Msajili wa vyama vya siasa nchini apinga CUF kufukuza wabunge wawili

CUF inatakiwa kuchukua maamuzi magumu ili kuondokana na Lipumba na CCM iliyo ndani ya CUF Lipumba.

Chama pekee ambacho kimedhihirisha kuwa na msimamo thabiti, kilichojengeka kitaasisi, ambacho wakati wote kimeshinda hila mbalimbali za mamluki, na chenye viongozi wasioingilika kwa pesa au tamaa ya cheo ni CHADEMA. Na ukweli huo ndio unaoifanya CHADEMA kuchukiwa na CCM na serikali yake kuliko chama chochote cha siasa.

CUF halisi wahamie CHADEMA, uchaguzi uitishwe upya kwenye majimbo yenye wabunge wa CUF, wagombea wawe wabunge wa CUF wa sasa. Baada ya uchaguzi, CHADEMA na CUF wafanye mabadiliko ya jina la chama ili kuakisi mwunganiko wa CUF na CHADEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo CUF ya Maalim Seif na CHADEMA wakiungana shida itakuja kwenye kugombea vyeo..huku Mbowe..huku Seif..huku Lowasa....hawa mafahali watatu hawawezi kukaa zizi moja
 
Hivi Seif kachanganyikiwa?

Anadhani yeye bado ni kiongozi CUF!


Ona Ccm Ilivyoharibu Uwezo Wa Kufikir Kwa Watanzagiza Hadi Mwanga Upatikane Na Kufuta Giza Vichwani Mwa Watanzagiza hadi Hiki Kizazi Kitoweke
 
Halafu Watu Wakiambiwa Ccm Ilitoka Madarakani Toka 1995 Wanakataa Kauli Za Mkapa Zinaonekana Sasa
 
Barua haimtambui maalim kama katibu mkuu alafu hiyo hiyo barua inamtambua maalim kama katibu mkuu.

Tz bado hatujabarikiwa
BARUA haijasema popote kuwa haimtambui maalim seif kama katibu mkuu bali imetanabaisha wazi kabisa kupitia vifungu vya katiba ya Cuf kuwa Magdalena Sakaya ndiye anayekaimu nafasi ya ukatibu mkuu hivyo ndiye anayefanya kazi zote za katibu mkuu mpk msajili atakapopata barua kutoka kwa Mwenyekiti kuwa hakuna kaimu tena mwenyewe (maalim seif) amerudi kiutendaji. Hivyo bado maalim ni katibu mkuu lkn hafanyi kazi kwa sasa na hawezi kufanya maamuzi yoyote ya kichama yakawa halali. Kifupi maalim seif bado katibu mkuu kwa jina (hewa) lkn mtendaji ni sakaya hope nimekuelewesha vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaji amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Cuf Maalim Seif Hamad, lakini kwenye content anaonyesha kutomtambua! Kuna tatizo hapa -Ni kwanini jaji huyu ameelekeza barua yake kwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Hamad lakini hapohapo anajidai kutomtambua kama Katibu Mkuu?

Dola inapambana kwa nguvu kubwa kuwapandisha hasira CUF ili wafanye vurugu kisha watumie vurugu hizo kukifuta chama. Vinginevyo serikali kwanini imechagua kujidhalilisha kwa kiwango hiki?
Wapi kwenye barua aliposema hamtambui kama karibu mkuu zaidi ya kusema maamuzi yake pamoja na kikao cha baraza kuu ni batili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lipumba anamtambua Maalim kama Katbu Mkuu*Mtoro* na ndo sababu nafasi yake inakaimiwa na naibu Katibu Mkuu Bara Bi Magdalena Sakaya.

So siku Maalim atakaporudi ofisini na kuomba radhi kwa makosa yake ya utoro atatambulishwa tena rasmi kama KM na ataendelea na majukumu yake kama kawaida.

Kwa sasa mawasiliano yoyote atakayofanya kwa mamlaka yoyote ni hewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa msioona mbali. Maana yake ni kwamba, huko mbele akiitisha kikao Seif ni batili na wanaweza kukamatwa kwa mkusanyiko usiokuwa halali....
 
Barua yenyewe ameiaddress.
Maalimu Seif Sharif
Katibu mkuu.
Halafu contents ya barua anasema hatambui, na mwanzo ameshamuita katibu mkuu,
Nchi ina kinyaa hii....
Hiyo mkuu ndio raha ya Kuishi Tanzania nchi ya miujiza na vigeugeu!
Huku anatambua kufukuzwa kwa wabunge huku anakataa kufukuzwa kwa wabunge wawili... kule anamkana hamtabui kwenye barua anamtabua!
Hakika weledi hufunikwa na tumbo
tujipe pole kwa hawa wataalamu wetu wa sheria na wenye mamlaka
 
Back
Top Bottom