Msala ambao siwezi usahau kamwe

Msala ambao siwezi usahau kamwe

Enzi za utoto wangu nilikuwa mtundu sana aisee.

Siku moja niko home choo chetu na jiko vilikuwa ni vya nyasi,sasa nikakaa nikaangalia zile nyasi kule juu nikasema aaah hivi mchana huu nikiweka njiti ya kiberiti itawaka kweli na kumaliza nyasi zote hizi ?

Faza enzi hizo ni mtata sana yaani.

Basi baada ya kuwaza nikasema sio kesi acha niweke njiti ya kibiriti niwashe nione kama itawaka kwa nyasi zote hizi.

Kidume nikawasha nikatulia kuskilizia mshindo,kuna kimoshi kikatoka alafu kikazimika nikasema aaah kumbe haiwezi kuwasha,nikaendelea kufanya mambo mengine.

Kumbe bhana ule moto ulikolea ndani kwa ndani ukawa unafukuta juu kunatoka moshi mimi niko ndani sina habari.

Kumbuka kuwa hapo nyumbani nilikuwa peke yangu watu wote hawapo.aisee nashangaa kuna mzee jirani yetu anakuja mbio sana anaita nikashangaa anaita nini huyuu ?,anakuja anasema motoooooo mootoooo moyo ukapiga paaap nikajiuliza moto ule nilowasha mie au moto ungine ? Nikajipa moyo nikasema ule wangu ulizimika huu utakuwa ni moto mwingine.

Daaah kutoka nje kutazama juu laaaaaa hawlaaaaa kitu chekunduuuu moto mkubwa unawaka alafu jua kali,daaah aisee nilipata sonona mana hapo sikuwaza tena huo moto bali niliwaza kichapo cha faza na maza maana wote walikuwa watata sana nikizingua.

Daaah basi yule mzee akahangaika sana kuzima ule moto huku mimi nikiwa nimepata butwaa la ghafla na mawazo tele kichwani mithili ya mtu mwenye familia.

Daaah mwisho mzee kauweza moto ukazimika lakini lile paa la nyumba la nyasi ukiangalia kwa juu ni kama mtu mwenye kipara namna ambavyo lilikuwa likionekana.

Ikabidi mzee anihoji mimi nokampa ukweli wote,na yeye waliporudi wazee akawasimulia kama nilivyomsimulia na hiyo wazazi wakatafsiri kwamba ni upumbavu wangu.

Mzee iwaasa wazee wasinipige lakini nahisi kwao ilisound"mumpigeee hasaa huyoo"

Daaaah

Daaaah

Daaahh.

Ushawahi kupigwa mpaka inafikia hatua ukioigwa na unanyamaza na ukiachwa ndo unalia ?

Mungu anitunzie wazazi wangu maana bila vile ningelikuwa toto sumbufu sana kwa sababu nilikuwa mtundu sana.

Baada ya soo hili nikasema mimi na majaribio ya kipuuzi baasi tenaaa nimekoma.
Dah we ndezi mwenzangu hahahahahhahaaaa nilifanya jaribio kama lako nikiwa darasa la 5 dah, nlikuwa natabia ya kutega njiti ya kiberiti juu ya ganda lake ile sehemu ya kuwaka inakuwa pale kwa kuwashia then nakisupport na kidole then nakipiga na kidole cha mkono mwingine, nlikuwa naenjoy kuona moto ukiruka na kuzima kama kimondo, siku hiyo si ukarukia kwenye kibanda cha nyasi kikateketea chote, ebwana e hakuna alie niona ila lawama zooote juu yangu, sio kwa kimavi kile mpka leo maza anilaumu anyway sikudundwa ila niliathirika tu kisaikolojia nlikosa aman kwa siku kadhaa
 
Dah we ndezi mwenzangu hahahahahhahaaaa nilifanya jaribio kama lako nikiwa darasa la 5 dah, nlikuwa natabia ya kutega njiti ya kiberiti juu ya ganda lake ile sehemu ya kuwaka inakuwa pale kwa kuwashia then nakisupport na kidole then nakipiga na kidole cha mkono mwingine, nlikuwa naenjoy kuona moto ukiruka na kuzima kama kimondo, siku hiyo si ukarukia kwenye kibanda cha nyasi kikateketea chote, ebawana e hakuna alie niona ila lawaza zooote juu yangu, sio kwa kimavi kile mpka leo maza anilaumu anyway sikudundwa ila niliathirika tu kisaikolojia nlikosa aman kwa siku kadhaa
Mkuu naipata hiyo.

Unakiweka kibiriti ubavu,then kidole kimoja unategesha ukiwa umesimamisha njiti upande wa barudi ugusane na upande wa kuwashia njiti.

Then unakipiga puuu.

Hahahhaha dah hatari sana.
 
Miaka ya 2020+ nipo zangu town napiga mishe zangu mara napokea simu wazazi wanadai tumekutafutia mchumba mkoani inabidi uje kuoa, dah!! Mm sina mpango hata wa kuoa mishe zenyewe za kuunga unga.nikajaribu kupinga wazee wakakomaa dah!

Nikaona isiwe tabu nikapanda ndinga hadi mkoa kufika ndio siku hiyo ya harusi kumcheki bi harusi kumbe nimesoma nae primary,basi harusi imefanyika,kumbe bi harusi nae ana msela wake wakitambo kamuaidi ndoa halafu yupo vizuri kipato,basi msela kapangana na demu wake wanipe msala ndo ishindikane,bi harusi nae wazazi wake wamemkomalia kama mm kwa kua wazazi wanajuana,

Basi tumefunga ndoa tumerudi nyumbani mara anakuja bibi yake bi harusi ananiambia mtoto ni bikra kwaiyo inabidi upige mzigo ili kesho ifanyike sherehe ya kumpongenza binti kwa kujitunza mm nikasema poa tu,kufika usiku si ndio inabidi nipigie show,ile namsaula nifanye ya yangu binti anapinga makelele nyumba nzima watu wameamka.

Kumbe kuna wageni kutoka sehemu mbali mbali walikuja kwenye sherehe,ikabidi wazee waje kujua kulikoni!! Aisee sita sahau binti anasema namlazimisha kumuingilia kinyume na maumbile.mbele ya wazazi wangu,nitafanyaje? Nani ataniamini kumbuka nilikua nakataa kuoa?

Inaoneka nimefanya makusudi dah!! Kulivyo kucha nikapanda bus nikarudi town sikutoka ndani wiki mbili hakuna Alie kua anaamini,ndoa ikaishia hapo,maisha yakaendelea demu akaenda kwa jamaa yake.

Kufika huko sasa kila wakilala mara wasikie wanachapwa bakora mara mauza mauza binti si akarudi kwa wazazi wangu kuomba msamaha na kueleza ukweli wote ulivyokua kuwa alipangwa afenye vile ili ndoa iharibike, kazi ikawa mm wataniambiaje maana nimeshachafuka mbele ya umma,basi nilikaa zaidi ya miaka 15 ndio nikasamehe.

Hivi sasa tuwasiliana kama mtu na rafiki yake japo yy hajapata wa kumuoa mpaka Sasa hivi.

Pole sana mkuu haya mambo ya kutafutiwa mke ni majanga kam hayo mtu analazimishwa kumbe moyo wake upo sehem nyingn mwisho wa siku ndio uninga km huo unafanyika
 
Enzi hizo sasa ukikaribia mwaka mpya mnatengeneza vi baruti mnaweka kwenye vichwa vya spoku za baiskeli mkiona watu wamekaa mnavitest pwaaaa watu wakishituka mnakimbia kwa furaha, lengo ni kwamba ikifika saa 6:01 kuanza mwaka mwingine mnavipiga kama kusherehekea mwaka mpya (watoto wa siku hizi hawayajui hayo)......

Basi bwana mwaka fulani huo nilidhamiria kuvunja rekodi ya kutengeneza baruti itakayounguruma kuzidi baruti nyingine zote pale mtaani na ikibidi mitaa ya jirani, mzee wangu alikuwa fundi makenika, kwenye makorokoro yake nilipata jeki moja ndogo ambayo ilikuwa imetolewa utumbo ikabaki wazi katikati.

Kuna kaka yangu alikuwaga ametoka Moshi (kama sikosei), huko alikuwa anafanya kazi kiwanda cha kutengeneza viberiti, alikuja na kisado kizima kimejaa unga wa baruti (sijui nae alikileta kwa madhumuni gani tu).....mi nikaiba ule unga wa baruti kwa ajili ya kutengeneza mzinga wangu.

Siku ya tar 31 December nikafanya maandalizi yote, lakini nikapata wazo moja kwamba sitoweza kwenda kukamua ile device pale ili kusababisha mlipuko, nilichokifanya nikategesha jiwe zito juu ya usawa wa lile komboro langu, nilikuwa nimelitega nyuma ya banda la mbuzi nyumba ya jirani yetu........

Bwana weeeeeee.......

Nikamshirikisha kijana wa ile nyumba ambae tulikuwa rika moja tu kuhusu mpango wangu, akataka aende akaangalie.....kufika akakuta nilivyolitega akasema eti nimekosea, akaanza kuliseti upya......

Aiseeeeeeee..........

Ilikuwa yapata kama saa 11 hivi za jioni mzigo ukaitika pale.......boonge ya kishindo, vumbi zito likatimka hewani, banda la mbuzi likaporomoka lote, harufu ya baruti ikasambaa eneo lote......cha kwanza nikakimbia hadi nyumbani, sina amani wazazi wanakimbizana kutafuta watoto wao.

Taarifa za baadae zikatoka......yule jamaa alikatika vidole vitatu vya mkono wa kushoto, ndama wawili wa mbuzi walikufa kifo cha kikatili sana......lakini yote kwa yote yule rafiki yangu (R.I.P) hakusema chochote kuhusu uhusika wangu kwenye kadhia ile.

Mama akajua moja kwa moja kuwa mimi ndio injinia wa ule mpango......jamani nilipigwa sio mchezo, hadi kuna muda nilikuwaga najiuliza kama mama hajawahi kupitia kozi zozote za kijeshi, maana nilipigwa staili zote za kwenye mieleka kuanzia hizi Rko za Rand Orton pigwa sana 619 za Rey Mystereo, chomeshwa kichwa chini kama Under taker, mara nibanwe mguu mmoja huku nimevutwa shingo kwa nyuma John Cena anavyofanyaga.......yani kilikuwa ni kipigo mchanganyiko. hadi nilipokuja kuanza kuangalia mieleka nikajiuliza hawa jamaa walimuiga mama au.......

Hilo likapita.....miezi kadhaa baadae nilikuja kuvurumua msala mwingine mzito sana, kwa kweli siwezi kuuelezea maana ulikuwa uondoke na roho yangu.
kiongozi umenivunja mbavu..
 
Daah hatari sana wajameni...sikuwahi kupigwa ktk maisha yangu Kama hiyo siku,niliona ulimwengu wote unanizomea aisee, iyo ilikua hivi miaka ya nyuma kidogo Niko na miaka kumi, ktk umri huo nilitokea kuwa mshabiki na mpenzi mkubwa sana mpira maeneo niliyokua naishi ni wanazi hasa wa mpira kwa kua labda ilikua ndio katikati ya jiji, akili yangu ilikua imechanganywa hasa na babu Ferguson kipindi iko man United ipo kwenye peak yake hasa, ni mwendo wa kunyanyua makwapa tu,nilitokea kuipenda sana "the red devil's", mechi zao zote za man u za kuanzia mchana siwezi kukosa hata siku moja niko radhi nitoroke shule nipitie bandani kucheki mechi, mzee alikua arsenal...nakumbuka ilikua uefa man utd anacheza ,ngoma ilikua saa 10:45 usiku aisee nikajiapiza kua iyo mechi siwezi kukosa hata iweje Mana sikuwahi kucheki usiku wa ulaya hata siku moja kipind iko nikiwa na hiyo miaka kumi, mda ukafika nikazama bandani mtt nilikuaga ni Mimi tu peke yangu hapo bandani na always pale watt ni bure kuingia, mechi ilianza nilikua na furaha kweli kuwachekiwachezaji sampuli ya kina ole Gunnar, Roy Keane na wenzake duuuh mechi iliisha kwa droo, mechi imeisha kila mmoja kwao Sasa njiani tuliongozana na watu kibao nikapata faraja kweli kuwa kumbe sipo pekeyangu usiku ule, bullshiiiit! tukaanza kupungua njiani mmojammoja kwa kua kila mtu Sasa anaingia chochoro hili Mara lile ilmradi kila mmoja afike kwao hatimaye nikafika nyumbani,nje Niko pekeangu Hapo miguu yote ikaisha nguvu,jasho adi miguuni daah nikajaribu kusukuma geti likawa limefungwa ndiiii, nkajsemea nkizubaa apa nje ntapigwa kabari nijiharshie bure Mana mitaa kipindi icho ilikua haifai kutolewa meno ilkua nje nje. mwanaume nikajikaza nikaparamia geti la home kwa fujo nikanasa vizuri vyuma vya juu nikajivuta adi juu kabisa hatimaye nikajipindua kwa ndani safi tu na kutua chini kudaadeki nliumia vbaya Mana chini kulikua na sakafu ngumu hatar nikajikaza huyo mnyama nkajiona nmewini, loooh kumbe mzee wangu alkua ananisubiri kwa hamu tu pale nilipoingiza pua yangu tu nikaitwa, "wee njooo apa, kumbe wewe ni fala hivi" nguvu zote zilipotea nkatamani nkimbie mzee alinikwida Apo kiunoni suruali ilkaribia kupanda kifuani, iyo ilikua saa saba usiku,mzee wangu alkua ni mtu wa mechanical aisee sijui alichukua vitu gani kutoka store yake nilichezea kichapo nilipigwa na nyaya, nilipigwa na fimbo, nilipigwa na kila aina ya takataka,makofi nilichezea yule mzee cjui alipitia jeshi nafkiri ,nibinuliwa kichwa chini miguu juu, tulikimbizana humo chumbani niliparamia kabati ila bado nyaya za mgongo zilnishukia vizuri,nikitaka kuingia uvunguni nixavutwa miguu Apo kofi la mgongo,nikitaka kushika mikono ya mzee ili asinipge tayar nishachotwa mtama basi nikabaki tu chini anipige hadi achoke nilivotulia chini naye akaniacha ananiangalia kwa hasira, akanambia kalale sasa saa nane usiku huu, ilikua saa nane nmefika chumbani changu nnacholala aisee mwili wote ulkua haufai umechakaa vbaya usiku huo siku lala niliwaza kua kesho nitoroke nyumbani tu nisepe, nilikua fala kweli...muvi za misheni za kijeshi nazo ziliniharibu nkawaza nitoroke nyumbani kibabe Kama jasusi...wiki nzima sikwenda shule kwa maumivu na ndo ilikua Mara ya Kwanza na ya mwisho mzee wangu kunipiga toka siku hiyo sijawahi kupigwa hadi nakua kabisa kwani nilikua na disclipne kubwa kwani ndo siku ambayo nilitoka utukutu uliokubuhu pale mtaani hadi kuwa mfano wa kuigwa kilichonibadilisha siyo kichapo kile Bali ni maneno aliyonambia mzee siku ile...
 
hapo kwenye kutoroka kama jasusi lazima ungekamatwa tena, na muda huo lazima staring angekuua kabisa
 
mamako kiboko.
nyie watu watoto zenu watakuwa watundu zaidi yenu. jiandaeni
Nimeskia uchungu,
Mungu atusaidie tu hakika, Maana hicho kitu Mama aliwahi nambia, 'ipo siku nawe utakuwa mzazi'...!

Hapa nawaza siku nije nipate hao watoto waje wasumbue kama nilivyosumbua, jamani..! Si nitakuwa nalia kila siku vile sikuhizi nimekuwa phaller..!
 
Sio wewe tu kuwa fala hata mimi sasa ivi nimekua fala wa kutupwa mpaka wenzangu wa utotoni wananiambia mama yako kakuweza mpaka kufikia hatua ya kutulia ivyo au kakuloga.......

Aisee ananiambia tu nawewe utakuja kuzaa ila kila nikijiangalia sina hata udhubutu wa kunyanyua mkono kumpiga mtu nahisi huyo mwanangu nitaishia kumuangalia tu na kulia mwenyewe
 
Hiyo misala tumeitatua sana kwa mbinde hizo harakati za kumpa denti mimba wakati na wewe bado ni denti zisikie tu kwa jirani.Kuna mwanangu yeye na demu wake walikua hata hawajui kama wamepeana mimba mpaka kwenye michezo ya UMISETA ndio demu anagundulika baada ya kuanguka wakati anacheza netball hapo mimba ina miezi 6.

Mwana siku hiyo hiyo akajiachisha shule nakutokomea kusiko julikana msala ukabaki kwangu niliyekua nashare nae ghetto. Nilizunguka sana Serikali ya kijiji na kuhudhuria vikao vya usuluhishi.

Na huo ndio ukawa mwisho wa mimi kukaa ghetto.

Vikao vya usuluhishi
 
Mambo ya kota yasikie tu aise nikakapa mimba katoto ka mkuu wa kikosi, the rest ni historia tu🤪🤪
 
Katika Maisha tunapitia mengi sanaa ila kuna mengine yanakuweka katika wakati mgumu hadi kufikia hatua ya kuona Mtihani huo ndio Mkubwa na haitokuja kutokea mwingine kuuzidi.

Nilipita na mtoto wa Anko, alikua mzuri kiasi kwamba sikuweza jizuia, alikua mwoga sana hata kuongea na mwanaume, Nafasi pekee ilikua kwangu, Tulikua age moja, Tukafanya yetu tukamaliza, kumbe alikua kwenye Siku zake za hatari banaa, Mwezi unakata haoni siku zake.

Alikua shule ya boarding hizi za St Mary's, akatafuta simu akanipigia kupitia namba ya shule tunatumia kuwasiliana yeye alikua hajui kua ile namba ni official kwa ajili ya wanafunzi akajua ni ya mshkaji. Nikaitwa, ya kua kuna simu kutoka kwa ndugu yako, Baada ya mda akapiga, Nilipokea mbele ya Mwl nikijua hamna shida ile napokea tuu ananiambia nina ujauzito.

Paaap, nikajaaa wenge, Kukata siwezi, kuongea siwezi maana wapo hapo, nikabaki najizungusha tuu pale, nikaona isiwe tabu nikamwambia pole sanaa, nikakata simu, nikaandika ile namba kwenye kiganja nikampa simu mwenzangu mwingine nikakimbilia haraka kwa mpishi kuomba simu, nikampigia,

Kumbe Sasa yeye alipoona nimemwambia pole na nikakata simu, akajua sijaelewa, na anajua simu ninayo, akatuma msg " Mimi .........nina ujauzito". Kwahio msg imebaki kule, ile ananiambia tuu hivyo, kwa mara nyingine tena chaap nikakata simu ili nirudi kule kucheki kama hakijasanuka niombe fasta nifute msg, kufika mda wa kupokea simu umeisha wana wote washasepa Simu ishapelekwa kwa Sista.

Kurudi kwa mlinzi angalau nimtafute tuongee vzr ananiambia namba za wanafunzi hua anafuta ukimaliza tuu, Daaadeki hapa sasa ndio tumbo la kuhara likaanza, kule shuleni kwao atatafutwa mwenye mimba(kila baada ya miezi kadhaa hua wanapimwa ujauzito), mimi,
huku shule kwetu taarifa ya kujaza mtoto wa watu, nyumbani Kuachilia mimba tuu, kutembea na mtoto wa anko ni mada nyingne.
Serikali nako kumpa mimba mwanafunzi.

Kila mazingira niliyokua nawaza nilikua naona kabisa sichomokii, hata kama shuleni wasipogundua mapema, Msg itaonekana, hata isipoonekana, akirudi home atajulikana. Nikiwaza Mawasiliano nimepoteza, Kumbuka wakati nakata simu kwa mpishi nilimwambia kua ile simu ni ya ofisi hivyo hawezi piga tena, na kwa mpishi kabla sijakata nilimwambia usipige nitakupigia hii simu si salama..., Kwahio suala la yeye kupiga hilo halipo tena, Na wakati naongea naye alikua anasikika kwa sauti ya kulia, nikiwaza hapo ndio nachoka.

Nikaongea na Mwl flani nikamwambia naomba unitaftie Mwl yoyote wa shule flani anitaftie ndugu yangu anasoma pale kuna jambo niongee naye, Nikampata, kabla ya yote nikamwambia nitumie namba ya haraka na salama mimi kumpata mda wowote, na mimi nikamtumia ya mdau flani hivi.

Basi tukajifanya tunasalimiana pale, nikakata simu akatuma namba kwenye msg na mimi nikatuma nikaandika kwenye Diary, nikasepa..
Baadae akanitafuta, nikamtuliza, inshu tunafanyaje, option ya kuitoa kila mtu anaogopa kumuanza mwenzake, inshu ikaja tumbambikie mtuu, mtihani ni hivii unambambikiaje mtuu nakati hata hamjawahi kutana(mimi ndiye niliyemla pekee).

Sasa kuna walimu walikua wanamsumbua sana pale, nikamwambia kama vipi mpe mmoja wapo. Kabla ya kufikia muafaka mawasiliano yakakata, baada ya siku hio hamna tena mazingira ya kuongea na simu maana kote mitihani ilikua inaanza, Inshu ikawa kule kwa sista, hapo nawaza ya kua washajua wanasubiri tuu siku tunafunga napewa vyangu(ndio kawaida mtu kutimuliwa siku ya kufunga).

Niliishi kwa mateso sijapata ona. Siku Tunamalizia mtihani mshkaji wangu akanifuata yaani simple tuu asijue nateseka akaniambia "we boya ile siku umenipa tuu simu ikaingia msg ya ujauzito nikaifuta jamaa umezidi" Nikasimama, nikamuuliza nilichosikia ni kweli au wenge?

Yule ndugu Sijawahi msahau mpaka leo hii. Baada ya ups and downs nyingi Sijui ni miujiza gani, dogo mwezi uliofuatia akapata siku zake. Kuna mambo mengine mengi ila hili ni mojawapo. Ilaa daah watu hatukomii, mtu unaapa kabisa kama hili likipita sitarudia, ila kesho kesho kutwa unarudia.

Share
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom