Benbulugu
JF-Expert Member
- Sep 14, 2016
- 875
- 1,259
Daahhh,mzeebaba umenikumbusha miaka ya2003 huko Niko Kwa uncle around darasa lapili hivi nilikua namtoto wauncle nae alikua darasa latatu,SASA kulikua kipindi cha mavuno ya pamba,kama ujuavyo pamba niuti wamgongo wamaeno ya simiyu nashinyanga,pamba ishavunwa iko ndani inasbiriwa kupelekea mnadani kwamkokoteni wang'ombe,Enzi za utoto wangu nilikuwa mtundu sana aisee.
Siku moja niko home choo chetu na jiko vilikuwa ni vya nyasi,sasa nikakaa nikaangalia zile nyasi kule juu nikasema aaah hivi mchana huu nikiweka njiti ya kiberiti itawaka kweli na kumaliza nyasi zote hizi ?
Faza enzi hizo ni mtata sana yaani.
Basi baada ya kuwaza nikasema sio kesi acha niweke njiti ya kibiriti niwashe nione kama itawaka kwa nyasi zote hizi.
Kidume nikawasha nikatulia kuskilizia mshindo,kuna kimoshi kikatoka alafu kikazimika nikasema aaah kumbe haiwezi kuwasha,nikaendelea kufanya mambo mengine.
Kumbe bhana ule moto ulikolea ndani kwa ndani ukawa unafukuta juu kunatoka moshi mimi niko ndani sina habari.
Kumbuka kuwa hapo nyumbani nilikuwa peke yangu watu wote hawapo.aisee nashangaa kuna mzee jirani yetu anakuja mbio sana anaita nikashangaa anaita nini huyuu ?,anakuja anasema motoooooo mootoooo moyo ukapiga paaap nikajiuliza moto ule nilowasha mie au moto ungine ? Nikajipa moyo nikasema ule wangu ulizimika huu utakuwa ni moto mwingine.
Daaah kutoka nje kutazama juu laaaaaa hawlaaaaa kitu chekunduuuu moto mkubwa unawaka alafu jua kali,daaah aisee nilipata sonona mana hapo sikuwaza tena huo moto bali niliwaza kichapo cha faza na maza maana wote walikuwa watata sana nikizingua.
Daaah basi yule mzee akahangaika sana kuzima ule moto huku mimi nikiwa nimepata butwaa la ghafla na mawazo tele kichwani mithili ya mtu mwenye familia.
Shida ni kwamba
Ilibidi auzime moto ule kwa maji ya ndani kwetu jikoni,na hilo jiko ambalo ndio kuna maji juu ndi kunawaka moto,ama kwa hakika ilikuwa shughuli pevu sana siku hiyo.
Mzee ikabidi ajitoe muhanga akawa anaingia ndani anachukua maji anakuja anazima.
Kwa hiyo nikawa na misala miwili.
1.msala wa kuwasha moto.
2.msala wa kumaliza maji ndani na kkulekwetu kusini maji ilikuwa shida miaka ile mpaka ununue kwa ndoo alafu mimi nakuja kumaliza maji kwa uzembe wa kuwasha moto.
Daaah mwisho mzee kauweza moto ukazimika lakini lile paa la nyumba la nyasi ukiangalia kwa juu ni kama mtu mwenye kipara namna ambavyo lilikuwa likionekana.
Ikabidi mzee anihoji mimi nokampa ukweli wote,na yeye waliporudi wazee akawasimulia kama nilivyomsimulia na hiyo wazazi wakatafsiri kwamba ni upumbavu wangu.
Yule Mzee aliwaasa wazee wangu wasinipige lakini nahisi kwao ilisound"mumpigeee hasaa huyoo"
Daaaah
Daaaah
Daaahh.
Ushawahi kupigwa mpaka inafikia hatua ukipigwa ndo unanyamaza na ukiachwa ndo unalia ?
Nahisi kipigo kile kilicontain kipigo cha kuwasha moto na kipigo cha kumaliza maji na kipigo cha kusumbua wazee wa watu.
Lakini uzuri walikuwa wananipiga maeneo mabayo siwezi kupata madhara makubwa,yani unapigwa maeneo ambayo unasikia maumovu lakini kufa hufi.
Mungu anitunzie wazazi wangu maana bila vile ningelikuwa toto sumbufu sana kwa sababu nilikuwa mtundu sana.
Baada ya soo hili nikasema mimi na majaribio ya kipuuzi baasi tenaaa nimekoma.
Thubuuutuuu...
Nikaja kufanya soo lingine la kuiba aisee(sikumbuki soo gani lilitangulia)
faza kazipanga shilingi mia nyingi usikuu mezani tena chumbani kwake.
Mimi nikavizia faza na maza wako nje kwa kujiamini nikasema hawaingii saivi,kidume nikazama ndani fresh.
Nilipozama ndani nikachomoa mia ya chini hizi za juu zikaparaganyika,nikashindwa kuzipanga.
Ishu nikajiuliza sasa faza kaijua kama nimeiba 100 itakuwaje ? Kidume nikasema solution ni kutawanya hizi pesa pururu mpararo tuu kama mbwai na iwe mbwai,basi kwa ujinga nikazitawanya zile pesa kama hazikupangwa vile alafu nikaondoka na shilingi mia yangu.
Daaaah ishu ikabuma tena siku hiyo usiku baba na mama wapo wote.
Mama alinitandika saana na kamba za ukili mpaka akili ikakaa sawa.
Ila huu ni wakati wa utoto sana around miaka 4- 7,umri huu mara nyingi mtoto anaona akipigwa naaonewa.
Usiku ulipongia tuko namtoto wauncle tukawa nakibatari kumbuka ndugu msomaji huku nivijijini nakujua naumeme kwahyo chanzo cha nishati nyakati zausiku nikibatari,ikawa tumewasha pale kibatari huku tumebaki nanjiti zaviberiti mikononi huku tukiwa tunavikoleza ktk miale yakinatari pale njiti kadhaa,zinakua zinatoa mlio wa" chwaaAAA"TULIFANYA vile mara kadhaa tukiharibu njiti zakiberiti ,ikafikia Mda tukaanza kubishana hivi hakackanjiti kakibwriti kanaweza kuchoma pamba yote hiii??mwingine anasema hakawezi namm nasema haiwezekani basi tujaribu ,nikachukia njiti yakiberiti nakuiweka ktk kibatari kinachowaka kisha nikakitupia ktk pamba,
Kusema kweli ndugu msomaji ilikua nijanga kubwa Sana kuwahi kutoa tulihangaika kuzima pamba ple namke WA uncle bila mafanikio,akapiga Kelele kuiwaita wanakijiji ili kuja kuzima Moto manaa ulikua mkubwa kiais cha kuleta taharuki,ilikufupisha story ,tulionekana buana watukutu natukaenda kuswekwa selo nakuleta hasara ya mamilioni ya pesa kwasababu haikuwaingia akilini,tulichapwa sticks mbele yahadhara viboko ishirini kila mmoja,nakupewa adhabu yakutolwenda shule week nzima nakuhakikisha tunachambua pamba Safi nailiyoungua ili ilikauzwe ,