Pole ndugu.. unajua hata wale ambao kiingereza ni lugha yao ya kwanza huwa wanashangaa sana wanapotusikiliza au kusoma kingereza chetu wabongo! tunapendaga kutumia maneno magumu magumu ili kuonyesha kwamba tunajua sana hii lugha. Uliwahi kusoma lugha alizokuwa anatumia mzee "Punch" miaka ile pale chuo kikuu cha Dar? Hata maprofesa wetu ukisoma taarifa zao utashangaa sana kwani wanatumia maneno magumu ambayo hata wenye lugha yao ni nadra kuyatumia...