Nataka kutumia Mitandao ya Kijamii kwa faida tu lakini nashindwa. Naombeni ushauri

Mazepine

Member
Nov 17, 2022
23
25
Habari wana Jf, ni matumaini yangu mpo salama, kwa wenye changamoto kidogo za kiafya au zingine zozote, basi Muumba awafanyie wepesi ndugu zangu.

Samahanini huenda uzi sijui kuupangilia vizuri lkn naombeni, tupitie between lines mnipe msaada wakuu.

Kama kichwa kinavyosomeka hapo juu, nataka na natamani sana niwe natumia mitandao ya kijamii kwa faida tu lakini nashindwa, najikuta natumia kwa mda mwingi na kuangalia mambo mengi ambayo kwangu mimi naona hayana faida, kwa mfano kwenye magroup ya WhatsApp kuwaona watu wanabishana, youtube naangalia vichekesho na habari zingine ambazo nahisi hazina maana kiasi cha kuchukua mda wangu mwingi lkn ndo hivyo zinakula mda wangu mwingi.

Ndugu wana JF mimi si mtumiaji wa mitandao mingi sana ya kijamii. Baadhi ya mitandao ninayotumia ni pamoja na.

1.whatsapp kwa sana na ni miongoni mwa zinazokula mda wangu
2. Facebook kidgo
3. YouTube kwa sana, hapa pia napoteza mda mwingi na fedha za bando
4. JamiiForum, huku pia natumia mda mwingi
5. Telegram, kidgo

Mitandao mingine nlizowah kutumia kidgo nkaachana nazo ni pamoja na
1. Instagram
2. Twitter
3. Quora
4. Linkedln

Hili la kutumia mda mwingi na raslimali fedha ni tatizo naamini kabsa sio kwangu tu lkn kwa vijanaa wengi tayri tuna uraibu wa social media, basi tu watu hawajui ama wanajua lkn hatuhangaiki kutafuta suluhisho

Lakini pia nikiri wazi kuwa mitandao ya kijamii pamoja na kwamba zinasababisha uraibu (addiction) lkn naamini mtumiaji akitumia vizuri hakika anaweza kufaidika sana pia na hichi ndicho nafsi (conscience) yangu inatamani sana, yaani kutumia kwa mda mchache sana na kwa mambo ambayo ni ya msingi tu

JE, BINAFSI NAFANYA JITIHADA GANI KUKABILIANA NA TATIZO?

nimeshachukua hatua mbalimbali za kupambana na hali hii na wakati mwingine nlitaka kabisa nifute mitandao ya kijamii. Baadhi ya jitihada ambazo nimezifanya ni pamoja na;

1. Kumute nofication permanently kweny magroup ya whatsapp yote ambayo, nahisi si ya muhimu na ambazo sitegemei kuwa kuna taarifa yoyote ninayotakiwa kuituma kwa mda huo (NB, kuna baadhi ya magroup ya whatsapp ambayo ni lazima ujumbe ukiingia niangalie huenda kuna taarifa natakiwa niitume kwa mabosi wangu)

2. Kuleft magroup yote ambayo nayaona hayana maana

3. Kutoangalia status kbsa, Whatsapp

4. Kuwa na simu ndgo. Hapa kwenye kuwa na simu ndogo nmejikuta naona ni mzigo kuwa na simu mbili. Af nimetokea sana kuizoea smartphone, ukiachana na upande wake wa kuingilia socia media, lkn pia inarahisisha vitu vingine vingi mfano naweka document kama vitabu nasoma (Kazi yangu inataka niwe najiuptodate), naweza kupiga picha kwa mahitaji mbalimbali, nkichat button hazipigi kelele, nk, so mwishowe nkaendelea na smart yangu nkatelekeza kitochi.

ATHARI GANI NAZIPATA?

Athari ambazo nazipata ni pamoja na;

1. Kupoteza mda mwingi sana, ambayo ningeweza kufanya mambo ya msingi kama vile kujifunza kitu kipya kwenye maisha yangu, NA HII HASA NDIO INAYONIUMA KUPITA MAELEZO.

2. Napoteza pesa nyingi pia, naweza kuunga bando la 2000 ambalo ni la wiki mara tatu mpaka nne kwa wiki.

3. Nakuwa nahisi kama nakuwa socially isolated, sina mda wa kupiga stori na familia au marafiki, lkn niweke wazi pia kuwa japokuwa mimi kwa asili si muongeaji sana, lkn nahisi kama hizi social media zinachangia zaidi kuwa kama nakuwa antisocial kinamna flan hivi

Nliwah kufikiria kufuta kabsa mitandao ya kijamii lkn sas mimi ni mtumishi wa umma (Tabibu) sas kuna magroup ya whatsApp ambayo wakuu wetu huko halmashauri hutumia kututumia taarifa mbalimbali, haya ndo yale ambayo sijayamute kwenye notfication, ili niweze kuona hzo taarifa na kama kuna agizo basi niweze kutekeleza, otherwise mimi ningefuta kabisa mitandao ya kijamii kwa mda mwingi angalau.

KWA KIFUPI, nishaurini nifanyeje niwe natumia hii mitandao kwa mda mfupi na kwa ishu muhimu tu baada ya hapo niachane nazo niendelee kufanya mambo yangu mengine?

Najua yawezekana kuna wadau walipata changamoto kama hii na pengine walipata namna ya kukabiliana nalo, nisaidieni, maana naona hizi social media zinanifanya nakuwa kwenye agenda za watu na kusahau zangu.

Naomba kuwasilisha
 
Tafuta lengo la kuweza kuwa sehemu ya kuleya mabadiliko positive katika dunia

Binafsi kwa sasa nachangia sana kujaribu kuwaweka watu katika njia inayompendeza Mungu.

Napata upinzani mkali ila nami naweka alama.
 
Upo wapi? Kazi yako nini?

Kama Dar fanya winga.

Mfano:

Unakikuta kiatu Insta David Sportwear anauza elfu 30, we unakipost status elfu 40 ukipata mteja unafuata.

Same unakuta mtu anauza simu laki 5 unapost 550k ukipata mteja unafaidika.
asante kwa ushauri, nipo mikoani mkuu, Natibu wagonjwa mkuu
 
elezea kidgo mkuu, huenda ukanipa mwanga
Mitandao ya kijamii ni kama kuwa mitaani tu sema kidijitali.

mtaani huwezi kuwa bize na mambo ya watu tu ama kulala siku nzima ama kupiga story tu, haya mambo tunafanya ila kuna kipimo chake hasa tukimaliza kufanya shughuli zetu zinazosaidia jamii ndio jioni tunaweza kwenda vijiweni, kupiga story, kwenda sehem za starehe, n.k.

Basi na kwenye mitandao hali ndivyo ilivyo, jaribu kutumia muda mwingi mitandaoni kujiufunza kitu positive ama kufanya kitu positive kinachoweza kukusaidia ama kusaidia wengine, baada ya hapo sasa ndio unaweza kuingia ingia kidogo kwenye vichekesho, mizaha, memes, mpira, magroup ya story, n.k.

Nje ya mitandao hakikisha una shughuli za kiamii unazifanya, kutumia sana mitandao isiwe sehemu kubwa ya maisha yako
 
Mitandao ya kijamii ni kama kuwa mitaani tu sema kidijitali.

mtaani huwezi kuwa bize na mambo ya watu tu ama kulala siku nzima ama kupiga story tu, haya mambo tunafanya ila kuna kipimo chake hasa tukimaliza kufanya shughuli zetu zinazosaidia jamii ndio jioni tunaweza kwenda vijiweni, kupiga story, kwenda sehem za starehe, n.k.

Basi na kwenye mitandao hali ndivyo ilivyo, jaribu kutumia muda mwingi mitandaoni kujiufunza kitu positive ama kufanya kitu positive kinachoweza kukusaidia ama kusaidia wengine, baada ya hapo sasa ndio unaweza kuingia ingia kidogo kwenye vichekesho, mizaha, memes, mpira, magroup ya story, n.k.
Shukran mkuu
 
Mkuu tafuta watu waliopo kwenye taaluma yako wafollow ,pia channel za YouTube zinazohusu taaluma yako ama skill ambazo unahitaji muda huu au kesho ila usisahau kuishi
 
Back
Top Bottom