Msala ambao siwezi usahau kamwe

Msala ambao siwezi usahau kamwe

Enzi za utoto wangu nilikuwa mtundu sana aisee.

Siku moja niko home choo chetu na jiko vilikuwa ni vya nyasi,sasa nikakaa nikaangalia zile nyasi kule juu nikasema aaah hivi mchana huu nikiweka njiti ya kiberiti itawaka kweli na kumaliza nyasi zote hizi ?

Faza enzi hizo ni mtata sana yaani.

Basi baada ya kuwaza nikasema sio kesi acha niweke njiti ya kibiriti niwashe nione kama itawaka kwa nyasi zote hizi.

Kidume nikawasha nikatulia kuskilizia mshindo,kuna kimoshi kikatoka alafu kikazimika nikasema aaah kumbe haiwezi kuwasha,nikaendelea kufanya mambo mengine.

Kumbe bhana ule moto ulikolea ndani kwa ndani ukawa unafukuta juu kunatoka moshi mimi niko ndani sina habari.

Kumbuka kuwa hapo nyumbani nilikuwa peke yangu watu wote hawapo.aisee nashangaa kuna mzee jirani yetu anakuja mbio sana anaita nikashangaa anaita nini huyuu ?,anakuja anasema motoooooo mootoooo moyo ukapiga paaap nikajiuliza moto ule nilowasha mie au moto ungine ? Nikajipa moyo nikasema ule wangu ulizimika huu utakuwa ni moto mwingine.

Daaah kutoka nje kutazama juu laaaaaa hawlaaaaa kitu chekunduuuu moto mkubwa unawaka alafu jua kali,daaah aisee nilipata sonona mana hapo sikuwaza tena huo moto bali niliwaza kichapo cha faza na maza maana wote walikuwa watata sana nikizingua.

Daaah basi yule mzee akahangaika sana kuzima ule moto huku mimi nikiwa nimepata butwaa la ghafla na mawazo tele kichwani mithili ya mtu mwenye familia.

Shida ni kwamba
Ilibidi auzime moto ule kwa maji ya ndani kwetu jikoni,na hilo jiko ambalo ndio kuna maji juu ndi kunawaka moto,ama kwa hakika ilikuwa shughuli pevu sana siku hiyo.

Mzee ikabidi ajitoe muhanga akawa anaingia ndani anachukua maji anakuja anazima.

Kwa hiyo nikawa na misala miwili.

1.msala wa kuwasha moto.

2.msala wa kumaliza maji ndani na kkulekwetu kusini maji ilikuwa shida miaka ile mpaka ununue kwa ndoo alafu mimi nakuja kumaliza maji kwa uzembe wa kuwasha moto.

Daaah mwisho mzee kauweza moto ukazimika lakini lile paa la nyumba la nyasi ukiangalia kwa juu ni kama mtu mwenye kipara namna ambavyo lilikuwa likionekana.

Ikabidi mzee anihoji mimi nokampa ukweli wote,na yeye waliporudi wazee akawasimulia kama nilivyomsimulia na hiyo wazazi wakatafsiri kwamba ni upumbavu wangu.

Yule Mzee aliwaasa wazee wangu wasinipige lakini nahisi kwao ilisound"mumpigeee hasaa huyoo"

Daaaah

Daaaah

Daaahh.

Ushawahi kupigwa mpaka inafikia hatua ukipigwa ndo unanyamaza na ukiachwa ndo unalia ?

Nahisi kipigo kile kilicontain kipigo cha kuwasha moto na kipigo cha kumaliza maji na kipigo cha kusumbua wazee wa watu.

Lakini uzuri walikuwa wananipiga maeneo mabayo siwezi kupata madhara makubwa,yani unapigwa maeneo ambayo unasikia maumovu lakini kufa hufi.

Mungu anitunzie wazazi wangu maana bila vile ningelikuwa toto sumbufu sana kwa sababu nilikuwa mtundu sana.

Baada ya soo hili nikasema mimi na majaribio ya kipuuzi baasi tenaaa nimekoma.

Thubuuutuuu...

Nikaja kufanya soo lingine la kuiba aisee(sikumbuki soo gani lilitangulia)

faza kazipanga shilingi mia nyingi usikuu mezani tena chumbani kwake.

Mimi nikavizia faza na maza wako nje kwa kujiamini nikasema hawaingii saivi,kidume nikazama ndani fresh.

Nilipozama ndani nikachomoa mia ya chini hizi za juu zikaparaganyika,nikashindwa kuzipanga.

Ishu nikajiuliza sasa faza kaijua kama nimeiba 100 itakuwaje ? Kidume nikasema solution ni kutawanya hizi pesa pururu mpararo tuu kama mbwai na iwe mbwai,basi kwa ujinga nikazitawanya zile pesa kama hazikupangwa vile alafu nikaondoka na shilingi mia yangu.

Daaaah ishu ikabuma tena siku hiyo usiku baba na mama wapo wote.

Mama alinitandika saana na kamba za ukili mpaka akili ikakaa sawa.

Ila huu ni wakati wa utoto sana around miaka 4- 7,umri huu mara nyingi mtoto anaona akipigwa naaonewa.
Wewe misala yako kama yangu,nilitia moto jiko likaungua lote ila msala alipewa braza kwa uzembe,nikaiba pesa za Mzee kidogo kidogo kama shilingi mia nane ,nilitandikwa balaa.Siwezi andika kwa kirefu Nina uzembe wa kuandika.
 
Enzi hizo sasa ukikaribia mwaka mpya mnatengeneza vi baruti mnaweka kwenye vichwa vya spoku za baiskeli mkiona watu wamekaa mnavitest pwaaaa watu wakishituka mnakimbia kwa furaha, lengo ni kwamba ikifika saa 6:01 kuanza mwaka mwingine mnavipiga kama kusherehekea mwaka mpya (watoto wa siku hizi hawayajui hayo)......

Basi bwana mwaka fulani huo nilidhamiria kuvunja rekodi ya kutengeneza baruti itakayounguruma kuzidi baruti nyingine zote pale mtaani na ikibidi mitaa ya jirani, mzee wangu alikuwa fundi makenika, kwenye makorokoro yake nilipata jeki moja ndogo ambayo ilikuwa imetolewa utumbo ikabaki wazi katikati.

Kuna kaka yangu alikuwaga ametoka Moshi (kama sikosei), huko alikuwa anafanya kazi kiwanda cha kutengeneza viberiti, alikuja na kisado kizima kimejaa unga wa baruti (sijui nae alikileta kwa madhumuni gani tu).....mi nikaiba ule unga wa baruti kwa ajili ya kutengeneza mzinga wangu.

Siku ya tar 31 December nikafanya maandalizi yote, lakini nikapata wazo moja kwamba sitoweza kwenda kukamua ile device pale ili kusababisha mlipuko, nilichokifanya nikategesha jiwe zito juu ya usawa wa lile komboro langu, nilikuwa nimelitega nyuma ya banda la mbuzi nyumba ya jirani yetu........

Bwana weeeeeee.......

Nikamshirikisha kijana wa ile nyumba ambae tulikuwa rika moja tu kuhusu mpango wangu, akataka aende akaangalie.....kufika akakuta nilivyolitega akasema eti nimekosea, akaanza kuliseti upya......

Aiseeeeeeee..........

Ilikuwa yapata kama saa 11 hivi za jioni mzigo ukaitika pale.......boonge ya kishindo, vumbi zito likatimka hewani, banda la mbuzi likaporomoka lote, harufu ya baruti ikasambaa eneo lote......cha kwanza nikakimbia hadi nyumbani, sina amani wazazi wanakimbizana kutafuta watoto wao.

Taarifa za baadae zikatoka......yule jamaa alikatika vidole vitatu vya mkono wa kushoto, ndama wawili wa mbuzi walikufa kifo cha kikatili sana......lakini yote kwa yote yule rafiki yangu (R.I.P) hakusema chochote kuhusu uhusika wangu kwenye kadhia ile.

Mama akajua moja kwa moja kuwa mimi ndio injinia wa ule mpango......jamani nilipigwa sio mchezo, hadi kuna muda nilikuwaga najiuliza kama mama hajawahi kupitia kozi zozote za kijeshi, maana nilipigwa staili zote za kwenye mieleka kuanzia hizi Rko za Rand Orton pigwa sana 619 za Rey Mystereo, chomeshwa kichwa chini kama Under taker, mara nibanwe mguu mmoja huku nimevutwa shingo kwa nyuma John Cena anavyofanyaga.......yani kilikuwa ni kipigo mchanganyiko. hadi nilipokuja kuanza kuangalia mieleka nikajiuliza hawa jamaa walimuiga mama au.......

Hilo likapita.....miezi kadhaa baadae nilikuja kuvurumua msala mwingine mzito sana, kwa kweli siwezi kuuelezea maana ulikuwa uondoke na roho yangu.
Huku Daslamu wanatengeneza sana
 
Uzi unatutaka tueleze mikasa ya kutisha sisi tunaeleza ya utotoni
C'mon guys tuna mikasa inayotisha zaidi ya ukubwani wekeni hapa
 
Ulimtafuna mtoto wa mjomba..😂😂😂

Ova
 
sitosahau miaka hiyo mtaani ziliingia baskeli fulani za kukodi,ilikua lisaa limoja ni sh 100 kama sikosei.sasa nyumbani kulikua na ng`ombe na mchungaji alikua kazinguliwa na mzee akawa amesepa hivyo nikaambiwa nifungulie ng`ombe nichunge chunge,basi bana nikatoa ng`ombe zikawa zinakula kula pale gafla akili ya kuchukua baskeli ya kukodi ikanijia mbaya zaidi baskeli wanazokodisha ni zile mountain ndogo za watoto zilinizuzua sana akili kipindi hicho,nikakodi baskeli pale ebana nikaenda mbali si nikasahau kama nilikua nachunga,ndama mmoja alikua anavuka akagongwa na gari mimi sina habari,akili ikanirud lisaa ndio linakaribia kuisha nirudishe baskel ya watu ukizingatia ilikua ukizidisha hata dakika tano unalipa mia ingine,nikapaki baskeli na kulipa gafla bin vuu mzee huyu hapa kanikamata sitosahau siku ile nilishushiwa kipigo heavy na mzee halafu mixer mapigo flani hivi kama karatee.unapigwa unapigwa mpk mwili unakua uashazoea husikii kitu wala machozi hayatoki,sorry kwa uandishi mbovu
 
sitosahau miaka hiyo mtaani ziliingia baskeli fulani za kukodi,ilikua lisaa limoja ni sh 100 kama sikosei.sasa nyumbani kulikua na ng`ombe na mchungaji alikua kazinguliwa na mzee akawa amesepa hivyo nikaambiwa nifungulie ng`ombe nichunge chunge,basi bana nikatoa ng`ombe zikawa zinakula kula pale gafla akili ya kuchukua baskeli ya kukodi ikanijia mbaya zaidi baskeli wanazokodisha ni zile mountain ndogo za watoto zilinizuzua sana akili kipindi hicho,nikakodi baskeli pale ebana nikaenda mbali si nikasahau kama nilikua nachunga,ndama mmoja alikua anavuka akagongwa na gari mimi sina habari,akili ikanirud lisaa ndio linakaribia kuisha nirudishe baskel ya watu ukizingatia ilikua ukizidisha hata dakika tano unalipa mia ingine,nikapaki baskeli na kulipa gafla bin vuu mzee huyu hapa kanikamata sitosahau siku ile nilishushiwa kipigo heavy na mzee halafu mixer mapigo flani hivi kama karatee.unapigwa unapigwa mpk mwili unakua uashazoea husikii kitu wala machozi hayatoki,sorry kwa uandishi mbovu
learning the hard way
 
Shule tuliambiwa Carbondioxide inazima moto, nikawaza zile dawa za kupuliza zinauaje wadudu nikajifikirisha nikasema itakuwa pia ina Carbondioxide hivyo ukiwapulizia inawazima pia, basi buana nikarudi home nikachukua utambi wa jiko la mchina ulioisha jikon nikautia kiberiti unawaka sawa sawa, nikaenda chumbani kuchukua dawa ya kupulizia enzi zile rungu ndio inaanza anza, nikaja kupulizia kwenye moto ili uzime, kilichotokea sasa..........
dumb ways to die ingia you tube andika hivyo
 
kuna kota fulani za tanesco sehemu zilikuwa wazi nyumba kama nne hivi,nikiwa mkubwa tu wa form 1.nikagundua uwepo wa nyuki katika moja ya paa la nyumba zile.

kusogea karibu nagundua kumbe wapo pale na wamezalisha na asali kabisa,nikatafakari nini nifanye ili kuivuna asali ile,sijui tu ilikuwajenikachukua manyasi nikayafunga kwenye fito ndefu nchani na kuyatia moto yakaanza kufuka moshi.mchana wa saa saba jua kali ng'ai ng'ai,baharia nataka niwatapeli nyuki asali yao,naona wakasemezana,sijakaa vyema nikachezea kama misumari mitatu hivi ya mkononi na usoni,nikaachia fito na kutoka mbio,hapa ndio niriharibu shughuli sasa.nyuki walisambaa wakafunga mtaa mzima,nikaingia ndani na kuanza kupiga kelele watu wafunge madirisha na milango,bahati yao waliwahi.

sasa aina ile ya kota madirisha yalikuwa ya vioo,watu wote ndani tukawa tunashuhudia watu wanavyopewa kibano na jeshi lililochokozwa mchana wa jua kali,kota zile zilikuwa jirani na za jeshi.wanajeshi waliokuwa wanatoka uraiani kwenda kambini kwao,walikutana na wanajeshi wenzao ambao wamevurugwa zaidi.basi movie ikawa ni kubwaga baiskeri na kutimua mbio itakavyowezekana maana jamaa wanaupiga mwingi sio kawaida.
muda ambao nilijutia upuuzi nilioufanya ni wakati ambao dada wa makamo akiwa na mtoto mgongoni na kuni na jembe katoka shamba,akakutana na wataleban wale,walimpa vitu mpaka akabwaga mtoto chini mbiooo,mtoto akawa analia pale chini,nyumba zote tukaanza kupiga mayowe asimwache pale lakini hasikii maskini,ole wako ufungue hata kioo kimoja waingie ndani,utajua hujuililikuwa tukio baya sana.Mungu mkubwa nyuki wakiwa kwenye taharuki namna ile huwa hawa deal na adui aliyelala.kwahiyo mtoto yule alilizwa na majeraha ya kwanza akiwa mgongoni.aliposhushwa hakuguswa tena.

wale jamaa walitawala anga wakafanikiwa kuchukua nchi ile kwa masaa kadhaa,mpaka jioni saa 11 ndio tukaanza kuona kama pilika zinarudi,watu wanapita bila pingamizi.yule mtoto kalia pale chini mpaka sauti imekauka,tukafungua vioo kwa machale,na kuanza kuelekea kule aliko,tunamkuta hajajeruhiwa kiivyo,ana kauvimbe tu kisogoni.mama yake alirudi usiku kumfata.

kesho yake nikawa mpole sana,jamaa mmoja akaniuliza,uliishawahi ona wapi asali inavunwa kienyeji mchana!!!nimetoa macho tu.

Daaah we jamaa kiboko aisee umeniongezea siku ya kuishi
 
Miaka ya 2020+ nipo zangu town napiga mishe zangu mara napokea simu wazazi wanadai tumekutafutia mchumba mkoani inabidi uje kuoa, dah!! Mm sina mpango hata wa kuoa mishe zenyewe za kuunga unga.nikajaribu kupinga wazee wakakomaa dah!

Nikaona isiwe tabu nikapanda ndinga hadi mkoa kufika ndio siku hiyo ya harusi kumcheki bi harusi kumbe nimesoma nae primary,basi harusi imefanyika,kumbe bi harusi nae ana msela wake wakitambo kamuaidi ndoa halafu yupo vizuri kipato,basi msela kapangana na demu wake wanipe msala ndo ishindikane,bi harusi nae wazazi wake wamemkomalia kama mm kwa kua wazazi wanajuana,

Basi tumefunga ndoa tumerudi nyumbani mara anakuja bibi yake bi harusi ananiambia mtoto ni bikra kwaiyo inabidi upige mzigo ili kesho ifanyike sherehe ya kumpongenza binti kwa kujitunza mm nikasema poa tu,kufika usiku si ndio inabidi nipigie show,ile namsaula nifanye ya yangu binti anapinga makelele nyumba nzima watu wameamka.

Kumbe kuna wageni kutoka sehemu mbali mbali walikuja kwenye sherehe,ikabidi wazee waje kujua kulikoni!! Aisee sita sahau binti anasema namlazimisha kumuingilia kinyume na maumbile.mbele ya wazazi wangu,nitafanyaje? Nani ataniamini kumbuka nilikua nakataa kuoa?

Inaoneka nimefanya makusudi dah!! Kulivyo kucha nikapanda bus nikarudi town sikutoka ndani wiki mbili hakuna Alie kua anaamini,ndoa ikaishia hapo,maisha yakaendelea demu akaenda kwa jamaa yake.

Kufika huko sasa kila wakilala mara wasikie wanachapwa bakora mara mauza mauza binti si akarudi kwa wazazi wangu kuomba msamaha na kueleza ukweli wote ulivyokua kuwa alipangwa afenye vile ili ndoa iharibike, kazi ikawa mm wataniambiaje maana nimeshachafuka mbele ya umma,basi nilikaa zaidi ya miaka 15 ndio nikasamehe.

Hivi sasa tuwasiliana kama mtu na rafiki yake japo yy hajapata wa kumuoa mpaka Sasa hivi.
Wanawake ni mapepo sana
 
Enzi hizo bhana bhana kipindi nipo form 2 katika shule flani hapa jijini Dar niliibaga gari nyumbani nikapata msala wa ajali,sasa ilikua hivi pale shuleni ilikua ni lazima form 2 wote kwenda shule siku za jumamosi na mimi nilikua simaind michongo ya kwenda shule jumamosi maana ilikua ndo siku yangu ya kuiba gari(Noah voxy)ya mzee na kula misele.

Ilikua ni rahisi kuiba gari na kula misele siku za jumamosi kwa sababu mbili,ya kwanza ni kwa sababu nyumbani hakuna sehemu ya kulaza gari so tulikua tunalipeleka sehemu wanapo laza magari na sababu ya pili ni kwamba siku za ijumaa mzee alikua anaenda kanisani kwenye mkesha kwahyo alikua anachelewa sana kuamka na kutoka nyumbani jumamosi alikua anatoka nyumbani saa nne au saa tano asubuhi sasa haya masaa manne Mimi ndo nilikua nayatumia vizuri

Basi bhana ulikua ndo mchezo wangu kila jumamosi najua nina masaa yangu manne saa moja mpaka saa nne asubuhi ya kupiga misele.Na sio kwamba nilikua nakatazwa kuendesha gari,hapana nilikua naruhisiwa kuendesha maana Mara nyingi mm au bro wangu ndo tulikua tunapeana zamu ya kwenda kulaza gari usiku na kulitoa asubuhi na kuliweka maeneo karibu na nyumbani so nilikua dereva mzuri na kuaminika na sometimes nilikua napeleka familia kanisani japokua sikuwa na leseni kwa sababu sikuwa nimefikisha miaka 18 ila tu sikuwa naruhusiwa kuchukua gari na kwenda ninapotaka mimi so nikipataga chance ya kuchukua ndiga basi naitumia ipasavyo,


Basi bhana siku za jumamosi saa moja mpaka saa nne asubuhi wakati wenzangu wakiwa shule mm ndo ilikua siku yangu ya misele na mara nyingi nilikua naendaga kwa mwanangu flani classmate wangu anaitwa Emma nae mambo yake kama mm tu na yeye anaiba gari kwao tunateleza,na alikua anakaa maeneo karibu na shule tunayosoma so tulikua tuna chukua credit sana kwa mademu na washkaji pale shule mpaka kuna jamaa pale shule akaniambia nimfundishe kuendesha gari akasema atatoa hela ya mafuta,nikamwambia freshi skilizia jumamosi basi jumamosi ikafika kama kawaida nikachukua funguo maana funguo ya gari ina sehemu yake special ya kuwekwa ilikua inawekwa kwenye showcase ya tv sebuleni so nikabeba funguo nikasepa nikamuelekeza mshkaji kuendesha then nikarudi home.


Twende Kwenye tukio lenyewe sasa, basi bhana siku yangu pendwa ya jumamosi ikafika nikaamka zangu saa kumi na mbili asubuhi nikabeba funguo ya gari huyoo nikaenda nikachukua gari nikaenda kwa mwanangu Emma lakini hakuwepo so nikageuza nikaendelea kuzunguka zunguka nilivomaliza mizunguko yangu apo mida ya saa tatu asubuh ivi nikawa narudi home sasa njiani nikapishana na jamaa flani nasoma nae shule moja ila yeye yupo kidato cha tatu alikua anaenda shule,
Akanisimamisha akaniambia naomba lifti hadi shule,nikamwambia mi nimechelewa narudisha gari nyumbani saiv,akasema poa akaendelea zake kutembea basi bhana mi nikaendelea ila sijui kiherehere gani kika niambia geuza kampe mshkaji lifti awahi shule japokua shule haikua mbali basi nikaenda mbele chap nikageuza.

Nikamfata mshkaji nikampa lifti mpaka shule tulivofika maeneo ya shule nikapaki nje ya fence ya shule lakini sio getini jamaa akanishukuru pale then akashuka akasepa,
Sasa ile sehem niliosimama na gari ni pembezoni mwa barabara yani niliitoa pembeni kidogo kama vile daladala zinavyosimamaga upande wa kushoto kuchukua abiria wa barabarani,sasa baada ya kumshusha mshkaji ilibidi nigeuze gari nirudi nilipotoka sasa nikacheck Kwenye side mirror kama Kuna gari inakuja nikaona hakuna so nikaitia gari barabarani ili nigeuze nisepe so gari nikaiweka katikati ya barabara yan Kama nimeziba njia hivi asa ile nimeiweka tu doh nikaskia kwa mbali honi na kufumba na kufumbua nikaskia kishindo kizito baaang!! ilikua ni bodaboda imekuja direct kujibamiza Kwenye mlango wa upande wa dereva na yule dereva wa boda boda akaangukia mtaroni na pikipiki ikaanguka kivyake dah nilibanwa na uharisho hapo hapo kwa hofu na nikaanza kuskia makelele ya watu wakisema kaua huyo kaua dah nilizidi kupagawa ukizingatia gari nimechukua bila ruhusa,sina leseni na sikuwa nimefikisha miaka 18.


Sasa pale akili ikawa na mambo mawili moja either nigeuze ndiga nisepe au nibaki ila nikaona wazo la kukimbia sio zuri maana maeneo hayo kulikua na kijiwe cha bodaboda kwahyo Kama ningekimbia lazima wangenifukuzia so nikaona hapa jambo la busara ni kutokimbia basi nikaitoa gari barabarani maana ilikua katikati ya barabara nikapaki pembeni, sasa nataka nishuke nafungua mlango haufunguki maana mlango wa upande wa dereva Ndo uliobamizwa ila nikajaribu kuufungua kwa nguvu ndo ukafunguka dah nikaona mlango umebonyezwa sana ndo nikazidi kuishiwa nguvu nitajibu nini nyumbani haha dah basi watu wakaja wakaniambia dogo ongea na huyo boda boda muyamalize mambo ya barabarani haya yanatokea nikawalewa basi yule boda boda akaiokota pikipiki yake afu akanifata amekasirika kweli jamaa alikua mweusi tiii afu anasura ngumu kweli huku sura yake ikiwa na vumbi kutokana na mzinga alioupata.


Nashukuru Mimi sikupata majeraha yoyote na yule dereva wa boda boda hakuumia pia ila mlango wa gari ndo ulibamizwa ukabonyea kwa ndani na pikipiki ilipinda steling.
Sasa wakati naongea na yule dereva wa boda boda alikuja mzee mmoja amevaa kiraia ameshika notebook na nilivomuona nikajua ni askari ila sikuwa na uhakika, sasa yule mzee akaniulza dogo una leseni? Aisee nilihisi kujinyea kwan nikajua moja kwa moja huyu ni askari,basi ikabidi nidanganye nikamwambia leseni ninayo nimeacha nyumbani, alivoskia vile akaondoka zake na alivosepa nikapata amani kidogo kumbe hakua askari ni raia tu.


Baada ya watu kuona ile ajali haina madhara na hakuna aliyeumia wakatuacha mm na Yule boda boda tumalizane,Jamaa akaniambia dogo Mimi sijaumia ila pikipiki yangu imepinda steling tunafanyaje sasa,maana kosa lilikua langu kuingiza gari bila tahadhari.sasa jamaa anataka nimlipe hela akatengeneze pikipiki yake na mimi mfukoni nilikua nina buku tu,(kumbuka nilikua form two) lakini nyumbani nilikua na akiba kama elfu hamsini hivi ambazo nilikua nasave kutoka Kwenye pocket money nilizokua napewa.Nilimwambia yule bodaboda ntakupa elfu ishirini ambayo iko nyumbani so aniache niende nikachukue afu nimletee akaniambia dogo siwezi kukuamini unaweza ukaenda usirudi,ila nilikua na simu Nokia Asha 200 nikamwambia basi naweka simu bond kaa nayo mm nikachukue hela ila tu nielekeze kijiwe chako na jina lako ndo ntakuletea hela unipe simu yangu. Jamaa akakubali akanielekeza kijiwe chake na jina lake maarufu ili nikimuulizia nimpate kirahisi basi nikampa simu kama bond.


Nikawasha gari nikaanza kurudi home kuchukua hela,nilikua na mawazo sana gari nililiona chungu na sijui nitajibu nini nyumbani, wakati nipo njiani kuna garage nikaona nikapata wazo la kwenda basi nikaingia garage ili nione Kama naweza kusolve msala.Nikaonana na fundi wa body za magari nikamueleza kilichotokea pale nikamwambia anisaidie kama mdogo wake maana nishaharibu na sijui nitajibu nn nyumbani,yule fundi akaniambia hapa kwa haraka haraka naweza tu nikasawazisha sehem iliyobonyezwa japokua haitokua kama zamani,nikamuuliza je nikitaka urekebishe irudi kama zamani akasema gharama zitaongezeka na sio zoezi la siku moja ili kunyoosha na kupiga rangi dah nilizidi kuishiwa nguvu.Hapo ni mida ya saa nne asubuhi. Tulichokubalina na fundi ni kwamba asawazishe tu kienyeji sehemu ilyobonyea basi na akanipa ujanja kwamba we ukienda nyumbani kaseme uligongwa na boda boda ndo akakupeleka gereji kurekebisha sehemu aliyokugonga hapo utakua umepata cha kujitetea nikasema sawa.


Fundi nilimwambia nitampa elfu ishirini akakubali ila nikamwambia hapa hela mfukoni sina (kumbuka nilikua nina buku tu) nikamwambia Kama vipi niende nyumbani nikachukue nikuletee akasema sawa wewe acha gari hapa mi nirekebishe wewe nenda kachukue hela hadi ukirudi ntakua nshamaliza.Basi nikaacha gari pale gereji fundi arekebishe mi nikapanda daladala ili niende home nikachukue hela chap nirudi. Mpaka hapo nilikua nadaiwa na dereva boda boda na fundi.jumla ya elfu Arobaini.Aisee bahati nzuri nilikua na akiba nyumbani. Nilivofika nyumbani nikamkuta mzee bado kalala na hiyo ikawa faida kwa upande wangu,nikazama chumbani kwangu chap nikabeba ile elfu hamsini,na nilikua na baskeli yangu mountain bike ina gear 10 nikachukua nikapiga pedeli kurudi gereji,ile siku nilinyonga baskeli kama nipo Kwenye Olympic.


Nilivofika gereji nikakuta fundi kashanyoosha body hivo hivo kienyeji ndo alikua anamalizia kufunga power window,alivomaliza nikampa elfu ishirini yake pale.Gari ilinyooka lakini haikua kama zamani maana kulikua na mabonde mabonde ila ni afadhali kidogo tofaut na hapo mwanzo ulivokua umebonyea kabisa,nilivomalizana na fundi nikapakia baskeli Kwenye gari ili niende kwa yule boda boda sasa.nilivofika kijiweni kwake nikamuona na yeye akaniona basi na yeye nikampa elfu ishirini yake na yeye akanipa simu yangu tukamalizana.Hakika ile ilikua jumamosi yenye majuto.


Nikaanza safari ya kurudi nyumbani sasa ili nirudishe gari,wakati nipo njiani nilikua na mawazo kinoma ila ndo ishatokea tena apo liwalo na liwe.Nilivofika gari nikaipaki maeneo ya karibu na nyumbani. Kisha nikaenda zangu nikarudisha funguo inapokaga nikajikausha kimyaa.Nilimkuta mzee ndo anajiandaa kutoka mida ya saa tano asubuhi, basi akachukua funguo akatoka,baada ya dakika kadhaa akarudi akiwa kavimba akaniuliza gari nimeifanya nn,Nikamwambia kile alichoniambia yule fundi kule gereji kwamba kuna boda boda alinigonga ndo akanipeleka gereji kunirekebishia,mzee aliwaka sana kwann sikumwambia mapema wakati tukio limetokea,nikamwambia ila boda boda alivonigonga alinitengenezea akasema sasa pale ndo ametengeneza nini gari ina mabonde mabonde unasema katengeneza basi mzee akafoka pale mi nipo kimya tu alivomaliza akasepa nashukuru hakunishushia kipigo.


Basi mzee alivosepa na kesi ikaisha maana hakuongelea tena hilo swala na Mimi nikajiapiza sitokuja kuendesha tena lile gari,na mzee akawa funguo haiachi hovyo kama zamani inafichwa kusikojulikana na baada ya muda mzee akaipeleka gari kunyooshwa upya na ikapigwa rangi gari nzima japokua nilijiapiza kutoendesha tena ila baada ya muda kupita hiyo ishu ikabaki story na nikaendelea na misele Kama kawa
 
Hahaha...dah

Kuna misala imenifanya nicheke sana, msala wa nyuki, sakramenti ya syrup na baruti...😁
 
Huu uzi mzuri sanaa, uzuri ni kwamba binadamu tunasahau haraka sana.
Tunarudi kule kuleee
IMG-20220106-WA0010.jpg
 
Mimi nilikuwa na kidemu flani amazing sana kimefungashia hatari kitoto cha form 3 mimi nipo chuo, mwaka wa kwanza, nikua nimepanga jirani basi kila usiku kinakuja napiga kinasepa mwanzo nikua natumia kondom mara kukazoea nikaanza kavu

Basi siku moja rafiki zake wakaja wakanikuta nimetulia zangu nje na headphone kubwa masikioni mara naitwa naambiwa najua unatembea flani ila usikubali kufanyanae pekupeku maana ana VVU ha ha ha ha ha ebama eheeee niliisi kuzimia , nikaanza kupewa mkasa mzima jinsi alivyopata VVU , yani baba yake alikufa na ngoma afu kuna mtu anapiga yeye na mama yake mana yake mama na mtoto wana share jamaaa kumbuka Mama na yeye yupo kwenye grid

wale watoto wanasema wananionea huruma kwani hawapendi nife, baada ya hapo wakaondoka, hapo hapo nikaisi naanza kuugua kwa wenge kusoma nikashindwa nikawa mtu wa kulala na mawazo tu, kuna boya mmoja jamaa yangu sana akagundua sipo sawa ikabidi nimweleze ukweli, jamaa lilivyojinga likaanza kujicheka badala ya kunipa pole


ila baadae jamaa akaniambia sikia we boya kama ana ukimwi niwake twende ukapime unaweza kuwa unajitesa kumbe huna , hapo ndio kimbembe kikaaanza nikamwambie sipimi mie hata polisi waje

basi imepita miezi kadhaa dogo alikuwa kasafiri mara yule dogo siku bado na mawazo mara kaja gheto anataka hapo kwanza picha ndio lilikuwa linaanza, nilimpa maneno kama yote na kutaka kumpiga dogo katulia kama anisikiii afu namaliza anasema kauli moja tu twende kupima, nikasema kama tukiwa wazima mimi na mademu ndio mwisho siku hiyo sirudii tena hadi nifunge ndoa


nikajikaza hivyo tukaenda ebana majibu tupo wote vizuri, hapo hapo kitoto kikasema rafiki zake uwa wanakaonea wivu na wanasambaza uongo kisa uzuri wake , baada ya hapo tukaendelea kama kawa hadi namaliza chuo baada ya hapo sijawai kukasikia tena
Kuna mshkaji wangu mmoja tulikua tunapenda kuharbiana sana, tulikua na utan ambao mpk wa kuumiza , yule jamaa matatizo kama haya yakuumiza moyo atakuacheka kwanza hata kabala ya kukupa msaada au ushauri dah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom