Msaidizi wa Kampeni wa Edward Lowassa mbaroni

Msaidizi wa Kampeni wa Edward Lowassa mbaroni

Wapinzani tu?
Acha mahaba. Kampeni zimeisha.

Huyo Jamaa Bashir sio mtanzania na hilo linafahamika wazi siku zote.

Hivyo Bashir hana haki ya kushiriki kupiga kura na kuwa kiongozi wa kisiasa ndani ya chama chochote tanzania.
Kitendo cha yeye kuwa mwanamkakati wa team lowassa tangu akiwa ccm na kuhama naye kwenda chadema kama inavyoripotiwa katika hilo gazeti ni jambo la hatari sana.

Kuna harufu kubwa ya uhalifu hapa kwa sababu yeye na wale raia wengine wa kigeni wenye asili ya kiasia na afrika magharibi wanatuhumiwa kuingilia mfumo wa tume.

Vyombo vya dola vifanye kazi yake, ukweli ujulikane na haki ipatikane.

Kuna kijana mwingine mtanzania huyu anaitwa yeriko nyerere. Huyu bwana tangu 'sheria ya cyber' imeanza maoni ya jumla ndani ya hili jukwaa ni kuwa lazima imtie mbaroni. Tena wengi walienda mbele na kusema asipokamatwa ni hiyo sheria basi sheria itakuwa haina maana.

Siku aliyokamatwa vilio vingi vikaanza mpaka ndank ya JF...ohoo anaonewa ...ohoo mara hivi mara vile.

Huyo Bashir alivyokuwa MD wa Stanbic Bank, serikali ilikuwa haijui?
Kwanini wasingemkamata toka alivyokuwa mwanamkakati wa Lowasa akiwa CCM?
Undumilakuwili wa vyombo vya usalama ndio huu. Ukiwa upande wao wanakunyamazia, ukienda kwa wapinzani wanakuona threat.
 
Kuwa MD wa Stanbic haihitaji kuwa mtanzania.
Baada ya wagombea kuchukua fomu za uteuzi na kupitishwa na tume walionya kuhusu mambo haya. Waliopuuza shauri yao.

Kosa kubwa ni hii tuhuma ya kuingilia mfumo wa tume. Tuache vyombo vya dola vifanye kazi yake. kama hii kesi kabambikiwa tutajua tu. Kesi itakufa na kitaeleweka. Itakuwa zamu yako kuwawajibisha waliombambikia kesi.
Lakini gazeti la bwana Mengi (aliyekaa jukwaa moja na mbowe na lowassa kupinga matokeo ya urais) kulalamikia kabla ya taarifa rasmi ya vyombo vya dola ina maswali mengi.

Katika hilo swala la kunyamaziana ukiwa upande flani ila ukiwa kambi nyingine ndo kelele nadhani chadema ndo inatia fora kwa sasa.

Kwa miaka nane imemtuhumu lowassa (mwana ccm) kuwa ni fisadi papa na kumtukana vilivyo na kumzomea mjukwaani (wakidai ni haki yao toka kwa Mungu).

Siku lowassa kachukua kadi ya chadema akawa "mwenzetu". Siku hiyo hiyi akawa msafi kuliko malaika na kutetewa kwa nguvu zote na wale wale waliomtukana jana yake.
Hakuna unafiki mbaya na utapeli wa kisiasa kama huo.
 
?????unafuraia kabisa tunavyonyanyaswa wapinzan??

Sifurahii hata kidogo.
Sio haki na inarudisha nyuma demokrasia.
Lakini pia sifurahishwi hata kidogo na hii tabia ya watu kulialia na kutanguliza mbele mahaba ya kisiasa kuliko maslahi ya taifa.

Nimemjibu mdau mmoja kuwa tuviache vyombo vya dola vifanye kazi yake..kama jamaa kabambikiwa kesi itajulikana hivi karibuni.
Na ikithibitika hivyo basi tushirikiane hivi hivi kuwalaani na kuwawajibisha waliombambikia kesi.

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=14593261

Huo ndo utawala wa sheria na hiyo ndiyo demokrasia. Ukivunja sheria hatupaswi kuangalia sura ama chama chako.
 
Sawa asante
 
Hii stori inanikumbusha BALOZI wa UCHINA alivyopanda kwenye majukwaa ya kisiasa huko shinyanga,sijui Mamlaka zilimkemea na kumuhoji?
 
Na wahalifu wote waliofanya vitendo vya hatari na haramu waachiwe huru?
Huu sio uhasama wa kisiasa kwa kuutazama tu.
Mbona viongozi wengi wa upinzani wala hawakamatwi, hawahojiwi wala kusumbuliwa?
Kuna tatizo mahali hasa raia wa kigeni wanapoona wana haki ya kutuchagulia rais.

Viongozi wengi wa kisiasa wangapi?maana viongoz tunaowajua wa kisiasa hapa bongo ni Slaa,Lissu,Mbowe,Lipumba,Mbatia,Mrema,Mtatiro,Zitto.
Kati ya hao nilowataja weee mwenyewe wachambue ambao aidha washawah kukamatwa au kupigwa mabomu na POLISI
 
Mimi naomba kuuliza kwanini Bashe alipotuhumiwa sio raia hakuwekwa ndani?
kuna sababu gani ya kumuweka mbaroni mtu kwa tuhuma za kutokuwa raia?
 
Mimi naomba kuuliza kwanini Bashe alipotuhumiwa sio raia hakuwekwa ndani?
kuna sababu gani ya kumuweka mbaroni mtu kwa tuhuma za kutokuwa raia?

Huyu jamaa tayari si mtanzania sio kwamba anatuhumiwa maana NA kibali anacho kinahonyesha ila kosa lake kwa nn anajihusisha NA siasa NA mbaya zaidi ni siasa hatarishi km mipango ya Ku hack system ya nec bashe tatizo lilikuwa uraia
 
Nani kakwambia ni upole wake huyo jamaa alikuwa tayari kufanya lolote we mshukuru mungu tiss wamewazidi akili
 
Mimi namwambia Lowassa na Mbowe, CCM watatumaliza tukiendelea kukaa kimya. They are coming on us with everything, we better act now while we still have the muscle.
sure broo...they must do something vinginevyo itakuwa too late
 
Huyu jamaa tayari si mtanzania sio kwamba anatuhumiwa maana NA kibali anacho kinahonyesha ila kosa lake kwa nn anajihusisha NA siasa NA mbaya zaidi ni siasa hatarishi km mipango ya Ku hack system ya nec bashe tatizo lilikuwa uraia
Ndivyo wanavyowadanganya na kuwaaminisha watanzania kuwa ulikuwepo mpango wa ku-hack system ya nec. Hizi ni propoganda za ki-Soviet union enzi za Cold War. Sikujua kuwa bado zinaweza kuwa effective enzi hizi za utandawazi! poor bongoland:-(
 
Wakuu,

Nimekua najiuliza maswali mengi sana bila majibu. Hivi kwa nini huyu Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond amezungukwa na watu wenye rekodi mbaya na watu wenye utata sana.

Wengi wa marafiki zake wana rekodi mbaya za uhalifu mfano Bashir Awale raia wa Kenya ambaye alijipenyeza hadi kuwa mwanakamati wa Lowassa. Pia kuna lile kundi la vijana 191 walokamatwa kwa makosa ya kimtandao ukiachilia mbali wengine wengi wanaojulikana kwa umafia wao.

Najiuliza maswali mengi endapo watanzania wasingemkata tarehe 25 Octoba Ikulu yetu takatifu ingekuaje na group la watu hawa wabaya waliomzunguka Edward.

MUNGU ANAIPENDA TANZANIA
 
Back
Top Bottom