Msaada wenu wa mawazo tafadhali, Maisha ya kuishi ukweni yamenishinda

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Nilikutana na mume wangu wote tukiwa 30+. Nilishakuwa na kwangu tofauti yangu na mwenzangu yeye anaishi kwao ingawa yeye ndiye alijenga nyumba.

Kama mwanaume aliyeoa anataka niishi kwao. Hataki kuingilia vitu alivyonikuta navyo. Maisha ya kuishi ukweni yamenishinda, ninatamani tununue kiwanja tujenge nyumba ya pamoja lakini mwenzangu haoni umuhimu huo.
 
Mama mkwe akiwa anaamua mnakula nini, mnafanya nini maisha yako yote mume wako ni unayemuita baba mkwe. Hata mkiishi ukweni mnapaswa mpewe chumba chenu baada ya miezi 3 ya kuoana mjue mnaishije.
Uelewe kuwa kabla sijaolewa nilikuwa na maisha yangu, sasa ghafla ninaanza maisha ya mama mkwe kuamua mtakula nini leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku mkihama ukweni.. Mtakiona cha mtema kuni
Nilikutana na mume wangu wote tukiwa 30+. Nilishakuwa na kwangu tofauti yangu na mwenzangu yeye anaishi kwao ingawa yeye ndiye alijenga nyumba.

Kama mwanaume aliyeoa anataka niishi kwao. Hataki kuingia is alivyonikuta navyo. Maisha ya kuishi ukweni yamenishinda, ninatamani tununue kiwanja tujenge nyumba ya pamoja lakini mwenzangu haoni umuhimu huo.

Jr
 
Hizi Mila za kizungu zinatuharibia familia
Hivi viwanawake tunavyovioa vinafikia mahali vinataka kuanza kukupangia
Ona kanapeleka hoja ya kujenga nyumba Bora hata kangekuja na hoja ya kufanya biashara kangeeleweka
Hivi wanawake huwa wanaboa sana, hivi nyumba nyumba nyumbaaaa nyumba ukikauliza hivi kwani wewe unalala nje?, hata majibu unakuta hakana kapo kapo tu.
Vinaacha kufikiria biashara vinabaki kusigana na mama mkwe
Piga business hata mama mke atakuheshimu sio kuwaza project za walemavu za kujenga nyumba
 
Nilikutana na mume wangu wote tukiwa 30+. Nilishakuwa na kwangu tofauti yangu na mwenzangu yeye anaishi kwao ingawa yeye ndiye alijenga nyumba.

Kama mwanaume aliyeoa anataka niishi kwao. Hataki kuingilia vitu alivyonikuta navyo. Maisha ya kuishi ukweni yamenishinda, ninatamani tununue kiwanja tujenge nyumba ya pamoja lakini mwenzangu haoni umuhimu huo.
Hapo ni kumshauri kwa nguvu zote
Muonyeshe Mazingira kuwa kukaa ukweni (kwako) haifai hata kama kajenga yeye

Anakukosea Sana
 
Back
Top Bottom