Msaada wenu, mtu anapost picha zangu kwenye mitandao bila ridhaa yangu

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,514
2,730
Kwa kifupi kuna dada nilishawahi kuwa na mahusiano nae kipindi cha nyuma kabla sijaoa, baadae nilioa tena kwa ndoa takatifu kanisani, katika siku za karibuni amekuwa akipost picha zangu katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kuandika maneno mbalimbali ya kidhalilishaji yanayoniletea shida sana kwenye ndoa yangu, kwenye familia yangu kiujumla kwa maana ndugu zangu wamekuwa wakisumbuliwa sana na hii hali, naombeni msaada wenu nifanyeje, sheria inasemaje.
 
Peleka mahakamani huyo haraka sana bila kumuonea huruma,nchi hii hatujalelewa kusema maneno ya ovyo ovyo.sheria imfunze kidogo.ni kosa kuchukua picha ya mtu na kuiweka mitandaoni na kuandika maneno yasiyostahili.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Kwa kifupi kuna dada nilishawahi kuwa na mahusiano nae kipindi cha nyuma kabla sijaoa, baadae nilioa tena kwa ndoa takatifu kanisani, katika siku za karibuni amekuwa akipost picha zangu ktk mitandao mbalimbali ya kijamii na kuandika maneno mbalimbali ya kidhalilishaji yanayoniletea shida sana kwenye ndoa yng, kwenye familia yng kiujumla kwa maana ndg zng wamekuwa wakisumbuliwa sana na hii hali, naombeni msaada wenu nifanyeje, sheria inasemaje.
Naomba kufahamu ni mitandao ipi ya kijamii ili nikupe maelekezo ya namna unaweza kureport matukio hayo ama ikiwezekana kuondoa kabisa picha zako kwenye mitandao hiyo.
 
Attachments

  • report-fb-fake-profile.png
    report-fb-fake-profile.png
    8.4 KB · Views: 81
Naomba kufahamu ni mitandao ipi ya kijamii ili nikupe maelekezo ya namna unaweza kureport matukio hayo ama ikiwezekana kuondoa kabisa picha zako kwenye mitandao hiyo.
Ana post instagram and Facebook, kwa kweli ananipa adha kubwa mno, alishaonywa mara moja akazifuta, kipindi hiki kaanza tena kwa kasi zaidi
 
Mkuu nenda katoe taarifa TCRA na Polisi
Nataka niende ila nilitaka nifahamu kwanza sheria inasemaje kuhusu hili ili niwe na uhakika wa kushinda na kulikomesha hili jambo kabisa na iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia km hizi.
 
Mkuu ripoti polisi haraka sana wachukue hatua.. ndoa hujengwa kwa gharama kubwa halafu mtu anakuja kukuchezeachezea
Kwa kweli anaisumbua sana ndoa yangu kwa sasa, ndg zangu nawa upande wa mke nao anawapa adha kubwa kwa kejeli na dhihaka anazozielekeza kwangu nakwa mke wng.
 
Tupe mfano wa picha mkuu

Sent from my D2403 using JamiiForums mobile app
Mfano wa namna gani?kuna baadhi ya picha tu alinipiga kipindi tuna mahusiano sasa tumeshaachana anaanza kupost na kuutweza utu wng kwa maneno ya karaha.
 
Peleka mahakamani huyo haraka sana bila kumuonea huruma,nchi hii hatujalelewa kusema maneno ya ovyo ovyo.sheria imfunze kidogo.ni kosa kuchukua picha ya mtu na kuiweka mitandaoni na kuandika maneno yasiyostahili.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Nashukuru sana ndg yng kwa ushauri wako, nitakufanyia kazi.
 
Mwambie mkeo aelewe, hao ndugu wa mke wako wamblock wasimfatilie, wewe mwenyewe mblock .Dawa ya Mjinga ni kumpuuzia tu. Mkikaa kimya bila kumjudge chochote ataacha.
 
Tumia karolaiti picha hizo zitakuwa sio za kwako.

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Hiviii kwelii unataka kutwambia umekosa cha kumfanya kabisa kabisaa mpakaa ufedheheke namna hiii? Mtu alishakuwa kituako jinsi yakumpata sidhan kama inakushinda nahis na Picha ulimtumia mwenyewe nakama anakupost sema anaandika caption za mahaba we unadata sababu umeoa na MKE na ndugu wamesanuka sasaa Kama hujuii taratibu zakufuataa. Tafuta zake nawewe post uandike madudu yako

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
Ana post instagram and Facebook, kwa kweli ananipa adha kubwa mno, alishaonywa mara moja akazifuta, kipindi hiki kaanza tena kwa kasi zaidi
Instagram na facebook zinaoption ya kureport picha hizo. Jaribu kureport hizo picha kupitia option hizo zinazopatika pembeni ya post/picha hiyo
instagram-report-image.png

Kwenye kureport ukiwa na ushahidi kuwa ni picha zako zitaondolewa haraka iwezekanavyo.
Endapo hatua hiyo haitaleta suluhisho, ni vyema kuwasiliana na polisi.
 
Instagram na facebook zinaoption ya kureport picha hizo. Jaribu kureport hizo picha kupitia option hizo zinazopatika pembeni ya post/picha hiyoView attachment 541246
Kwenye kureport ukiwa na ushahidi kuwa ni picha zako zitaondolewa haraka iwezekanavyo.
Endapo hatua hiyo haitaleta suluhisho, ni vyema kuwasiliana na polisi.
Nashukuru kwa ushauri wako.
 
Back
Top Bottom