,uliishawahi ona wapi asali inavunwa kienyeji mchana!!!nimetoa macho tu.
Daa nimecheka kichizi, jamaa ulitaka kuchukua Mali ya watu mchana kweupe
 
Enzi za utoto wangu nilikuwa mtundu sana aisee.

Siku moja niko home choo chetu na jiko vilikuwa ni vya nyasi,sasa nikakaa nikaangalia zile nyasi kule juu nikasema aaah hivi mchana huu nikiweka njiti ya kiberiti itawaka kweli na kumaliza nyasi zote hizi ?

Faza enzi hizo ni mtata sana yaani.

Basi baada ya kuwaza nikasema sio kesi acha niweke njiti ya kibiriti niwashe nione kama itawaka kwa nyasi zote hizi.

Kidume nikawasha nikatulia kuskilizia mshindo,kuna kimoshi kikatoka alafu kikazimika nikasema aaah kumbe haiwezi kuwasha,nikaendelea kufanya mambo mengine.

Kumbe bhana ule moto ulikolea ndani kwa ndani ukawa unafukuta juu kunatoka moshi mimi niko ndani sina habari.

Kumbuka kuwa hapo nyumbani nilikuwa peke yangu watu wote hawapo.aisee nashangaa kuna mzee jirani yetu anakuja mbio sana anaita nikashangaa anaita nini huyuu ?,anakuja anasema motoooooo mootoooo moyo ukapiga paaap nikajiuliza moto ule nilowasha mie au moto ungine ? Nikajipa moyo nikasema ule wangu ulizimika huu utakuwa ni moto mwingine.

Daaah kutoka nje kutazama juu laaaaaa hawlaaaaa kitu chekunduuuu moto mkubwa unawaka alafu jua kali,daaah aisee nilipata sonona mana hapo sikuwaza tena huo moto bali niliwaza kichapo cha faza na maza maana wote walikuwa watata sana nikizingua.

Daaah basi yule mzee akahangaika sana kuzima ule moto huku mimi nikiwa nimepata butwaa la ghafla na mawazo tele kichwani mithili ya mtu mwenye familia.

Shida ni kwamba
Ilibidi auzime moto ule kwa maji ya ndani kwetu jikoni,na hilo jiko ambalo ndio kuna maji juu ndi kunawaka moto,ama kwa hakika ilikuwa shughuli pevu sana siku hiyo.

Mzee ikabidi ajitoe muhanga akawa anaingia ndani anachukua maji anakuja anazima.

Kwa hiyo nikawa na misala miwili.

1.msala wa kuwasha moto.

2.msala wa kumaliza maji ndani na kkulekwetu kusini maji ilikuwa shida miaka ile mpaka ununue kwa ndoo alafu mimi nakuja kumaliza maji kwa uzembe wa kuwasha moto.

Daaah mwisho mzee kauweza moto ukazimika lakini lile paa la nyumba la nyasi ukiangalia kwa juu ni kama mtu mwenye kipara namna ambavyo lilikuwa likionekana.

Ikabidi mzee anihoji mimi nokampa ukweli wote,na yeye waliporudi wazee akawasimulia kama nilivyomsimulia na hiyo wazazi wakatafsiri kwamba ni upumbavu wangu.

Yule Mzee aliwaasa wazee wangu wasinipige lakini nahisi kwao ilisound"mumpigeee hasaa huyoo"

Daaaah

Daaaah

Daaahh.

Ushawahi kupigwa mpaka inafikia hatua ukipigwa ndo unanyamaza na ukiachwa ndo unalia ?

Nahisi kipigo kile kilicontain kipigo cha kuwasha moto na kipigo cha kumaliza maji na kipigo cha kusumbua wazee wa watu.

Lakini uzuri walikuwa wananipiga maeneo mabayo siwezi kupata madhara makubwa,yani unapigwa maeneo ambayo unasikia maumovu lakini kufa hufi.

Mungu anitunzie wazazi wangu maana bila vile ningelikuwa toto sumbufu sana kwa sababu nilikuwa mtundu sana.

Baada ya soo hili nikasema mimi na majaribio ya kipuuzi baasi tenaaa nimekoma.

Thubuuutuuu...

Nikaja kufanya soo lingine la kuiba aisee(sikumbuki soo gani lilitangulia)

faza kazipanga shilingi mia nyingi usikuu mezani tena chumbani kwake.

Mimi nikavizia faza na maza wako nje kwa kujiamini nikasema hawaingii saivi,kidume nikazama ndani fresh.

Nilipozama ndani nikachomoa mia ya chini hizi za juu zikaparaganyika,nikashindwa kuzipanga.

Ishu nikajiuliza sasa faza kaijua kama nimeiba 100 itakuwaje ? Kidume nikasema solution ni kutawanya hizi pesa pururu mpararo tuu kama mbwai na iwe mbwai,basi kwa ujinga nikazitawanya zile pesa kama hazikupangwa vile alafu nikaondoka na shilingi mia yangu.

Daaaah ishu ikabuma tena siku hiyo usiku baba na mama wapo wote.

Mama alinitandika saana na kamba za ukili mpaka akili ikakaa sawa.

Ila huu ni wakati wa utoto sana around miaka 4- 7,umri huu mara nyingi mtoto anaona akipigwa naaonewa.
 
WWe
Enzi hizo sasa ukikaribia mwaka mpya mnatengeneza vi baruti mnaweka kwenye vichwa vya spoku za baiskeli mkiona watu wamekaa mnavitest pwaaaa watu wakishituka mnakimbia kwa furaha, lengo ni kwamba ikifika saa 6:01 kuanza mwaka mwingine mnavipiga kama kusherehekea mwaka mpya (watoto wa siku hizi hawayajui hayo)......

Basi bwana mwaka fulani huo nilidhamiria kuvunja rekodi ya kutengeneza baruti itakayounguruma kuzidi baruti nyingine zote pale mtaani na ikibidi mitaa ya jirani, mzee wangu alikuwa fundi makenika, kwenye makorokoro yake nilipata jeki moja ndogo ambayo ilikuwa imetolewa utumbo ikabaki wazi katikati.

Kuna kaka yangu alikuwaga ametoka Moshi (kama sikosei), huko alikuwa anafanya kazi kiwanda cha kutengeneza viberiti, alikuja na kisado kizima kimejaa unga wa baruti (sijui nae alikileta kwa madhumuni gani tu).....mi nikaiba ule unga wa baruti kwa ajili ya kutengeneza mzinga wangu.

Siku ya tar 31 December nikafanya maandalizi yote, lakini nikapata wazo moja kwamba sitoweza kwenda kukamua ile device pale ili kusababisha mlipuko, nilichokifanya nikategesha jiwe zito juu ya usawa wa lile komboro langu, nilikuwa nimelitega nyuma ya banda la mbuzi nyumba ya jirani yetu........

Bwana weeeeeee.......

Nikamshirikisha kijana wa ile nyumba ambae tulikuwa rika moja tu kuhusu mpango wangu, akataka aende akaangalie.....kufika akakuta nilivyolitega akasema eti nimekosea, akaanza kuliseti upya......

Aiseeeeeeee..........

Ilikuwa yapata kama saa 11 hivi za jioni mzigo ukaitika pale.......boonge ya kishindo, vumbi zito likatimka hewani, banda la mbuzi likaporomoka lote, harufu ya baruti ikasambaa eneo lote......cha kwanza nikakimbia hadi nyumbani, sina amani wazazi wanakimbizana kutafuta watoto wao.

Taarifa za baadae zikatoka......yule jamaa alikatika vidole vitatu vya mkono wa kushoto, ndama wawili wa mbuzi walikufa kifo cha kikatili sana......lakini yote kwa yote yule rafiki yangu (R.I.P) hakusema chochote kuhusu uhusika wangu kwenye kadhia ile.

Mama akajua moja kwa moja kuwa mimi ndio injinia wa ule mpango......jamani nilipigwa sio mchezo, hadi kuna muda nilikuwaga najiuliza kama mama hajawahi kupitia kozi zozote za kijeshi, maana nilipigwa staili zote za kwenye mieleka kuanzia hizi Rko za Rand Orton pigwa sana 619 za Rey Mystereo, chomeshwa kichwa chini kama Under taker, mara nibanwe mguu mmoja huku nimevutwa shingo kwa nyuma John Cena anavyofanyaga.......yani kilikuwa ni kipigo mchanganyiko. hadi nilipokuja kuanza kuangalia mieleka nikajiuliza hawa jamaa walimuiga mama au.......

Hilo likapita.....miezi kadhaa baadae nilikuja kuvurumua msala mwingine mzito sana, kwa kweli siwezi kuuelezea maana ulikuwa uondoke na roho yangu.
We Jamaa Wewe🤣🤣🤣🤣🤣
 
Akili za wanawake wanazijua wenyewe. Wengi hufanya maamuzi ya kuwaletea majuto sana Baadae
Miaka ya 2020+ nipo zangu town napiga mishe zangu mara napokea simu wazazi wanadai tumekutafutia mchumba mkoani inabidi uje kuoa, dah!! Mm sina mpango hata wa kuoa mishe zenyewe za kuunga unga.nikajaribu kupinga wazee wakakomaa dah!

Nikaona isiwe tabu nikapanda ndinga hadi mkoa kufika ndio siku hiyo ya harusi kumcheki bi harusi kumbe nimesoma nae primary,basi harusi imefanyika,kumbe bi harusi nae ana msela wake wakitambo kamuaidi ndoa halafu yupo vizuri kipato,basi msela kapangana na demu wake wanipe msala ndo ishindikane,bi harusi nae wazazi wake wamemkomalia kama mm kwa kua wazazi wanajuana,

Basi tumefunga ndoa tumerudi nyumbani mara anakuja bibi yake bi harusi ananiambia mtoto ni bikra kwaiyo inabidi upige mzigo ili kesho ifanyike sherehe ya kumpongenza binti kwa kujitunza mm nikasema poa tu,kufika usiku si ndio inabidi nipigie show,ile namsaula nifanye ya yangu binti anapinga makelele nyumba nzima watu wameamka.

Kumbe kuna wageni kutoka sehemu mbali mbali walikuja kwenye sherehe,ikabidi wazee waje kujua kulikoni!! Aisee sita sahau binti anasema namlazimisha kumuingilia kinyume na maumbile.mbele ya wazazi wangu,nitafanyaje? Nani ataniamini kumbuka nilikua nakataa kuoa?

Inaoneka nimefanya makusudi dah!! Kulivyo kucha nikapanda bus nikarudi town sikutoka ndani wiki mbili hakuna Alie kua anaamini,ndoa ikaishia hapo,maisha yakaendelea demu akaenda kwa jamaa yake.

Kufika huko sasa kila wakilala mara wasikie wanachapwa bakora mara mauza mauza binti si akarudi kwa wazazi wangu kuomba msamaha na kueleza ukweli wote ulivyokua kuwa alipangwa afenye vile ili ndoa iharibike, kazi ikawa mm wataniambiaje maana nimeshachafuka mbele ya umma,basi nilikaa zaidi ya miaka 15 ndio nikasamehe.

Hivi sasa tuwasiliana kama mtu na rafiki yake japo yy hajapata wa kumuoa mpaka Sasa hivi.
 
Niliiba dawa ya mtoto (mdogo wangu) hizi syrup tamu za watoto, nikaimimina kwenye glass, nikakatakata vipande vya viazi nikaweka mezani najifanya padre naongoza ibada,
ile syrup nimefanya ndio divai na vile vipande vya viazi ndio mkate, wadogo zangu ndio waumini Kipigo nilichokipata siku hiyo sitakisahau,
Dah.... JF.... Halafu Kuna mijitu ilitaka kuua Huu mtandao.... Wafe wao... Hawajui jinsi Gani Familia ya JF Tunaburudika Humu ndani na kusahau Mambo ya too na stress zingine
 
Nimecheka kifala
kuna kota fulani za tanesco sehemu zilikuwa wazi nyumba kama nne hivi,nikiwa mkubwa tu wa form 1.nikagundua uwepo wa nyuki katika moja ya paa la nyumba zile.

kusogea karibu nagundua kumbe wapo pale na wamezalisha na asali kabisa,nikatafakari nini nifanye ili kuivuna asali ile,sijui tu ilikuwajenikachukua manyasi nikayafunga kwenye fito ndefu nchani na kuyatia moto yakaanza kufuka moshi.mchana wa saa saba jua kali ng'ai ng'ai,baharia nataka niwatapeli nyuki asali yao,naona wakasemezana,sijakaa vyema nikachezea kama misumari mitatu hivi ya mkononi na usoni,nikaachia fito na kutoka mbio,hapa ndio niriharibu shughuli sasa.nyuki walisambaa wakafunga mtaa mzima,nikaingia ndani na kuanza kupiga kelele watu wafunge madirisha na milango,bahati yao waliwahi.

sasa aina ile ya kota madirisha yalikuwa ya vioo,watu wote ndani tukawa tunashuhudia watu wanavyopewa kibano na jeshi lililochokozwa mchana wa jua kali,kota zile zilikuwa jirani na za jeshi.wanajeshi waliokuwa wanatoka uraiani kwenda kambini kwao,walikutana na wanajeshi wenzao ambao wamevurugwa zaidi.basi movie ikawa ni kubwaga baiskeri na kutimua mbio itakavyowezekana maana jamaa wanaupiga mwingi sio kawaida.
muda ambao nilijutia upuuzi nilioufanya ni wakati ambao dada wa makamo akiwa na mtoto mgongoni na kuni na jembe katoka shamba,akakutana na wataleban wale,walimpa vitu mpaka akabwaga mtoto chini mbiooo,mtoto akawa analia pale chini,nyumba zote tukaanza kupiga mayowe asimwache pale lakini hasikii maskini,ole wako ufungue hata kioo kimoja waingie ndani,utajua hujuililikuwa tukio baya sana.Mungu mkubwa nyuki wakiwa kwenye taharuki namna ile huwa hawa deal na adui aliyelala.kwahiyo mtoto yule alilizwa na majeraha ya kwanza akiwa mgongoni.aliposhushwa hakuguswa tena.

wale jamaa walitawala anga wakafanikiwa kuchukua nchi ile kwa masaa kadhaa,mpaka jioni saa 11 ndio tukaanza kuona kama pilika zinarudi,watu wanapita bila pingamizi.yule mtoto kalia pale chini mpaka sauti imekauka,tukafungua vioo kwa machale,na kuanza kuelekea kule aliko,tunamkuta hajajeruhiwa kiivyo,ana kauvimbe tu kisogoni.mama yake alirudi usiku kumfata.

kesho yake nikawa mpole sana,jamaa mmoja akaniuliza,uliishawahi ona wapi asali inavunwa kienyeji mchana!!!nimetoa macho tu.
 
Nilipokuwa mdogo katika michezonya kibaba tulioana Mimi na mtoto wa Mama yangu mdogo

Sitosahau tulipiga denda French kiss chini ya shuka

Ile incident inatembea Hadi Leo japo tukikutana no salamu tu sijui yeye anakumbuka
No salam inamaana alichukia mpka leo
 
kuna kota fulani za tanesco sehemu zilikuwa wazi nyumba kama nne hivi,nikiwa mkubwa tu wa form 1.nikagundua uwepo wa nyuki katika moja ya paa la nyumba zile.

kusogea karibu nagundua kumbe wapo pale na wamezalisha na asali kabisa,nikatafakari nini nifanye ili kuivuna asali ile,sijui tu ilikuwajenikachukua manyasi nikayafunga kwenye fito ndefu nchani na kuyatia moto yakaanza kufuka moshi.mchana wa saa saba jua kali ng'ai ng'ai,baharia nataka niwatapeli nyuki asali yao,naona wakasemezana,sijakaa vyema nikachezea kama misumari mitatu hivi ya mkononi na usoni,nikaachia fito na kutoka mbio,hapa ndio niriharibu shughuli sasa.nyuki walisambaa wakafunga mtaa mzima,nikaingia ndani na kuanza kupiga kelele watu wafunge madirisha na milango,bahati yao waliwahi.

sasa aina ile ya kota madirisha yalikuwa ya vioo,watu wote ndani tukawa tunashuhudia watu wanavyopewa kibano na jeshi lililochokozwa mchana wa jua kali,kota zile zilikuwa jirani na za jeshi.wanajeshi waliokuwa wanatoka uraiani kwenda kambini kwao,walikutana na wanajeshi wenzao ambao wamevurugwa zaidi.basi movie ikawa ni kubwaga baiskeri na kutimua mbio itakavyowezekana maana jamaa wanaupiga mwingi sio kawaida.
muda ambao nilijutia upuuzi nilioufanya ni wakati ambao dada wa makamo akiwa na mtoto mgongoni na kuni na jembe katoka shamba,akakutana na wataleban wale,walimpa vitu mpaka akabwaga mtoto chini mbiooo,mtoto akawa analia pale chini,nyumba zote tukaanza kupiga mayowe asimwache pale lakini hasikii maskini,ole wako ufungue hata kioo kimoja waingie ndani,utajua hujuililikuwa tukio baya sana.Mungu mkubwa nyuki wakiwa kwenye taharuki namna ile huwa hawa deal na adui aliyelala.kwahiyo mtoto yule alilizwa na majeraha ya kwanza akiwa mgongoni.aliposhushwa hakuguswa tena.

wale jamaa walitawala anga wakafanikiwa kuchukua nchi ile kwa masaa kadhaa,mpaka jioni saa 11 ndio tukaanza kuona kama pilika zinarudi,watu wanapita bila pingamizi.yule mtoto kalia pale chini mpaka sauti imekauka,tukafungua vioo kwa machale,na kuanza kuelekea kule aliko,tunamkuta hajajeruhiwa kiivyo,ana kauvimbe tu kisogoni.mama yake alirudi usiku kumfata.

kesho yake nikawa mpole sana,jamaa mmoja akaniuliza,uliishawahi ona wapi asali inavunwa kienyeji mchana!!!nimetoa macho tu.
Dah wee boya umenichekesha sana
 
Miaka ya 2020+ nipo zangu town napiga mishe zangu mara napokea simu wazazi wanadai tumekutafutia mchumba mkoani inabidi uje kuoa, dah!! Mm sina mpango hata wa kuoa mishe zenyewe za kuunga unga.nikajaribu kupinga wazee wakakomaa dah!

Nikaona isiwe tabu nikapanda ndinga hadi mkoa kufika ndio siku hiyo ya harusi kumcheki bi harusi kumbe nimesoma nae primary,basi harusi imefanyika,kumbe bi harusi nae ana msela wake wakitambo kamuaidi ndoa halafu yupo vizuri kipato,basi msela kapangana na demu wake wanipe msala ndo ishindikane,bi harusi nae wazazi wake wamemkomalia kama mm kwa kua wazazi wanajuana,

Basi tumefunga ndoa tumerudi nyumbani mara anakuja bibi yake bi harusi ananiambia mtoto ni bikra kwaiyo inabidi upige mzigo ili kesho ifanyike sherehe ya kumpongenza binti kwa kujitunza mm nikasema poa tu,kufika usiku si ndio inabidi nipigie show,ile namsaula nifanye ya yangu binti anapinga makelele nyumba nzima watu wameamka.

Kumbe kuna wageni kutoka sehemu mbali mbali walikuja kwenye sherehe,ikabidi wazee waje kujua kulikoni!! Aisee sita sahau binti anasema namlazimisha kumuingilia kinyume na maumbile.mbele ya wazazi wangu,nitafanyaje? Nani ataniamini kumbuka nilikua nakataa kuoa?

Inaoneka nimefanya makusudi dah!! Kulivyo kucha nikapanda bus nikarudi town sikutoka ndani wiki mbili hakuna Alie kua anaamini,ndoa ikaishia hapo,maisha yakaendelea demu akaenda kwa jamaa yake.

Kufika huko sasa kila wakilala mara wasikie wanachapwa bakora mara mauza mauza binti si akarudi kwa wazazi wangu kuomba msamaha na kueleza ukweli wote ulivyokua kuwa alipangwa afenye vile ili ndoa iharibike, kazi ikawa mm wataniambiaje maana nimeshachafuka mbele ya umma,basi nilikaa zaidi ya miaka 15 ndio nikasamehe.

Hivi sasa tuwasiliana kama mtu na rafiki yake japo yy hajapata wa kumuoa mpaka Sasa hivi.
Aisee, huu msala walikufanyia unyama sana kaka

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom