Msaada wenu wa mawazo tafadhali, Maisha ya kuishi ukweni yamenishinda

kabla hujaolewa ungemwambia mwenza kua huwezi kuishi ukweni nadhani ungeipata suluhu kuliko sasa
 
Mifano yako haina uhalisia wowote,unatoa mifano ya masperstar toka lini diamond aliwahi kufunga ndoa???.
Mwanamke kukaa na ndugu wa mwanaume hicho ndio kipimo cha upendo wake kwako,na inavyoonekana wewe mke wako anakupelekesha.
 
Kwani mume wako hela ya matumizi huwa anamwachia mama yake au wewe??? Hadi mama mkwe apange mnakula nini??
 
Wewe ni mbinafsi kama walivyowanake wengi wa kiafrica kutaka kutawala nyumba,wewe ni sehemu ya familia ya mumeo kwani ukiishi na ndugu wa mume wako kuna tatizo gani??? Mbona jamii nyingi hapa duniani kama wahindi ,waarabu na hata baadhi ya wazungu wanaishi kindugu na maisha yanakwenda.acheni ubinafsi nyie wanawake.
 
Baadhi ya wanawake ni wa hovyo sana! Wengi wao hawapendi kuishi ukweni sababu kubwa wanaona ikitokea jamaa amefariki inawawia vigumu kubaki na mali.

Wanataka muishi kama 2 ili ikitoa umefariki iww rahisi ku take control ya mali,hamna lolote la ziada.
 
ndo tatizo la kuolewa na vijinaume vya kiswahili, kwendaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Acha zako wewe hivi umemwelewa vizuri mwenzio anaishi na mama mkwe mpaka na ma wifi zake na waume zao nao huwa wanakuja kutamia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kabla ya kuwowana hukuyaona hayo......au ndo mapenzi ni giza nene.....kumepambazuka wajishtukia...komaa...kuna siku na wewe utakuwa mama mkwe.....tafakari....
 
Maisha hayajakushinda changamoto ndo znakupa tabu hapo suluhisho ni kumwambia mumeo japo inatakiwa utumie akili nzuri katika maelezo mana kunamahusiano makubwa sana kati ya mama na mwanaye.
 
Mwanamke anaachana na baba na mama ake anaambatana na mumewe....vivyo hivyo mwanaume asa unanipeleka kwenu kutafuta nini, ndugu zako sjawakataa ila lazima tuwe na maisha yetu shoga angu
 
Hapa anapaona kwake kwasababu nyumba amejenga yeye lakini tunaishi na familia yake yote hata madada walioolewa wamo ndani na waume zao.
Duh pole sana, ila omba mungu na wewe endelea kupambana kumshauri mumeo taratibu tu, amini usiamini kuna siku ataelewa..
 
Haswa, safi kabisa kabisa...
 
Huyo jamaa anayumba huwezi ishi na mke ukweni

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndiye unayumba, kuna mda inakubidi uishi na wazazi wako kulingana maybe ni wazee sana na hakuna wa kuwatazama zaidi yako, au wewe ndo mtoto wa pekee katika tumbo la wazazi wako, je utawakimbia ili iweje, sema mifumo ya uendeshaji wa familia ndiyo hutofautiana
 
Yeah, upo sahihi
 
Huu uzi unazidi kunichanganya tu sisi tunaoishi kwa wazazi, life lenyewe halina welekeo sahihi
 
Suala la kuishi kwenu eti kisa sjui umezaliwa peke yako halina mashiko labda la uzee na uangalizi km wamefikia umri wa kutokujiweza,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…