Msafara wa mh. Nahodha Wapigwa Mawe Tunduma-Mbeya

Hata mimi nashangaa jiji la dar mbona mmelala?
Kichekesho!Dar es salaam kuna kitu kimoja ikifanyika sensa halafu ukaweka kipengele kinachohusu Dini then utajua wakazi walio wengi Dar ( ukiondoa majimbo ya watu wa kuja au wasio wazawa kufuatana na tafsiri ya Iddi Simba) utagundua ni masikini wanaoshinda kwa mlo mmoja na wamepumbazwa na itikadi ya Cuf chama cha Dini Fulani. Kwani wanaaswa kwenye Nyumba za ibada kwamba kule ikulu hakuna Kafir kwa hiyo maandamano au kuipinga Ccm na Cuf ni kinyume cha dini yao. Kwa Hilo ccm na Cuf wamefanikiwa. You can't have a powerful opposition Kama akina Kova wapo. Kama kuna mwenye ubishi jaribu Kinondoni, Ilala au Temeke moto utakuwakia of course na elimu duni inachangia. If you think It's a joke ask the disgraceful Iddi Simba na pesa za EPA!
 
Yule jamaa Job Ndugai akiona hoja kama hizi hapa JF anapata hasira kweli...ngoja nimuongezee hasira "NADHANI HII NDIO KAZI ILIYOBAKAI KUFANYWA NA WATANZANIA HASA VIJANA...."
 
Hao vijana washughurikiwe,kwani huyo ni kiongozi wa kitaifa anahitaji heshima yake,hata kama alikuwa ktk kuimalisha chama bado huko hakuharalishi wao kumpopoa kwa mawe,

wangetumia busara tu hata kwa kuelezea hisia kwa maneno lakini sio mawe

leo tunafurahia ni CCM kesho madaraka yatashikwa na chama kingine hayo mambo yatajirudia tena
 
Nyinyi mnafurahia watu kurusha mawe akili zenu kidogo zina mafuta ya taa mawe hayabadilishi madaraka pakichukuliwa hatua za kisheria hakika nyinyi ndio mwanzo kusema serekali inaonea raia zake la muhimu ukifika uchaguzi watu wende kwa wingi kupiga kura na kuleta mageuzi sio mawe wala maandamano ya sio kuwa na tija
Sina uhakika kama unajua vizuri maana ya neno "tija"
 
Wakitaka Tunduma ichafuke na wasikanyage tena pale wajaribu kuwaondoa hao wafanya biashara!
 
Watawala wetu hawajifunzi yanayoendelea duniani. A wave of change. Change against oppression. The oppressed r rising up n raising their voices. Voices of agony. Voices against oppressors.
Oppressors and their children are getting drunk. Sitting on the backs of the oppressed. These r their chairs. The oppressed r whispering. Voices r heard only among the oppressed.
Oppressors r drinking n dancing. No longer do they understand each other.
Time is ripe 4 the oppressed to take their matchets n slain their oppressors.
Nahodha is sailing in the boat of oppressors.
 
hapa ndo nashindwa kuwaelewa hawa watawala wetu yaani bado tu wanashindwa kutofautisha kati ya kazi za chama na serikali basi kama ni hivyo yale mavx ya chama pale HQ yakasaidie kufanya kazi za wizara,na kama kulikua na vibahasha vya kaki,ni kutoka magogoni au kaka nape ndo aliviratibu?
 
kwa nini ukombozi unaanzia pembeni wakati Dar wengi wajuzi wa kuongea tu vitendo ziro, kwa sisi vijana usharobaro unazidi sana na milegezo ya suluari, na wengi ni watoto waliosomea( FM Academia) Joke, hawana habari na mabadiliko na hawasikii Redio, TV wala kusoma Interneti, wao ni Bongo Star Move, Bongo Fleva, Masikio yanabanwa sana na mambo ya kidunia kama vile mziki wa Kibonngo na kuvaa vizuri ili wavamiwe na wakina mama walioua wame zao ili wapate mali kirahis, ndio hawa wasuka nyere na kutoga masikio.

Ya kulaumu ni serikali ya MWINYI iliyoondoa JKT. Watotot wengi hawajiwezi kazzi melegezo , hata nguvu hawana kabisa kwani chakula chao ni chips na mayai, hawa ndio wanaoomba baba zao wafe ili walithi.
 
Saturday, 04 February 2012 08:08
ALIKUWA KATIKA ZIARA YA CHAMA MBEYA, ASHANGAA VIJANA KUMPIGA, AAGIZA POLISI WAWASHUGHULIKIE

nahodha-vuai-top.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Shamsi Vuai Nahodha​


Stephano Simbeye, Tunduma.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, jana alionja 'joto ya jiwe' baada ya msafara wake kupigwa mawe alipokuwa kwenye ziara ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya.Tukio hilo la tatu kwa viongozi wa Serikali kushambuliwa mkoani Mbeya, lilitokea eneo la Soko la Tunduma (Kisimani), wilayani Tunduma.

Habari zilieleza kuwa tukio hillo lilitokea wakati Waziri huyo na msafara wake walikuwa wanapita kuelekea ofisi za CCM Kata ya Tunduma ambako alitakiwa kufanya mkutano wa hadhara.

Ilikuaje?

Dalili za machafuko zilianza wakati msafara huo unapita kwa baadhi ya vijana wanaofanya biashara ya kubadilisha fedha sokoni hapo kuanza kujipanga barabarani wakizomea na kupiga miluzi.

Wengi wa vijana hao walisikika wakilaumu kitendo cha Waziri huyo wa Mambo ya Ndani kutumia magari ya Serikali katika msafari wake wa kichama.

"Haya ni matumizi mabaya ya mali za umma," alisikika akisema mmoja wa vijana hao.

Vijana hao walianza kumzomea waziri huyo huku baadhi wakirusha mawe kabla ya kudhibitiwa na polisi waliokuwa wanasaidiana na walinzi wa CCM maarufu kwa jina la Green Guard.

Katika sekeseke hilo vijana wawili walikamatwa na kukabidhiwa katika Kituo cha Polisi cha Tunduma.

Hata hivyo, Mkuu wa kituo hicho ambaye hakutaka kutajwa gazetini kwa kile alichoeleza kuwa yeye sio msemaji wa polisi, alikiri kuwapokea vijana hao na kueleza kuwa wanaendelea kuwafanyia mahojiano.

Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Yusuf Haonga alisema wamechukua hatua hiyo kwa vile Waziri huyo aliwachanganya kwa kutumia magari ya Serikali akiwa kwenye ziara ya chama.

"Hawa wanatuchanganya, inakuwaje wanatumia rasilimali za nchi kwa kazi za chama. Pesa hizo si zingetumika kuhudumia wagonjwa waliolala mahosipitalini badala yake wanazitumia wao,"alisema Haonga.

Haonga alisema kuwa kitendo cha Waziri akiwa mtumishi wa umma kufanya ziara ya kichama kwa magari ya Serikali, kiliwakera na waliamua kumtupia mawe ili kutoa onyo kwa viongozi wengine wa Seriakali.

Hata hivyo, habari zingine zilieleza kuwa vijana waliomrushia mawe Waziri huyo ni wafuasi wa Chadema.

Gazeti hili lilishuhudia baadhi ya vijana wakiwa na bendera za chama hicho cha upinzani ambao pia walikuwapo kwenye msafara huo uliomalizikia kwenye mkutano huo wa hadhara.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alipopulizwa kuhusu tukio hilo alihoji "Unataka niseme nini? Mimi niko Dar es Salaam na tukio hilo limefanyika Mbeya."

Aliendelea, "Ndio kwanza unaniambia (mwandishi). Inabidi nijue nini kilitokea na kama kweli ni vijana wa Chadema nijue walikasirishwa na nini."

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu suala hilo alijibu," Sina taarifa."

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo, Abbas Kandoro jana alishindwa kuzungumzia tukio hilo kwa kile alichoeleza kuwa yuko kwenye safari ya kikazi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliohutubiwa na Nahodha, mwenyekiti wa CCM Kata ya Tunduma, Daniel Mwashiuya alisema kuna kikundi cha watu ambacho kimeanza kupoteza amani ya mji wa Tunduma kutekeleza matakwa yao ya kisiasa.

Alisema "mazingira tunayokwenda nayo kwa sasa si mazuri kwa ustawi wa mji wetu hivyo Wanatunduma tujiepushe na kuvunja amani tuliyoizoea ili isije ikapotea," alisema

Kauli ya Waziri Nahodha

Akihutubia mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo, Waziri Nahodha alisema hajapendezwa tukio hilo na kuhoji, "Kama limefanyika kwangu hali ikoje kwa watu wengine?"

Alisema kamwe hawezi kuacha hali hiyo ya uvunjifu wa amani iendelee na kuiagiza polisi mkoani Mbeya kuchukua hatua haraka dhidi ya kikundi hicho cha watu aliowaita wahuni.

Waziri Nahodha pia amepiga marufuku biashara haramu ya kubadilisha fedha katika eneo hilo.

Alisema mtu anayetaka kuendelea kufanya kazi hiyo itabidi afuate taratibu zinazotakiwa ili aweze kuihalalisha biashara yake.

"Sokoni pana biashara za aina mbalimbali zilizo halali na haramu, lakini nawaagiza polisi chini ya Kamanda wenu wa Mkoa, mkae muangalie namna ya kurejesha amani mahali hapo. Sasa likizo basi," alisema Nahodha.

Waziri Nahodha alisikitishwa na taarifa za kuendelea kuvunjika kwa amani katika mji wa Tunduma ambapo aliwataka wananchi wa mji huu kuthamini amani iliyojengeka kwa muda mrefu.

Aliwataka wasidhani kwamba amani iliyopo imeshuka kutoka Mbunguni na kwa sababu hiyo wao wenyewe wailinde na kuidumisha kwa kushirikiana na polisi kwa njia ya ulinzi shirikishi.

Historia ya matukio

Hili ni tukio la tatu kwa viongozi wa kitaifa kuzomewa katika mji wa Tunduma ambapo mwaka 2010, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, alizomewa katika eneo hilo alipokuwa akipita kutokea mkoani Rukwa katika ziara za kampeni za uchaguzi.

Mwaka 2009, Mwenge wa Uhuru ulilazimika kubadili njia ghafla kufuatia dalilili za uvunjifu wa amani.

Tukio jingine ilikuwa ni Oktoba, 2008, ambapo msafara wa Rais Jakaya Kikwete kushambuliwa kwa mawe kwenye kijiji cha Kanga, wilayani Chunya.

Tukio hilo lilitokea katika Kijiji hicho wakati msafara wa Rais ukiwa njiani kuelekea Mbeya mjini ukitokea mji wa Mwakwajuni wilayani Chunya ambako alikuwa amefanya ziara.
Kwa mujibu wa habari hizo magari sita yaliyokuwa kwenye msafara huo yalishambuliwa kwa mawe na baadaye vijana kadhaa walikamatwa.

Ilidaiwa kuwa waliofanya tukio walikuwa wamejipanga pembeni mwa barabara na baada ya magari manne ya mwanzo kupita, likiwamo la Rais Kikwete, ndipo mawe yalianza kuvurumishwa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa wananchi hao walikasirishwa na kitendo cha kushindwa kumwona Rais Kikwete baada ya kumsubiri kwa muda mrefu ili awahutubia na kusikiliza kero zao.
 
Wananchi wanaanza kuwaamkia Viongozi kwa Vibao; inakuja atabidi waanze kuishi mahotelini Dar

sasa anawatishia polisi watachunguza
 
Pumbavu wote nyie mnaoshabikia maasi.

Pumbafu wewe mwenyewe na waliozaa jipu kubwa kama wewe kwenye ubongo wako kuna msuli ndio maana unaropoka pumba. Kuiba bilion 10 za wizara ya ujenzi sio uhalifu? Ni mfano tu. Kutumia kodi za walalahoi kunadi chama kinachotutesa na inflation sio uhalifu?
 
anadai kama yeye amefanyiwa hivyo na wengine itakuwaje... sijui anataka apigwe nani zaidi ya yeye
 
Naomba nisaidiwe, ni nahodha yule mkoloni wa Kizanzibari anayewatawala watanganyika kupitia wizara ya mambo ya ndani? Kama ni hivyo hii habari imenikumbusha KIBANGA AMPIGA MKOLONI, tETETETETEEEEEEEEEE?!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kama ni Kweli alikuwa anatumia Magari ya Serikali kwa Shughuli za Kichama alikuwa anastahili kabisa Kupigwa. Nawapongeza wote waliotupa Japo jiwe.
 
hakutandikwa hata moja la kichwa??

Hahahahahaaaa........tatizo ccmafisadi!! Chama kichafu kina madoa na hayatoki tunahitaji kitambaa kipya nacho.....chama cha upinzani kushika hatamu......watachezea sana mawe mwaka Huu.......wapi Nape?
 
Back
Top Bottom