Msafara wa mh. Nahodha Wapigwa Mawe Tunduma-Mbeya

Msafara wa mh. Nahodha Wapigwa Mawe Tunduma-Mbeya

Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi la leo, msafara wa waziri wa mambo ya ndani mh. Nahodha umepigwa mawe na vijana wa huko tunduma. Kisa ni kwamba vijana hawakufuruhishwa na kitendo cha kumuona waziri akitumia magari ya serikali akiwa katika shughuli za kuimarisha chama chake huko Mbeya. Vijana wanahoji kwa nini rasimali hizo zisitumike kusaidia wananchi wengine kama vile wagonjwa walioko hospitalini? Hivi ndivyo nchi yetu inavyokwenda kwa sasa.

Source: Mwananchi

Leo hapa mbeya ni adha tupu,kila saa barabara zinafungwa kupisha msafara wake wenye magari zaidi ya kumi ya serikali,afu serikali inalalamikia ukata!
 
Hizi na dalili tosha za kwamba nchi inakuwa ngumu kutawalika...inabidi wamtafute mwekezaji awasaidie kwenye hili pia.Unachukua gari la serikali kwenda kwenye shughuli za kichama!!,wake up CCM people are not that blinded by ignorance as they used to be.
 
Ni habari nzuri kwa wapigania ukombozi wa nchi yetu.

Wafurahie kwani ndo wamefika level nzuri na wajipe moyo na kujipanga zaidi ktk kumng'oa nduli CCM
 
hakutandikwa hata moja la kichwa??


Hahahahah lol! Watanzania wamechoka banaaa...Sasa shuhudia kama nchi nzima ikiamua kuvurumisha mawe dhidi ya viongozi wote wa juu wa magamba kutokana na gharama za maisha kutoshikika....patakuwa hapatoshi sijui watakimbilia wapi.
 
Wangemua kabisa,hawa CCM wametufikisha kwenye umaskini hu
 
safiiiiiiiiiiiii sana huko magamba lazima wakione cha moto wanadhani watu wanapelekwesha kama ngo'mbe wanaokwenda kulima?Aliendaje mbeya bila kuuliza alama za nyakati zimekaaje huko mwenye nchi mwenyewe walimpopoa sembuse yy
 
da kwetu mbeya pazur, nimepakumbuka... Wanyambara cie hatupendag zarau
 
Mimi nawasikitikia watanzani kuwapa dhamana watu wanaoogopa kuchimba na kuondoa mizizi ya matatizo yao. Wanatumia mamilioni ya fedha kushughulikia matokeo ya matatizo hayo. Si rais, waziri, mbunge na hata polisi wote hakuna anayejiuliza kwanini watu wanawatendea hivyo? Wenyewe wamekariri jibu moja tu, kuwa ni watu wanaotaka kuvuruga amani jibu ambalo watanzania tunahisi yawezekana uwezo wao wa kufikiri ni mdogo au ziro kabisa au hawatujali na wameamua kuficha ukweli wakidhani hatujui nini kiini cha tatizo. Ndiyo maana wahusika wametaja sababu lakini hakuna anayewaamini. Ama kweli tuna viongozi ambao dah!
 
Siku hizi niko bize namwomba Mungu watawala kama hawa wafe.
 
Taratibu jamani, kokoto hazitasaidia zaidi ya kujeruhi na wananchi wasio na kosa. People's power haitakiwi kuwa expressed kwa kokoto.

Kwa hali hii upunzani bado wana safari ndefu kutwaa mamlaka ya nchi. Jazba zimewajaa sasa utamwongoza nani kwa jazba? tafakarini:llama:
 
Hahahahah lol! Watanzania wamechoka banaaa...Sasa shuhudia kama nchi nzima ikiamua kuvurumisha mawe dhidi ya viongozi wote wa juu wa magamba kutokana na gharama za maisha kutoshikika....patakuwa hapatoshi sijui watakimbilia wapi.
Kumbe nyie simbilisi kulia ni jadi yenu?

Kumbe hata huyu kipenzi chenu wa sasa hivi ndugu JK mlikuwa mnamuona takataka?
 
Back
Top Bottom