Msajili wa Hazina Ndg. Lawrence Mafuru hajui au kashasahau lugha ya Taifa ya Kiswahili?

Nani alikwambia ukimbie umande? :D:D:D By the way, kiswahili hakina misamiati ya kutosheleza kuelezea hayo mambo ya kitaalam aliyokuwa anayazungumzia.
Mfano neno 'liquidity' kwa kiswahili ni 'maji maji' kwa hiyo kama angezungumza kwa Kiswahili lugha ya taifa angesema kuwa
'benki nyingi zina kosa hewa (suffocate) kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, kitu ambacho kwa Mbongo wa kawaida angesema kuwa kama benki zinakosa hewa kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, si waende DAWASCO? :(:(:(
 
wewe hujui kiswahili ndio maana unadhani hakina misamiati ya kujitosheleza. pia kumbuka misamiati kwenye lugha inakua kadri mizizi ya lugha inavyotumika. hebu tuondelee mning'inio wa ukoloni. kwa taarifa yako mimi sikukimbia umande, huko ilikozaliwa lugha ya malkia nimepita vya kutosha. mswahili fakhari yangu kiswahili
Kiswahili Kama lugha inajitosheleza..
Shida ni sis Ndio hatujitoshelezi kwa maana ya kukosa maarifa yetu Ya ndani.. Na kuishia kujifunza maarifa ya wenzetu ambayo kuyatafsiri moja moja Kweny lugha yetu ni taabu..
Kila taaluma ina misamiati mahsusi "jargons" ambayo hutumika kwenye taaluma husika.. Sasa tuambie kwenye taaluma Ya banking tuna maarifa gani ya ndani ambayo tunaweza kuyasema kwa lugha ya Kiswahili.. Au ndo tunasubir kutafsir tusiyoyajua..
Huyo jamaa Yuko sahihi Sana kwa Maana Kuna visawe mahususi ambayo havina tafsir mahususi kwenye lugha ya Kiswahili ambapo unaweza kutafsir na ikapoteza Maana.
 
wewe hujui kiswahili ndio maana unadhani hakina misamiati ya kujitosheleza. pia kumbuka misamiati kwenye lugha inakua kadri mizizi ya lugha inavyotumika. hebu tuondelee mning'inio wa ukoloni. kwa taarifa yako mimi sikukimbia umande, huko ilikozaliwa lugha ya malkia nimepita vya kutosha. mswahili fakhari yangu kiswahili
Kiswahili kwenye mambo ya kitaaluma ni kichanga sana... Tafiti zetu ni ndogo na hazijitoshelezi
 
Nilfikiri ni mimi tu ndo nilikuwa nalibaini hili, kiufupi mshkaji anapenda sana michomeko ya kimalkia, na baadh ya ndg zang wengi watokao ukanda ule wakipata kacheo tu utawajua tu kwa kutupia vijimaneno visiyo na maana kwenye uwasilishaji wao.
Chuki binafsi Mkuu
 
HNIC

Kila fani ina lugha na msamiati wake.

"Banking Industry" ina "lugha" au misamiati yake, halikadhalika kwa "Healthcare Industry", "Hospitality industry" na kadhalika.

Kutegemea kuwa Mafuru atakuekeza mambo ya banking bila terminology za kibenki ni upunguani wa hali ya juu.

Mafuru kujitahidi sana kutafsiri terminology za kibenki kwani alijuwa kuna mapunguani kama wewe hamtamuelewa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Dah nimeona nikigonga "like" itaonekana ni moja. Nakugongea "like" 50 kwa mpigo. Hata mimi wa MEMKWA nimemuelewa sana Mafuru na sasa naelekea field kupiga kazi. Lazima nirudi nikiwa tajiri na bado ntakuta watu wanaendelea kulalamika na lugha ya Mafuru hapa jukwaani.
 
Nani alikwambia ukimbie umande? :D:D:D By the way, kiswahili hakina misamiati ya kutosheleza kuelezea hayo mambo ya kitaalam aliyokuwa anayazungumzia.
Mfano neno 'liquidity' kwa kiswahili ni 'maji maji' kwa hiyo kama angezungumza kwa Kiswahili lugha ya taifa angesema kuwa
'benki nyingi zina kosa hewa (suffocate) kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, kitu ambacho kwa Mbongo wa kawaida angesema kuwa kama benki zinakosa hewa kwa kuwa hazina maji maji ya kutosha, si waende DAWASCO? :(:(:(
Kiswahili kina misamiati ya kutoshaleza lugha yake sema tatizo lililopo ni kukalili kile alicho kisoma kwa lugha aliyosomea yeye ila sio kweli kwa huyo mtoa mada alivyosema kuwa asilia 90 katumia lugha ya malkia sidhani kama kweli anajua kutafuta asilimia katika vitu
 
Hii video imenisaidia kujua kuwa kumbe serikali imerudisha 500B tu kurudi BOT? Hapa mwenye akili lazima ajiulize kuwa kuna kitu kinafanyika
Na pale alipokuwa clouds tv 360 alisema tatizo sio helabya serikali maana hata hiyo BOT ni sehemu ya mfumo wa kibenki ambapo benki zinaweza kukopa na kuwakopesha wateja wao. Tatizo kuna trilion 1.4 ambazo ni mikopo isiyolipika. Maana yake mabenki yamekopesha wateja ambao hawawezi kuirudisha hivyo pengo kwa mabenki ni kubwa maana hiyo hela iko mtaani na haiwezi kurudi bank.
 
Nimesikiliza na nimetazama video za huyu Msajili wa Hazina wakati anatoa taarifa kwa umma juu ya hali ya mzunguko wa fedha nchini ambao unaleta mtafaruku mkubwa ndani ya hii nchi ya watu zaidi ya milioni 50 na ninasikitika kusema kuwa huyu ndugu pamoja na jitihada zake za kutaka kutujuza sisi wananchi kuhusu hii kadhia ya ya fedha lakini mfano mbovu sana wa viongozi wetu.

Inawezekana vipi kuwa mtu mwenye dhamana kubwa kama Lawrence Mafuru aitishe mkutano na vymbo vya habari halafu anatumia zaidi ya asilimia 90 ya maneno yake kuongea maneno mengi ya Kiingreza kilichojaa misamiati migumu ya kiingereza ambacho Mtanzania wa kawaida hawezi kumuelewa? Naamini kabisa kuwa Mafuru nia yake haikuwa kutujuza yanayoendelea bali ni kutughilibu na maneno mengi ya kiingereza ambayo hayaeleweki.

Hili tatizo nimeliona sana kwa viongozi wetu wakiwepo Bungeni, wakiongea kwenye runinga au radio na mbaya zaidi mpaka miswada na sheria zetu nayo inaandikwa kwa kiingereza ambacho asilimia kubwa ya watanzania hawaelewi na inafanana sana mikataba mibovu ya kilaghai ya wakoloni.

Nikirudi kwa huyu Ndugu Lawrence Mafuru, je hajui kuongea Kiswahili fasaha cha kueleweka au mbwembwe ya kutaka kutuvuruga na kutughilibu tusielewe haya mambo nyeti ya kitaifa?

Wito kama tumefikia hatua ya kuwapa madaraka wasiojua lugha ya Taifa bas serikali iajiri watu kutoka BAKITA kwenye kila idaya ya serikali ili mawasiliano awe mopes kwa na wananchi

Na kama imeshindikana naomba Ndugu Magufuli toa agizo kuwa hawa watu wa serikali waongee kwa kikswahili ili wananchi wapate kuwaelewa na wasiojua Kiswahili wapelekwe kwenye kozi maalum ya kujua hii lugha ya Taifa (kwa gharama zao)

Ushahidi wa ghilba ya Lawrence Mafuru huu hapa:

Alikuwa anataka baba kilaza asielewe alichozungumza baada ya kujua ngeli ni zero
 
Mimi namfagilia huyu Mafuru. He has excellent communication skills, both verbal and non-verbal. Hapo ndipo utang'amua hakupata huo wadhifa mkubwa alio nao kwa kubabaisha.
 
Mabenki hayampendi ndugu mafuru lakini hamna namna inabidi mabenki yatafute wateja waache kutegemea serikali.
 
Nimesikiliza na nimetazama video za huyu Msajili wa Hazina wakati anatoa taarifa kwa umma juu ya hali ya mzunguko wa fedha nchini ambao unaleta mtafaruku mkubwa ndani ya hii nchi ya watu zaidi ya milioni 50 na ninasikitika kusema kuwa huyu ndugu pamoja na jitihada zake za kutaka kutujuza sisi wananchi kuhusu hii kadhia ya ya fedha lakini mfano mbovu sana wa viongozi wetu.

Inawezekana vipi kuwa mtu mwenye dhamana kubwa kama Lawrence Mafuru aitishe mkutano na vymbo vya habari halafu anatumia zaidi ya asilimia 90 ya maneno yake kuongea maneno mengi ya Kiingreza kilichojaa misamiati migumu ya kiingereza ambacho Mtanzania wa kawaida hawezi kumuelewa? Naamini kabisa kuwa Mafuru nia yake haikuwa kutujuza yanayoendelea bali ni kutughilibu na maneno mengi ya kiingereza ambayo hayaeleweki.

Hili tatizo nimeliona sana kwa viongozi wetu wakiwepo Bungeni, wakiongea kwenye runinga au radio na mbaya zaidi mpaka miswada na sheria zetu nayo inaandikwa kwa kiingereza ambacho asilimia kubwa ya watanzania hawaelewi na inafanana sana mikataba mibovu ya kilaghai ya wakoloni.

Nikirudi kwa huyu Ndugu Lawrence Mafuru, je hajui kuongea Kiswahili fasaha cha kueleweka au mbwembwe ya kutaka kutuvuruga na kutughilibu tusielewe haya mambo nyeti ya kitaifa?

Wito kama tumefikia hatua ya kuwapa madaraka wasiojua lugha ya Taifa bas serikali iajiri watu kutoka BAKITA kwenye kila idaya ya serikali ili mawasiliano awe mopes kwa na wananchi

Na kama imeshindikana naomba Ndugu Magufuli toa agizo kuwa hawa watu wa serikali waongee kwa kikswahili ili wananchi wapate kuwaelewa na wasiojua Kiswahili wapelekwe kwenye kozi maalum ya kujua hii lugha ya Taifa (kwa gharama zao)

Ushahidi wa ghilba ya Lawrence Mafuru huu hapa:

Yaika chikaka, yaika! masika, mwamba, omuuta, chikomati. Pale Majita panahitaji maombi.
 
Back
Top Bottom