Msaada wana JF hivi kumiliki laini ya muamala inahitaji mtaji kiasi gani?

complexi

Member
Jul 6, 2021
67
82
Habarii JF.

Mimi ni mwanachuo,lakini kutokana na hali ya maisha ya sasa nimeona nijitafutia kitu kidogo ambacho kitanipa msingi mara nikihitimu masomo yangu

Kwahiyo nimepata wazo la kumiliki laini japo moja ya muamala lakini sijui mtaji shingapi natakiwa niwe nayo na namna gani ya kuendesha

Naombeni msaada wenu wana Jamiii.
 
UTAWEZA KUFANYA MIAMALA NA KUSOMA KWA WAKATI MMOJA? WHAT IF UKISTICK NA MASOMO KWANZA? AU WEKEZA HELA MAHALI KAMA AKIBA UKIMALIZA SHULE NDIO UANZE?
 
Kwanza naomba kukupa Hongerà kwa ujasiri wa Kuamua kutafuta chanzo Cha mapato wakati upo masomoni..

Mfumo wa elimu kwa Sasa unahitaji wanafunzi Kama wewe wenye kuangalia future yao.usisikilize hao wanaosema mshika wawili moja humponyoka! Chuo ni elimu ya watu wanaojitambua ndio maana Kuna waajiliwa.

Sasa komaa na Masomo alafu ukija mtaani ndio utajua.

Taratibu za kupata Raini ya uwakala
1.Tafuta TIN number na kitambulisho Cha Taifa au namba, alafu nenda makao makuu ya Vodacom au Airtel utapewa bure hizo Raini.

Nasema hivi nikiwa Kama wakala mstaafu.
 
Kwa mitazamo hii ndio maana wazungu wanatupiga gape kila siku. Yaaani Investment isubiri kumaliza chuo..?
 
SHIDA UNAKURUPUK KWANZA BILA KUSOMA KAMA NILITOA OPTIONS

YEAH INAWEZEKANA FANYA UTAFITI KWANZA MAANA USIJE UKAINGIA MKUKUMKUKU UKAISHIA KUPIGWA HELA YAKO BUREE

MTAJI WA LAKI MBILI, TATU, TANO NA KUENDELEA UNAANZA MDOGO MDOGO
 
Kwanza naomba kukupa Hongerà kwa ujasiri wa Kuamua kutafuta chanzo Cha mapato wakati upo masomoni..

Mfumo wa elimu kwa Sasa unahitaji wanafunzi Kama wewe wenye kuangalia future yao.usisikilize hao wanaosema mshika wawili moja humponyoka! Chuo ni elimu ya watu wanaojitambua ndio maana Kuna waajiliwa.

Sasa komaa na Masomo alafu ukija mtaani ndio utajua.

Taratibu za kupata Raini ya uwakala
1.Tafuta TIN number na kitambulisho Cha Taifa au namba, alafu nenda makao makuu ya Vodacom au Airtel utapewa bure hizo Raini.

Nasema hivi nikiwa Kama wakala mstaafu.
Safi.

Akingoja amalize shule akirudi mtaani atakutana na kodi ya chumba, buku za bando, bili ya umeme, bili ya maji, Demu anataka hela ya kusuka.

Asirudie kosa tulilolifanya tulio wengi.
 
Kwanza naomba kukupa Hongerà kwa ujasiri wa Kuamua kutafuta chanzo Cha mapato wakati upo masomoni..

Mfumo wa elimu kwa Sasa unahitaji wanafunzi Kama wewe wenye kuangalia future yao.usisikilize hao wanaosema mshika wawili moja humponyoka! Chuo ni elimu ya watu wanaojitambua ndio maana Kuna waajiliwa.

Sasa komaa na Masomo alafu ukija mtaani ndio utajua.

Taratibu za kupata Raini ya uwakala
1.Tafuta TIN number na kitambulisho Cha Taifa au namba, alafu nenda makao makuu ya Vodacom au Airtel utapewa bure hizo Raini.

Nasema hivi nikiwa Kama wakala mstaafu.
Shukrani kwa maelezo yako nianze kuya fanyia kazi.
 
Back
Top Bottom