Msaada wenu waungwana wa Jamii Forums

Aug 19, 2020
66
55
Heshima yenu wakuu:​

Mimi ni kijana wa kiume mkazi wa Dar es salaam na katika harakati za kielemu nimefanikiwa kuhitimu kidato cha sita.​

Pia kupitia marafiki nimefanikiwa kuwa na ujuzi wa kutumia Computer na applications zake mbalimbali ikiwemo namna ya ku install hizo apps na kuzitumia na kwa kiasi fulani (sio sana) naweza kutafuta chanzo cha tatizo na kulirekebisha kama sio kubwa sana endapo litatokea kwa upande wa hardware na kidoooogo software.​

Kwa upande mwingine mimi ni kijana ambaye napenda na niko tayari kujifunza mambo mapya yahusuyo maisha kwa ujumla na naomba nikiri kwamba si utayari tu bali nafundishika kweli.​

Lengo la kuja kwenu ndugu zangu ni kuomba msaada kwa yeyote ambaye anaweza kunisaidia kazi/kibarua au hata connection ambayo itanisaidia kupata kazi/kibarua cha kuweza kuingiza kipato bila kujali ni kikubwa ama kidogo kwasababu hicho kikubwa kilianza kidogo pia, na kwenye hilo sijali sana hata kama itakuwa haihusiani na mambo ya taaluma niko tayari.​

Kila mtu ana namna yake ya kusaidia anaweza asiwe na namna ya kusaidia hiyo kazi/kibarua ila akawa na uwezo wa kutoa fedha kama mtaji pia halitakuwa jambo baya, kwa maana hiyo ni kwamba sijaweka limitations katika hilo muhimu ni kupata kitu kitakachoniwezesha kutengeneza kipato regardless ni kidogo au kikubwa.​

Nimekuja kwenu ndugu zangu kwasababu nina imani ya dhati (kutoka moyoni) kwamba Jamii Forums ni sehemu sahihi na ambayo mtu yeyote anaweza kupata msaada kwasababu wapo watu wenye nyoyo za kusaidia.​

Najua hali ya kiuchumi ni ngumu ndugu zangu lakini naamini naweza kupata msaada na hatimaye tukafurahia uwepo wetu hapa dunia pamoja kwahiyo tafadhalini ndugu zangu naombeni mnisaidie.​

NB: 1. Kila mtu huwa ana maoni yake kutokana na kulitazama kwake jambo na huwa hatuna budi kuheshimu maoni ya kila mtu.​

2. Simpangii mtu namna ya kutoa maoni ila pia sidhani kama ni kitu kizuri kuchukulia kuomba kwangu msaada in a negative way kwasababu mpaka kuja huku ni kweli nina uhitaji na namaanisha.​

Majukumu mema na naomba kuwasilisha waungwana.​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom