singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
Siasa za Visasi. Hatutakubali nchi iendeshwe kwa visasi vya mtu mmoja mwenye madhaifu yake
Tunajua kinachofanyika tarehe 5,Novemba.
ninachojiuliza ni kuwa huyu mtu amekuwa hapa nchini kama mtumshi wa benki na amekuwa akisafiri Je? amekuwa akitumia hati ya nchi gani? kama ni Tanzania alikuwa mtu Maaufu kama CEO wa benki kubwa kwanini hakuweza kugundulika? Je kugundua muda huu uweledi wa Uhamiaji katika kukamata wanaofoji hati za kusafiria za Tanzania utapimwaje? na kwanini mtu wa Uhamiaji hajalitolea maelezo? ah maswali mengi???????
Mkuu tatizo na wewe unaleta ushabiki bila mantiki.
Hebu fuatilia gazeti la Nipashe imekiri kuwa jamaa ni mkenya. Pia kibali chake cha kuishi nchini kama mgeni imewekwa. Sasa unabisha nini? Mlikuwa mnamtumia mkenya mwenye asili ya kisomali kama mshauri wenu wa kisiasa. Lazima tuhoji watanzania uzalendo wenu na wa mgombea wenu.[/QUOTE
Hakuna kitu kibaya kama ulofa wa akili,kukaa miaka mingi nchi ambayo sio yako hakukupi kuwa raia wa nchi husika ,ndio maana unaweza beba box miaka kibao nchi za watu lakini huwezi kupiga kura na kupewa passi ya nchi husika bila kutimiza vigezo,pia huruhusiwa kushiriki mambo ya siasa kama wewe sio mwananchi wa nchi husika,halafu huyu mheshimiwa amedanganya kuwa kazaliwa Dodoma wakati si kweli alikuja hapa kwa mgongo wa CITI bank na akahamia benki ingine ,mafisadi wakampa pasi na kumfanya ni mtanzania,akina Masha wana la kujibu.
Ben kweli unajishushia hadhi kwa maneno unayoongea ,naona umekuwa kipofu wa sheria za nchi,kwa mtu anayejiita mtafiti na anashindwa kufanya utafiti ndio ajibu majibu sahihi ni kuidharilisha taaluma ya utafiti.Hivi wewe Ben unaweza vuka Rombo ukaenda Taveta ukajiandikisha kuwa wewe ni raia wa Kenya ,ukapiga kura wakati unajua kisheria haki hiyo huna na ukashiriki kwenye kampeni za kisiasa wakati unajua wewe sio Mkenya ,halafu ukikamatwa utadai ni siasa za upinzani,wenzetu linapokuja suala la uraia na usalama wa nchi siasa za majitaka huweka pembeni,na utaifa huchukua nafasi.Mkuu Ben unazungumzia novemba ipi? Hii au ya mwakani? Au hapo kwenye tarehe nia typing erra?
Ikiwa wewe ni Mtanzania halafu humtambui rais huo ni uhaini. Hukumu yake kwenye baadhi ya nchi ni kunyongwa hadi kufa. Tahadhari ichukuliwe.