Msaada wenu wa mawazo tafadhali, Maisha ya kuishi ukweni yamenishinda

kabla hujaolewa ungemwambia mwenza kua huwezi kuishi ukweni nadhani ungeipata suluhu kuliko sasa
 
Unafikiri kwanini ndoa ya Alikiba na Diamond zimishindwa kuendelea? Kwasbb ya kuishi nyumba moja na ndgu pamoja na wazazi. Unatakiwa ukae mbali na ndugu pamoja na wazazi yaani unatakiwa ujenge nyumba mbali na nyumbani na uishi wewe na watoto wako. Ndugu zako pamoja na wazazi wako wanapaswa wawe wanakuja kukusalimia na kuondoka. Mimi kwao na mke wangu tukitaka kwenda kusalimia huwa siwezi kukaa siku 3. Ni 2 tu nakuondoka. Hii ya kurundikana nyumba moja ni kutafutiana lawama
Mifano yako haina uhalisia wowote,unatoa mifano ya masperstar toka lini diamond aliwahi kufunga ndoa???.
Mwanamke kukaa na ndugu wa mwanaume hicho ndio kipimo cha upendo wake kwako,na inavyoonekana wewe mke wako anakupelekesha.
 
Kwani mume wako hela ya matumizi huwa anamwachia mama yake au wewe??? Hadi mama mkwe apange mnakula nini??
 
I had the same case akati naolewa mume wangu amejenga anaishi na familia yake, na mimi nshakuwa na mambo yangu na nina kwangu, nlivoolewa kila mtu abaki na cha kwake nihamie kwake tukaishi na mama mkwe sjui na mawifi lakini nlifanya kutafuta nyumba nkachukua vile vitu vya ndanj nikaweka nyumba nikapangisha tukafuatana na mume tukapanga uku tukijenga yetu.......hakuna usumbufu wala wa kuuliza wakiulizana wanaulizana wenyewe
Wewe ni mbinafsi kama walivyowanake wengi wa kiafrica kutaka kutawala nyumba,wewe ni sehemu ya familia ya mumeo kwani ukiishi na ndugu wa mume wako kuna tatizo gani??? Mbona jamii nyingi hapa duniani kama wahindi ,waarabu na hata baadhi ya wazungu wanaishi kindugu na maisha yanakwenda.acheni ubinafsi nyie wanawake.
 
Baadhi ya wanawake ni wa hovyo sana! Wengi wao hawapendi kuishi ukweni sababu kubwa wanaona ikitokea jamaa amefariki inawawia vigumu kubaki na mali.

Wanataka muishi kama 2 ili ikitoa umefariki iww rahisi ku take control ya mali,hamna lolote la ziada.
 
Nilikutana na mume wangu wote tukiwa 30+. Nilishakuwa na kwangu tofauti yangu na mwenzangu yeye anaishi kwao ingawa yeye ndiye alijenga nyumba.

Kama mwanaume aliyeoa anataka niishi kwao. Hataki kuingilia vitu alivyonikuta navyo. Maisha ya kuishi ukweni yamenishinda, ninatamani tununue kiwanja tujenge nyumba ya pamoja lakini mwenzangu haoni umuhimu huo.
ndo tatizo la kuolewa na vijinaume vya kiswahili, kwendaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Baadhi ya wanawake ni wa hovyo sana! Wengi wao hawapendi kuishi ukweni sababu kubwa wanaona ikitokea jamaa amefariki inawawia vigumu kubaki na mali.

Wanataka muishi kama 2 ili ikitoa umefariki iww rahisi ku take control ya mali,hamna lolote la ziada.
Acha zako wewe hivi umemwelewa vizuri mwenzio anaishi na mama mkwe mpaka na ma wifi zake na waume zao nao huwa wanakuja kutamia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kabla ya kuwowana hukuyaona hayo......au ndo mapenzi ni giza nene.....kumepambazuka wajishtukia...komaa...kuna siku na wewe utakuwa mama mkwe.....tafakari....
 
Maisha hayajakushinda changamoto ndo znakupa tabu hapo suluhisho ni kumwambia mumeo japo inatakiwa utumie akili nzuri katika maelezo mana kunamahusiano makubwa sana kati ya mama na mwanaye.
 
Wewe ni mbinafsi kama walivyowanake wengi wa kiafrica kutaka kutawala nyumba,wewe ni sehemu ya familia ya mumeo kwani ukiishi na ndugu wa mume wako kuna tatizo gani??? Mbona jamii nyingi hapa duniani kama wahindi ,waarabu na hata baadhi ya wazungu wanaishi kindugu na maisha yanakwenda.acheni ubinafsi nyie wanawake.
Mwanamke anaachana na baba na mama ake anaambatana na mumewe....vivyo hivyo mwanaume asa unanipeleka kwenu kutafuta nini, ndugu zako sjawakataa ila lazima tuwe na maisha yetu shoga angu
 
Hapa anapaona kwake kwasababu nyumba amejenga yeye lakini tunaishi na familia yake yote hata madada walioolewa wamo ndani na waume zao.
Duh pole sana, ila omba mungu na wewe endelea kupambana kumshauri mumeo taratibu tu, amini usiamini kuna siku ataelewa..
 
Naomba nikupe pole kwa yanakukuta, hili ni tatizo la mwanamke kuolewa na mtoto wa mama.
Kama amejenga nyumba ili wazazi wake waishi hapo, yeye ingekuwa busara angeenda kupanga na kuanza maisha mapya na mkewe ili wawe huru na kufurahia ndoa yenu.
Mimi japo nilijenga nyumba kwa ajili ya wazazi wangu na nilikuwa naishi nao, ila nilivyotaka kuoa, nilienda kupanga nyumba upande mzima.
Ila now nami nipo kwangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haswa, safi kabisa kabisa...
 
Huyo jamaa anayumba huwezi ishi na mke ukweni

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndiye unayumba, kuna mda inakubidi uishi na wazazi wako kulingana maybe ni wazee sana na hakuna wa kuwatazama zaidi yako, au wewe ndo mtoto wa pekee katika tumbo la wazazi wako, je utawakimbia ili iweje, sema mifumo ya uendeshaji wa familia ndiyo hutofautiana
 
Hizi Mila za kizungu zinatuharibia familia
Hivi viwanawake tunavyovioa vinafikia mahali vinataka kuanza kukupangia
Ona kanapeleka hoja ya kujenga nyumba Bora hata kangekuja na hoja ya kufanya biashara kangeeleweka
Hivi wanawake huwa wanaboa sana, hivi nyumba nyumba nyumbaaaa nyumba ukikauliza hivi kwani wewe unalala nje?, hata majibu unakuta hakana kapo kapo tu.
Vinaacha kufikiria biashara vinabaki kusigana na mama mkwe
Piga business hata mama mke atakuheshimu sio kuwaza project za walemavu za kujenga nyumba
Yeah, upo sahihi
 
Huu uzi unazidi kunichanganya tu sisi tunaoishi kwa wazazi, life lenyewe halina welekeo sahihi
 
Wewe ndiye unayumba, kuna mda inakubidi uishi na wazazi wako kulingana maybe ni wazee sana na hakuna wa kuwatazama zaidi yako, au wewe ndo mtoto wa pekee katika tumbo la wazazi wako, je utawakimbia ili iweje, sema mifumo ya uendeshaji wa familia ndiyo hutofautiana
Suala la kuishi kwenu eti kisa sjui umezaliwa peke yako halina mashiko labda la uzee na uangalizi km wamefikia umri wa kutokujiweza,
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom