JUDIKAY
Senior Member
- Jul 20, 2021
- 104
- 157
Enzi hizo sasa ukikaribia mwaka mpya mnatengeneza vi baruti mnaweka kwenye vichwa vya spoku za baiskeli mkiona watu wamekaa mnavitest pwaaaa watu wakishituka mnakimbia kwa furaha, lengo ni kwamba ikifika saa 6:01 kuanza mwaka mwingine mnavipiga kama kusherehekea mwaka mpya (watoto wa siku hizi hawayajui hayo)......
Basi bwana mwaka fulani huo nilidhamiria kuvunja rekodi ya kutengeneza baruti itakayounguruma kuzidi baruti nyingine zote pale mtaani na ikibidi mitaa ya jirani, mzee wangu alikuwa fundi makenika, kwenye makorokoro yake nilipata jeki moja ndogo ambayo ilikuwa imetolewa utumbo ikabaki wazi katikati.
Kuna kaka yangu alikuwaga ametoka Moshi (kama sikosei), huko alikuwa anafanya kazi kiwanda cha kutengeneza viberiti, alikuja na kisado kizima kimejaa unga wa baruti (sijui nae alikileta kwa madhumuni gani tu).....mi nikaiba ule unga wa baruti kwa ajili ya kutengeneza mzinga wangu.
Siku ya tar 31 December nikafanya maandalizi yote, lakini nikapata wazo moja kwamba sitoweza kwenda kukamua ile device pale ili kusababisha mlipuko, nilichokifanya nikategesha jiwe zito juu ya usawa wa lile komboro langu, nilikuwa nimelitega nyuma ya banda la mbuzi nyumba ya jirani yetu........
Bwana weeeeeee.......
Nikamshirikisha kijana wa ile nyumba ambae tulikuwa rika moja tu kuhusu mpango wangu, akataka aende akaangalie.....kufika akakuta nilivyolitega akasema eti nimekosea, akaanza kuliseti upya......
Aiseeeeeeee..........
Ilikuwa yapata kama saa 11 hivi za jioni mzigo ukaitika pale.......boonge ya kishindo, vumbi zito likatimka hewani, banda la mbuzi likaporomoka lote, harufu ya baruti ikasambaa eneo lote......cha kwanza nikakimbia hadi nyumbani, sina amani wazazi wanakimbizana kutafuta watoto wao.
Taarifa za baadae zikatoka......yule jamaa alikatika vidole vitatu vya mkono wa kushoto, ndama wawili wa mbuzi walikufa kifo cha kikatili sana......lakini yote kwa yote yule rafiki yangu (R.I.P) hakusema chochote kuhusu uhusika wangu kwenye kadhia ile.
Mama akajua moja kwa moja kuwa mimi ndio injinia wa ule mpango......jamani nilipigwa sio mchezo, hadi kuna muda nilikuwaga najiuliza kama mama hajawahi kupitia kozi zozote za kijeshi, maana nilipigwa staili zote za kwenye mieleka kuanzia hizi Rko za Rand Orton pigwa sana 619 za Rey Mystereo, chomeshwa kichwa chini kama Under taker, mara nibanwe mguu mmoja huku nimevutwa shingo kwa nyuma John Cena anavyofanyaga.......yani kilikuwa ni kipigo mchanganyiko. hadi nilipokuja kuanza kuangalia mieleka nikajiuliza hawa jamaa walimuiga mama au.......
Hilo likapita.....miezi kadhaa baadae nilikuja kuvurumua msala mwingine mzito sana, kwa kweli siwezi kuuelezea maana ulikuwa uondoke na roho yangu.
[emoji23][emoji23][emoji23]